Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Magufuli katutenda deni la taifa, trilioni 78 Samia msalabani

Jamhuri October 26, 2021

Na Deodatus Balile

Kazi hii ya uandishi wa habari moja ya majukumu yake ni kuanika ukweli minong’ono inapotawala katika jamii.

Kwa sasa kuna minong’ono mingi. Minong’ono imeanza baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza hadharani mkopo wa Sh trilioni 1.3, alioukopa kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na akatangaza miradi lukuki itakayotekelezwa kwa kutumia mkopo huo.

Miongoni mwa miradi ya kihistoria ni ujenzi wa madarasa ya sekondari 15,000 nchi nzima na madarasa ya shule za msingi 3,000.

Kwa sasa inakadiriwa kuwa nchi ina upungufu wa madarasa 11,000, lakini Rais Samia ameamua kuona mbali.

Ameamua kufuta mfumo wa zima moto, ambapo kila mwaka wazazi wanakabwa koo vijijini kuchangia ujenzi wa madarasa.

Baadhi ya wazazi pia wameanza minong’ono kuwa watoto wao wamepewa mikopo kidogo, yaani Sh 600,000 kama ada vyuoni.

Hawajui kuwa miaka yote imekuwa hivyo na wakati mwingine wengi wanakuwa hawapati kabisa hata senti tano ya mkopo.

Sitanii, naomba nizungumzie kwa ufupi miezi sita ya Rais Samia akiwa Rais wa Tanzania baada ya kuapishwa Machi 19, 2021.

Nakumbuka vema kilichotokea, maana baada ya kifo cha Rais John Magufuli kulitokea kama sintofahamu hivi.
Wapo watu walioamini Rais Samia angeendelea kuwa Kaimu Rais, baadhi walidhani tunakwenda kwenye uchaguzi mpya na wengine hawakufahamu nini kitatokea.

Asubuhi ya Machi 18, 2021 niliamkia studio za Televisheni ya Taifa (TBC1) na TBC Taifa (radio) kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba.

Hii ilikuwa ni baada ya kifo cha Rais John Magufuli, kilichotokea Machi 17, 2021. Ikumbukwe wiki moja kabla nilikuwa nimefanya mahojiano na kituo cha Star TV nikasema tuambiwe bayana Rais Magufuli yuko wapi na anafanya nini.

Machi 18 pamoja na kwamba nilikuwa bado Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo baadaye nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TEF Mei 22, 2021, ilinilazimu kutoa ufafanuzi huo uliokuwa tamko zito.

Sitanii, tamko nililolitoa lilizaa kuapishwa kwa Rais Samia kuwa Rais wa Awamu ya Sita Machi 19, 2021. Nilirejea Katiba ya Tanzania (1977) Ibara ya 37(5) inayosema: “Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.”

Kwa mara ya kwanza kupitia makala hii ninakisema kilichotokea baada ya tamko hilo. Walinipigia simu watu wengi wakiwa na hofu.

Baadhi hawakufahamu Katiba inasemaje. Walinishutumu wakidai nimetangaza utaratibu wa kwangu, kwani baada ya kifo cha Rais kinachofuata ni uchaguzi.

Hii ilinipa shida kuona hata baadhi ya wabunge hawakufahamu nini kinafuata baada ya kifo hicho. Machi 18, 2021 itabaki kuwa siku ya kihistoria kwangu, kwani ujumbe nilioutoa ulitangazwa katika radio zote za ndani na za kimataifa na siku moja baadaye Rais Samia akaapishwa.

Sitanii, leo ninazungumzia mzigo wa madeni ambao Rais Magufuli amelitwisha taifa letu. Nimetangulia kusema na ninarudia, mimi ni msema kweli. Wala sipepesi macho katika kusema ukweli.

Wakati Rais Magufuli kwa miaka mitano yote alikuwa anawaaminisha Watanzania kuwa nchi inajenga miundombinu na inanunua ndege kwa kutumia fedha zetu wenyewe, uhalisia ni kinyume chake.

Kwa kipindi cha miaka mitano tu, Rais Mafuguli amekopa fedha nyingi kuliko fedha zote alizokopa Rais Benjamin Mkapa kwa miaka 10 aliyokaa madarakani.

Kwa miaka mitano, amekopa pia fedha nyingi kuliko alizokopa Rais Jakaya Kikwete kwa miaka 10 naye aliyokaa madarakani.

Rais Mkapa alirithi madeni mengi mno. Alipambana nayo, akaiingiza nchi katika Mpango wa Kusamehe Madeni Nchi Maskini (HIPC) na hadi anatoka madarakani, Tanzania ilikuwa inadaiwa Sh trilioni 20 tu.

Rais Kikwete wakati wake deni la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 23, hivyo akatoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 43 kwa miaka 10. Rais Magufuli kwa miaka mitano tu, deni la taifa limeongezeka kwa Sh trilioni 29 na kufikia Sh trilioni 72 hadi anafariki dunia Machi, 2021.

Sitanii, kwa kasi hii ya ukopaji ina maana kama angekaa madarakani kwa miaka 10 kamili na akaendelea na kasi ya ukopaji wa wastani wa Sh trilioni 29 kwa miaka mitano, basi angetoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 101 kufikia mwaka 2025.

Kuna jambo baya halisemwi. Rais Magufuli amekopa mikopo ya kibiashara inayoanza kulipwa baada ya miaka mitatu na inapaswa kulipwa ndani ya miaka minane, ikiwa na riba za kati ya asilimia 6 na 8.

Baadhi ya mikopo hii imeiva tayari. Imeanza kukuza deni la taifa kwa kasi kutokana na riba. Deni la taifa sasa limefikia Sh trilioni 78.

Kwa vyovyote vile iwavyo, Rais Samia anapaswa kuchukua hatua za haraka, ikiwamo kuunda timu ya majadiliano na wakopeshaji kwa ajili ya kubadili masharti ya mikopo ya kibiashara aliyochukua Rais Magufuli.

Anapaswa kuomba msamaha wa riba na pengine kuomba kuongezewa muda wa kulipa deni kama ulivyo utaratibu wa mikopo kwa serikali nyingi duniani.

Mikopo mingi kwa serikali huwa inalipwa kati ya miaka 20 hadi 50 kulingana na ukubwa wa mkopo na hutozwa riba kati ya asilimia 0.3 hadi asilimia 1. Mikopo ya aina hii inapatikana katika Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo Duniani, Benki ya Maendeleo Afika na nyingine za aina hii.

Kwa bahati mbaya na kwa masikitiko makubwa, kwa miaka mitano Wazungu tuliowaita mabeberu, ila tukawa tunakopa fedha zao kupitia benki za biashara. Kwa hali halisi, madeni haya yakiiva yote, ikiwa hakuna majadiliano ya dharura kuomba marekebisho ya masharti ya mikopo tuliyochukua chini ya Rais Magufuli, itafika mahala asilimia 60 ya bajeti ya taifa letu itakuwa inakwenda kulipa madeni. Waliomo serikalini watajua la kufanya katika hili.

Sitanii, ninafahamu baadhi ya wasomaji watakuwa wanaanza kufuka moshi kwa kusema ukweli huu. Wanajiuliza taarifa hizi nimezipata wapi? Taarifa hizi si za siri. Ziko wazi kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Nimepitia taarifa za mapitio ya mwenendo wa uchumi tangu mwaka 2000 hadi 2021. Zipo mtandaoni na zinaonyesha deni lilivyokua hatua kwa hatua. Kwa nia ya kuweka uelewa unaofanana, ifuatayo ni hali ya deni la taifa tangu mwaka 2005 hadi 2021.

Oktoba 2005, deni la nje lilikuwa USD milioni 8,361.9 sawa na Sh 19,286,471,493,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 1,712,800,000,000. Jumla kuu ya deni wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani lilikuwa Sh 20,999,271,493,000 (Sh trilioni 20.9). Nimekokotoa hesabu hizi kwa kutumia viwango vya BoT vya kuuza dola ya Marekani ambavyo ni USD 1 kwa Sh 2,306.47.

Oktoba 2015, wakati Rais Kikwete anatoka madarakani deni la nje lilikuwa USD milioni 15,321.3, sawa na Sh 35,338,118,811,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 7,826,200,000,000. Jumla kuu deni la nje na deni la ndani lilikuwa ni Sh 43,164,318,811,000 (Sh trilioni 43.1).

Deni la taifa lilianza kupanda kwa kasi Oktoba 2016. Deni la nje lilipanda na kuwa USD milioni 16,407.6 sawa na Sh 37,843,637,172,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 10,089,000,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 47,932,637,172,000 (Sh trilioni 47.9).

Oktoba 2017 deni la nje lilipanda kwa kasi kubwa na kufikia USD milioni 19,074.4 sawa na Sh 43,994,531,368,000. Kutokana na makandarasi kutolipwa deni la ndani nalo lilikua na kufikia Sh 12,563,300,000,000. Jumla kuu ya deni kwa mwaka huo likawa Sh 56,557,831,368,000 (Sh trilioni 56.5).

Oktoba 2018, deni la nje lilizidi kupanda na kuwa USD milioni 20,759.1 sawa na Sh 47,880,241,377,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 14,116,100,000,000. Jumla kuu ikawa Sh 61,996,341,377,000 (Sh trilioni 61.9).

Oktoba 2019, mwanamume aliongeza tena deni la taifa, deni la nje likafikia USD milioni 22,569.4, sawa na Sh 52,055,644,018,000, huku deni la ndani likipanda na kufikia Sh 14,187,400,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 66,243,044,018,000 (Sh trilioni 66.2).

Oktoba 2020, deni la nje lilipanda na kufikia USD milioni 23,599.3, sawa na Sh 54,431,077,471,000, huku deni la ndani likifikia Sh 15,608,500,000,000. Jumla kuu ikafikia Sh 70,039,577,471,000 (Sh trilioni 70).

Machi, 2021 wakati Rais Magufuli anafariki dunia, deni la nje la Tanzania lilikuwa limefikia USD milioni 24,429.2, sawa na Sh 56,345,216,924,000. Deni la ndani nalo lilipanda na kufikia Sh 16,116,500,000,000. Jumla kuu, deni la taifa lilifikia 72,461,716,924,000 (Sh trilioni 72.4).

Kilichofuata baada ya hapo, madeni yameanza kuiva kwa ajili ya kulipwa, huku mengine yakizalisha riba ya kufa mtu.

Makandarasi wengi Tanzania wanadai mabilioni kati ya hizo Sh trilioni 16 ambazo ni deni la ndani hawajalipwa siku nyingi. Kutokana na hali hiyo, madeni haya yaliyokopwa bila mpangilio katika benki za biashara yameanza kuwa msalaba kwa Rais Samia.

Taarifa ya hali ya Uchumi ya BoT ya Septemba, 2021 inayorejea mwezi Agosti, 2021 kutokana na mazingira hayo, deni la nje limekua na kufikia USD milioni 25,956.1 sawa na Sh 59,866,965,967,000, huku deni la ndani nalo likikua na kufikia Sh 18,225,000,000,000. Ukuaji huu unafanya kiwango cha deni la taifa kufikia jumla kuu ya Sh 78,091,965,967,000 (trilioni 78).

Sitanii, deni hili likigawanywa kwa Watanzania milioni 60, bila kujali mkubwa na mdogo, kila Mtanzania anadaiwa Sh 1,301,533 (Sh milioni 1.3). Hata hivyo, wataalamu wa uchumi wanasema deni hili si tishio kwa uchumi wa taifa letu kwa sasa kwani liko katika uwiano wa asilimia 30 kwa uchumi wa taifa letu, wakati kuna mataifa Afrika ambayo tayari yana uwiano wa asilimia 54 ya deni kwa uchumi wa nchi zao, ila wanaionya serikali iepuke mikopo ya kibiashara ina riba kubwa, masharti mabaya na inalipwa kwa muda mfupi.

Pale Dodoma, tumeona Rais Samia ameanzisha utaratibu mpya wa ukweli na uwazi katika mikopo. Ameeleza fedha alizokopa zitafanya nini kwa kuorodhesha miradi itakayotekelezwa na akatueleza amezikopa kutoka wapi.

Ninajiuliza, hivi ilikuwa ni kwa faida ya nani Rais Magufuli na wapambe wake kuficha ukweli kuwa miradi ya reli, barabara, umeme, ujenzi wa hospitali na mingine mingi aliyoijenga alikuwa anakopa?

Hivi sisi kama tungejua anakopa, tungemzuia? Lakini si tungepata fursa ya kumshauri asichukue mikopo ya kibiashara inayoanza kututoa utumbo sasa? Mungu ibaariki Tanzania.

Copyright ©2021. Gazeti la Jamhuri
Naona Mheshimiwa Dkt Mipango ambaye alikuwa Waziri wa Fedha atupe jibu nini kimesababisha deni la taifa kuongezeka kwa kasi kwa kipindi cha miaka 5. Na muhimu kwa Watanzania wapate kujua hizi Fedha zilifanya kazi gani
 
Arrghh JPM alifanya bogus deals

nmeona post umeandika mama nae atanunua madege kwa style hiohio, vp kuna faida nyingine ambazo sisi raia hatuzijui ama
ni yaleyale ya kujikosha?
Hamna cha faida wala nini...

Na kama faida ipo haiwezi kuendana na uwekezaji unaofanyika hata kidogo....

Unajua hapo kabla hakuna hoja waliyokuwa wanapenda kuitumia kama eti ATCL itaongeza chachu ya utalii...

Niliuliza mara kadhaa hapa ni watalii kutoka pande zipi za dunia wanaoshindwa kutembelea Tanzania kwa sababu tu hatuna ndege... sijawahi kujibiwa hili swali!!

Kama ni kusafirisha watalii ndani ya nchi kutoka destination moja hadi nyingine, tayari tulishakuwa na FastJet na Precision Air; na kampuni zingine zinazomiliki ndege ndogo kama vile Coastal.

Matokeo yake, tukana bora kuwafanyia fitina FastJet ili ATCL waweze kufanya vizuri, matokeo yake hadi sasa hakuna jipya!! Kodi kutoka kwa FastJet tunakosa, huko ATCL kwenyewe ndo hivyo tena!!
 
PUNGUZA MBWEMBWE ZA KUJITIA UJUAJI WAKATI MWEUPE...

Wakati unajugamba kusoma Public Finance, nimesoma Uchumi, kwahiyo hayo mambo unayoyasikia juu juu, mwenzako ninayasomea

Narudia... Brady Bond ni matokeo ya 80's Financial Crisis na sio 70's!

Middlemen are everywhere in a modern business... hapa tunazungumzia CORRUPTION THROUGH MIDDLEMEN...

Kwenye Sakata la Radar.... Middleman alipiga za kutosha...

Kwenye mkopo wa Stanbic, Middle Man alipiga mabilion...

Kwenye sakata la Msumbimbi... Middle Men walipiga mabilioni!! Hicho ndicho kinazungumziwa!

Naona unahangaika kunielezea kuhusu Brady Bond ingawaje sio msingi wa mjadala huu!!! Narudia... suala la Brady Bond nimelisoma mara kadhaa! Sijaanza kulisoma jana wala juzi unlike wewe unaehangaika sasa kunipa historia inayofahamika nachumi yeyote yule!!

Hapa naachana rasmi na wewe....

Mara kadhaa nimekuambia huna ufahamu na haya mambo, ndo maana mara kadhaa unaongea vitu vya ajabu, nikikukosoa, unaenda ku-Google na kurudi na hoja nyingine! Matokeo yake, tunafanya kazi ya kuzunguka kuzunguka tu mle mle!!

Kama umesahau, hiki ndicho uliongea:-

Huna cha kuniambia "if you don't know" wakati ni mwenyewe ndje hujui!!

Unajisahaulisha kwamba juzi tu hapa ulisemama the main source ya fedha za IMF ni:-

NIkakupinga, halafu unarudi kujifanya kunielimisha kwa kitu ambacho nilikuwa nakifahamu na ni wewe mwenyewe ndie ulkuwa hufahamu!!

Halafu narudia... mambo mengine unatakiwa kutumia akili!!!

Hivi unaamini kabisa IMF wana uwezo wa ku-control mikopo kulinganisha na private banks wenyewe?

Yaani IMF hawa hawa ambao kila siku wanadindishiwa na Wakopaji ndo wawe na uwezo wa kusimamia mikopo ya wengine wakati hata ya kwao wenyewe maji yakizidi unga, wanaamua kusamehe!!!

We all know dunianiani kuna multilateral agreements zinazolinda hizi private institutions, na serikali nyingi zimewahi kupelekwa MiGA! Umeshawahi kusikia kuna nchi imefikishwa MIGA na IMF?
Nikikwambia ninafahamu ‘public finance’ with that reasoning I can do any ‘bullion search’ based my analysis of the case study (hapa ndipo personal intelligence inapotumika kwenye google research, you need to have the foundation first and understand the topic).

02A8FAF0-D44B-4502-BEEE-C4DB24AC1AC9.jpeg

Kwa upande wa serikali ya Mozambique kwa sababu wanaamini wahusika wa huo ufisadi raisi, AG, Benki Kuu na waziri wa fedha ndio walikuwa washiriki wa ufisadi (with their involvement DMO na anyother mechanism to prevent stress zilizimwa, kwa msaada wa Credit Suisse kutofuata procedures).

Serikali yao imefungua kesi ya kufuta baadhi ya hilo deni; kama uta google zaidi utakutana na taasisi za nchi yao zinazoelewa ‘public finance’ deni lote lifutwe kwa kutofuata IMF/WB fire walls; mfano (Mozambique watchdog urges Credit Suisse to fully cancel scam-linked debt)

Hiyo corrupt regime ndio iliyosaini hiyo mikataba ya ovyo na Credit Suisse; ndio hao hao waliotoa baraka za kuchimba gas yao; ndio aina ya viongozi watu kama na wewe Zitto mnawaona mfano wa kuigwa. Bila ya hata kusoma terms za mikataba yao.

Narudia tena wewe huna reasoning capacity ya mambo unayohamasisha zaidi ya kuwaingiza mbumbumbu mkenge na mikogo sijui ulikuwa mbeba mikoba wa beberu gani kwenye research zake.
 
Hizo hospital za kanda unazoengelea ulishawahi kuzitembelea au unaziona kwenye picha,
Majengo yake ni uchafu mtupu, je kuna huduma gani za maana katika majengo hayo?.

Mbona mbeya alishindwa kuifanya iwe kama Bugando,Kcmc na Muhimbili?.

Tumekulia maisha ya umaskini hivyo hudhani gorofa/jengo ndiyo kiwango cha huduma.

Jamaa vitu vyake vyote alivyovifanya uongo ulikuwa mwingi sana, wala hakuwa na uchungu na fedha ya nchi yetu bali aliangalia kuufurahisha moyo wake uliojaa maisha ya sifa.
We inaonekana umejaa chuki tu dhidi ya JPM, unataka kusema majengo ya hizo hospital hayana viwango kweli?!!!

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Nikikwambia ninafahamu ‘public finance’ with that reasoning I can do any ‘bullion search’ based my analysis of the case study (hapa ndipo personal intelligence inapotumika kwenye google research, you need to have the foundation first and understand the topic).

View attachment 1990330

Kwa upande wa serikali ya Mozambique kwa sababu wanaamini wahusika wa huo ufisadi raisi, AG, Benki Kuu na waziri wa fedha ndio walikuwa washiriki wa ufisadi (with their involvement DMO na anyother mechanism to prevent stress zilizimwa, kwa msaada wa Credit Suisse kutofuata procedures).

Serikali yao imefungua kesi ya kufuta baadhi ya hilo deni; kama uta google zaidi utakutana na taasisi za nchi yao zinazoelewa ‘public finance’ deni lote lifutwe kwa kutofuata IMF/WB fire walls; mfano (Mozambique watchdog urges Credit Suisse to fully cancel scam-linked debt)
WHAT'S YOUR EXACT POINT HERE...

Naona bado unazunguka zunguka mle mle tu...

We jamaa una matatizo gani?!! Huelewi, au hiyo lugha iliyoandika hizo taarifa unazo-Google inakupa taabu?

Hapa zimethibitishwa kashfa kubwa za corruption kati ya Credit Suisse na Msumbiji!

Watu tunaponda hii mikopo ya taasisi binafsi kama hawa Credit Suisse

JPM ndo kakopa kutoka kwa Credit Suisse ambao mara kwa mara wamekuwa wakikumbwa na tuhuma za ufisadi !!

Lakini ni wewe wewe ndie unatetea mikopo ya JPM kwa Credit Suisse..

Pamoja na hayo, jioni kabisa ndo unadai...
Hiyo corrupt regime ndio iliyosaini hiyo mikataba ya ovyo na Credit Suisse; ndio hao hao waliotoa baraka za kuchimba gas yao;
Wakati hilo nishasema since Day 1 kwamba...
Hata Msumbiji walikopeshwa USD 1 Billion na Credit Suisse wakati ambao taifa hilo lilipogundua gas ya kutosha!!!

With huge gas discovery in Tanzania, hakuna private bank inayoweza kuacha kuikopesha! And FYI, hizo benki binafsi zinaweza kuwa comfrtable zaidi kumkopesha Samia kuliko JPM ambae alikuwa branded kwamba hatabiriki!!
Na ulivyo poyoyo, bila aibu unasema:-
ndio aina ya viongozi watu kama na wewe Zitto mnawaona mfano wa kuigwa. Bila ya hata kusoma terms za mikataba yao.
Wewe si ndo unatetea hiyo mikopo kutoka Credit Suisse?! Sasa anayetetea na anayeponda, ni nani anawaona hao watu kama ni mfano wa kuigwa?!

We jamaa BURE KABISA
Narudia tena wewe huna reasoning capacity ya mambo unayohamasisha zaidi ya kuwaingiza mbumbumbu mkenge na mikogo sijui ulikuwa mbeba mikoba wa beberu gani kwenye research zake.
1. Unatetea mikopo kutoka Credit Suisse
2. Unafahamu kwamba mikopo ya Credit Suisse kwa Msumbiji imeambatana na grand corruption

In contrary, napinga mikopo ya Credit Suisse and other private banks kwa hoja kwamba hawa jamaa wanatumia sana corruption, na higher interest rate

Lakini pamoja na yote hayo, mimi ninayepinga mikopo ya Credit Suisse unaamini naziona hizo Corrupt Gangs ndo nmfano wa kuigwa...

Hivi najadiliana na mtu wa aina gani hapa?! Do you really have what it takes to argue these matters?

Halafu hadi hapo bado unajiona una reasoning yoyote?!

Halafu inaelekea HUJUI kwanini hiyo screenshot wamesema huo mkopo ulikuwa "...unconstitutional and illegal under Mozambique Law"

Kwa kukosa ufahamu unadhani serikali ilikuwa haifahamu...

Unashindwa hata kujiuliza ikiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara ya Fedha walikuwa wanafahamu, sasa ni serikali ipi iliyokuwa haifahamu!!

FYI, wamesema ni unconstitutional and illegal under Mozambique Laws kwa sababu Bunge halikujulishwa, lakini serikali walikuwa wanafahamu A-Z...

Na ndo maana jana nilikuambia hapa bank ya kibeberu haiwezi kutoa mkopo kwa taasisi ya serikali bila guarantee kutoka serikalini!!!

MR. REASONING... TRY HARDER TO REASON COZ' YOU DON'T SOUND LIKE A REASONING GUY!
 
WHAT'S YOUR EXACT POINT HERE...

Naona bado unazunguka zunguka mle mle tu...

We jamaa una matatizo gani?!! Huelewi, au hiyo lugha iliyoandika hizo taarifa unazo-Google inakupa taabu?

Hapa zimethibitishwa kashfa kubwa za corruption kati ya Credit Suisse na Msumbiji!

Watu tunaponda hii mikopo ya taasisi binafsi kama hawa Credit Suisse

JPM ndo kakopa kutoka kwa Credit Suisse ambao mara kwa mara wamekuwa wakikumbwa na tuhuma za ufisadi !!

Lakini ni wewe wewe ndie unatetea mikopo ya JPM kwa Credit Suisse..

Pamoja na hayo, jioni kabisa ndo unadai...

Wakati hilo nishasema since Day 1 kwamba...

Na ulivyo poyoyo, bila aibu unasema:-

Wewe si ndo unatetea hiyo mikopo kutoka Credit Suisse?! Sasa anayetetea na anayeponda, ni nani anawaona hao watu kama ni mfano wa kuigwa?!

We jamaa BURE KABISA

1. Unatetea mikopo kutoka Credit Suisse
2. Unafahamu kwamba mikopo ya Credit Suisse kwa Msumbiji imeambatana na grand corruption

In contrary, napinga mikopo ya Credit Suisse and other private banks kwa hoja kwamba hawa jamaa wanatumia sana corruption, na higher interest rate

Lakini pamoja na yote hayo, mimi ninayepinga mikopo ya Credit Suisse unaamini naziona hizo Corrupt Gangs ndo nmfano wa kuigwa...

Hivi najadiliana na mtu wa aina gani hapa?! Do you really have what it takes to argue these matters?

Halafu hadi hapo bado unajiona una reasoning yoyote?!
You are full of self grandiose.

Msingi wa mada ni Magufuli alikopa sana private.

Quote yangu ya kwanza uliyochukua ilikuwa inasema, hilo aliwezakani yaani Magufuli akope kwa kuficha; IMF na WB wakijua mziki wake utakuwa mwingine.

Nikatolea mfano wa sakata la Mozambique na kinachoendelea madhara ya kukopa bila IMF na WB kujua.

Ukaja kuleta nonsense zako za uhuru wa nchi kukopa without them (IMF na WB) na kuleta habari za ‘Paris Club’ which you have limited knowledge off at the same time introducing the concept of public debt in our arguments.

Sasa hivi unakuja kuniambia mjadala wetu unahudu uzuri sijui ubaya wa kukopa private banks; ndio nilichoandika icho kwenye post yangu uliyo quote hadi kufikia hapa?

Sio lazima niwe sawa all the time I get a lot of things wrong, but if you gonna challenge ppl at least bear the reasoning to do so.

Una unga unga tu nikisema nikuchimbe kuhusu Macaulay economic formula ya ku assess uwezo wa nchi kulipa deni ata kama hatuna data zote za nchi husika. Kuelewa tu naongelea nini kwako mziki mwingine bila ya ku google (kibaya zaidi nina economic formula nyingi za ku assess public finances) zinazotumiwa na international lenders mbele yangu based on public finance assessments.

Sio kila mtu anajua kila kitu ndio maana unioni kuwachokoza engineers wa JF najua mipaka yangu; ila ukiamua kuchallenge mtu (haya sio mashindano) hakuna kushindwa kuna kupata new knowledge but the. make sure you know your staff from the roots sio ku google na kuja na cheap points most of which are ignored trust me kwa sababu ilikuwa nikisoma tu naona limitations zako either za misinterpretation or finance reasoning.

Asubuhi njema.
 
Mzee wakati wa Mwendazake hiyo tovuti ya BoT si ilikuwepo, mbona hukuitumia na kuleta taarifa kama hizi? Nakumbuka kuna wakati gazeti lako lilisifiwa hadharani na JPM kwa kuibua uozo sijui bandarini ama wapi lakini hili ambalo unasema linatutoa utumbo hukulisema. Leo ndio umeliona, kweli ya Mungu mengi.
Tena mazito, yetu macho...!
 
Look at you

Hivi unadhani private banks wanajikopeshea tu nchi za Africa au ata wachina tukienda kukopa.

Hujui ata misingi ya ring fence walizopewa DMO na analysis frameworks such as:
Halafu hapa umejigamba wewe ni Mtalaamu wa Public Finance, kwahiyo utaalamu wako unakuongoza kwenye kufanya research...

Unaonaje basi, kutoka kwenye hiyo link yako, ukiifuata mwenyewe kisha u-copy kipengele kinachotoa muongozo kwa Private Banks kukopesha nchi maskini...

Halafu mbona nina mashaka kwamba inawezekana hata hujui tofauti kati ya World Bank na IMF? Anyway, tuache hilo la kujua tofauti.... weka hiyo part inayotoa mwongozo!!
Kukusaidia tu personal nina ‘public finance’ module nzima mbele yangu endorsed by all international donors stakeholder IMF, WD and the rest na nishaisoma yote kitambo.
Still you've proved you've little understanding...

Halafu, mona mara kwa mara huwa unaandika "WD" badala ya "WB".... is it a mere mistake au nichukulie kwamba ni sababu tosha kabisa ya kwanini mara kwa mara umekuwa ukiongea vitu irrelevant!

To mention few, there's here...
Sasa kumaliza matatizo ya defaults za mikopo kipindi hiko yaani (kuanzia late 70-80’s) kwa kuelewa private banks ndio mzozo wa tatizo because they were unregulated and the cause of high debt. IMF na WD walishauri mikopo
And here
Kama nilivyokwambia awali ata private banks can source loans outside just IMF/WD as middlemen.
And many more..
Not only does it contain the history of policy evolution bali ata complicated various ecomoic formulas and variants to use in computation; all of which I know. Thiugh the chances of evolving to such discussion were small with your understanding on the subject matter, ila tungefika huko utakutana na mziki mwingine kabisa sidhani kama midundo yake unaweza cheza.
YOTE HAYO, wala sina haja nayo manake HAIWEZEKANI kila wakati uwe unatoka nje ya mstari...

Link ni yako mwenyewe...

Mimi nakuomba jambo moja TU kutoka kwenye hiyo link... onesha sehemu walipo-outline masharti kwa Private Banks wanapotaka kukopesha kwa nchi maskini. Hapo ndipo nimekuwa nikikueleza mara kwa mara!!

Hayo mambo ya polisi hujui chochote!! Unajigamba kwamba umesoma Public Finance lakini hayo mambo ni ya kiuchumi, na sio finance!!

Mtu yeyote aliyesoma uchumi at college level, keshayasoma sana hayo ma-policy darasani!! Wewe kama umeyasoma, basi umeyagusa gusa tu kama tulivyogusa gusa wengine kwenye finance wakati core study ni economy!

So, STOP hizi mbwembwe zako za kwamba sijui umesoma Public Finance, and all that crap!
So given any case study and the standard reasoning related to public finance norms I know what to google to get the right articles to answer any query of yours and dig even deeper to challenge you are understanding on the same issue.
Sasa mbona kila wakati unakuja na irrelevant materials?! Au umesoma Public Finance kupitia Mature Age Entry?!
On this Creddit Suisse saga (ndio maana nikakwambia unahitaji foundation of the discipline to argue).
Mengi uliyosema kuhusu Credit Suisse umedanganya, na nimekuonesha ni wapi ulidanganya; na ndo maana baada ya kukuonesha uongo wako, ndo ukaanza kuleta habari za FCA wakati wewe ulidai ni IMF ndio waliwatia adabu Credit Suisse!
Kwa sababu hujui ata tofauti ya varying government debts na shughuli za DMO kwa tafsiri za IMF and why wahusika wa huo ufisadi Mozambique officials thought it was import to bypass the international set firewall.
Pamoja na kujua kwako, umeshindwa kabisa kuonesha ni namna gani unajua!!
Like I told you public finance reasoning is based on social science and it is influenced by historical events leading to formulation of IMF/WB policies on risk assesments which every nation has to adhere too.
Wacah wewe...

Unataka kuleta nondo kuhusu formulationm of IMF/WB policies on risk assessment tena? Samahani bhana, tusifike mbali kote huko manake ikiwa mambo madogo tu umeshindwa kuyatolea ufafanunuzi, ukifika hadi huko si itakuwa balaa?

WAIT... nimekosea!! Kwenye hizo nondo za police formulation, mi niwekee kipengele ya muongozo wa private banks tu; ITANITOSHA!!
In addition to that kuelewa sababu za fines walizopewa hao watu nje ya box you need to have studied accountancy (aspects of auditing) na sheria zake kwa nchi husika ndio zilizotumika kuwaadhibu.
Fine ambazo hata wewe mwenyewe ulikuwa hujui zimetokana na nini!!!

Man, acha porojo!! Duniani kote, especially with the influence of the United State, kulitungwa sheria za kudhibiti Financial Crimes!!

Target ya kwanza kwa US, ilikuwa prevention of money laundering baada ya kuonekana mabenki mengi yanatumika kupitishia pesa za kufadhili ugaidi.

In addition to that, illegal businesses like arms and drug trafficking, zilikuwa zinatumia benki across the global kutakatisha pesa chafu!!!

Hapo ndipo kukapitishwa tight financial crimes acts across the global!

Kwa wafuatiliaji wa mambo, watakumbuka hiyo act Tanzania ilileta sokomoko kweli kweli bungeni, kwa sababu Wabunge Waislamu waliona sheria ni kama wanawalenga Waislamu!

Kwahiyo acha porojo zako wewe... hakuna cha kusoma accountancy hapo!!

We jamaa una viroja sana!!
As far as national debt is concerned it is not a good idea to hide it from IMF and WB kwa sababu likija hadharani kuna consequences zake ata nchi za ulaya; just ask Greece bila EU na Angela Merkel mziki wao ungekuwa mwingine.
Sasa hilo linahusiana nini?!

Au umeamua kubadilika?! Au unajisahaulisha ulidai kosa lililotokea Msumbiji ni kwa Credit Suisse kutopata approval ya IMF?! Au unamaanisha ni hao Credit Suisse ndio walitakiwa kuwaeleza IMF kuhusu deni la Msumbiji?
Eti $200 million kwa mujibu wako ilifutwa kupunguzwa interest ya deni; hivi interest inafutwa kwa kupunguza amount of loan au interest rate set; sasa huko sina files isipokuwa finance ni uwanja wangu nilikuacha kwa sababu ningesema nijibu kila upuuzi wako tungekesha.

Kilatha 👋 done with this thread.
Angalia

Wapi nimesema ilifutwa kupunguzwa interest ya deni? Hiki ndicho nilisema kuhusu 200M:-
Kwanza hiyo 200M sio kwamba walilazimishwa...

Narudia... chanzo cha sakata hili sio IMF kama unavyojaribu kuaminisha watu bali financial regulators wa US, UK na Uswisi. Baada ya wao kufanya uchunguzi, ndipo wakagundua violation of money laundering control na massive corruption!

Hiyo 200M uliyoitaja bila kufahamu undani wake, inahusishwa na settlement ya corruption kwa sababu, uchunguzi ulithibitisha maofisa wa benki kuweka kibindoni zaidi ya USD 50 Million na Wafanyakazi wa Serikali ya Msumbiji na wenyewe waliweka kibindoni zaidi ya USD 130M!
Hicho nilichosema kinafana na hizo porojo zako?

Hubu nijuze jambo moja...

Kama una Genetic Understanding Problem, please let me know kuliko kupotezeana muda!
 
Halafu hapa umejigamba wewe ni Mtalaamu wa Public Finance, kwahiyo utaalamu wako unakuongoza kwenye kufanya research...

Unaonaje basi, kutoka kwenye hiyo link yako, ukiifuata mwenyewe kisha u-copy kipengele kinachotoa muongozo kwa Private Banks kukopesha nchi maskini...

Halafu mbona nina mashaka kwamba inawezekana hata hujui tofauti kati ya World Bank na IMF? Anyway, tuache hilo la kujua tofauti.... weka hiyo part inayotoa mwongozo!!

Still you've proved you've little understanding...

Halafu, mona mara kwa mara huwa unaandika "WD" badala ya "WB".... is it a mere mistake au nichukulie kwamba ni sababu tosha kabisa ya kwanini mara kwa mara umekuwa ukiongea vitu irrelevant!

To mention few, there's here...

And here

And many more..

YOTE HAYO, wala sina haja nayo manake HAIWEZEKANI kila wakati uwe unatoka nje ya mstari...

Link ni yako mwenyewe...

Mimi nakuomba jambo moja TU kutoka kwenye hiyo link... onesha sehemu walipo-outline masharti kwa Private Banks wanapotaka kukopesha kwa nchi maskini. Hapo ndipo nimekuwa nikikueleza mara kwa mara!!

Hayo mambo ya polisi hujui chochote!! Unajigamba kwamba umesoma Public Finance lakini hayo mambo ni ya kiuchumi, na sio finance!!

Mtu yeyote aliyesoma uchumi at college level, keshayasoma sana hayo ma-policy darasani!! Wewe kama umeyasoma, basi umeyagusa gusa tu kama tulivyogusa gusa wengine kwenye finance wakati core study ni economy!

So, STOP hizi mbwembwe zako za kwamba sijui umesoma Public Finance, and all that crap!

Sasa mbona kila wakati unakuja na irrelevant materials?! Au umesoma Public Finance kupitia Mature Age Entry?!

Mengi uliyosema kuhusu Credit Suisse umedanganya, na nimekuonesha ni wapi ulidanganya; na ndo maana baada ya kukuonesha uongo wako, ndo ukaanza kuleta habari za FCA wakati wewe ulidai ni IMF ndio waliwatia adabu Credit Suisse!

Pamoja na kujua kwako, umeshindwa kabisa kuonesha ni namna gani unajua!!

Wacah wewe...

Unataka kuleta nondo kuhusu formulationm of IMF/WB policies on risk assessment tena? Samahani bhana, tusifike mbali kote huko manake ikiwa mambo madogo tu umeshindwa kuyatolea ufafanunuzi, ukifika hadi huko si itakuwa balaa?

WAIT... nimekosea!! Kwenye hizo nondo za police formulation, mi niwekee kipengele ya muongozo wa private banks tu; ITANITOSHA!!

Fine ambazo hata wewe mwenyewe ulikuwa hujui zimetokana na nini!!!

Man, acha porojo!! Duniani kote, especially with the influence of the United State, kulitungwa sheria za kudhibiti Financial Crimes!!

Target ya kwanza kwa US, ilikuwa prevention of money laundering baada ya kuonekana mabenki mengi yanatumika kupitishia pesa za kufadhili ugaidi.

In addition to that, illegal businesses like arms and drug trafficking, zilikuwa zinatumia benki across the global kutakatisha pesa chafu!!!

Hapo ndipo kukapitishwa tight financial crimes acts across the global!

Kwa wafuatiliaji wa mambo, watakumbuka hiyo act Tanzania ilileta sokomoko kweli kweli bungeni, kwa sababu Wabunge Waislamu waliona sheria ni kama wanawalenga Waislamu!

Kwahiyo acha porojo zako wewe... hakuna cha kusoma accountancy hapo!!

We jamaa una viroja sana!!

Sasa hilo linahusiana nini?!

Au umeamua kubadilika?! Au unajisahaulisha ulidai kosa lililotokea Msumbiji ni kwa Credit Suisse kutopata approval ya IMF?! Au unamaanisha ni hao Credit Suisse ndio walitakiwa kuwaeleza IMF kuhusu deni la Msumbiji?

Angalia

Wapi nimesema ilifutwa kupunguzwa interest ya deni? Hiki ndicho nilisema kuhusu 200M:-

Hicho nilichosema kinafana na hizo porojo zako?

a nijuze jambo moja...

Kama una Genetic Understanding Problem, please let me know kuliko kupotezeana muda!
Mambo ya Public Finance uwezi debate acha

Kidali

Ni kwa mamlaka gani FCA wameweza toa adhabu zao na sheria zipi wametumia kutoa hizo in respect of their articles.

Similarly US wametumia sheria zipi kutoa maamuzi yao?
 
You are full of self grandiose.

Msingi wa mada ni Magufuli alikopa sana private.
NDIYO... kumbe ulitaka sote tujitoe ufahamu kama wewe kutetea mikopo ya private banks!
Quote yangu ya kwanza uliyochukua ilikuwa inasema, hilo aliwezakani yaani Magufuli akope kwa kuficha; IMF na WB wakijua mziki wake utakuwa mwingine.
Kuna mahala popote nilipozungumzia JPM kuwaficha IMF?!

Btw, hivi hoja ilikuwa serikali kuificha IMF, au kwamba private banks haziwezi kukopesa nchi maskini bila approval ya IMF?! Kama unataka kujisahaulisha, wewe huyu hapa chini:-
Hivi unadhani mabeberu ata kwa kupitia private banks yanakopesha nchi maskini bila ya IMF na WB kufanya stress test kama unaweza kulipa madeni yako huko mbele based on your tax collections.
Kwamba, eti private banks haziwezi kukopesha bila IMF!
Nikatolea mfano wa sakata la Mozambique na kinachoendelea madhara ya kukopa bila IMF na WB kujua.
Ulichosema sio madhara ya KUKOPA bila approval ya IMF bali KUKOPESHA bila approval! Na kama hilo nalo unataka kujisahaulisha, post yako hii hapa:-
Embu fuatilia sakata la ‘Credit Suisse’ linaloendelea wamelimwa fine ya $475 million na kulazimishwa kufuta deni $200 million walilokopesha taasisi ya serikali msumbiji; yote kwa sababu huo mkopo ulitolewa kwa siri bila ya kuwaambia IMF na WD.
Kwahiyo acha porojo zako
Ukaja kuleta nonsense zako za uhuru wa nchi kukopa without them (IMF na WB) na kuleta habari za ‘Paris Club’ which you have limited knowledge off at the same time introducing the concept of public debt in our arguments.
Kuna nonsense kama hiyo ya kukataa ulichoandika mwenyewe?!

Kuna nonsense kama hiyo upande mmoja unadai kosa ni private bank kukopesha bila approval ya IMF, na upande mwingine unadai serikali haiwezi kukopa bila approval ya IMF...

Hivi kuna nonsense kama hiyo?! Oh! Lemme guess... maybe you know that's more than being nonsense!
Sasa hivi unakuja kuniambia mjadala wetu unahudu uzuri sijui ubaya wa kukopa private banks; ndio nilichoandika icho kwenye post yangu uliyo quote hadi kufikia hapa?
IKiwa hata hapo juu nimekuonesha jinsi gani unavyobadilika badilika, hivi unajua kweli huu mjadala unahusu nini?!
Sio lazima niwe sawa all the time I get a lot of things wrong, but if you gonna challenge ppl at least bear the reasoning to do so.
You been WRONG MANY TIMES... swallow it!

Au unataka nianze kukuorodheshea uongo ambao umeusema hapa?
Una unga unga tu nikisema nikuchimbe kuhusu Macaulay economic formula ya ku assess uwezo wa nchi kulipa deni ata kama hatuna data zote za nchi husika. Kuelewa tu naongelea nini kwako mziki mwingine bila ya ku google (kibaya zaidi nina economic formula nyingi za ku assess public finances) zinazotumiwa na international lenders mbele yangu based on public finance assessments.
We jamaa una viroja sana...

Ulichoandika ni hiki hapa:-
Not only does it contain the history of policy evolution bali ata complicated various ecomoic formulas and variants to use in computation; all of which I know. Thiugh the chances of evolving to such discussion were small with your understanding on the subject matter, ila tungefika huko utakutana na mziki mwingine kabisa sidhani kama midundo yake unaweza cheza.
Kwahiyo kuandika hivyo kumbe ulilenga kuonesha unajua ma-formula?! What's so special kutoka kwenye hicho ulichoandika?!

Narudia, pamoja na mara kwa mara kujigamba sijui umesoma hiki, mara mtalaamu wa kile lakini maelezo yako yanaonesha upo mweupe mno!!
Sio kila mtu anajua kila kitu ndio maana unioni kuwachokoza engineers wa JF
Of course lakini tatizo ni kwamba, hata unachojigamba kukijua, bado HUKIJUI... yaani unaruka ruka tu!
 
Public Finance juu ya uwezo ku debat, sasa basi

Kidali

Ni kwa mamlaka gani FCA wameweza toa adhabu zao na sheria zipi wametumia kutoa hizo in respect of their articles.

Similarly US wametumia sheria zipi kutoa maamuzi yao?
Acha kuruka ruka... jibu kwanza hii hoja:-
Mimi nakuomba jambo moja TU kutoka kwenye hiyo link... onesha sehemu walipo-outline masharti kwa Private Banks wanapotaka kukopesha kwa nchi maskini. Hapo ndipo nimekuwa nikikueleza mara kwa mara!!
 
Basically I can’t type right knows either page inakuwa changed au cursor inaruka; mod mkundu ushaanza kumuwasha kwa debate isiyomuhusu ananilletea fujo.

Angalia hiyo (ya) chini ya kidali sijui imefikaje hapo.

Hawa watu awajazoea mijadala ya moto

Good morning
Acha kuruka ruka wewe

Nilichokutaka ufanye ni hiki hapa chini:-
Mimi nakuomba jambo moja TU kutoka kwenye hiyo link... onesha sehemu walipo-outline masharti kwa Private Banks wanapotaka kukopesha kwa nchi maskini. Hapo ndipo nimekuwa nikikueleza mara kwa mara!!
You don't need to type anything... just COPY and PASTE, and that's it!!!
 
Taja mradi wowote uliokamilika unaozidi 2t ukiachia ndege za cash zisizo na tija. Au unadhani bado watu ni wajinga?
Basi tusaidiane hizo hela alizokuwa anakopa alikuwa anazificha wapi. Tuchunguze account zake
 
Shujaa huwa halilii bunduki! Kama aliogopa basi aendelee kuogopa badala ya kuleta unafiki
Ndugu yangu Kimbunga, mbona unakuwa soo NAIVE, 98% ya wanasiasa ni wanafiki, uhai wao umo kwenye unafiki na uongo. Tukitaka wasiwe wanafiki basi sisi ndio tunakuwa wanafiki. Unafiki ndio kula yao.
 
Magufuli katutenda deni la taifa, trilioni 78 Samia msalabani

Jamhuri October 26, 2021

Na Deodatus Balile

Kazi hii ya uandishi wa habari moja ya majukumu yake ni kuanika ukweli minong’ono inapotawala katika jamii.

Kwa sasa kuna minong’ono mingi. Minong’ono imeanza baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza hadharani mkopo wa Sh trilioni 1.3, alioukopa kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na akatangaza miradi lukuki itakayotekelezwa kwa kutumia mkopo huo.

Miongoni mwa miradi ya kihistoria ni ujenzi wa madarasa ya sekondari 15,000 nchi nzima na madarasa ya shule za msingi 3,000.

Kwa sasa inakadiriwa kuwa nchi ina upungufu wa madarasa 11,000, lakini Rais Samia ameamua kuona mbali.

Ameamua kufuta mfumo wa zima moto, ambapo kila mwaka wazazi wanakabwa koo vijijini kuchangia ujenzi wa madarasa.

Baadhi ya wazazi pia wameanza minong’ono kuwa watoto wao wamepewa mikopo kidogo, yaani Sh 600,000 kama ada vyuoni.

Hawajui kuwa miaka yote imekuwa hivyo na wakati mwingine wengi wanakuwa hawapati kabisa hata senti tano ya mkopo.

Sitanii, naomba nizungumzie kwa ufupi miezi sita ya Rais Samia akiwa Rais wa Tanzania baada ya kuapishwa Machi 19, 2021.

Nakumbuka vema kilichotokea, maana baada ya kifo cha Rais John Magufuli kulitokea kama sintofahamu hivi.
Wapo watu walioamini Rais Samia angeendelea kuwa Kaimu Rais, baadhi walidhani tunakwenda kwenye uchaguzi mpya na wengine hawakufahamu nini kitatokea.

Asubuhi ya Machi 18, 2021 niliamkia studio za Televisheni ya Taifa (TBC1) na TBC Taifa (radio) kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba.

Hii ilikuwa ni baada ya kifo cha Rais John Magufuli, kilichotokea Machi 17, 2021. Ikumbukwe wiki moja kabla nilikuwa nimefanya mahojiano na kituo cha Star TV nikasema tuambiwe bayana Rais Magufuli yuko wapi na anafanya nini.

Machi 18 pamoja na kwamba nilikuwa bado Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo baadaye nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TEF Mei 22, 2021, ilinilazimu kutoa ufafanuzi huo uliokuwa tamko zito.

Sitanii, tamko nililolitoa lilizaa kuapishwa kwa Rais Samia kuwa Rais wa Awamu ya Sita Machi 19, 2021. Nilirejea Katiba ya Tanzania (1977) Ibara ya 37(5) inayosema: “Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.”

Kwa mara ya kwanza kupitia makala hii ninakisema kilichotokea baada ya tamko hilo. Walinipigia simu watu wengi wakiwa na hofu.

Baadhi hawakufahamu Katiba inasemaje. Walinishutumu wakidai nimetangaza utaratibu wa kwangu, kwani baada ya kifo cha Rais kinachofuata ni uchaguzi.

Hii ilinipa shida kuona hata baadhi ya wabunge hawakufahamu nini kinafuata baada ya kifo hicho. Machi 18, 2021 itabaki kuwa siku ya kihistoria kwangu, kwani ujumbe nilioutoa ulitangazwa katika radio zote za ndani na za kimataifa na siku moja baadaye Rais Samia akaapishwa.

Sitanii, leo ninazungumzia mzigo wa madeni ambao Rais Magufuli amelitwisha taifa letu. Nimetangulia kusema na ninarudia, mimi ni msema kweli. Wala sipepesi macho katika kusema ukweli.

Wakati Rais Magufuli kwa miaka mitano yote alikuwa anawaaminisha Watanzania kuwa nchi inajenga miundombinu na inanunua ndege kwa kutumia fedha zetu wenyewe, uhalisia ni kinyume chake.

Kwa kipindi cha miaka mitano tu, Rais Mafuguli amekopa fedha nyingi kuliko fedha zote alizokopa Rais Benjamin Mkapa kwa miaka 10 aliyokaa madarakani.

Kwa miaka mitano, amekopa pia fedha nyingi kuliko alizokopa Rais Jakaya Kikwete kwa miaka 10 naye aliyokaa madarakani.

Rais Mkapa alirithi madeni mengi mno. Alipambana nayo, akaiingiza nchi katika Mpango wa Kusamehe Madeni Nchi Maskini (HIPC) na hadi anatoka madarakani, Tanzania ilikuwa inadaiwa Sh trilioni 20 tu.

Rais Kikwete wakati wake deni la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 23, hivyo akatoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 43 kwa miaka 10. Rais Magufuli kwa miaka mitano tu, deni la taifa limeongezeka kwa Sh trilioni 29 na kufikia Sh trilioni 72 hadi anafariki dunia Machi, 2021.

Sitanii, kwa kasi hii ya ukopaji ina maana kama angekaa madarakani kwa miaka 10 kamili na akaendelea na kasi ya ukopaji wa wastani wa Sh trilioni 29 kwa miaka mitano, basi angetoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 101 kufikia mwaka 2025.

Kuna jambo baya halisemwi. Rais Magufuli amekopa mikopo ya kibiashara inayoanza kulipwa baada ya miaka mitatu na inapaswa kulipwa ndani ya miaka minane, ikiwa na riba za kati ya asilimia 6 na 8.

Baadhi ya mikopo hii imeiva tayari. Imeanza kukuza deni la taifa kwa kasi kutokana na riba. Deni la taifa sasa limefikia Sh trilioni 78.

Kwa vyovyote vile iwavyo, Rais Samia anapaswa kuchukua hatua za haraka, ikiwamo kuunda timu ya majadiliano na wakopeshaji kwa ajili ya kubadili masharti ya mikopo ya kibiashara aliyochukua Rais Magufuli.

Anapaswa kuomba msamaha wa riba na pengine kuomba kuongezewa muda wa kulipa deni kama ulivyo utaratibu wa mikopo kwa serikali nyingi duniani.

Mikopo mingi kwa serikali huwa inalipwa kati ya miaka 20 hadi 50 kulingana na ukubwa wa mkopo na hutozwa riba kati ya asilimia 0.3 hadi asilimia 1. Mikopo ya aina hii inapatikana katika Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo Duniani, Benki ya Maendeleo Afika na nyingine za aina hii.

Kwa bahati mbaya na kwa masikitiko makubwa, kwa miaka mitano Wazungu tuliowaita mabeberu, ila tukawa tunakopa fedha zao kupitia benki za biashara. Kwa hali halisi, madeni haya yakiiva yote, ikiwa hakuna majadiliano ya dharura kuomba marekebisho ya masharti ya mikopo tuliyochukua chini ya Rais Magufuli, itafika mahala asilimia 60 ya bajeti ya taifa letu itakuwa inakwenda kulipa madeni. Waliomo serikalini watajua la kufanya katika hili.

Sitanii, ninafahamu baadhi ya wasomaji watakuwa wanaanza kufuka moshi kwa kusema ukweli huu. Wanajiuliza taarifa hizi nimezipata wapi? Taarifa hizi si za siri. Ziko wazi kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Nimepitia taarifa za mapitio ya mwenendo wa uchumi tangu mwaka 2000 hadi 2021. Zipo mtandaoni na zinaonyesha deni lilivyokua hatua kwa hatua. Kwa nia ya kuweka uelewa unaofanana, ifuatayo ni hali ya deni la taifa tangu mwaka 2005 hadi 2021.

Oktoba 2005, deni la nje lilikuwa USD milioni 8,361.9 sawa na Sh 19,286,471,493,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 1,712,800,000,000. Jumla kuu ya deni wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani lilikuwa Sh 20,999,271,493,000 (Sh trilioni 20.9). Nimekokotoa hesabu hizi kwa kutumia viwango vya BoT vya kuuza dola ya Marekani ambavyo ni USD 1 kwa Sh 2,306.47.

Oktoba 2015, wakati Rais Kikwete anatoka madarakani deni la nje lilikuwa USD milioni 15,321.3, sawa na Sh 35,338,118,811,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 7,826,200,000,000. Jumla kuu deni la nje na deni la ndani lilikuwa ni Sh 43,164,318,811,000 (Sh trilioni 43.1).

Deni la taifa lilianza kupanda kwa kasi Oktoba 2016. Deni la nje lilipanda na kuwa USD milioni 16,407.6 sawa na Sh 37,843,637,172,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 10,089,000,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 47,932,637,172,000 (Sh trilioni 47.9).

Oktoba 2017 deni la nje lilipanda kwa kasi kubwa na kufikia USD milioni 19,074.4 sawa na Sh 43,994,531,368,000. Kutokana na makandarasi kutolipwa deni la ndani nalo lilikua na kufikia Sh 12,563,300,000,000. Jumla kuu ya deni kwa mwaka huo likawa Sh 56,557,831,368,000 (Sh trilioni 56.5).

Oktoba 2018, deni la nje lilizidi kupanda na kuwa USD milioni 20,759.1 sawa na Sh 47,880,241,377,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 14,116,100,000,000. Jumla kuu ikawa Sh 61,996,341,377,000 (Sh trilioni 61.9).

Oktoba 2019, mwanamume aliongeza tena deni la taifa, deni la nje likafikia USD milioni 22,569.4, sawa na Sh 52,055,644,018,000, huku deni la ndani likipanda na kufikia Sh 14,187,400,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 66,243,044,018,000 (Sh trilioni 66.2).

Oktoba 2020, deni la nje lilipanda na kufikia USD milioni 23,599.3, sawa na Sh 54,431,077,471,000, huku deni la ndani likifikia Sh 15,608,500,000,000. Jumla kuu ikafikia Sh 70,039,577,471,000 (Sh trilioni 70).

Machi, 2021 wakati Rais Magufuli anafariki dunia, deni la nje la Tanzania lilikuwa limefikia USD milioni 24,429.2, sawa na Sh 56,345,216,924,000. Deni la ndani nalo lilipanda na kufikia Sh 16,116,500,000,000. Jumla kuu, deni la taifa lilifikia 72,461,716,924,000 (Sh trilioni 72.4).

Kilichofuata baada ya hapo, madeni yameanza kuiva kwa ajili ya kulipwa, huku mengine yakizalisha riba ya kufa mtu.

Makandarasi wengi Tanzania wanadai mabilioni kati ya hizo Sh trilioni 16 ambazo ni deni la ndani hawajalipwa siku nyingi. Kutokana na hali hiyo, madeni haya yaliyokopwa bila mpangilio katika benki za biashara yameanza kuwa msalaba kwa Rais Samia.

Taarifa ya hali ya Uchumi ya BoT ya Septemba, 2021 inayorejea mwezi Agosti, 2021 kutokana na mazingira hayo, deni la nje limekua na kufikia USD milioni 25,956.1 sawa na Sh 59,866,965,967,000, huku deni la ndani nalo likikua na kufikia Sh 18,225,000,000,000. Ukuaji huu unafanya kiwango cha deni la taifa kufikia jumla kuu ya Sh 78,091,965,967,000 (trilioni 78).

Sitanii, deni hili likigawanywa kwa Watanzania milioni 60, bila kujali mkubwa na mdogo, kila Mtanzania anadaiwa Sh 1,301,533 (Sh milioni 1.3). Hata hivyo, wataalamu wa uchumi wanasema deni hili si tishio kwa uchumi wa taifa letu kwa sasa kwani liko katika uwiano wa asilimia 30 kwa uchumi wa taifa letu, wakati kuna mataifa Afrika ambayo tayari yana uwiano wa asilimia 54 ya deni kwa uchumi wa nchi zao, ila wanaionya serikali iepuke mikopo ya kibiashara ina riba kubwa, masharti mabaya na inalipwa kwa muda mfupi.

Pale Dodoma, tumeona Rais Samia ameanzisha utaratibu mpya wa ukweli na uwazi katika mikopo. Ameeleza fedha alizokopa zitafanya nini kwa kuorodhesha miradi itakayotekelezwa na akatueleza amezikopa kutoka wapi.

Ninajiuliza, hivi ilikuwa ni kwa faida ya nani Rais Magufuli na wapambe wake kuficha ukweli kuwa miradi ya reli, barabara, umeme, ujenzi wa hospitali na mingine mingi aliyoijenga alikuwa anakopa?

Hivi sisi kama tungejua anakopa, tungemzuia? Lakini si tungepata fursa ya kumshauri asichukue mikopo ya kibiashara inayoanza kututoa utumbo sasa? Mungu ibariki Tanzania.

Copyright ©2021. Gazeti la Jamhuri
Balile ni elimu duni! Ana uwezo duni wa uchambuzi wa mambo lakini anaamini anajua sana.
Tangu alipoandika ripoti ya Makonda kwa kutumwa na Nape, nikaona ni kichwa kibovu. He works like any Kapo!
 
Back
Top Bottom