Gavana wa zamani wa Bank Kuu ya Tanzania ametuwa juzi, kinyemela. Inasemekana baada ya hali yake kuwa nafuu kidogo, Balali amerudi mara moja kutoa "taarifa muhimu" kama alivyodai mwenyewe alipoongea na watu wa karibu waliokuwa naye jana jioni na kwamba hataki kuonekana kwenye jamii ingawa amekubali kufanya mahojiano kwa masharti ya kurushwa hewani baada ya yeye kuishia kusikojulikana tena.
Balali ambaye alionekana mdhoofu na kutokuwa na mengi amesema atatoa vielelezo vyake vyote na hataacha kitu ingawa wasi wasi wake ni kwamba akisema yote anayoyafahamu basi taifa linaweza kulazimika kufanya uchaguzi mkuu upya. Inaelekea Balali amejifunza mbinu za kutoa taarifa kwa style ya Osama.
Tutawaletea habari zaidi leo jioni baada ya "mheshimiwa" huyo kukutana na vyanzo vyetu kwa maelezo zaidi.