Balile can you be trusted baada ya kumzunguka Mbowe ?

Folks please do not entertain this guy na mambo yake anapoteza mwlekeo wa mada kila mahali .Naomba turudi kumjua Balile ni mtu wa aina gani na madhara yake kwa jamii .

you should of be an example, mbona wewe unanientateini ? kama unadhani upo smart, ungeendelea tu na mada, na kunipuuzia ! mwishowe utaonekana wewe .........!!

The-Simpsons-Mr-Burns-Excel.jpg
 
Mtu anapouza uwezo wake wa kufikiri ni sawa na mtu anayeuza haki yake ya kuwa binadamu. Kama Balile anayoyafanya yanatokana na imani yake kuwa yuko upande sahihi basi ni vigumu sana kumuonesha kuwa amekosea. Lakini kama anachofanya anajua ni kutokana na pesa mfukoni basi ajue siyo tu anasaliti ukweli lakini anaisaliti dhamira yake.

Kwani, ukishajua ukweli hauna budi kuufuata popote utakapokupeleka.
 
.Naomba turudi kumjua Balile ni mtu wa aina gani na madhara yake kwa jamii .

Ninaomba kusema something here,

1. Balile alikuwa a very dear friend wa baadhi ya members hapa huko nyuma, sasa ninaomba wale waliokuwa karibu naye na kumsifia sana huko nyuma kwamba sasa watueleze kwanza exactly walikuwa na uhusiano wa aina gani na huyu Balile huko nyuma alipokuwa "safi", usafi wake ulikuwa nini?

2. Kama ninaelewa vizuri yanayosemwa sasa kuhusu huyu Balile, ni kwamba kuna usaliti ameufanya, ni upi huo? na amemfanyia nani? Je huo "usaliti" wake una madahara kwa taifa ambalo ndio hasa kama sikosei our reason for being here at JF?

Kwa wale mnaoelewa vizuri hii ishu hebu ikateni vizuri ili tuelewe exactly kinachosemwa aginst huyu Balile hapa ni nini maana wengine tusije fuata mkumbo tu bila kuelewa kinachoendelea, ukifuatia kwamba huyu mkuu alipomaliza shule huko UK, hapa JF tuli-dedicate a thread ya kumpongeza sana kuwa ni shujaaa wa taifa, what happened now?
 
Mtu anapouza uwezo wake wa kufikiri ni sawa na mtu anayeuza haki yake ya kuwa binadamu. Kama Balile anayoyafanya yanatokana na imani yake kuwa yuko upande sahihi basi ni vigumu sana kumuonesha kuwa amekosea. Lakini kama anachofanya anajua ni kutokana na pesa mfukoni basi ajue siyo tu anasaliti ukweli lakini anaisaliti dhamira yake.

Kwani, ukishajua ukweli hauna budi kuufuata popote utakapokupeleka.

Mzee ujumbe wako ni ushauri tosha ila inategemea jamaa na akili zake sasa .
 
Wakulu mimi ninasubiri majibu ya maswali yangu hapo juu, kabla sijamkoma nyani mchana saa hizi hizi kweupee on this ishu!

Otherwise, nitaiangalia kwa pembeni hii topic.
 
Wakulu mimi ninasubiri majibu ya maswali yangu hapo juu, kabla sijamkoma nyani mchana saa hizi hizi kweupee on this ishu!

Otherwise, nitaiangalia kwa pembeni hii topic.

Mkuu Es unaweza kuanza kusoma upya kuanzia mwanzo kuna mengi yamesemwa na utaelewa maana na mimi nimeanzia huko ndiyo nimefika .Kama kweli habari nzima ni ukwel hadi tukio la wiki moja nzima basi jamaa ni hatari kuliko Ukimwi na TB
 
Ninaomba kusema something here,

1. Balile alikuwa a very dear friend wa baadhi ya members hapa huko nyuma, sasa ninaomba wale waliokuwa karibu naye na kumsifia sana huko nyuma kwamba sasa watueleze kwanza exactly walikuwa na uhusiano wa aina gani na huyu Balile huko nyuma alipokuwa "safi", usafi wake ulikuwa nini?

2. Kama ninaelewa vizuri yanayosemwa sasa kuhusu huyu Balile, ni kwamba kuna usaliti ameufanya, ni upi huo? na amemfanyia nani? Je huo "usaliti" wake una madahara kwa taifa ambalo ndio hasa kama sikosei our reason for being here at JF?

Kwa wale mnaoelewa vizuri hii ishu hebu ikateni vizuri ili tuelewe exactly kinachosemwa aginst huyu Balile hapa ni nini maana wengine tusije fuata mkumbo tu bila kuelewa kinachoendelea, ukifuatia kwamba huyu mkuu alipomaliza shule huko UK, hapa JF tuli-dedicate a thread ya kumpongeza sana kuwa ni shujaaa wa taifa, what happened now?

nasubiri kusikia hayo majibu yao kwa hamu sana, na tutaweka tofauti kwa kulinganisha huo usafi waliouona kipindi kile hadi hivi sasa wanaposema jamaa ovyo,msaliti n.k !
 
Mkuu Es unaweza kuanza kusoma upya kuanzia mwanzo kuna mengi yamesemwa na utaelewa maana na mimi nimeanzia huko ndiyo nimefika .Kama kweli habari nzima ni ukwel hadi tukio la wiki moja nzima basi jamaa ni hatari kuliko Ukimwi na TB

Mkuu kwanza karibu sana maana ulikuwa "umepotea" sana na kwenye hili jina, mimi simtetei Balile, isipokuwa ninataka ukweli, wewe unajua kuwa nimeisoma hii topic toka mwanzo, ndio nikaishia kuuliza swali langu sasa either una majibu ya swali langu au huna, au?
 
Ninaomba kusema something here,

1. Balile alikuwa a very dear friend wa baadhi ya members hapa huko nyuma, sasa ninaomba wale waliokuwa karibu naye na kumsifia sana huko nyuma kwamba sasa watueleze kwanza exactly walikuwa na uhusiano wa aina gani na huyu Balile huko nyuma alipokuwa "safi", usafi wake ulikuwa nini?

Mzee hili umelirudia tena na mimi nilikuwa nasubiri majibu, lakini unaweza kutusaidia kwa kusema ni nani hawa "waliokuwa karibu" naye huko nyuma ili tuwaulize moja kwa moja.

2. Kama ninaelewa vizuri yanayosemwa sasa kuhusu huyu Balile, ni kwamba kuna usaliti ameufanya, ni upi huo? na amemfanyia nani? Je huo "usaliti" wake una madahara kwa taifa ambalo ndio hasa kama sikosei our reason for being here at JF?

Sijui kama ni usaliti au nini lakini inaonekana kuwa baada ya kupelekwa masomoni na mwajiri mmoja, aliporudi akatimkia kwenda kwa mwajiri mwingine. Sasa sijui kama kulikuwa na mkataba wa kumtaka akimaliza kusoma arudi kwa mwajiri wa awali au kama nafasi yake ya kwenda kusoma ilikuwa ni kitendo cha shukrani tu au vipi. So, na miye nasubiri jibu.


Kwa wale mnaoelewa vizuri hii ishu hebu ikateni vizuri ili tuelewe exactly kinachosemwa aginst huyu Balile hapa ni nini maana wengine tusije fuata mkumbo tu bila kuelewa kinachoendelea, ukifuatia kwamba huyu mkuu alipomaliza shule huko UK, hapa JF tuli-dedicate a thread ya kumpongeza sana kuwa ni shujaaa wa taifa, what happened now?

Well tusubiri lakini nadhani kuna taarifa tayari zimetolewa ya nini kinachozungumziwa..
 
Mtanzania Mbowe alimwajiri Balile kufanya kazi kwene gazeti lake .Mbowe hakuwahi kuingia news room na kusema andika haya ama acha haya .Hil hata leo Balile aje hapa aseme.Ubaya wa Mbowe na kwamba alimwamini sana huyu kijana na hata wajanja waliposema awe naye makini maana alianza kwenda kwenye mtandao na akawa anatumia gazeti lake kuwasemea wana mtandao bado aliamini kwamba ni uhuru wa habari lakini kumbe mwenzake alikuwa kwenye payroll.Now nimesema mengi kwmaba the guy sasa anafanya yale Rostam anayo yasema wazi wazi .Nataka ujue kwamba mimi niko kwenye fani tofauti ila namjua Balile na hata majuzi wana habari wenzake walimkimbia na haya ndiyo wanayo yasema ndiyo maana nikaona kwa kuwa nimeyapata basi nilete hapa na nyie myajue kwamba Balile ni hatari na ananuka .Kumbuka tena kwamba Mbowe na Tanzania Daima haliingilii hata sasa yeye anaamini katika uhuru wa kuandika habari na yeye anaamini katika pure business na wale alio waajiri.Sasa kweli mtu anaweza kukufanyia haya ? Ama ni imani ya na huruma ya kumpa kazi na kumpa Uhariri Mkuu kitu ambacho hata yeye alikuwa muoga sana lakini alipewa moyo na akawa hapo alipo ?

Mkuu so far hii inaweza kuwa at least a serious charge against Balile, sasa what this has to do na taifa? Kwangu inaonekana kama ni personal ishu ambayo sisi wananchi hatuielewi vizuri na ilipaswa kumaliziwa huko pembeni, kwa sababu haitugusi kwenye taifa, unless kuna something sielewi!
 
Nimesoma hii thread tangu mwanzo mpaka hapa. Sitaki kumlaumu mtu yeyote kutokana na yale yanayojadiliwa, lakini naomba kujulishwa kama ni jambo la busara kuanza kujadili WATU badala ya HOJA? Upo uwezekano mkubwa kuwa HOJA zinajengwa na WATU na kuwa matendo ya watu ndiyo yanayoathiri HOJA hizo. Lakini mwelekeo wa yanayojadiliwa inaonekana (kwa mtazamo wangu) kana kwamba anatafutwa Balile ajadiliwe kama Balile. Katika kufanya hivyo wapo waliojikuta wakichanganyana na kuanza kujadiliana wao (rejea majibishano ya watu kadhaa na Kada Mpinzani).
Huyo Balile kama amefanya hayo, ni vema lawama ijengwe juu yake kwa kuangalia jinsi matendo yake yalivyoathiri mustakabali wa maisha ya watu na hilo litatoa HOJA mbayo inaweza kuwa na mashiko. Naomba nieleweke kuwa sisemi kuwa kinachojadiliwa hakina msingi, sisipokuwa naona kuna hatari ya kuingiza mambo ambayo ni too personal na kuyafanya yachukue nafasi ya hoja nzito zinazopaswa kujadiliwa kwa kina.
 
Nimesoma hii thread tangu mwanzo mpaka hapa. Sitaki kumlaumu mtu yeyote kutokana na yale yanayojadiliwa, lakini naomba kujulishwa kama ni jambo la busara kuanza kujadili WATU badala ya HOJA? Upo uwezekano mkubwa kuwa HOJA zinajengwa na WATU na kuwa matendo ya watu ndiyo yanayoathiri HOJA hizo. Lakini mwelekeo wa yanayojadiliwa inaonekana (kwa mtazamo wangu) kana kwamba anatafutwa Balile ajadiliwe kama Balile. Katika kufanya hivyo wapo waliojikuta wakichanganyana na kuanza kujadiliana wao (rejea majibishano ya watu kadhaa na Kada Mpinzani).
Huyo Balile kama amefanya hayo, ni vema lawama ijengwe juu yake kwa kuangalia jinsi matendo yake yalivyoathiri mustakabali wa maisha ya watu na hilo litatoa HOJA mbayo inaweza kuwa na mashiko. Naomba nieleweke kuwa sisemi kuwa kinachojadiliwa hakina msingi, sisipokuwa naona kuna hatari ya kuingiza mambo ambayo ni too personal na kuyafanya yachukue nafasi ya hoja nzito zinazopaswa kujadiliwa kwa kina.

Shukrani kwa kuliona hili !
 
Nimesoma hii thread tangu mwanzo mpaka hapa. Sitaki kumlaumu mtu yeyote kutokana na yale yanayojadiliwa, lakini naomba kujulishwa kama ni jambo la busara kuanza kujadili WATU badala ya HOJA? Upo uwezekano mkubwa kuwa HOJA zinajengwa na WATU na kuwa matendo ya watu ndiyo yanayoathiri HOJA hizo. Lakini mwelekeo wa yanayojadiliwa inaonekana (kwa mtazamo wangu) kana kwamba anatafutwa Balile ajadiliwe kama Balile. Katika kufanya hivyo wapo waliojikuta wakichanganyana na kuanza kujadiliana wao (rejea majibishano ya watu kadhaa na Kada Mpinzani).
Huyo Balile kama amefanya hayo, ni vema lawama ijengwe juu yake kwa kuangalia jinsi matendo yake yalivyoathiri mustakabali wa maisha ya watu na hilo litatoa HOJA mbayo inaweza kuwa na mashiko. Naomba nieleweke kuwa sisemi kuwa kinachojadiliwa hakina msingi, sisipokuwa naona kuna hatari ya kuingiza mambo ambayo ni too personal na kuyafanya yachukue nafasi ya hoja nzito zinazopaswa kujadiliwa kwa kina.

Nothings is too or personal hapa . Jamaa anauliza kw atabia hizo can Balile be trusted ? Ndilo swali .Maana Balile ni mwandishi na sasa anatoa habari kwa Umma .Is the same Balile alikuwa AR kumsafisha Lowasa na sasa umeona alikuwa anasuka jungu kubwa dhidi ya Mengi , na hata kutaka kusema uongo kwamba Karamagi na Rostam wanamtishia maisha yake ili kujiosha na uozo unao liliwa hapa .Sumu ya uongo ikimwagwa na kuwaingia watu ina athari kubwa kwa Taifa .Jamaa anauliza can he be trusted kwa aina hii ya uandishi na tabia zake sasa ?Maana yeye akindia hasomi yeye na mkewe hapana .Tunasoma sote .
 
Kila la heri Tanzania Daima... (21/10/2007)

Deodatus Balile



LEO naandika makala hii nikiwa na siku chache kabla ya kurejea nchini Tanzania. Ninarejea baada ya kuhitimu masomo yangu ya shahada ya uzamili katika masuala ya uongozi wa biashara (MSc Business Management).

Najua matarajio ya wengi baada ya kuhitimu masomo katika ngazi hii, walitarajia nirejee nchini na kuendelea kufanya kazi na gazeti la Tanzania Daima.

Nimekuwa na Kampuni ya Free Media Limited kwa karibu miaka sita sasa. Mawasiliano yangu na mmiliki wa Kampuni ya Free Media Limited, Freeman Mbowe, juu ya kuanzishwa kwa chombo hiki cha habari yalianza katika vikao visivyo rasmi mwishoni mwa mwaka 2001.

Tangu wakati huo tuliendelea kuwa na mawasiliano ya karibu na nilimpa ushauri wa kitaalamu juu ya uanzishwaji wa vyombo vya habari.

Vikao viliendelea usiku na mchana na wakati mwingine tulifanya vikao kwa njia ya simu. Mwaka 2003 tulifikia uamuzi wa msingi wa kuanzisha gazeti la kila siku.

Tulichagua majina kadhaa ambapo karibu yote tulikuta yamesajiliwa tayari na tulijaribu kuwasiliana na mtu mmoja atuuzie jina tulilolipenda sana la Tanzania Yetu, lakini alitukatalia, hivyo ikabidi nifanye ukarabati wa wazo na kulisajili gazeti hili kama Tanzania Daima.

Hatua hii tuliifikia baada ya kuwa pia tumepitia mchakato wa majina mengi juu ya ni jina lipi ingepewa kampuni mama ya kuzalisha magazeti haya. Yupo rafiki yangu mmoja ambaye leo ni mwandamizi katika kampuni moja ya magazeti, wakati nikizungumza naye alinishauri tuchanganye jina la mmiliki na wazo la uhuru wa vyombo vya habari, hivyo kampuni hiyo tuiite; Free Media Limited. Nililikubali wazo hili na nikalipeleka kwa mmiliki ambaye naye alilikubali pia.

Harakati za usajili wa kampuni mama ziliendelea hadi Agosti, mwaka 2004, tulipofanikiwa kuisajili kampuni hiyo. Wakati huo kulikuwapo na mkanganyiko juu ya nini kingefanyika. Serikali kupitia bajeti yake ya Juni, 2004 ilikuwa imetangaza kufuta ada za leseni na mamlaka nyingi zilikuwa zimechanganyikiwa bila kujua ni leseni zipi zilistahili kufutiwa ada na zipi zilipishwe. Hata hivyo, sisi tuliamua tulipie leseni yetu kuepusha kuchelewa kwa majibu kutoka Hazina.

Mambo yalikwenda mpwito mpwito. Huku nikikimbizana na usajili, nilikuwa na mikutano na vikao visivyoisha na mmiliki wa kampuni hiyo, Mbowe, ambapo wakati mwingine tulilazimika kukaa ofisini hadi majogoo. Niliendelea na hatua za usajili wa gazeti kwa Msajili wa Magazeti, ambapo Septemba, 2004 nilifanikiwa kupata usajili wa gazeti la Tanzania Daima. Tuliweka lengo la kuanzishwa gazeti hili Oktoba, lakini kwa bahati mbaya au nzuri, ukarabati wa jengo ulikuwa haujakamilika, nami nikatapa safari ya kwenda Montreal, Canada, ambako nilikaa kwa wiki mbili.

Niliporejea nchini niliendeleza mawasiliano ya kina na waandishi na wahariri niliotarajia wangeungana nasi kuanzisha gazeti hili.

Wapo wengi walioonyesha nia lakini wakaishia njiani. Nitakuwa mtovu wa fadhila nikishindwa kuwataja kwa majina japo watendaji wakuu na nyadhifa zao kwenye mabano. Manyerere Jackton (Mhariri wa Habari), Deus Ngowi (Mhariri wa Makala), Eric Anthony (Mhariri wa Michezo), Ansbert Ngurumo (Mhariri Tanzania Daima Jumapili) na Joster Ramadhan (Naibu Mhariri wa Michezo).

Idara nyingine zilishikiliwa na watu muhimu kama Michael Budigila (Meneja Usambazaji), Twalib Mungulu (Meneja wa Matangazo), Ibony Maalim (Mshauri Graphics), hayati Pius Massawe (Meneja Msaidizi Usambazaji), Amour Nkrumah (Mkuu Kitengo cha Kompyuta), Said Salim (Msanifu), Godbless Naftari (Mhasibu) na dereva maarufu, Cyprian Mwigune.

Mimi nilibeba wadhifa wa Uhariri Mkuu, ambapo nilifanya kazi zote za utendaji katika kampuni.

Ndoto yetu ilitimia Desemba 1, 2004, lakini tumshukuru dada mmoja (jina linahifadhiwa), kwani kwa waliokuwapo wanakumbuka jinsi programu mpya ya Quark Express ilivyotutenda. Almanusra gazeti lisiende mitamboni kwani ilikuwa kila wataalamu wetu wakigusa kifungo hiki cha kompyuta mambo yanamwagika kama ubwabwa.

Dada huyu baada ya kumaliza kazi ofisini kwake, tulimwamsha kwa simu usiku wa manane. Ashukuriwe Ansbert Ngurumo, aliyekuwa na simu yake, vinginevyo historia hii isingeanzia hapo.

Baada ya hapo mambo yalikwenda mpwito mpwito na waliokuwa wakikataa kazi wakati tunaanzisha wakaanza kunipigia simu wenyewe wakiomba kazi kutokana na mafanikio makubwa liliyopata gazeti la Tanzania Daima katika kipindi kifupi kufikia Mei, mwaka 2005.

Hili lilitokana na ubunifu wa hali ya juu wa wahariri vijana waliokuwa wakibatizwa kila aina ya majina ikiwamo ‘chemical reaction’. Wachache waliokuwa wakituombea mabaya, utendaji wetu ukawafumba vinywa!

Nimeeleza utangulizi huu kwa nia ya kukufahamisha mpendwa msomaji wangu kuwa makala hii itakuwa ni makala yangu ya mwisho na ukomo wa utumishi wangu katika gazeti la Tanzania Daima na Kampuni ya Free Media Limited kwa ujumla wake.

Uamuzi huu nimeufikia baada ya maafikiano ya pande zote mbili; kwa nia njema, masilahi na usitawi wa pande zote (mutual benefit).

Sikustaafu kazi ya habari, na baada ya si muda mrefu nitakuwa tena katika uwanja wa habari, ila kwa sasa ni mapema mno kueleza nitafanya kazi ipi, lini na wapi. Kadiri na kwa uharaka wowote itakavyotokea, huko nitakakokuwa nikifanya kazi mpendwa msomaji wangu nitakujulisha niko wapi na nafanya nini.

Hata hivyo, napenda kuchukua fursa hii kukushukuru wewe msomaji wangu kwani umekuwa nguzo ya utendaji wa kampuni hii. Bila wewe kama mteja na kukubaliana na mawazo au habari tulizokuwa tukichapisha, basi gazeti hili lisingeweza kukua na kufikia hatua hii liliyopo.

Napenda kuchukua fursa hii pia kuwashukuru wafanyakazi wa Free Media Limited kwa kipindi cha karibu miaka minne tuliyofanya kazi wote. Nilishuhudia nidhamu, ubora, kujituma na moyo wa uzalendo wenye ncha kali kuliko mkuki. Haya yalinifariji sana na kufurahia kufanya kazi na timu hii.

Matokeo ya kujituma na ubunifu wetu, yameiwezesha Kampuni ya Free Media Limited kukua kwa haraka na kuvuna matunda kwa kupanuka.

Hili lilituwezesha kuanzisha gazeti la michezo la Sayari Februari 11, mwaka 2005 na baadaye wavuti wa Free Media Limited, www.freemedia.co.tz. Nikiwa hapa Uingereza kwa mwaka mzima na zaidi sasa, nimekuwa nikipokea sifa na pongezi nyingi kwa kazi hii. Nami nasema asanteni nyote.

Pia napenda kuushukuru uongozi wa Free Media Limited kwa kunipa nafasi ya kuongoza kampuni hii. Uzoefu nilioupata wa ndani na nje ya kazi umekuwa fundisho kubwa kwangu na pengine msingi wa utendaji huko niendako.

Natumaini nilijituma kwa kadiri ya uwezo wangu wote, na sikumwangusha mwekezaji katika kuhakikisha malengo tuliyoyaweka ya kulitumikia taifa kwa usawa kupitia chombo hiki bila ubaguzi wa rangi, dini, itikadi, wajihi, jinsia wala kabila, nililitimiza.

Ni matumaini yangu kuwa ndugu yangu Absalom Kibanda, kwa muda wa mwaka mmoja alioiendesha kampuni hii tayari anao uzoefu wa kutosha na nimtakie kila la heri katika kuendeleza mapambano haya.

Mwisho, wafanyakazi wenzangu nawahakikishia kuwa bado nawapenda kwa kiwango na moyo sawa na nilivyokuwa nanyi.

Mungu awabariki nyote na awajalie afya njema. Nasema, kila la heri Tanzania
Daima
 
Makala hii iliandikiwa MONDULI, ikiwa mwendelezo wa makala za 'kumsafisha' EL, na aliyeiandika aliituma Mtanzania, wakaitazama, wakaiogopa, ikapelekwa RAI mhariri akaikataa, ndipo ikaanza kuzunguka magazeti mengine, wahariri wakaigomea. Imekuwa kwenye mzunguko, hadi ikanifikia mimi, na haijahaririwa hata kidogo. Jisomee wenyewe (kwa maslahi ya taifa).

Tunamtosa Lowassa pasipo sababu?

na deodatus balile

KWA muda mrefu sasa sijaandika makala kuchambua au kuzungumzia lolote kati ya yaliyotokea katika Taifa letu yakatikisha misingi ya nchi. Yametokea masuala kadhaa ikiwamo ripoti ya Benki Kuu (BoT) juu ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ikaja Ripoti ya Richmond, iliyozaa msukosuko wa aina yake, hadi Waziri Mkuu wa Tisa wa Jamhuri yetu, Edward Lowassa, akajiuzulu.

Muda niliokaa kimya, umenipa fursa ya kutafakari nini kilikuwa kikiendelea katika Taifa letu. Wakati mwingine ni vyema kuwa mkimya na kutazama, hali inayokuweka kwenye nafasi nzuri ya kubaini pumba na mchele.

Sitalizungumzia hili la BoT. Ripoti ya BoT iliyowasilishwa serikalini na kutangazwa rasmi na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, siku ya Januari 9, 2008, ilinipasua mtima. Nasema sitaizungumzia kwa maana kila ninapoifikiria machozi hunilengalenga.

Wenye hizo kampuni 22 wamechota kadiri walivyoweza. Napenda kuamini kuwa katika hili hakuna ajali ya aina yoyote, bali ulikuwa mpango mkakati uliotekelezwa kisayansi. Wahusika wengi leo wamepumzika wanakula nchi, misukosuko yote imehamia Richmond!

Fukuto, upepo na hali ya hewa tayari imechafuka. Neno ufisadi sasa limekuwa kifungua kinywa, chakula cha mchana na kinywaji wakipendacho wengi. Ni msamiati unaokuwa kwa kasi kubwa. Huko mitaani leo imefikia hata mwenye kumiliki line mbili za simu anaitwa fisadi.

Rais Jakaya Kikwete wakati anazungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Februari hii, amefafanua kwa kirefu kashfa ya Richmond. Ameeleza kukerwa kwake, lakini kabla ya kuhitimisha akamtetea Lowassa. Akawaambia wazee wa Dar es Salaam kuwa yaliyomkumba Lowassa ni ajali ya kisiasa.

Hii ndiyo hoja ninayotaka kuijadili leo. Msemo kuwa "Baniani mbaya, lakini kiatu cheke dawa" au "mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni", ndiyo msingi wa mjadala wangu.

Nilitaka kumjadili aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Dk. Harrison Mwakyembe, lakini pengine kwa kukaa kimya nimepata fursa ya kumfahamu, naye akapata fursa ya kukarabati kauli yake.

Mwanzo Dk. Mwakyembe alisema Richmond ni kampuni ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa na swahiba wake, Rostam Aziz. Hapa ilikuwa wakati anawasilisha bungeni Ripoti ya Kamati Teule. Alisisitiza kuwa ilihitaji moyo wa uzalendo wa hali ya juu mtu kuwataja viongozi hawa wawili.

Hata hivyo, wakati anafanya majumuisho baada ya michango ya wabunge, Dk. Mwakyembe kidogo alibadilika. Tambo na mbwembwe japo hazikuisha, zilipungua. Kwa hakika alikarabati kauli yake na kusema kwamba hakuna popote katika ripoti hiyo wanapotajwa Lowassa na Rostam kuwa wamiliki wa Richmond.

Napenda kuamini kauli hii ya Mwakyembe aliyoitoa wakati wa majumuisho ndiyo yenye kushikamana. Kwa kwaida wakati tupo jeshini, tulikuwa tukiambiwa kuwa amri zote ni halali, ila askari anapaswa kutekeleza ya mwisho. Niazime busara hiyo, kukubaliana na kauli ya mwisho ya Dk. Mwakyembe juu ya umiliki wa Richmond.

Sasa sitajadili mkanganyiko uliotokea na kumfanya Balozi Fulgence Kazaura aikane Kamati kwa barua aliyodai kuwa hajapata kuwaeleza maneno yaliyomfanya Mwakembe na wajumbe wengine wa Kamati Teule waamini kuwa Richmond ilikuwa kampuni ya Lowassa na Rostam.

Nasema hili nalo silijadili tena, kwani Mwakyembe tayari amekwishaweka kumbukumbu sawa, ila jambo moja tu niliseme. Najiuliza na nadhani wapo wengi wenye kujiuliza juu ya mkanganyiko wa maadili, hasa unapokuja utendaji wa kamati hizi.
Kwamba nafahamu Dk. Mwakyembe ni mwanasheria aliyebobea na mwandishi mwandamizi, hapo ndipo nazidi kupata shida kidogo. Kaka yetu huyu amefundisha na anaendelea kufundisha Watanzania wengi wa rika mbalimbali.

Kwamba katika mafundisho yake amekuwa akisisitiza suala la kuaminiana na kulinda vyanzo (confidentiality and anonymity). Na kwamba Daktari huyu wa sheria anajua kuwa maneno ya mitaani wengine wanapenda kuyaita "ushu ushu" (hearsays), kamwe hayawezi kusimama kama ushahidi mbele ya sheria.

Daktari wetu huyu ameamua kutunga kanuni mpya za uandishi na ushahidi mahakamani. Kwamba anonymity and confidentiality, kwake si muhimu tena na wala havina madhara kwa Kamati Teule nyingine zijazo, ikiwa ilitokea kwamba kweli aliumwa sikio. Kazaura tayari amekana kumuuma sikio, ila hili halijibiki.

Kwake daktari huyu, maneno ya mitaani anayoyaitwa kuumwa sikio, yana nguvu kuliko ushahidi wa kiapo! Namheshimu sana daktari huyu, na wala hapa simsimangi, ila najaribu kufikisha fikra zangu kwako wewe msomaji juu ya falsafa hii mpya.

Jingine ninalodhani halihitaji ujasiri kulisema ni hili la kutompa fursa ya kumhoji Waziri Mkuu, aliyejiuzulu ndugu Lowassa. Kwa hulka ya ubinadamu ni rahisi wajumbe wa kamati kujitetea, lakini hapo ndipo umimi (egoism) unathibitika.

Iwapo ningeazima maneno ya Biblia Takatifu, inasema mtende mwenzio sawa na utakavyo utendewe wewe. Na Biblia inasema kipimo hicho hicho ukitumiacho kumpimia mwenzio, ndicho kitakachotumika kukupimia haki yako mbele ya safari.

Hili nalo sipendi kulisemea sana kwani Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amelisemea vizuri. Hoja iliyotumiwa Kamati Teule kuwa ukubwa wa cheo cha Waziri Mkuu uliwazuia kumhoji Lowassa inaacha maswali mengi.

Jaji Warioba anasema yeye akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, aliwahi kuhojiwa. Alikwenda mbali zaidi akafafanua kuwa hata Ali Hassan Mwinyi, alipata kuhojiwa akiwa Rais.

Hapa ndipo pa kujiuliza. Ilikuwaje Kamati hii haikupata kumbukumbu hizi nyeti na kubaini kuwa kumuhoji Waziri Mkuu si jambo geni kwa Tanzania? Wapo wanaosema Kamati hii ilikuwa na ajenda ya siri, ila binafsi sipendi kuamini hivyo.

Nimesema tangu mwanzo kuwa masuala haya yamejadiliwa kwa kina na wadau mbalimbali. Ifahamike wazi kuwa simtetei Lowassa, Rostam wala Dk. Mwakyembe katika hili, ila nasimamia msingi wa hoja. Najiuliza nani msaliti kati ya Lowassa na hao waliomtenda au kutenda yaliyomfikisha alipo leo.

Hapo juu nilisema Rais Kikwete amesema yaliyompata Lowassa ni ajali ya kisiasa. Maneno ya Rais Kikwete, yanakwenda sambamba hoja ya Dk. Ibrahim Msabaha, japo ilipuuzwa na Dk. Mwakyembe. Msabaha alisema haya yamekwishatokea, lakini Bunge lijadili mwelekeo na hatima ya taifa siku za usoni, hasa yanapopaswa kufanywa maamuzi kwenye kipindi cha dharura.

Hoja hii wapo wenye kusema inaweza kushughulikiwa kwa kutumia utaratibu wa international shopping sawa na lilivyopendekeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakati wa mchakato. Nasema hilo linawezekana, lakini kuna kila sababu ya kufikiria kuwa na utaratibu wa wazi jinsi ya kutatua matatizo ya kitaifa wakati wa dharura.

Ni kiongozi wa ajabu pekee, ambaye angeweza kukaa kimya kutokana na hali ya umeme ilipokuwa imefikia. Sheria ya manunuzi inataka siku 45 za kuitisha zabuni, ikiwa na maana kuwa zilihitajika siku 45 za kuitisha zabuni, huku taifa likizidi kutumbukia gizani. Narudia, siwatetei Richmond katika hili wala yeyote awaye, ninachojadili ni hoja ya utaratibu wa kutumika wakati wa dharura utakaokubalika kwa jamii yote ya Watanzania pasipo mikwaruzano.

Najua nitaandika makala kadhaa kuhusiana na mada hii, ila leo nataka nijikite katika Lowassa ni mtu wa aina gani. Lowassa huyu huyu tuliyemshangilia kama mkombozi, leo ndiye tunampiga mawe na kupendekeza asulubiwe.

Kama si Lowassa, viwanja vya Mnazi Mmoja vingekuwa maghorofa ya akina Baghdad. Tunajua Lowassa alivyosimama kidete bungeni mwaka 1994, na kuamuru uzio wa mabati uvunjwe uliokuwa umezungushiwa viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam. Lowassa huyu huyu alifuta umiliki wa viwanja vya tajiri mmoja anayetamba sana jijini Dar es Salaam, ambapo leo ndipo yamejengwa majengo ya PPF, International House na majengo mengine kadhaa.

Lowassa huyu huyu aliwafukuza nchini kampuni ya City Water mwaka 2005 waliposhindwa kutimiza masharti yaliyokuwamo kwenye mkataba. City Water walikwenda mahakamani, lakini hasilani hawakushinda kesi. Wakatakiwa kuilipa Serikali ya Tanzania sh bilioni 15.

Ni Lowassa huyu huyu aliyesimamia ujenzi wa shule za sekondari za kata. Hoja kwamba hazina walimu ni sahihi, lakini lipo swali la kujiuliza. Hivi kipi bora, kutokuwa na vyote viwili; shule na walimu au kuanza na kimoja.

Wapo wenye hoja sahihi kabisa kuwa Serikali ingeanza na kufundisha walimu kabla ya kujenga shule, lakini walimu hawa hawa iwapo wangehitimu na kukosa ajira, hoja hii hii ingegeuzwa na kudaiwa kuwa Serikali ilipaswa kujenga shule kwanza kabla ya kufundisha walimu. Kwamba shule zinapokuwapo, kasi ya mahitaji ya walimu inakuwa na mashiko (real) badala ya dhahania (imaginary). Hakuna safari isiyokuwa na hatua ya mwanzo.

Ni Lowassa huyu huyu aliyesimamia chakula cha njaa kikasambazwa kila tarafa, kata hadi kijiji. Ni Lowassa huyu huyu aliyepunguzaji foleni jijini Dar es Salaam kwa utaratibu wa njia tatu. Kwamba leo karibu barabara zote za jiji la Dar es Salaam zinapanuliwa kwa maelekezo yake.

Nimetangulia kusema kuwa kwa kipindi kirefu sikuweza kuandika makala yoyote kutokana na mazingira iliyowasilishiwa Ripoti ya Richmond.

Kwamba mwanzo Dk. Mwakyembe aliamua kuwaeleza Watanzania kuwa Lowassa ni fisadi, lakini wakati wa majumuisho akakarabati kauli yake. Hili la kukarabati kauli yake ndilo limeanza kunifunua macho. Nikaanza kujiuliza maswali mengi.

Nikajiuliza Dk. Mwakyembe alishindwa nini kutoa ufafanuzi huu kwamba Lowassa habanwi kwa ufisadi bali kwa uwajibikaji wa pamoja kama msimamizi mkuu wa shughuli za serikali, hasa pale Lowassa alipojieleza na kufafanua alivyoonewa.

Mbona mmoja wa wajumbe wa Kamati, Lucas Selelii alisimama na kusahihisha aliyoamini kuwa Lowassa aliyapotosha katika hotuba yake fupi ya kujiuzulu? Dk. Mwakyembe alipobaini kuwa Lowassa alikuwa hajaisoma vyema ripoti hiyo kwa nini hakusimama kuweka kumbukumbu sawa kuwa hahusiki katika ufisadi bali kushindwa kusimamia watendaji wake?

Kwamba Dk. Mwakyembe akiyajua hayo, akakaa kimya kwa siku nne mfululizo wabunge nao wakajadili hoja iliyopotoshwa, Dk. Mwakyembe akijua kuwa wanajenga hoja katika dhana isiyo sahihi, hadi watu wanapendekeza Lowassa anyongwe, afilisiwe na matusi ya kila aina!

Mwakyembe alishindwa nini kusimama katikati ya mjadala na kuomba mwongozo wa Spika akafafanua hayo aliyoyasema kwenye majumuisho ya hoja, kwa nia ya kuepusha wabunge wasijadili hoja isiyo sahihi? Hapa kuna namna.

Lowassa ameonyesha uungwana wa hali ya juu. Yeye ameamua kujiuzulu wadhifa aliokuwanao. Hata hivyo, siamini kama atakubali kufa kibudu. Ingawa jamii imekwishaamini hayo yaliyosemwa juu yake, bado anayo fursa.

Anaweza kusimama akaueleza umma yaliyojiri kwa nia ya kuweka kumbukumbu sawa. Ni katika hatua hii najiuliza nani msaliti. Najiuliza iwapo Lowassa ni msaliti au kasalitiwa?

Nimalizie makala hii, kwa kachavusha fikra zetu. Rais Kikwete amesema yaliyomkuba Lowassa ni ajali ya kisiasa. Naamini Lowassa alipokuwa akifanya maamuzi mengi kati ya niliyoyataja hapo juu, tulimshangilia na kumsifia kama kiongozi shupavu.

Najua fika Tanzania ina kiu ya viongozi wenye kuthubutu. Viongozi wanaoweza kufikiri na wakatenda bila hofu.

Lowassa ni mmoja wao. Siwezi kumsemea, natumaini yeye anayo maelezo mazuri katika hili, ila kuna kila dalili kuwa hakutendewa haki hata kabla ya Kamati Teule kuundwa. Swali ni je, utamaduni huu wa kumalizana unatupeleka wapi?

deobalile@yahoo.com
0713404827
 
Wakuu ni waandishi wengi sana walioandika this kind of articles na hapa JF tuwakatalia kata kata, SHY akiwa mmojawapo, na tuli-deal na context za article kwanza, as opposed na mwandishi,

Now this article inahusiana nini na Balile kumzunguka Mbowe? Maana kama ni taifa Lowassa alishatoka, sasa hiii article haiwezi kumsaidia anything na hapa JF tulishazikaataa this kind of articles na ndio maana hazijaja tena hapa.
 
Wakuu ni waandishi wengi sana walioandika this kind of articles na hapa JF tuwakatalia kata kata, SHY akiwa mmojawapo, na tuli-deal na context za article kwanza, as opposed na mwandishi,

Now this article inahusiana nini na Balile kumzunguka Mbowe? Maana kama ni taifa Lowassa alishatoka, sasa hiii article haiwezi kumsaidia anything na hapa JF tulishazikaataa this kind of articles na ndio maana hazijaja tena hapa.
Mkuu FMES,

Hiyo Richmond sasa ni vita kati ya makundi ya CCM, hata mimi najiuliza Mbowe hapa kasalitiwa vipi?

Kwahiyo waandishi, wanasiasa, wana JF ambao tunatofautiana juu ya suala la Richmond lilivyoamuliwa bungeni, basi na sisi tunahusika katika kumsaliti Mbowe.

Huyu Balile, CHADEMA na Mbowe wamekula naye, wakafundisha uandishe wa kisiasa, sasa the chickens are coming home to roost, wanaanza kupiga kelele.

Wacha sisi wengine tufaidi, si Wahenga walisema, mkuki kwa Nguruwe, kwa binadamu mchungu? Dawa ni kutokutumia mkuki kabisa, vinginevyo unaweza kukuchoma hata kwa bahati mbaya.
 
Wakuu,
Nimeisoma ile makala ya mwisho Balille aliyoiandika kuaga Tanzania Daima, nimebaini yafuatayo.

1. Balile aliondoka Tanzania Daima baada ya kuafikiana na mwajiri wake, hivyo hakumzunguka au hakuchoropoka kuelekea huko aliko, hivyo hoja ya kuwa alimgeuka Mbowe kwa kuondoka Tanzania Daima ni dhaifu, labda kama kuna jingine.

2. Balile "hakuokotwa" na Mbowe na kuja kupewa uhariri mkuu kama walivyodai baadhi ya wachangiaji; alikuwa na mawasiliano na Mbowe na pia alimpa ushauri wa kitaalamu katika uanzishwaji wa gazeti hilo. Au labda amedanganya kwenye makala hiyo?

Sasa naomba kuuliza huu usaliti wake na hii habari inayomhusu yeye na Mengi na Rostam na Karamagi mbona siielewi maana yake? Nini kinachoendelea hapa?

Halafu hii habari ya kurekodiana kisirisiri, je ni sawa kisheria ikiwa unayem-rekodi hajui unafanya hivyo au bila ridhaa yake? Ikiwa madai yake aliyoyatoa hapo ni kweli sasa si usalama wake utazidi kuwa mdogo? Kama kuna kitu sielewi hebu niwekeni sawa wakulu!
 
Hivi suluhisho la matatizo ya nchi hii ni kuchagua rais toka vyama vya upinzani au ni mfumo mzima wa uendeshaji wa serikali yenyewe? Tunajuaje kwamba rais toka upinzaia hataweka mafisadi kwenye serikali yake?

Tuangalie kiini cha tatizo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom