Balali Atoweka

Tatizo la viongozi wetu ni kutaka kucoment katika kila kitu anachoulizwa hata kama hana data, na hii inadhibitisha kuwa ndani ya serikali ya JK na CCM hakuna msimamo mmoja kuhusiana na maswala mbalimbali yanayo affect jamii yetu, kila mtu anaongea kulingana na anavyoona inafaa.

Inawezekana hili swala halikuwahi hata kuongelewa kwenye kikao cha baraza la mawaziri, ndo maana hakuna msimamo mmoja. Hii ni sawa na swala la Mh. Shemhuna (samahani kama nimekosea) kuropoka kuwa hakutakuwa na serikali ya mseto halafu kesho yake katibu mwenezi wa CCM anakanusha kuwa yule ameongea kwa niaba yake, mbona hakutaja kuwa yale yalikuwa maoni yake na si ya CCM, Mbona Mkullo na yeye ametumia statement za kuonyesha kuwa anawakilisha serikali.

Mh. Mkullo umejidhalilisha sana hata kabla ya Ikulu kubrand maneno yale kama mawazo yako, wewe ni nani mpaka umtafute Balali, au kuwa waziri wa fedha unakuwa polisi pia, usifanye watu wakaanza kutilia mashaka CV yako kwa maneno madogo ambayo ungeweza kusema no comment.
 
Jana Nimejiuliza sana,Hivi Mkurugenzi wa mawasillianao anaitisha Press Conference ya kuongelea masuala mazito kama hayo .Yeye ni kama nani?

Huu uzandiki na 'uhuni',Rais alimfukuza kazi Balali kutokana la ubadhirifu(kwa maana yao),then leo aje atokee mfanyakazi wa ikulu asme kwamba Balali yuko huru.

Tatizo sio balali tatizo ni pesa zetu,kama liiba azirudishe,na aseme ni nani anazo
 
Jana Nimejiuliza sana,Hivi Mkurugenzi wa mawasillianao anaitisha Press Conference ya kuongelea masuala mazito kama hayo .Yeye ni kama nani?

Huu uzandiki na 'uhuni',Rais alimfukuza kazi Balali kutokana la ubadhirifu(kwa maana yao),then leo aje atokee mfanyakazi wa ikulu asme kwamba Balali yuko huru.

Tatizo sio balali tatizo ni pesa zetu,kama liiba azirudishe,na aseme ni nani anazo

Kaka sheria za tanzania ni kwa ajiri ya wanyonge na sio kwa watu wote, wale watu wa EPA waliforge documents wakaiba pesa lakini mlala hoi akiforge kidogo anakamatwa siku hiyohiyo na kuwekwa gerezani wakati hawa wanambembelezwa, na hakuna hata mmoja atakaekwenda gerezani kwani wao sio watu wa magereza.
 
Jana Nimejiuliza sana,Hivi Mkurugenzi wa mawasillianao anaitisha Press Conference ya kuongelea masuala mazito kama hayo .Yeye ni kama nani?

Huu uzandiki na 'uhuni',Rais alimfukuza kazi Balali kutokana la ubadhirifu(kwa maana yao),then leo aje atokee mfanyakazi wa ikulu asme kwamba Balali yuko huru.

Tatizo sio balali tatizo ni pesa zetu,kama liiba azirudishe,na aseme ni nani anazo

watamuachiaje awe huru kama wameshakubali kuwa wamemfukuza kwa ubadhilifu
 
Balali kusakwa

2008-05-09 09:07:43
Na Mashaka Mgeta


Serikali imesema itamsaka Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Balali mahali popote alipo muda utakapowadia.

Kwa mujibu wa ofisi ya Rais, mbali na Dk. Balali, aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Bw. Andrew Chenge, `amewekwa kiporo` ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili kufanyika, na hatimaye kuchukuliwa hatua kulingana na matokeo yatakayopatikana.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Bw. Salva Rweyemamu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Ikulu, jijini Dar es Salaam jana.

Jana, gazeti hili lilimkariri Waziri wa Fedha na Mambo ya Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo, akisema serikali haijui mahali alipo Dk. Balali, na kwamba timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, inaendelea kushughulikia masuala yote yanayohusiana na Gavana huyo wa zamani wa BoT.

Hata hivyo, katika maelezo yake, Bw. Rweyemamu alisema hatua ya Rais Kikwete kumfukuza kazi Dk. Balali, ilimfanya (Balali) kuwa raia wa kawaida, mwenye uhuru wa kuishi mahali popote anapotaka, alimradi havunji sheria.

Taarifa zilizotolewa kwa mara ya mwisho na aliyekuwa Waziri wa Fedha, Bi. Zakhia Meghji, zilisema Dk. Balali alikuwa katika hospitali moja huko Boston nchini Uingereza, akipata matibabu ya ugonjwa ambao hata hivyo haukujulikana.
``Balali ni raia wa kawaida mwenye mambo binafsi, hivi sasa hatafutwi, lakini ukifika wakati wa kufanya hivyo, serikali itajua yupo wapi na tutampata tu,`` alisema.
Dk. Balali alifukuzwa kazi na Rais Kikwete, baada ya ripoti ya ukaguzi iliyofanywa na kampuni ya Ernst and Young kubaini vitendo vya ufisadi, vilivyosabaisha upotevu wa mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Hatua ya kufukuzwa kazi ilitangazwa wakati Dk. Balali, akidaiwa kuwa Marekani kwa ajili ya matibabu.

Kwa upande mwingine, Bw. Rweyemamu, alisema uamuzi wa kumkamata na kumfungulia mashtaka Bw. Chenge, utafikiwa baada ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili kukamilika.

Bw. Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, anatuhumiwa kuhifadhi takribani Dola 1,000,000 za Marekani kwenye benki iliyoko katika visiwa vya Jersey, Uingereza, fedha zinazohisiwa zilipatikana kwa njia ya ufisadi katika ununuzi wa rada, wakati wa serikali ya awamu ya tatu, iliyoongozwa na Bw. Benjamin Mkapa.

``Tukisema tumkamate Chenge sasa hivi, kutakuwa na kelele kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu na hata ninyi waandishi wa habari. Tusubiri uchunguzi ukamilike,`` alisema.

Aidha, alisema Rais Jakaya Kikwete, bado hajafikia uamuzi wa kumtangaza Waziri wa Miundombinu, kuziba nafasi iliyoachwa na Bw. Chenge.

``Suala la kumtangaza Waziri wa Miundombinu litafanywa kwa umma na si kificho, hivyo wananchi wasubiri tu, kwa sababu suala hili haliwezi kufanyika kinyemela,`` alisema.

Pia Bw. Rweyemamu, alisema suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar baina ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), inastahili kufikiwa kwenye meza ya mazungumzo.

CUF ilitangaza kutoendelea na mazungumzo hayo baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kuazimia kuwa makubaliano ya kuundwa serikali ya mseto visiwani humo, yanapaswa kupata ridhaa ya wananchi, kupitia kura za maoni.

Msimamo wa CUF ni kwamba suala la kura ya maoni halikuwepo katika ajenda za mazungumzo baina ya vyama hivyo.

SOURCE: Nipashe

Hivi kumbe Balali alikuwa anatibiwa Boston, Uingereza??? No wonder Mwanakijiji hakufanikiwa kumuona na kumuhoji. Mwanakijiji badala ya kumtafuta Boston, US, jaribu Boston Uingereza. Kwi kwi kwiiii!!!!
 
jamaa Naona Hakujiandaa Vizuri Kutupiga Changa La Macho Akaamua Kukurupuka Tu Na Kesha Lopoka Pumba Tu.hana Jipya Mbona Mwanzo Alikuwa Anashindwa Kujibu Balali Kalazwa Hospital Gani Na Serikali Ilikuwa Inalipa Gharama Za Matibabu Kupitia Kwa Nani?? Alichemka Saizi Anatueleza Utumbo Anajua Bado Ss Ni Wadanganyika Bado.
 
Back
Top Bottom