Balali alishakufa hatukuambiwa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Kwa vile Balali alipelekwa kwenye matibabu huko Marekani, matibabu ambayo yalisababisha alazwe kwa muda mrefu;

Kwa vile hali yake haikuwa nzuri na iliendelea kuwa mbaya hadi kumlazimisha amuombe Rais amruhusu aachie ngazi

kwa vile Rais hakukubali Balali ajiuzulu na baadaye kumtimua kazi akiwa mahututi kitandani;

Kwa vile Rais aliamua kuunda kamati maalumu ya kuchunguza wizi wa EPA na mhusika mkuu wa sakata hilo alidaiwa kuwa ni mahututi;

Kwa vile kwa muda mrefu sasa viongozi wetu wamekuwa wakituambia kuwa hawajui aliko Balali jambo ambalo limerudiwa tena hapo jana na Waziri Mkuu

Kwa vile Balali alikuwa mgonjwa mahututi, hana kazi, na serikali haijui alipo

Hivyo basi, madai ya serikali kuwa wakimtaka watampata hayana ukweli; Kuwa serikali ikimhitaji mtu wasiyejua alipo wataweza kumpata kwa haraka, kimsingi madai hayo ya serikali na kauli hizo hazina msingi wowote.

Kwa sababu,

Balali alishafariki na kuzikwa huko huko majuu baada ya hali yake kuwa mbaya. Na kwa vile serikali haijui alipo hawana njia yoyote ya kujua liliko kaburi lake na hawana ujuzi wowote kuwa ni mzima au ni marehemu.

Hivyo, basi anayesubiri kumuona Balali akirudi Tanzania mzima anasubiri mvua jangwani!!

RIP Balali!!

NB: Kama ni mzima bado, serikali imejuaje wakati hawajui aliko?
 
Na alale mahali pema. Amin.

Asante Mzee Mwanakijiji kwa hizi taarifa.
 
Kwa hiyo ndugu wenye kutoa watoe pole labda hatimaye serikali itapata ujasiri wa kuwaambia ukweli alikofia Balali...
 
Kwa hiyo ndugu wenye kutoa watoe pole labda hatimaye serikali itapata ujasiri wa kuwaambia ukweli alikofia Balali...

Kama atakuwa alishakufa itakuwa aibu kwa serikali yetu. Lakini mimi kinacho nishangaza tuhuma zinazo mkabili Balali(Dr.) ni nyingi mno ni muhujumu uchumi inakuwaje nchi inayojisifu katika medani ya kimataifa kuwa ni wanademokrasia na utawala bora halafu wakiwa wanaongoza watu masikini zaidi duniani wanatumia muda mwingi kuonyesha kuwa hawana haraka kumtafuta muhalifu aliyesababisha kutopea mamilioni ya walala pu.

Hata kuna jambo kubwa sana ambalo tumefichwa sisi wadanganyika, kwa nini hatafutwi, kwa nini Megji alisema alimudanganya na sasa wanasema amepona hata hawezi kuja kujibu tuhuma za kumdanganya Waziri.

Je kuna haja ya kumuuliza megji kama kweli Balali alimudanganya au la? Au na yeye atakuwa Bubu kama yule mzee aliyesema ameisha staafu siasa wakati anaudhuria vikao vya chama?
 
What?...
Mwanakijiji mkuu ebu nipashe vizuri hizi habari ni katika mtililiko wa kujiuliza ama ndio habari kamili?
 
Mkandara, ni katika kufuatilia habari ambazo zimekuwa zikiminywa kwa muda mrefu; katika kujiuliza uliza ndiko nimehitimisha kuwa Balali alishakufa, kwani ushahidi wa kimazingira unaonesha kuwa haiwezekani akawa hai; tatizo ni kuupata mwili.
 
mmkjj
Tatizo ni mwiili au kichwa?
mwana wa kijiji unaonyesha unayo mengi ya kutumwagia lakini kama una tubaniabani hivi hebu tupe mzee
 
Mwanakijiji,

Je umefanya jitihada zozote kujua jambo hilo hata kwa kuulizia ndugu, jamaa na marafiki au ndio wamefanya "memorandum of understanding" na serikali?
 
mkuu, sijui kama umewahi kumsikia mpepelezi wa kwenye Sherlock Holmes... baada ya kuangalia ushahidi wa kimazingira na kauli za mashahidi wote ni wazi kuwa haiwezekani kuwa Balali bado yuko hai. Tunachosubiri ni serikali kukiri kuwa alishatutoka na watuambie lini mwili unarudishwa.
 
Haya mmkjj
Huo ndio mwisho wetu woote hata kama hajafa lakini atakufa tuu
mungu ampe anacho stahili kutokana na aliyo yatenda na wenzake pia
 
mkuu, sijui kama umewahi kumsikia mpepelezi wa kwenye Sherlock Holmes... baada ya kuangalia ushahidi wa kimazingira na kauli za mashahidi wote ni wazi kuwa haiwezekani kuwa Balali bado yuko hai. Tunachosubiri ni serikali kukiri kuwa alishatutoka na watuambie lini mwili unarudishwa.

Mkuu,

Je unazungumzia Mystery of the Mummy Walkthrough au The Mystery of the Persian Carpet'

Napenda hicho cha pili kwamba kifo cha mpiga rangi kinaleta utata kwani amekutwa amekufa na ameviringishwa katika kapeti la "Persian".
 
Kazi kweli kweli.... Ajuaje hajui anajua, lakini sina hakika kama serikali inajua kwamba haijui, maana serikali yetu ya sasa haijui na haijui kwamba haijui. Inayumba sawa na iliyolaaniwa na wazazi ama "Albadiri ya mbayana imewaumbua!!!" Sasa ni mshike mshike wanakulana wao kwao kama mbwa mwitu walafi
 
What????????????????????????????????? Mai wasu wee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!Mama yangu.!!!!!!!! This is ridiculous.

Serikali inatamba kuwa hawana haja na bwana huyu huku wakijua kuwa hayupo tena duniani? Hii ni kututukana wananchi na kutuona mahayawani kabisa.

Nina wasiwasi kabisa kuwa serikali ina mkono katika kifo cha jamaa huyu kama ni kweli kuwa hatunaye duniani tena. Itakuwa Mkapa, Kikwete., Mramba, na Meghji wanahusika na upotevu wa roho ya bwana huyu.

Mwenyezi Mungu ni jukumu llako kumhukumu mwenzetu huyu kulingana na jinsi alivyokutumikia hapa duniani. Tunakuomba umwanganzie mtu mwingine yeyote atuambie yaliyokuwa moyoni mwa marehemu huyu, kama ni marehemu kweli kweli.
 
Duh!!! Ngoja nitafute popcorns na large drink nianze kuangalia movie...serikali haijui au haitaki tujue kuwa inajua?
 
lakini serikali imesema wakitaka kumpata watampata kwani wana "mkono mrefu" kitu ambacho kinanilazimisha kuamini:

a. Serikali inajua Balali alipo lakini inawadanganya wananchi kuwa "haijui"
b. Serikali kweli haijui Balali alipo na hivyo haijui kama yu hai au ameshatutoka.
c. Kama wanajua ni mzima basi wanajua aliko vinginevyo wanajuaje ni mzima na hivyo inaturudisha kwenye "a"
d. Kama kweli Balali alishakufa na serikali haijui kama alikufa hivyo maneno yao wakitaka kumpata watampata inawaonesha kuwa "hawajui" Balali aliko na hawawezi kumpata!

Hivyo swali la msingi kuhusu Balali siyo "wapi" alipo, bali yu mzima au yu mfu?
 
Jamani wacheni story za uzushi, Balali yupo safi na anadunda hapa US. Kuna source zangu zinasema alikuwa kwenye condo yake huko Boston, kabla ya kwenda zake DC. Balali hajafa and i think its not fair kusema mambo yasio na evidence.

Kama amekufa please tuonyesheni evidence, picha za msiba, cheti cha kifo, anything kuprove the point. Other than that i think hili lina sound more Kasheshe au Udaku.
 
Back
Top Bottom