Balalli alikuwa shahidi ama mtuhumiwa?

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
26,331
25,236
Nachukua fursa hii kutoa tena changamoto kwa serikali yetu kuhusiana na hii Saga ya EPA.

Wote sasa tunakubaliana kuwa Marehemu Ballali alikuwa ni either shahidi ama mtuhumiwa kwenye shauri hili la EPA.

Wote pia tunatambua kuwa serikali imeshawahi kutoa kauli mbali mbali pale walipokuwa wakibanwa kuhusiana na uhusikaji wa Ballali kama kinara wa Scandal hii ya kiharamia.

Hivyo basi...Kabla sijaanza kuzitaja kauli zote za serikali kuhusiana na maswali ya ni kwanini Ballali hakuhojiwa wala kukamatwa..Naishauri serikali itoe tamko lake kama Ballali alikuwa ni shahidi ama mtuhumiwa.

Na kama bado inaamini kuwa hakuwa mtuhumiwa wala shahidi then tunahitaji paper trail yote ili tujue nani alipiga signature na kwanini!
Baada ya hapo then tunataka kujua ni kivipi kesi hii itaendelea bila ya ushahidi wake kuwepo ama kama ushahidi wake ulishachukuliwa na tume ya uchunguzi.

Vyovyote vile ni muhimu kwa serikali kutoa Tamko rasmi hili tuweze kuendelea mbele na shauri ili ambalo kama serikali isipokuwa makini then kushikilia kwao upande wa makali huku wakiendelea kuwa wabishi kutawa cost more than it already has.
 
Silva alisema ballali ni huru na wala serikali haina shida naye (kabla hajafariki)

Tunataka tamko lao jipya ili tujue moja!
Kwasababu si walisema kama akihitajika?
Sasa keshakufa..Tunataka watuambie kama wameshagundua kuwa alikuwa akihitajika ama bado wanaamini kuwa ushahidi wake hautakaa uhitajike.
 
Kauli za serikali kuhusiana na EPA VS Ballali:

1)haitajiki..Tukimuhitaji tutampata.
2)Tunajua aliko.
3)Hatujui aliko
4)Tunamtafuta.
5)Ni mgonjwa.
6)Ana afya..Ni mzima.
7)Ni mgonjwa..amelazwa
8)Tumetuma maofisa 7 kumtafuta washington na Boston.
9)Ni huru.
10)Si shahidi
11)Si mtuhumiwa.

NB:Mustafa Mkullo.."Nilienda Washington nikamtafuta sikumpata"
Mh J.Kikwete.."Kifo cha Ballali ni mapenzi ya Mungu"

Ni wakati wa serikali kutoa tamko lao wakati huu ili sisi wananchi tujue moja.

Ni muhimu sana kwa serikali kufanya hivyo kwasababu sasa Ballali ameshakufa na kuna minon'gono kuwa ni serikali yenyewe imeamua kumwua Ballali ili asitajwe tena kwenye kesi ya EPA wala ushahidi wake usitumike.

Na ili pia tukubali kuwa kifo chake ni mapenzi ya Mungu kama vile Mh rais anavyotaka tuamini..

Then maswali ya wananchi kuhusiana na kuhusika ama kutohuisika kwa Ballali yajibiwe ili tuweze kujua mustakabali wa shauri hili tata la EPA.

Tunajua pia kuwa Mh Rais alisema kuwa kamati haiwezi kutaja siri nyingine ili kuepusha uchunguzi usiharibike..Lakini ni wazi kuwa kutaja mashahidi ama watuhumiwa hakuharibu ushahidi bali kutaja waliyosema ndio kunaweza kuwa matatizo.

Serikali haijawahi kusema kama Ballali ni shahidi ama mtuhumiwa na sikumbuki kama wameshawahi kuwataja watuhumiwa ama mashahidi!

Kuwataja watuhumiwa ama mashahidi ni haki ya Mtanzania na serikali inawezekana iliwahoji kina Ballali na wenzake kwa kigezo kile walichokitumia kuwa wananchi wapeleke taarifa.

Serikali pia inaweza kudai kuwa kamati ilikuwa ni ya uchunguzi tu na mshahidi na watuhumiwa watatajwa mara baada ya kesi kufunguliwa rasmi mahakamani! Kwangu madai hayo yatashinikiza fikra kuwa serikali imefanya usanii kwa watanzania!

Ni wazi serikali inaweza kusema kuwa Ballali kama raia wengine naye alipeleka taarifa zake kwa kamati hiyo ya rais.

Na kama imefanya hivyo..Then tunaomba ripoti ili tuweze kujua kuwa nani alikuwa kama shahidi na nani kama mtuhumiwa,pia ni kesi gani watakayoifungua dhidi ya hao watuhumiwa ambao bado haijaamua kuwatangaza licha ya kwamba Dk Slaa alikwisha fanya hivyo pale mwembe Yanga.
 
what if ukijibiwa balali hakuwa shahidi wala mtuhumiwa utafanyaje? wanaweza kukujibu hivi, balali was a nuisance.....and they are happy he is gone
 
what if ukijibiwa balali hakuwa shahidi wala mtuhumiwa utafanyaje? wanaweza kukujibu hivi, balali was a nuisance.....and they are happy he is gone

Wakisema siyo shahidi wala mtuhumiwa then tunataka ripoti zote za Audit,pamoja na hiyo ya kamati ya EPA aliyoiunda Mh Rais.

Tukishaona ripoti zote hizo then tutajua kama tukubaline na serikali,wewe,na MKJJ... Kuwa Ballali hakuwa shahidi wala mtuhumiwa kwenye ujambazi aliousimamia wakati akiwa Kiongozi mkuu wa BOT.
 
Haya...Hii imeshakuwa hoja ya mchanganyiko kwasababu kuna watu walikuwa wakiamini Ballali apewe kinga badala ya kukamatwa!
HIVI KWELI HOJA KUWA BALLALI ALITAKIWA AWE SHAHIDI AMA MTUHUMIWA ISHAKUWA HOJA BINAFSI YA JMUSHI?
 
Ndugu zangu kama kuna watu ambao hawataki Ballali awe branded kama mtu aliyekuwa akihitajika ama kama shahidi ama mtuhumiwa then wana lao jambo!
Juhudi tunazofanya ni kuhakikisha imani ya wananchi haipotei hapa JF.
 
jamani msimamo wa watz walio wengi (ukiondoa mafisadi wa size zote) ni kua apatikanapo mtu na makosa ya kifisadi asulubiwe!!!!!!! pia wafilisiwe jamani kama ametangulia mbele ya haki je akipatikana na hataia afilisiswe au ndo ushahidi umeenda na maji??????????????? nielimisheni jamani.
 
Hapo jmushi maswali meeeeeeeeeengi lakini yanakosa majibu.......subilini report ya fisadi Mwanyika na Mwema ndio tutajua kama alikuwa shahidi au mtuhumiwa kwani hapo tutajadili kisha tutakosa majibu...alafu tusubili dada zake watue bongo watuambie wosia alio acha marehemu labda Mkono atakuwa anajua nasikia alikuwa kule....
 
Hakuna tena muda mwingi wa kusubiri kwasababu hicho ndicho Serikali wanachokitaka ili kesi ijifie yenyewe!

Ripoti ni lazima itoke ili tujue hao mashahidi na watuhumiwa ambao ni wengine zaidi ya Ballali na wengineo waliotajwa kwenye LIST OF SHAME!

Watanzania hii ndiyo nafasi tuliyonayo ya kuibana serikali!
Kwasababu ndugu zangu..Kama serikali ikiendelea na msimamo wake kuwa Ballali hakuwa mtuhumiwa wala shahidi...Then msahau kuhusu haki kutendeka!

NB:Kumbuka serikali ilisema kuwa Ballali sio mtuhumiwa wala shahidi na kuwa hawajamuhoji..Ila watamuhoji kama wakimhitaji!

Mara ya mwisho kwa serikali kumuhitaji Ballali ni pale walipowatuma wale maofisa saba marekani!
Lakini hatujui kama walimkuta akiwa mzima ama la kwasababu mara baada ya wao kufika hapa ndio ghafla tukasikia kuwa Ballali amekufa!
Hivyo ni lazima uelewe hapa kuwa kuna michezo michafu ya pande mbili ambazo ama zikiwa na nia moja..Ama zikiwa ninapigana...Sisi tuko hapa kuhakikisha kuwa pande hizo mbili zinazopigana ama kuwa na nia moja hazipelekei mwisho mbaya wa kukosa haki kwa mtanzania.
 
what if ukijibiwa balali hakuwa shahidi wala mtuhumiwa utafanyaje? wanaweza kukujibu hivi, balali was a nuisance.....and they are happy he is gone

Well katika hili na Marehemu Balali ni kwamba alikuwa ni mtuhumiwa ambaye serikali iliamua kumuweka juu ya sheria!!! Na kwa sasa hivi nina uhakika wanasheherekea kwa kusema "Good Riddance."

Huyu alikuwa ni Mtuhumiwa namba moja katika Sakata Zima! Nasikitika kwa nini amekufa kabla ya hii kashfa haijamaliza kuchunguzwa!!!

Sasa utaona ambavyo tume ya EPA itafanya kazi kwa kasi ya ajabu!
 
Nina hamu sana ya kuiona hiyo ripoti ili nijue kama watuhumiwa na mashahidi walikuwa ni kina nani na kama walihojiwa ama la.
 
Jmushi
Haya yako ndiyo maswali ya watu wote. Mimi huku Tanganyika niliko nakuambia kila kona watu wanaulizana maswali haya haya. Na kwa kweli si uongo nimesikia hata wana chukua chako mapema wakiguna kuhusu kifo cha huyu bwana na pesa zetu zitakavyopotea. Halafu si unajua siku za kukabidhi ripoti yenyewe hiyo ni wiki chache tu zijazo? Utasikia mwenyewe jinsi watakavyojiuma jiuma. Lakini hata hivyo waelewe hailiwi pesa ya mtu hapa. Tutabanana nao mpaka kieleweke.
 
Nashukuru mkuu kwa kunieleza hali halisi ya huko!
Na mimi nafurahi kwasababu ninaamini kwamba jitihada zetu si za bure...Na pia Taifa letu linahitaji watu wa kujitolea.
 
Back
Top Bottom