figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
My Take:
Hii Barua imeandikwa kimafumbo mafumbo, hawajafunguka vizuri. Ila kwa hisia zangu, hawa masheikh wanaoongelewa ni wale walioenda kwa Mchungaji Gwajima siku ya Jumapili kumtembelea na kuhudhuria ibada yake. Mmoja ambaye namkumbuka alijitambulisha kama Sheik Khalif ambaye ni Msomi na Mtaalam wa Kiislam ambaye amesoma Misri kwenye chuo kinaitwa Al-Azhar University - Jāmiʻat al-Azhar (al-Sharīf)
Kanisa la Ufufuo na Uzima kuna habari waliitoa wakisema
"JUMAPILI 26/03/2017: Jumapili ya leo Ufufuo na Uzima tumekuwa na ugeni wa kutembelewa na Mashehe kwa sababu Ufufuo na Uzima ni rafiki wa waislam. “Anasema Shekhe dini ya uislam haizuii mtu kuwa na rafiki asiye Muislam” ameendelea kusema Ugomvi wa kidini ni uchoyo, kila tunalofanya tufanye kwa kuhakikisha watu wanaishi kwa Amani na furaha. Pia amesema ifike mahali Serikaliyetu itumie watu kama Askofu Gwajima kuitangaza Tanzania na vivutio vilivyopo Tanzania na isiwe kuwasakama na kuwasumbua."
Vilevile Kanisa la ufufuo na Uzima walitembewa na Watu wengine ambao ni Wasanii wa Bongo Movie "Kitale na Mjomba wake ambao ni Waislam Pia.
Nmejaribu kuweka picha wakiwa Kanisani Kwa Gwajima. Hizi Picha zimepigwa katika kanisa la ufufuo na Uzima Tanzania ambalo lipo Ubungo karibu na Kituo cha TANESCO kama unaelekea Kimara.