Osaka
JF-Expert Member
- Jun 21, 2011
- 1,762
- 551
watajilipua aiseeee..!! Wakapate mabikira ahera
Hii ni kufuru mkuu!
watajilipua aiseeee..!! Wakapate mabikira ahera
Nitakusamehe tu kwa sababu ndio post yako ya kwanza hii, lakini hapa hatuna topic ya wakazi wa Dar, na hii JF ina member dunia nzima na wanaochangia thread hii sasa hivi wapo nchi mbalimbali, kwa hiyo kama unataka kutoa pole kwa wakazi wa Dar anzisha thread yako au tafuta humu inayohusiana utaikuta.Polen xana wakaaz wa dar es salaam kwa maafa yaliyowakuta pia kwa ndugu zetu waliopoteza maisha mwenyezi mungu aziweke roho za marehem pema peponi, mungu alitoa mungu ametwaa jina lake lihimidiwe. Wahusika wa miundo mbinu tekelezen wajib wenu wa kurekebisha miundombinu ili kunusuru maisha ya watanzania. Kwa ndugu zangu waishio mabondeni jaman hamen mabo yameharibika.
Kweli wana hoja lakini hawana uwezo wa kui draft na kui present kama walivyofanya wenzao.something is wrong ila WAANDAMANAJI WANAHOJA YA MSINGI WANAJUA KITU.
"Kupinga maridhiano ya serikali na makanisa juu ya misaada wanayopewa katika huduma za jamii, hakuna mantiki yoyote la msingi ni Waislamu kujihalalishia mikataba kwa kujiwekea miundo mbinu na huduma za jamii za kutosha kielimu na kiafya ili tundelee," alisema Shehe Salum.
Haya ndio mawazo ya mtu mwenye akili timamu. Uislamu wa namna hii utaisogeza mbele Tanzania na kupunguza ufukara unaoletwa na fikra duni za watu kama MS na Topical.
Meseji sent and delivered to Malaria Sugu and Faiza ForxKupinga maridhiano ya serikali na makanisa juu ya misaada wanayopewa katika huduma za jamii, hakuna mantiki yoyote la msingi ni Waislamu kujihalalishia mikataba kwa kujiwekea miundo mbinu na huduma za jamii za kutosha kielimu na kiafya ili tundelee, alisema Shehe Salum.[/URL]
Tanzania kuna waislam wa ukweli na waislam fake,waislam fake ndio wanaotusumbua na kurudisha nyuma maendeleo,kazi yao kubwa ni kulalama tu kila uchwao,kazi hawafanyi ila wanapenda kushinda kwenye kahawa na kucheza bao.
Mabingwa au Mashababi(Al-shabab)wa Mihadhara ya Kashfa za dini zingine, kama vile Khidmat Daawat'l Islamiya na wengineo!Hivi hawa wahadhiri ni watu gani?, naomba kujuzwa, niwahadhiri wa madrasa au vyuo gani?. Nikipatajibu nitarudi kujadiri.
Daniel Rutoryo na Abdallah Mdangwe
SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhaji Alhad Musa Salum amewataka waislamu wa mkoa huo na nchini kwa ujumla kutoshiriki maandamano yaliyoandaliwa na Umoja wa Waadhiri wa Kiislamu nchini Desemba 23, mwaka huu.
Hivi karibuni umoja huo wa wahadhiri wa Kiislamu ulitangaza kufanya maandamano hayo kupinga mambo mawili, ambayo ni makuabaliano kati ya makanisa na serikali na kuchelewa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.
Akizungumza na waandishi habari jana jijini Dar es Salaam, akiliwakilisha Baraza la Kuu la Waislamu (BAKWATA), Shehe Salum alisema hakubaliani na taarifa iliyotolewa na wahadhiri hao na kuwataka Waislamu wasishiriki katika maandamano hayo.
Alhaji shehe Salum alisema haamini kama maandamano yatakuwa suluhishi la upatikanaji wa haki za Waislam ikiwemo kuanzishwa Mahakama hiyo ya Kadhi.
Sisi Baraza la Waislamu Tanzania hatuamini kama maandamano ndio suluhisho la haki za binadamu au hiyo mahakama ya Kadhi, njia hiyo ya wananchi kuandamana itaishia kupigwa mabomu tu, alisema Shehe Salum.
Alifafanua kwamba, sababu wanayoeleza wahadhiri hao haina mashiko kwa sababu tayari suala la uanzishwaji wa mahakma hiyo ya kadhi lipo mezani na linashughulikiwa na serikali.
Kupinga maridhiano ya serikali na makanisa juu ya misaada wanayopewa katika huduma za jamii, hakuna mantiki yoyote la msingi ni Waislamu kujihalalishia mikataba kwa kujiwekea miundo mbinu na huduma za jamii za kutosha kielimu na kiafya ili tundelee, alisema Shehe Salum.
Alisisitiza, Bakwata inayo mikakati madhubuti ya kuhakikisha sheria za mahakama ya Kadhi zinaingizwa katika katiba mpya.
Shehe huyo wa mkoa aliitaka jamii kuondoa wasiwasi kwani itajihusisha na masuala ya mirathi, ndoa, talaka na malezi ya watoto kwa Waislamu tu.Alisema serikali inapaswa kuruhusu nchi kujiunga na Jumuiya ya Kiislam DunianI (OICC) kwani jumuiya hii hutoa misaada kwa wanajamii kupitia serikalini na si kwa Waislamu pekee hii ni kwa manufaa ya watanzania wote.
Viongozi wa dini na siasa
Kuhusu viongozi wa dini, aliwataka kutojihusisha na siasa wala wanasiasa kutumia dini ili kujijengea umaarufu katika jamii kwani hiyo itapelekea kuwagawa wananchi, kutokana na imani tofauti za kidini.
Shehe Salum aliwataka wanasiasa wasijihushishe na viongozi wa dini kujinufaisha kisiasa huku pia viongozi wa dini nao wakiacha kujihusisha na masuala ya siasa ili kutopoteza imani zilizojengeka kwa wananchi
chanzo: Bakwata yapinga maandamano ya wahadhiri wa Kiislam
Hivi hawa wahadhiri ni watu gani?, naomba kujuzwa, niwahadhiri wa madrasa au vyuo gani?. Nikipatajibu nitarudi kujadiri.
Mabingwa au Mashababi(Al-shabab)wa Mihadhara ya Kashfa za dini zingine, kama vile Khidmat Daawat'l Islamiya na wengineo!
Hili nalo neno kutoka kwa mwenye fikra pevu kidini na kimtazamo Maralia Sugu na ndugu yako F.Fox mpo?
Ila tujadili hili ndugu,kote Bakwata wameenda sawa lakini alipofika ktk alama nyekundu mhhhhhhhhhhhh..................!!!!! Ktk katiba kadhi inatafuta nini badala ya ktk misaafu na misikiti yenu?Na hii OIC mnayong'ang'ania sababu ni misaada tu au kuna jingine?Kama ni misaada si mumkubalie Cameroon matakwa yake mpate misaada kibao. Hivi ni kweli akili zetu hazina lingine la kufikiri kujikomboa zaidi ya kutegemea misaada.Na inamaana ninyi (waislam) tu ndiyo mnaiona hiyo misaada wengine hawaioni.Ujinga huu ndiyo umetufikisha hapa tulipo mawazo na mtazamo finyu wa Viongozi wetu.
Kama kiongozi wa bakwata ana mtazamo huo na uelewa huo Je muumini wa kawaida atakuwaje?
Ila heri ya Bakwata kuliko wahadhiri wenu japo nilidhani wahadhili wangekuwa na ufahamu mpana zaidi lakini inadhihilisha kinyume chake.
Haya ndio mawazo ya mtu mwenye akili timamu. Uislamu wa namna hii utaisogeza mbele Tanzania na kupunguza ufukara unaoletwa na fikra duni za watu kama MS na Topical.
polen xana wakaaz wa dar es salaam kwa maafa yaliyowakuta pia kwa ndugu zetu waliopoteza maisha mwenyezi mungu aziweke roho za marehem pema peponi, mungu alitoa mungu ametwaa jina lake lihimidiwe. Wahusika wa miundo mbinu tekelezen wajib wenu wa kurekebisha miundombinu ili kunusuru maisha ya watanzania. Kwa ndugu zangu waishio mabondeni jaman hamen mabo yameharibika.