Pope
Senior Member
- Dec 3, 2007
- 117
- 0
Wakuu ni waandishi wengi sana walioandika this kind of articles na hapa JF tuwakatalia kata kata, SHY akiwa mmojawapo, na tuli-deal na context za article kwanza, as opposed na mwandishi,
Now this article inahusiana nini na Balile kumzunguka Mbowe? Maana kama ni taifa Lowassa alishatoka, sasa hiii article haiwezi kumsaidia anything na hapa JF tulishazikaataa this kind of articles na ndio maana hazijaja tena hapa.
Wakuu,
Nimeisoma ile makala ya mwisho Balille aliyoiandika kuaga Tanzania Daima, nimebaini yafuatayo.
1. Balile aliondoka Tanzania Daima baada ya kuafikiana na mwajiri wake, hivyo hakumzunguka au hakuchoropoka kuelekea huko aliko, hivyo hoja ya kuwa alimgeuka Mbowe kwa kuondoka Tanzania Daima ni dhaifu, labda kama kuna jingine.
2. Balile "hakuokotwa" na Mbowe na kuja kupewa uhariri mkuu kama walivyodai baadhi ya wachangiaji; alikuwa na mawasiliano na Mbowe na pia alimpa ushauri wa kitaalamu katika uanzishwaji wa gazeti hilo. Au labda amedanganya kwenye makala hiyo?
Sasa naomba kuuliza huu usaliti wake na hii habari inayomhusu yeye na Mengi na Rostam na Karamagi mbona siielewi maana yake? Nini kinachoendelea hapa?
Halafu hii habari ya kurekodiana kisirisiri, je ni sawa kisheria ikiwa unayem-rekodi hajui unafanya hivyo au bila ridhaa yake? Ikiwa madai yake aliyoyatoa hapo ni kweli sasa si usalama wake utazidi kuwa mdogo? Kama kuna kitu sielewi hebu niwekeni sawa wakulu!
Kiukweli jamani naungana na mimi kuuliza ni nini hasa tunapaswa kujadili hapa?
Kuikweli nilikuwa mpenzi wa Tanzania Daima kwani nilipenda kusoma upande wa pili wa shilingi na Tanzania Daima lilikuwa linatoa habari ambazo haziibebi serikali kwa upande wowote.
Huyu mtu aliamua kuacha kazi kwa makubaliano na Muajiri wake sasa tatizo hapo liko wapi? any way inaweza kuwa na tofauti kimtazamo lakini nafikiri "...MASUALA YA KAZI SI NDOA YA KIKRISTO AMBAYO INASEMA ALICHOKIUNGANISHA MUNGU BINADAMU ASIKITENGANISHE..."
Kuendelea kumjadili Balile ni kumjenga pasi na sababu!!
Balile msaliti kuondoka Tanzania Daima?
Waandishi ni kama wacheza mpira lilianzishwa Mwananchi walichukua kila mtu toka Majira hadi wapika chai akiwemo Balile leo uliza ni wangapi wamebaki huko mwananchi?
Kalamu ni silaha ukiitumia vizuri au vibaya unaweza kujenga au kubomoa.