Balile: Magufuli katutenda, deni la nje lafikia shilingi Trillion 78

Mzee wakati wa Mwendazake hiyo tovuti ya BoT si ilikuwepo, mbona hukuitumia na kuleta taarifa kama hizi? Nakumbuka kuna wakati gazeti lako lilisifiwa hadharani na JPM kwa kuibua uozo sijui bandarini ama wapi lakini hili ambalo unasema linatutoa utumbo hukulisema. Leo ndio umeliona, kweli ya Mungu mengi.
Balile ni Yuda Iskariote
Mkuu 50% ya project ni kubwa! Sema unachuki na JPM ndo maana hauoni alichofanya JPM hakujipendekeza kwao walikuja wenyewe baada ya kuona mziki wake! Angalia project kama zifuatazo
•Tanzania haikuwahi kuw ana Radar tokea uhuru amejenga nne kwa mkupuo Dar,mwanza,mbeya na klimanjaro
•Tanzania haikuwahi kuwa na Mahakama zakisasa tokea uhuru mahakama standard zilikuwa ni zile za kanda! Leo tunazungumzia mahaka zenye miundombinu ya kisasa!
•Nchi hii ilikuwa na hospital kubwa za kanda nyinhi za mashirika ya dini leo hii tuna hospital kubwa za hadhi ya kitaifa kule Musoma, mtwara,mbeya n.k Wao waliopita hawakufanya haya si kwa kuwa hawakuweza tu bali hata utendaji wao haukuwa katika viwango vya JPM!
•Vituo vya afya,hospital za wilaya, masoko.
•Uanzishwaji wa masoko ya madini mfano soko la dhahabu Geita limeinbiza takribani trilion tatu kwa miaka miwili na nusu!
•Upanuzi wa bandari hapo Dar, mtwara ma tanga!
•Ufufuami wa treni kutokea Dar mpaka moshi/arusha!
•Ujenzi wa flyover,busisi,mto wami n.k

Hayo ni ambo yanahitami usimamizi na fedha kwa hiyo kama matokeo yanaonekana kukopa kwake hakuna shida! Hata nyumbani kwako ukikopa benki ili ujenge nyumba na ukajenga kwa ubora na ikaonekana hakuna mtu atakaye kulaum! Ila kwa vile mmezoea maneno sio utendaji endeleeni kumsifia huyu mama ambaye hana hata historia ya utendaji kwenye maisha yake, kitu pekee kimemfikisha hapo ni kubebwa na siasa!
Zuzu wewe.
 
Kwa hiyo waandishi wote walikaa kimya? Kusema kwamba tumekopa iwe shida? Mbona BoT walikuwa wakiweka kwenye website yao, mbona wap hawakupata shida? Unafiki tu
BOT ni chombo cha serikali. Alikuwa anaamua yeye habari gani itoke na habari gani isitoke. Kuhusu waandishi wa habari, kuna walipigwa kama Makonda alivyovamia vituo vya Clouds kuwapiga waandishi wa habari, wengine hawajulikani walipo na wengine kama Ansbert Ngurumo wameikimbia nchi kuokoa maisha yao.
 
Tupe na thamani ya miradi iliyotokana na deni, kama uwiano wa deni na uchumi kukua ni 30% huko kutendwa kunatokeaje?

Anzia upanuzi wa bandari, SGR, Upanuzi wa highways, mabarabara ya mitaa, stand za mabasi nchi nzima, New mwendokasi roads, vituo vya afya nchi nzima, Hospitali za wilaya nchi nzima, Mashule, Ndege, upanuzi wa viwanja, ujenzi wa Dodoma plus Ikulu ya Chamino, usambazaji umeme kila kijiji, vivutio vya utalii, Hydropower ya Nyerere na vingine vingi. Ulitegemea hela haitumiki?

Then go back angalia uwiano wa uchumi na ukuaji wa madeni! Njoo kwenye probability means of return. Angalia makusanyo per annual sio kuandika kinafiki.
Sukuma gang limepata maumivu kuona jini lake limebagazwa
 
Wacha wee....

Hatimae umetoa reference ile ile ya UK Financial Regulator....

Acha kuruka ruka ngugu mtetezi wa mikopo ya mabeberu!!

Ulisema walioendesha hiyo show ni IMF, nami nikakuambia ni UONGO! Nilikuambia Credit Suisse walikuwa wanachunguzwa na UK Financial Regulator, US Financial Regulator pamoja na Swiss Financial Regulator kwa sababu mkopo waliotoa ulikiuka misingi ya money laundering pamoja na kugubikwa na corruption!!!

Na ni hao ndio walifikisha kesi mahakamani! Hapa unajifanya kuleta reference, halafu unaacha details za kilichopelekea CS kupigwa faini kwamba:-

View attachment 1989187
Sasa hao FCA ni IMF hao? We jamaa vipi wewe?

Na ili kuendelea kutetea uongo wako, hoja za msingi kwenye hiyo ripoti ya FCA umeziruka, na moja wapo ni hii hapa:-

Haya... onesha kwenye hiyo ripoti ni wapi wamesema Credit Suise hawakuwa approved na IMF kutoka mkopo! Au weka hiyo ripoti hapa tuone popote ilipotajwa IMF!

Halafu unaniambia kwamba Credit Suisse walisamehe $200M wakati nilishasema tayari kwamba:-

Mbona unaruka ruka wewe?!

In short ni kwamba hukuwa ni details... ulikurupuka kuongea kitu ambacho hukutafiti huku ukibaki kujimwambafai kwamba eti u mtaalamu wa Public Finance, na kuleta porojo za namna gani IMF hutoa mikopo!!

Mjadala wetu ni wapi tumeongelea deni letu la taifa? Kitu ambacho niliku-challenge ni pale ulipoonesha kwamba it's okay kukopa private banks kwa sababu hizo banks huwa hazitoi mkopo kwa nchi maskini bila kupewa hidhini IMF Approval...

Na ukaendelea kudai kwamba, hata JK na Mkapa sio kwmaba hawakutaka kukopa kwa private banks bali walikuwa hawakupesheki!

Hapo ndipo nikakuambia suala la kukopa private banks sio la kuonea fahari kwa sababu mikopo ya hawa jamaa inaambatana na janja janja nyingi including corruption!

Na nikakupa hadi mfano wa serikali ya JK ilipokopa over USD 600 Million Stanibic ambayo na yenyewe walimwingizia middle man zaidi ya Shilingi 10 Billion za Tannzani!

Au unaeleza hayo katika harakati zako za kutetea hiyo mikopo iliyochukuliwa?

Sasa inahusiana na mjadala wetu? Btw, unadhani TANESCO wanaweza kuchukua mkopo bila guarantee ya serikali?! Na kwa akili yako, TANESCO wakishindwa kulipa unadhani nani atakuwa responsibile?

Look at you...

Eti hizo kampuni zilienda kukopa bila idhini ya serikali na hapo hapo serikali ikawadhamini?!

Unadhamini vipi kitu ambacho hujakibariki? Hivi unajua unachokiongea wewe?

Hujui unachokiongea...

Angalau ungesema "...wewe unaenda KUKOPA"!

IMF wana-deal na serikali na sio taasisi inayokopesha!!

Na ndo maana nikakupa mfano wa ANY LENDER VS ANY DEBTOR!

As long as Credit Suisse ndio walitoa mkopo, hapo ni CS ndio walikuwa na wajibu wa kufahamu loan portfolio ya Mozambique ili kujiridhisha endapo wataweza kulipa, lakini sio Credit Suisse kutaka approval ya IMF kabla ya kutoa mkopo!!

Na hiyo sababu ya ANY LENDER VS ANY DEBTOR ndiyo iliwaingiza (sio kwenye kesi) IMF kwa Msumbiji!

Kwamba, IMF walitaka kutoa mkopo kwa Msumbiji lakini uchunguzi wa named Financial Regulators ukafichukua mkopo waliochukua Msumbiji kwa Credit Suisse! Mkopo huo wa CS hukufahamika na IMF, na ndo maana wakaamua ku-cancel mkopo waliotaka kuwapa Mozambique!

Ni nani waliosema hivyo? Ni IMF, au?!

Achana na habari za IMF kwenye hii mada kwa sababu unachanganya madesa! Na hizo sio taratibu za kimataifa za kukopesha nchi maskini bali ni taratibu zinazo-apply duniani kote!!

However, as a banker, kuna more risky customers! Sasa unaokutana na mteja wa aina hiyo, unatakiwa kuwa makini zaidi katika kufuata operation procedures!!

Kwa kuchanganya changanya mambo tu, u hodari!

Yaani CEO wa Private Bank afukuzwe kazi kwa sababu hakufuata taratibu za IMF?!

We jamaa acha kuongea mambo usiyoyajua!! Fine, umesema wewe ni mtaalamu wa Public Finance lakini HUJUI LOLOTE KUHUSU MAMBO YA KIBENKI!!

Huyo CEO atafukuzwa endapo taratibu hazikufuatwa, including kufanya DUE DILIGENCE!!

Uzuri wa mabenki ni mmoja! Kama umefuata taratibu zote, kisha ukatoa mzigo lakini ukaishia kwa wajanja! Au finally ikagundulika mliowapa pesa ni matapeli... hapo bankers hawawezi kuwa held responsible unless kama hawakufanya due diligence ya kutosha!

Kwamba, watu wanaweza kuja na docs ZOTE zinazoonekana ni halali, kwa mfano kutoka Serikali X! Hapo ukifuata taratibu zote na ukatoa mzigo kwa kutumia hizo docs... utakuwa free kwenye kipengele cha kufuata taratibu!

Lakini je, ulifanya Due Diligence kujiridhisha mamlaka husika zinahusika na hizo docs zinazoonekana ni legit?

Back in the days iliwahi kutokea issue kama hiyo pale NMB Morogoro Rd Branch!

Wajanja wameenda pale na docs ZOTE HALALI kutoka Wizara ya Afya! Jamaa wakafungua akaunti kama signatories wa wizara! Ulipoingizwa mpunga tu, jamaa wakatoa mzigokutoka kwenye akaunti, na wakapotea!

Hapo NMB Morogoro Rd Branch walifuata taratibu zote za kufungua akaunti lakini hawakufanya due diligence kujiridhisha kwamba zilitoka kwenye mamlaka halali!!

Kuna "Wajanja" wengine wanaitumia sana BRELA kupiga mpunga!! Kwa mfano, watu wanaweza kwenda benki na legit docs za kampuni X maybe inayofanya kazi na serikali! Hapo wataenda hadi na Docs za BRELA kuthibitisha existence ya kampuni husika!

Sasa bankers wakiwa makini kwenye due diligence, wanaweza kukuta ni kweli kampuni ipo, na imesajiriwa BRELA lakini walio mbele yako sio TRUE OWNERS wa kampuni husika! Sasa kwanini wamekuja kufungua akaunti ya kampuni ambayo sio yao?

More likely, watakuwa wamepiga cheque ya kampuni husika, na wanajua ili kutoa pesa kutoka kwenye hiyo cheque, ni LAZIMA wafungue akaunti yenye jina lililopo kwenye cheque (of that company)!

Naona unageuza gia angani...

Kwahiyo sasa ni "...nchi maskini kwenda kukopa bila ya kuongea na IMF" na sio tena:-

Yaani umeshasahau ulisema hata hizo private banks za mabeberu hazikopeshi nchi maskini bila IMF kufanya yao, halafu hapa unapinduka na kusema nchi maskini haziwezi kukopa kwenye private banks bila IMF kufanya yao!!

Na hata kwenye post yako hii umesahau ulisema:-

Hivi hiyo sentensi inamaanisha nini kama sio private banks kutokopesha nchi maskini bila kufuata miongozo ya IMF?

Halafu few hours ago, ulileta fix zingine kwamba mapato makubwa ya IMF yanatokana na mikopo wanayochukua kutoka private banks!

Kituko ni pale unapojaribu kuaminisha watu kwamba MWENYE PESA YAKE/CREDITOR, yaani Private Banks, hawezi kukopesha bila kupewa idhini DEBTOR wake wakati huyo Creditor wala haendeshi shughuli zake chini ya mamlaka ya huyo anayemdai!

Ona fix ulizokuwa unapiga watu mwanzoni kabla sija-reveal uongo wako na hatimae ukabadilika na kuanza kuongelea habari za FCA!!

Hebu twende taratibu ndugu mwananchi...

Credit Suisse wamepewa za uso na IMF au FCA, pamoja na other finacial regulators (SEC & FINMA)?

Endelea tu kuchanganya madesa....

Btw, ni nani alikudanganya "...private banks wakaja na Brady Bonds"?!

Hivi unafahamu huyo ni Brady ni nani?!

FYI, kwanza hiyo crisis haikutokea in 70's bali in 80's!!

Na Brady Bond ni matokeo ya ku-fail mpango wa awali ambao ulinzishwa na James Baker, na program yenyewe ilikuwa inaitwa Baker Plan!!

Failure ya Baker Plan, iliyokuwa imeletwa na James Baker during Reagan Administartion, ndiyo ikaleta Brady Plan during Bush Sr Administration!

Both, James Baker na Nicholus Brady at the time walikuwa Treasury Secretaries. Hivyo basi, Brady Bond zilizotokana na Brady Plan ilikuwa ni mpango wa Serikali ya Marekani na sio private banks!!

Umebaki tambo tu lakini HUJUI LOLOTE....

Na hivi unakumbuka ulisema eti nakupotezea muda ingawaje hujaacha kuni-quote?!

Hatimae nimebaini ni wewe ndie unanipotezea muda manake mara kwa mara unaleta mambo tofauti lakini unayaleta bila kuwa na ufahamu nayo!!

So, stay blessed, coz' you're the one now wasting my time!

Jifunze kwanza kusimama kwenye hoja moja, na ukija na hoja tofauti basi iwe inalenga kukazia hoja ya msingi iliyobeba mjadala!!

On top of that, unapoleta hizo hoja tofauti basi uwe na uelewa wa hicho unacholeta! Sio tu unampelekea bosi chai, njiani unasikia kwa mbali watu wwanazungumzia Brady Bonds na hatimae unafanikiwa kudaka mawili matatu, kutoka kwao, basi hapo hapo unakurupuka kuja hapa kabla hujawa na uelewa whicho ulichosikia!!
Salaleh we jamaa unaishi kwenye dunia yako kutokana na huo uchambuzi ulioleta. Like I said much of your interpretation is based on face value of the articles perused and limited understanding of finance applications in general (leave alone cluelessness of public finances).

Ndio maana nimekwambia una unga unga tu; some of us can tell. Why so?

Ni hivi kuna finances and economics (are mainly governed with social sciences rules) which yield international practice and norms kutokana na historical context (past experience) na ndivyo ilivyo kwenyr public finance policies.

On historical context ni hivi madeni ya late 70’s na 80’s (duniani) yalitokana na Private Banks kukopesha nchi maskini recklessly especially in Latin America without proper checks. Mainly kwa sababu walikuwa wanapata hizo hela za kukopesha kirahisi kutoka kwa Investor’s wa nchi za kiarabu.

That’s normal practice in banking kuwa na middleman kwenye kukopesha nchi kupitia hela za watu wengine even IMF and WD are doing the same thing (actually na ili pia ni tatizo ata kwenye sakata la Mozambique has I will explain in a short while).

Sasa kumaliza matatizo ya defaults za mikopo kipindi hiko yaani (kuanzia late 70-80’s) kwa kuelewa private banks ndio mzozo wa tatizo because they were unregulated and the cause of high debt. IMF na WD walishauri mikopo inayowezekana ifutwe waanze on clean slate kwa kuhakikisha wana regulate mikopo ya nchi maskini kwenda mbele to miniminise the risks of default.

What you also need to know source ya IMF na WB capital ni hela ambazo zinatolewa na nchi tajiri kusaidia nchi maskini but only on specific social project na ndio mikopo yenye riba ndogo; also kuna hela za private banks ambazo zinariba kubwa kidogo.

Additional as source of national capital kuna private banks wanaotoa mikopo bila ya kupitia IMF na WB kwa riba kubwa zaidi.

Kutatua matatizo ya mikopo ya zama hizo (late 70-80’s) nchi tajiri zilifuta mikopo yake; however private banks zikakataa wote including wale wanaotoa hela kupitia International funds na individual banks.

kwenye kutatua changamoto za mikopo ya private banks IMF/WB wakaja na two new loan restructuring solutions.

Banks zinazoambatana na ‘Paris Club’ wao waliona shida ya madeni kama short term liquity issue wakaenda na mtindo wa kutaka kulipwa mbele kwa kushusha riba, na private banks zinazoambatana na ‘London Club’ wakafuata ushauri wa marekani kupitia ‘Brady Bonds’.

Either way hayo matatizo ya kulimbikizia nchi madeni ilibidi yatafutiwe suluhisho la moja kwa moja yasijirudie tena.

Ndipo hapo IMF/WB wakaja na mapendekezo kila nchi katika wizara yake ya fedha lazima iwe na DMO yenye jukumu la kuangalia madeni yote ya nchi i.e kwa kujumuisha madeni ya serikali kuu, taasisi zake na serikali za mitaa. Hii itasaidia kujua risk za default on guaranteed loans based on nations cash flow.

Sasa nini kimetoka Mozambique serikali iliyopita ilivuka hizo fire wall za international supervisors; hilo deni lilifichwa kwa kusaidiwa na Credit Suisse, kwa sababu waliokopa ni taasisi ambao wanalipa wenyewe kwa mapato ya shughuli zao (ndio maana nikakupa mfano wa TANESCO)

E5C3EA82-1295-456F-80EC-B174850C8F71.jpeg


Hiyo mikopo ilipita without firewalls za nchi (Mozambique) as recommended by IMF stress tastes, between 2012 and 2015

Waliotoa siri ni serikali mpya iliyoingia madarakani late 2015 baada ya kuona kuna mikopo wanalipa ambayo aifuata process sahihi za kimataifa.

511B68F2-F9D3-46C7-80AD-CA599EE0238C.jpeg


Kilichofuata based on what IMF can do baada ya kugundua kumbe kuna watu wamekopesha Mozambique without adhering to due process; given their influence position. Wanachoweza fanya ni kusitishs mkopo wao uliokuwa njiani (based on their risk assessment) na wakifanya ivyo hakuna atakae kukopa.

FF7B6A64-2EBF-4665-8BCB-05E3F4D15981.jpeg


Hiko ndio IMF inachoweza fanya baada ya kutoa taarifa.

Kilichofuata ndio mlolongo wa cascading events FCA watatumia ‘Companies Act 2006’ and ‘Governance code of conduct 2010’ kutoa adhabu kutokana na matendo Credit Suisse based on their jurisdiction kwa sababu subsidiary company iliyosajiliwa ipo nchini kwao; so it’s subjected to those rules. Ndio maana wametoa adhabu kutokana mambo husika yanayohusiana na sheria zao za rushwa mainly money laundering and so forth.

Alikadhalika US wanahusika kwa sababu hela za hiyo mikopo wafadhali wake wametoka kwao (ni hela za U.S Investor’s ndio zimetumika kutoa huo mkopo kupitia Credit Suisse). Kama nilivyokwambia awali ata private banks can source loans outside just IMF/WD as middlemen.

Kwa sababu hizo hela ni za Investor’s kutoka US hiyo inatoa nafasi kwa US regulators ‘Security Exchange Council’ kutumia sheria zao zinazowapa mamlaka ya kumlinda investor wao amongst them ni ‘Sarbanes Oxley Act 2002’.

Ndio maana nakwambia hujui; unaandika ujinga mtupu, so far uelewi hata hilo deni lilikopwa na taasisi za serikali sio wizara ndio maana alikuonekana kwenye budget.

Sasa najiuliza hivi unaelewa kweli mziki wa Bandari ya Bagamoyo na LNG (hizo ni business finance mziki wake ni mnene maradufu from public finance) kama unasoma vitu vyepesi ata historical context hujui.

Hayo mambo unayorukia hesabu zake shyt is very complicated tofauti na ujinga unaoandikaga, sema na njaa zako.
 
Kukopa is inevitable, mataifa yote yanakopa ili mambo yao yaende.

Ndugu muandishi angejikita zaidi kwenye matumizi ya huo mkopo ili tuone thamani yake, atufahamishe pia sehemu ya mkopo iliyomegwa na mwendazake kwa matumizi binafsi ili tupate uhalali wa kulitupia mawe kaburi.

Tsh 1.5 trillion na Tsh 1.9 trillion zilizoripotiwa na CAG ASSAD !!!
 
Salaleh we jamaa unaishi kwenye dunia yako kutokana na huo uchambuzi ulioleta. Like I said much of your interpretation is based on face value of the articles perused and limited understanding of finance in general (leave alone cluelessness of public finances).

Ndio maana nimekwambia una unga unga tu; some of us can tell. Why so?

Ni hivi kuna sectors (mainly with social sciences) influence international practice and norms kutokana na historical context (past experience) moja wapo ni hii ya public finance policies.

Ni hivi madeni ya late 70’s na 80’s yalitokana na Private Banks kukopesha nchi maskini recklessly especially in Latin America without proper checks. Mainly kwa sababu walikuwa wanapata hizo hela za mikopo kirahisi kutoka kwa Investor’s wa nchi za kiarabu.

That’s normal practice banks kuwa middleman kwenye kukopesha nchi kupitia hela za watu wengine even IMF and WD are doing the same thing (actually na ili pia ni tatizo ata kwenye sakata la Mozambique has I will explain in a short while).

Sasa kumaliza matatizo ya defaults za mikopo kipindi hiko (late 70-80’s) kwa kuelewa private banks ni tatizo. IMF na WD walishauri mikopo inayowezekana ifutwe waanze on clean slate kwa kuhakikisha wana regulate mikopo ya nchi maskini inakuwa regulated to miniminise the risks of default.

Sasa source ya IMF na WB capital ni hela ambazo zinatolewa na nchi tajiri kusaidia nchi maskini but only on specific social project na ndio mikopo yenye riba ndogo; also kuna hela za private banks ambazo zinariba kubwa kidogo. Na kuna private banks wanatoa mikopo bila ya kupitia IMF na WB kwa riba kubwa zaidi.

Kutatua matatizo ya mikopo ya zama hizi nchi tajiri zilifuta mikopo yake; private banks zikakataa wote wale wanaotoa hela kupitia International funds na private banks. Ndio wakaja na new restructuring za kulipa madeni kwa upande wa banks.

Banks na zinazoambatana ‘Paris Club’ wao walichukulia shida ya madeni kama short term liquity issue wakaenda na mtindo wa kutaka kulipwa mbele; na private banks zinazoambatana na ‘London Club’ wakafuata ushauri wa marekani kupitia ‘Brady Bonds’.

Either way hayo matatizo ya kulimbikizia nchi madeni ilibidi yatafutiwe suluhisho; ndipo hapo IMF/WB wakaja na mapendekezo kila nchi katika wizara yake ya fedha lazima iwe na DMO yenye jukumu la kuangalia madeni yote ya nchi i.e serikali kuu, taasisi zake, serikali za mitaa na kuyajumuisha. Hii itasaidia kujua risk za default on guaranteed loans based on nations cash flow.

Sasa nini kimetoka Mozambique serikali iliyopita ilivuka hizo fire wall za international supervisors; hilo deni lilifichwa kwa kusaidiwa na Credit Suisse

View attachment 1990265

Huo mkopo ulipita without firewalls za nchi as recommended by IMF. Waliotoa siri ni serikali mpya iliyoingia madarakani late 2015 baada ya kuona mkopo aujafuata process sahihi.

View attachment 1990268

Kilichofuata based on what IMF can do given their influence position. Kusitisha mkopo wao uliokuwa njiani baada ya kuona kumbe kuna watu awaja record baadhi ya mikopo.

View attachment 1990269

Hiko ndio IMF inachoweza fanya baada ya kutoa taarifa.

Kilichofuata ndio mlolongo wa cascading events FCA watatumia ‘Companies Act 2006’ and ‘Governance code of conduct 2010’ kutoa adhabu kutokana na matendo Credit Suisse based on their jurisdiction kwa sababu subsidiary company iliyosajiliwa ipo nchini kwao. Ndio maana wataongea wametoa adhabu kutokana mambo husika yanayohusiana na sheria zao rushwa, money laundering and so forth.

Alikadhalika US wanahusika kwa sababu hela za hiyo mikopo W afadhali wake wametoka kwao (ni hela za U.S Investor’s ndio zimetumika kutoa huo mkopo kupitia Credit Suisse).

Hiyo inatoa nafasi kwa US regulators ‘Security Exchange Council’ kutumia sheria zao zinazowapa mamlaka ya kumlinda investor wao amongst them ni ‘Sarbanes Oxley Act 2002’.

Ndio maana nakwambia hujui; unaandika ujinga mtupu, so far uelewi hata hilo deni lilikopwa na taasisi za serikali ndio maana alikuonekana kwenye budget.

Sasa najiuliza hivi unaelewa kweli mziki wa Bandari ya Bagamoyo na LNG (hizo ni business finance mziki wake ni mnene maradufu from public finance) maana that shyt is very complicated tofauti na ujinga unaoandikaga, sema na njaa zako.
Umeeleza vyema sana mkuu

Vp kama tukikataa kulipa hili deni letu hao creditors watachkua hatua gani?
 
Umeeleza vyema sana mkuu

Vp kama tukikataa kulipa hili deni letu hao creditors watachkua hatua gani?
Provided umepitia IMF/WB kinachofuata ni SAP (Structural Adjustment Policies).

Ukigoma SAP wao washakufanyia analysis ya mapato yako ni kama tairi la F1 car (lina laps zake before its worn out) ukizidisha lap linapasuka.

In other words wana control monetary policies za nchi maskini; you can’t just print new money like US can or manipulate the gold standard as they wish with their central bank.

To get credit you have to go through them. Ukiaribu chamoto utakiona. Tuwaulize hao hao Msumbiji nini kiliwakuta baada ya IMF yakubaini mkopo wa siri na kusitisha mkopo na wafadhili kuacha kwa ushauri wa IMF.

Kuna upuuzi mwingine unasoma humu unajisemea, mweh. Mimi tu mkaidi Max angeweza ku protect wachangiaji kwa asilimia JF ingekuwa na wamwaga nondo. Kuna watu nawajua wana uwezo wakudadavua hayo mambo zaidi; at the same time kuna watu ukiwasoma unaona huyu sio tu kwamba unga unga bali hata elementary knowledge hana.
 
Na kuna mtu hapo juu nimemwambia inabidi tukae kwa kutulia kwa sababu mambo bado sana...

Ukitoa hizo 1.3 Trillion... SGR haijafika popote! Kwahiyo Serikaya ya Chifu Hangaya itaendelea kukopa kwa ajili ya SGR!!

Kuna Bwawa la Umeme... huko nako wataendelea kukopa!!

Kwa hayo mawili, siwezi kumlaumu kwa sababu hakuna namna... tushaingia shipa!!

Lakini kama hiyo haitoshi, wameingia mkataba wa kununua ndege zingine wakati zilizopo bado ni loss-making with no predictable feature!!

Hapo tena, atakopa pesa! Na IMF hawawezi kukukopesha eti ukanunue ndege! Hapo atalazimika kwenda private banks ambazo zimejaa janja janja nyingi, including corruption and riba zisizo rafiki!!
Mkuu mimi nadhani kukopa sio ishu tukope tu ili mambo yaende. USA inadaiwa $ 17.6 tril na mambo yao ni supa, Japs $ 9 tril nao wako byee .... Sisi haka ka $ 33.7 bill naona bado tuko njema tu kulingana na gali yetu.

Shida ipo kwenye kusimamia na kudhibiti matumizi ya hii mikopo!
 
Provided umepitia IMF/WB kinachofuata ni SAP (Structural Adjustment Policies).

Ukigoma SAP wao washakufanyia analysis ya mapato yako ni kama tairi la F1 car (lina laps zake before its worn out) ukizidisha lap linapasuka.

In other words wana control monetary policies za nchi maskini; you can’t just print new money like US can or manipulate the gold standard as they wish with their central bank.

To get credit you have to go through them. Ukiaribu chamoto utakiona. Tuwaulize hao hao Msumbiji nini kiliwakuta baada ya IMF yakubaini mkopo wa siri na kusitisha mkopo na wafadhili kuacha kwa ushauri wa IMF.

Kuna upuuzi mwingine unasoma humu unajisemea, mweh. Mimi tu mkaidi Max angeweza ku protect wachangiaji kwa asilimia JF ingekuwa na wamwaga nondo. Kuna watu nawajua wana uwezo wakudadavua hayo mambo zaidi; at the same time kuna watu ukiwasoma unaona huyu sio tu kwamba unga unga bali hata elementary knowledge hana.
Mkuu mimi sipo kwenye battle yenu wewe na Mkuu Chige 🙌, maana mimi sio financial expert, I'm just curious to know how big boys role dice.

Ningependa unijibu in layman terms, watatufanya nini hawa mabwana kama tukiwakataa? Kama Zimbabwe??
 
Kam
Kwa hiyo waandishi wote walikaa kimya? Kusema kwamba tumekopa iwe shida? Mbona BoT walikuwa wakiweka kwenye website yao, mbona wap hawakupata shida? Unafiki tu
Kama kutetea uhai ni jambo la kinafki basi mimi naona iko vyema tu mkuu.

07 September 2017, bwana mmoja alinyeshewa mvua ya risasi(magazine nzima) kwasababu hizohizo. Mungu wake mkubwa sana ndio maana bado tupo naye hadi leo hii.
 
Magufuli katutenda deni la taifa, trilioni 78 Samia msalabani

Jamhuri October 26, 2021

Na Deodatus Balile

Kazi hii ya uandishi wa habari moja ya majukumu yake ni kuanika ukweli minong’ono inapotawala katika jamii.

Kwa sasa kuna minong’ono mingi. Minong’ono imeanza baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza hadharani mkopo wa Sh trilioni 1.3, alioukopa kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na akatangaza miradi lukuki itakayotekelezwa kwa kutumia mkopo huo.

Miongoni mwa miradi ya kihistoria ni ujenzi wa madarasa ya sekondari 15,000 nchi nzima na madarasa ya shule za msingi 3,000.

Kwa sasa inakadiriwa kuwa nchi ina upungufu wa madarasa 11,000, lakini Rais Samia ameamua kuona mbali.

Ameamua kufuta mfumo wa zima moto, ambapo kila mwaka wazazi wanakabwa koo vijijini kuchangia ujenzi wa madarasa.

Baadhi ya wazazi pia wameanza minong’ono kuwa watoto wao wamepewa mikopo kidogo, yaani Sh 600,000 kama ada vyuoni.

Hawajui kuwa miaka yote imekuwa hivyo na wakati mwingine wengi wanakuwa hawapati kabisa hata senti tano ya mkopo.

Sitanii, naomba nizungumzie kwa ufupi miezi sita ya Rais Samia akiwa Rais wa Tanzania baada ya kuapishwa Machi 19, 2021.

Nakumbuka vema kilichotokea, maana baada ya kifo cha Rais John Magufuli kulitokea kama sintofahamu hivi.
Wapo watu walioamini Rais Samia angeendelea kuwa Kaimu Rais, baadhi walidhani tunakwenda kwenye uchaguzi mpya na wengine hawakufahamu nini kitatokea.

Asubuhi ya Machi 18, 2021 niliamkia studio za Televisheni ya Taifa (TBC1) na TBC Taifa (radio) kufanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dk. Ayub Rioba.

Hii ilikuwa ni baada ya kifo cha Rais John Magufuli, kilichotokea Machi 17, 2021. Ikumbukwe wiki moja kabla nilikuwa nimefanya mahojiano na kituo cha Star TV nikasema tuambiwe bayana Rais Magufuli yuko wapi na anafanya nini.

Machi 18 pamoja na kwamba nilikuwa bado Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambapo baadaye nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TEF Mei 22, 2021, ilinilazimu kutoa ufafanuzi huo uliokuwa tamko zito.

Sitanii, tamko nililolitoa lilizaa kuapishwa kwa Rais Samia kuwa Rais wa Awamu ya Sita Machi 19, 2021. Nilirejea Katiba ya Tanzania (1977) Ibara ya 37(5) inayosema: “Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya 40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakayekuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua asilimia hamsini ya wabunge wote.”

Kwa mara ya kwanza kupitia makala hii ninakisema kilichotokea baada ya tamko hilo. Walinipigia simu watu wengi wakiwa na hofu.

Baadhi hawakufahamu Katiba inasemaje. Walinishutumu wakidai nimetangaza utaratibu wa kwangu, kwani baada ya kifo cha Rais kinachofuata ni uchaguzi.

Hii ilinipa shida kuona hata baadhi ya wabunge hawakufahamu nini kinafuata baada ya kifo hicho. Machi 18, 2021 itabaki kuwa siku ya kihistoria kwangu, kwani ujumbe nilioutoa ulitangazwa katika radio zote za ndani na za kimataifa na siku moja baadaye Rais Samia akaapishwa.

Sitanii, leo ninazungumzia mzigo wa madeni ambao Rais Magufuli amelitwisha taifa letu. Nimetangulia kusema na ninarudia, mimi ni msema kweli. Wala sipepesi macho katika kusema ukweli.

Wakati Rais Magufuli kwa miaka mitano yote alikuwa anawaaminisha Watanzania kuwa nchi inajenga miundombinu na inanunua ndege kwa kutumia fedha zetu wenyewe, uhalisia ni kinyume chake.

Kwa kipindi cha miaka mitano tu, Rais Mafuguli amekopa fedha nyingi kuliko fedha zote alizokopa Rais Benjamin Mkapa kwa miaka 10 aliyokaa madarakani.

Kwa miaka mitano, amekopa pia fedha nyingi kuliko alizokopa Rais Jakaya Kikwete kwa miaka 10 naye aliyokaa madarakani.

Rais Mkapa alirithi madeni mengi mno. Alipambana nayo, akaiingiza nchi katika Mpango wa Kusamehe Madeni Nchi Maskini (HIPC) na hadi anatoka madarakani, Tanzania ilikuwa inadaiwa Sh trilioni 20 tu.

Rais Kikwete wakati wake deni la taifa liliongezeka kwa Sh trilioni 23, hivyo akatoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 43 kwa miaka 10. Rais Magufuli kwa miaka mitano tu, deni la taifa limeongezeka kwa Sh trilioni 29 na kufikia Sh trilioni 72 hadi anafariki dunia Machi, 2021.

Sitanii, kwa kasi hii ya ukopaji ina maana kama angekaa madarakani kwa miaka 10 kamili na akaendelea na kasi ya ukopaji wa wastani wa Sh trilioni 29 kwa miaka mitano, basi angetoka madarakani deni la taifa likiwa Sh trilioni 101 kufikia mwaka 2025.

Kuna jambo baya halisemwi. Rais Magufuli amekopa mikopo ya kibiashara inayoanza kulipwa baada ya miaka mitatu na inapaswa kulipwa ndani ya miaka minane, ikiwa na riba za kati ya asilimia 6 na 8.

Baadhi ya mikopo hii imeiva tayari. Imeanza kukuza deni la taifa kwa kasi kutokana na riba. Deni la taifa sasa limefikia Sh trilioni 78.

Kwa vyovyote vile iwavyo, Rais Samia anapaswa kuchukua hatua za haraka, ikiwamo kuunda timu ya majadiliano na wakopeshaji kwa ajili ya kubadili masharti ya mikopo ya kibiashara aliyochukua Rais Magufuli.

Anapaswa kuomba msamaha wa riba na pengine kuomba kuongezewa muda wa kulipa deni kama ulivyo utaratibu wa mikopo kwa serikali nyingi duniani.

Mikopo mingi kwa serikali huwa inalipwa kati ya miaka 20 hadi 50 kulingana na ukubwa wa mkopo na hutozwa riba kati ya asilimia 0.3 hadi asilimia 1. Mikopo ya aina hii inapatikana katika Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo Duniani, Benki ya Maendeleo Afika na nyingine za aina hii.

Kwa bahati mbaya na kwa masikitiko makubwa, kwa miaka mitano Wazungu tuliowaita mabeberu, ila tukawa tunakopa fedha zao kupitia benki za biashara. Kwa hali halisi, madeni haya yakiiva yote, ikiwa hakuna majadiliano ya dharura kuomba marekebisho ya masharti ya mikopo tuliyochukua chini ya Rais Magufuli, itafika mahala asilimia 60 ya bajeti ya taifa letu itakuwa inakwenda kulipa madeni. Waliomo serikalini watajua la kufanya katika hili.

Sitanii, ninafahamu baadhi ya wasomaji watakuwa wanaanza kufuka moshi kwa kusema ukweli huu. Wanajiuliza taarifa hizi nimezipata wapi? Taarifa hizi si za siri. Ziko wazi kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Nimepitia taarifa za mapitio ya mwenendo wa uchumi tangu mwaka 2000 hadi 2021. Zipo mtandaoni na zinaonyesha deni lilivyokua hatua kwa hatua. Kwa nia ya kuweka uelewa unaofanana, ifuatayo ni hali ya deni la taifa tangu mwaka 2005 hadi 2021.

Oktoba 2005, deni la nje lilikuwa USD milioni 8,361.9 sawa na Sh 19,286,471,493,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 1,712,800,000,000. Jumla kuu ya deni wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani lilikuwa Sh 20,999,271,493,000 (Sh trilioni 20.9). Nimekokotoa hesabu hizi kwa kutumia viwango vya BoT vya kuuza dola ya Marekani ambavyo ni USD 1 kwa Sh 2,306.47.

Oktoba 2015, wakati Rais Kikwete anatoka madarakani deni la nje lilikuwa USD milioni 15,321.3, sawa na Sh 35,338,118,811,000 na deni la ndani lilikuwa Sh 7,826,200,000,000. Jumla kuu deni la nje na deni la ndani lilikuwa ni Sh 43,164,318,811,000 (Sh trilioni 43.1).

Deni la taifa lilianza kupanda kwa kasi Oktoba 2016. Deni la nje lilipanda na kuwa USD milioni 16,407.6 sawa na Sh 37,843,637,172,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 10,089,000,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 47,932,637,172,000 (Sh trilioni 47.9).

Oktoba 2017 deni la nje lilipanda kwa kasi kubwa na kufikia USD milioni 19,074.4 sawa na Sh 43,994,531,368,000. Kutokana na makandarasi kutolipwa deni la ndani nalo lilikua na kufikia Sh 12,563,300,000,000. Jumla kuu ya deni kwa mwaka huo likawa Sh 56,557,831,368,000 (Sh trilioni 56.5).

Oktoba 2018, deni la nje lilizidi kupanda na kuwa USD milioni 20,759.1 sawa na Sh 47,880,241,377,000, huku deni la ndani nalo likipanda na kuwa Sh 14,116,100,000,000. Jumla kuu ikawa Sh 61,996,341,377,000 (Sh trilioni 61.9).

Oktoba 2019, mwanamume aliongeza tena deni la taifa, deni la nje likafikia USD milioni 22,569.4, sawa na Sh 52,055,644,018,000, huku deni la ndani likipanda na kufikia Sh 14,187,400,000,000. Jumla kuu ya deni ikafikia Sh 66,243,044,018,000 (Sh trilioni 66.2).

Oktoba 2020, deni la nje lilipanda na kufikia USD milioni 23,599.3, sawa na Sh 54,431,077,471,000, huku deni la ndani likifikia Sh 15,608,500,000,000. Jumla kuu ikafikia Sh 70,039,577,471,000 (Sh trilioni 70).

Machi, 2021 wakati Rais Magufuli anafariki dunia, deni la nje la Tanzania lilikuwa limefikia USD milioni 24,429.2, sawa na Sh 56,345,216,924,000. Deni la ndani nalo lilipanda na kufikia Sh 16,116,500,000,000. Jumla kuu, deni la taifa lilifikia 72,461,716,924,000 (Sh trilioni 72.4).

Kilichofuata baada ya hapo, madeni yameanza kuiva kwa ajili ya kulipwa, huku mengine yakizalisha riba ya kufa mtu.

Makandarasi wengi Tanzania wanadai mabilioni kati ya hizo Sh trilioni 16 ambazo ni deni la ndani hawajalipwa siku nyingi. Kutokana na hali hiyo, madeni haya yaliyokopwa bila mpangilio katika benki za biashara yameanza kuwa msalaba kwa Rais Samia.

Taarifa ya hali ya Uchumi ya BoT ya Septemba, 2021 inayorejea mwezi Agosti, 2021 kutokana na mazingira hayo, deni la nje limekua na kufikia USD milioni 25,956.1 sawa na Sh 59,866,965,967,000, huku deni la ndani nalo likikua na kufikia Sh 18,225,000,000,000. Ukuaji huu unafanya kiwango cha deni la taifa kufikia jumla kuu ya Sh 78,091,965,967,000 (trilioni 78).

Sitanii, deni hili likigawanywa kwa Watanzania milioni 60, bila kujali mkubwa na mdogo, kila Mtanzania anadaiwa Sh 1,301,533 (Sh milioni 1.3). Hata hivyo, wataalamu wa uchumi wanasema deni hili si tishio kwa uchumi wa taifa letu kwa sasa kwani liko katika uwiano wa asilimia 30 kwa uchumi wa taifa letu, wakati kuna mataifa Afrika ambayo tayari yana uwiano wa asilimia 54 ya deni kwa uchumi wa nchi zao, ila wanaionya serikali iepuke mikopo ya kibiashara ina riba kubwa, masharti mabaya na inalipwa kwa muda mfupi.

Pale Dodoma, tumeona Rais Samia ameanzisha utaratibu mpya wa ukweli na uwazi katika mikopo. Ameeleza fedha alizokopa zitafanya nini kwa kuorodhesha miradi itakayotekelezwa na akatueleza amezikopa kutoka wapi.

Ninajiuliza, hivi ilikuwa ni kwa faida ya nani Rais Magufuli na wapambe wake kuficha ukweli kuwa miradi ya reli, barabara, umeme, ujenzi wa hospitali na mingine mingi aliyoijenga alikuwa anakopa?

Hivi sisi kama tungejua anakopa, tungemzuia? Lakini si tungepata fursa ya kumshauri asichukue mikopo ya kibiashara inayoanza kututoa utumbo sasa? Mungu ibariki Tanzania.

Copyright ©2021. Gazeti la Jamhuri
Hakuna jitu la hovyo na nafiki kama Balile. Lenyewe hufikiria kulakula tu. Huyu hana tofauti na Msiba aka Musiba. Wanafikiri kwa matumbo badala ya vichwa au tuseme makalio.
 
Mkuu mimi sipo kwenye battle yenu wewe na Mkuu Chige 🙌, maana mimi sio financial expert, I'm just curious to know how big boys role dice.

Ningependa unijibu in layman terms, watatufanya nini hawa mabwana kama tukiwakataa? Kama Zimbabwe??
Nimekuelezea kama ukuelewa

What ‘structural adjustment policies’ are.

Utaki kwa lugha rahisi mfano F1 tyre niliokupa kama ujauelewa ni hivi.

Wewe una mapato ya tsh elfu 30 kwa week (for simplification pursposes) kwa siku unatumia tsh elfu 10 minimum; sasa utamaliza week kwa mapato hayo bila ya kukopa au kuongeza uzalishaji. Dunia ndio imekubana hapo.

To get out of that rat trap in the long run you need plan on ways to add value on what you can produce; sasa kuingia kwenye mjadala huo tunahama kutoka kwenye finance kwenda kwenye uchumi.

Alamsiki.
 
Mkuu mimi nadhani kukopa sio ishu tukope tu ili mambo yaende. USA inadaiwa $ 17.6 tril na mambo yao ni supa, Japs $ 9 tril nao wako byee .... Sisi haka ka $ 33.7 bill naona bado tuko njema tu kulingana na gali yetu.

Shida ipo kwenye kusimamia na kudhibiti matumizi ya hii mikopo!
Man,

Mimi sina matatizo na kukopa, nina matatizo na wale wanaoona fahari kukopa kwenye benki za kibiashara wakati kila mfuatiliaji wa haya mambo, anafahamu makali ya kukopa benki za kibiashara...

Na wanaonea fahari kukopa benki za kibiashara sio kwa sababu za kitaalamu, bali kwavile aliyekopa hiyo mipesa ni JPM, na kwao JPM IS ALWAYS RIGHT, basi hata kama alichokifanya kinaonekana wazi sio sawa, WAO WATATETEA TU...

Mchukulie huyo Kilatha, yaani bila aibu anafikia kusema:-
Unadhani mzungu mjinga, JK na Mkapa sio kwamba walikua awataki kukopa, sema walikuwa awakopesheki na hela ilikuwa aifanyi kazi iliyokopewa.
Hivi kuna mwenye akili timamu anayeweza kuamini porojo kama hizo?

Yaani Western Financial Institutions ziwe na imani zaidi na JPM ambae alikuwa wala hatabiriki kesho ataamuka na balaa gani, halafu wasimuamini Kijana Wao Mpendwa Benjamin Mkapa?!

Lakini kwanini kaongea hayo... kwa sababu tu hiyo mikopo imechukuliwa na "JPM" na yupo tyari kutetea na ku-justify lolote hata kama ni la kijinga!!
 
Man,

Mimi sina matatizo na kukopa, nina matatizo na wale wanaoona fahari kukopa kwenye benki za kibiashara wakati kila mfuatiliaji wa haya mambo, anafahamu makali ya kukopa benki za kibiashara...

Na wanaonea fahari kukopa benki za kibiashara sio kwa sababu za kitaalamu, bali kwavile aliyekopa hiyo mipesa ni JPM, na kwao JPM IS ALWAYS RIGHT, basi hata kama alichokifanya kinaonekana wazi sio sawa, WAO WATATETEA TU...

Mchukulie huyo Kilatha, yaani bila aibu anafikia kusema:-

Hivi kuna mwenye akili timamu anayeweza kuamini porojo kama hizo?

Yaani Western Financial Institutions ziwe na imani zaidi na JPM ambae alikuwa wala hatabiriki kesho ataamuka na balaa gani, halafu wasimuamini Kijana Wao Mpendwa Benjamin Mkapa?!

Lakini kwanini kaongea hayo... kwa sababu tu hiyo mikopo imechukuliwa na "JPM" na yupo tyari kutetea na ku-justify lolote hata kama ni la kijinga!!
Arrghh JPM alifanya bogus deals

nmeona post umeandika mama nae atanunua madege kwa style hiohio, vp kuna faida nyingine ambazo sisi raia hatuzijui ama
ni yaleyale ya kujikosha?
 
Nimekuelezea kama ukuelewa

What ‘structural adjustment policies’ are.

Utaki kwa lugha rahisi mfano F1 tyre niliokupa kama ujauelewa ni hivi.

Wewe una mapato ya tsh elfu 30 kwa week (for simplification pursposes) kwa siku unatumia tsh elfu 10 minimum; sasa utamaliza week kwa mapato hayo bila ya kukopa au kuongeza uzalishaji. Dunia ndio imekubana hapo.

To get out of that rat trap in the long run you need plan on ways to add value on what you can produce; sasa kuingia kwenye mjadala huo tunahama kutoka kwenye finance kwenda kwenye uchumi.

Alamsiki.
Kumeshakucha mkuu!
 
Salaleh we jamaa unaishi kwenye dunia yako kutokana na huo uchambuzi ulioleta. Like I said much of your interpretation is based on face value of the articles perused and limited understanding of finance applications in general (leave alone cluelessness of public finances).

Ndio maana nimekwambia una unga unga tu; some of us can tell. Why so?
PUNGUZA MBWEMBWE ZA KUJITIA UJUAJI WAKATI MWEUPE...
Ni hivi kuna finances and economics (are mainly governed with social sciences rules) which yield international practice and norms kutokana na historical context (past experience) na ndivyo ilivyo kwenyr public finance policies.
Wakati unajugamba kusoma Public Finance, nimesoma Uchumi, kwahiyo hayo mambo unayoyasikia juu juu, mwenzako ninayasomea
On historical context ni hivi madeni ya late 70’s na 80’s (duniani) yalitokana na Private Banks kukopesha nchi maskini recklessly especially in Latin America without proper checks. Mainly kwa sababu walikuwa wanapata hizo hela za kukopesha kirahisi kutoka kwa Investor’s wa nchi za kiarabu.
Narudia... Brady Bond ni matokeo ya 80's Financial Crisis na sio 70's!
That’s normal practice in banking kuwa na middleman kwenye kukopesha nchi kupitia hela za watu wengine even IMF and WD are doing the same thing (actually na ili pia ni tatizo ata kwenye sakata la Mozambique has I will explain in a short while).
Middlemen are everywhere in a modern business... hapa tunazungumzia CORRUPTION THROUGH MIDDLEMEN...

Kwenye Sakata la Radar.... Middleman alipiga za kutosha...

Kwenye mkopo wa Stanbic, Middle Man alipiga mabilion...

Kwenye sakata la Msumbimbi... Middle Men walipiga mabilioni!! Hicho ndicho kinazungumziwa!
Sasa kumaliza matatizo ya defaults za mikopo kipindi hiko yaani (kuanzia late 70-80’s) kwa kuelewa private banks ndio mzozo wa tatizo because they were unregulated and the cause of high debt. IMF na WD walishauri mikopo inayowezekana ifutwe waanze on clean slate kwa kuhakikisha wana regulate mikopo ya nchi maskini kwenda mbele to miniminise the risks of default.
Naona unahangaika kunielezea kuhusu Brady Bond ingawaje sio msingi wa mjadala huu!!! Narudia... suala la Brady Bond nimelisoma mara kadhaa! Sijaanza kulisoma jana wala juzi unlike wewe unaehangaika sasa kunipa historia inayofahamika nachumi yeyote yule!!
What you also need to know source ya IMF na WB capital ni hela ambazo zinatolewa na nchi tajiri kusaidia nchi maskini but only on specific social project na ndio mikopo yenye riba ndogo; also kuna hela za private banks ambazo zinariba kubwa kidogo.
Hapa naachana rasmi na wewe....

Mara kadhaa nimekuambia huna ufahamu na haya mambo, ndo maana mara kadhaa unaongea vitu vya ajabu, nikikukosoa, unaenda ku-Google na kurudi na hoja nyingine! Matokeo yake, tunafanya kazi ya kuzunguka kuzunguka tu mle mle!!

Kama umesahau, hiki ndicho uliongea:-
Besides if you do not know ata hela wanazotoa IMF na WD asilimia kubwa ni za private banks; sema zinakuwa channeled through them ili ku control mikopo ya nchi na kuminimise risk za default.
Huna cha kuniambia "if you don't know" wakati ni mwenyewe ndje hujui!!

Unajisahaulisha kwamba juzi tu hapa ulisemama the main source ya fedha za IMF ni:-
Besides if you do not know ata hela wanazotoa IMF na WD asilimia kubwa ni za private banks; sema zinakuwa channeled through them ili ku control mikopo ya nchi na kuminimise risk za default.
NIkakupinga, halafu unarudi kujifanya kunielimisha kwa kitu ambacho nilikuwa nakifahamu na ni wewe mwenyewe ndie ulkuwa hufahamu!!

Halafu narudia... mambo mengine unatakiwa kutumia akili!!!

Hivi unaamini kabisa IMF wana uwezo wa ku-control mikopo kulinganisha na private banks wenyewe?

Yaani IMF hawa hawa ambao kila siku wanadindishiwa na Wakopaji ndo wawe na uwezo wa kusimamia mikopo ya wengine wakati hata ya kwao wenyewe maji yakizidi unga, wanaamua kusamehe!!!

We all know dunianiani kuna multilateral agreements zinazolinda hizi private institutions, na serikali nyingi zimewahi kupelekwa MiGA! Umeshawahi kusikia kuna nchi imefikishwa MIGA na IMF?
 
Man,

Mimi sina matatizo na kukopa, nina matatizo na wale wanaoona fahari kukopa kwenye benki za kibiashara wakati kila mfuatiliaji wa haya mambo, anafahamu makali ya kukopa benki za kibiashara...

Na wanaonea fahari kukopa benki za kibiashara sio kwa sababu za kitaalamu, bali kwavile aliyekopa hiyo mipesa ni JPM, na kwao JPM IS ALWAYS RIGHT, basi hata kama alichokifanya kinaonekana wazi sio sawa, WAO WATATETEA TU...

Mchukulie huyo Kilatha, yaani bila aibu anafikia kusema:-

Hivi kuna mwenye akili timamu anayeweza kuamini porojo kama hizo?

Yaani Western Financial Institutions ziwe na imani zaidi na JPM ambae alikuwa wala hatabiriki kesho ataamuka na balaa gani, halafu wasimuamini Kijana Wao Mpendwa Benjamin Mkapa?!

Lakini kwanini kaongea hayo... kwa sababu tu hiyo mikopo imechukuliwa na "JPM" na yupo tyari kutetea na ku-justify lolote hata kama ni la kijinga!!
Look at you

Hivi unadhani private banks wanajikopeshea tu nchi za Africa au ata wachina tukienda kukopa.

Hujui ata misingi ya ring fence walizopewa DMO na analysis frameworks such as:

To name a few.

Kukusaidia tu personal nina ‘public finance’ module nzima mbele yangu endorsed by all international donors stakeholder IMF, WD and the rest na nishaisoma yote kitambo.

Not only does it contain the history of policy evolution bali ata complicated various ecomoic formulas and variants to use in computation; all of which I know. Thiugh the chances of evolving to such discussion were small with your understanding on the subject matter, ila tungefika huko utakutana na mziki mwingine kabisa sidhani kama midundo yake unaweza cheza.

So given any case study and the standard reasoning related to public finance norms I know what to google to get the right articles to answer any query of yours and dig even deeper to challenge you are understanding on the same issue.

On this Creddit Suisse saga (ndio maana nikakwambia unahitaji foundation of the discipline to argue).

Kwa sababu hujui ata tofauti ya varying government debts na shughuli za DMO kwa tafsiri za IMF and why wahusika wa huo ufisadi Mozambique officials thought it was import to bypass the international set firewall.

Like I told you public finance reasoning is based on social science and it is influenced by historical events leading to formulation of IMF/WB policies on risk assesments which every nation has to adhere too.

In addition to that kuelewa sababu za fines walizopewa hao watu nje ya box you need to have studied accountancy (aspects of auditing) na sheria zake kwa nchi husika ndio zilizotumika kuwaadhibu.

As far as national debt is concerned it is not a good idea to hide it from IMF and WB kwa sababu likija hadharani kuna consequences zake ata nchi za ulaya; just ask Greece bila EU na Angela Merkel mziki wao ungekuwa mwingine.

Eti $200 million kwa mujibu wako ilifutwa kupunguzwa interest ya deni; hivi interest inafutwa kwa kupunguza amount of loan au interest rate set; sasa huko sina files isipokuwa finance ni uwanja wangu nilikuacha kwa sababu ningesema nijibu kila upuuzi wako tungekesha.

Kilatha 👋 done with this thread.
 
Mzee wakati wa Mwendazake hiyo tovuti ya BoT si ilikuwepo, mbona hukuitumia na kuleta taarifa kama hizi? Nakumbuka kuna wakati gazeti lako lilisifiwa hadharani na JPM kwa kuibua uozo sijui bandarini ama wapi lakini hili ambalo unasema linatutoa utumbo hukulisema. Leo ndio umeliona, kweli ya Mungu mengi.
Mwendazake alisema anapenda umbeya sana kama alivyoupata wa bandai kupitia jamhuri
 
Back
Top Bottom