Balali's death: MCHANGA WA MACHO?

Kidzogolae

Senior Member
Apr 20, 2008
133
2
Jamanie, hivi ni kweli kuwa yule muhehe Balali kafariki? Kusema kweli, kama amefariki, mimi nawapa pole sana wanandugu wake. kwasababu anaweza kuwa alitumika kama chambo tu kwa mafisadi walio na madaraka kuliko yeye, akajikuta na yeye analazimika kufanya mambo ya kifisadi kwasababu system iliyoko juu yake inataka hivyo.eg.fedha za kampeni etc.

Lakini, kwa ninyi wenzangu ambao mko US kwasasa, naombeni jamani, tena naombeni. kama ikiwezekana, mtu akipata walau picha ya maiti yake moja tu, mimi ningejitahidi hata kuinunua. hapo ndo ningeamini kama kweli amekufa. lakini kama hatutaona picha za maiti yake, ambayo nasikia wataichoma moto kama baniani/yaani wataibanika hadi awe majivu wamuweke kwenye kiberiti(sina uhakika hapa lakini, ila nimesikia tu watu wanasema hivyo, pamoja na kwamba yeye sio baniani, naamini watamzika kama kawaida tu), ingekuwa vizuri sana kama tukiona maiti yake. isije ikawa mchanga wa macho tu, selikali inataka kuzima ushahidi wa mambo mengi, kumbe yeye anaendelea kupeta tu huko Majuu ili soo lizime. hii inawezekana kwasababu, hii soo kwa kikwete ni mziki mzito sana kuutatua. na anatakiwa kusacrifice makambare mengi sana kwa kufumba macho bila huruma wala kuwaangalia usoni. hivyo, kwa mtu mwenye ushahidi wa mdomo kama balali, asije kuwa amefichwa tu tukaamini kuwa amekufa kumbe yu hai. Naomba selikali ituonyeshe na iingilie kati.

Kwanini familia yake US haitaki hata watz kuhudhuria maziko yake? kunani pale? kwanini mtz ambaye anao uwezo wa kusafirisha maiti hadi hapa tz anazikwa US kitu ambacho sio kawaida ya wabongo?kunani pale? mimi siamini kama huyu jamaa amefariki kweli. kama kuna mtu mwenye ushahidi mzuri zaidi ya huo wa selikali, naomba aprove. asanteni wana JF.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom