Wa kulaumiwa ni mume, labda hamtunzi bint wa watu maskini!
Maisha ni magumu, hospital hela, maziwa ya mtoto hela,nyumba anayoishi inahitaji kodi uji wa ulezi wa mtoto hela kwa ujumla kila utakachogusa ni hela na sehemu ya kupatia kipato hakuna,siungi mkono kitendo alichokifanya cha kuzunguka na mtoto mtaani lakini pia anahitaji huruma huyo mama.
Wa kulaumiwa ni mume, labda hamtunzi bint wa watu maskini!
Katika pitapita yangu leo, nimekutana na picha hizi kwenye mitandao mbalimbali ya jamii.Mwanamke amekamatwa Akijiuza Usiku Huku akiwa na mtoto wake mdogo Tukio hili lilitokea katika kamakamta ya machangu mitaa ya buguruni Dar es salaa
hiyo ni hatari sana,maisha bora ya muheshimiwa ndiyo hayo!!! kasi mpya Ari mpya na Nguvu mpya Maisha bora kwa kila Mtaznia CCM hoye!!
Simtetei huyo mama kwa kosa alilolifanya, atalipia kosa lake kadiri ya taratibu za kisheria au za kijamii. Nisichokubaliana nacho ni udhalilishaji wa namna alivyomatwa, karibu kuchaniwa nguo, kupigwa picha na kusambazwa kwa picha zake. kuna watu ambao tayari maisha yamewadhalilisha, tusiwaongezee mzigo zaidi. Ficheni basi hata sura yake, isijetokea kwamba mwisho wa siku, hana makosa lakini sura yake imeshasambazwa kwamba ni kahaba.
Sumbalawinyo kuna ugumu na ugumu ndugu yangu usiuombeeugumu wa maisha hautatuliwi kwa kuuza mbunye