BAKWATA waunga mkono Uchaguzi Kurudiwa Zanzibar

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Bakwata wameunga mkono uchaguzi wa Zanzibar kurudiwa.

Kauli hiyo imetolewa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam leo.

Mambo yameiva sasa game ni BAKWATA na Imoja wa Ulaya.

CUF watafuata ushauri upi? Muda utaongea.

Chanzo: Azam Tv
=================

Wakati Chama cha wananchi CUF ambacho ni chama kikuu cha Upinzani visiwani Zanzibar kikiwa kimesusia uchaguzi wa marudio ambao unafanyika Marchi 20 ya mwaka huu,Baraza la Waislam (BAKWATA) limesema marudio ya uchaguzi huo ndo njia ya kipee ya kurudisha amani visiwani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu mkoani hapa,heikh alhadj Mussa Salum amesema Bakwata wanaunga mkono Tangazo la ZEC la kurudiwa kwa uchaguzi hu.

“Uchaguzi huu wa marudio kwetu Bakwata tunaona ndio njia ya kipekee ya kukiweka kisiwa cha Zanzibar kuwa sehemu ya Amani na utulivu,natumia nafasi hii kuwaomba chama cha CUF kushiriki uchaguzi huu” Amesema Sheikh Salum.

Sheikh Salum ameongeza kwa kusema kuwa hata kiongozi wa jumuiya ya Uamsho Visiwani Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmad amemwandikia barua na kumweleza kuwa kurudiwa kwa uchaguzi kutasaidia kurudisha Amani visiwani humo.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo limeipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jitihada mbalimbali inazofanya za kuimarisha nidhamu, kubana matumizi na kukuza uchumi.

"Pia tunaipongeza serikali ya awamu ya tano, inayoongozwa na Mh. John Magufuli, kutokana na hatua mbali mbali inazozichukua zenye lengo la kuimarisha nidhamu hasa kwa watumishi wa umma, hatua mabazo zimeanza kuleta tija kubwa ka taifa letu kama wote hivi leo tunavyoweza kushuhudia jinsi pato la serikali likongezeka mwezi hadi mwezi”, alisema Sheikh alhadj Mussa Salum na kuongeza;

“Aidha tunaipongeza kwa dhamira yake ya kubana na kupunguza matumizi ya serikali, na badala yake kuelekeza fedha kwenye huduma za jamii na watanzania tumeshaanza kunufaika na huduma hizo kama vile suala la elimu bure."
 
Bakwata wameunga mkono uchaguzi wa Zanzibar kurudiwa.Kauli hiyo imetolewa na shekh mkuu wa dar es salaam leo.
Mambo yameivya sasa game ni bakwata na umoja wa ulaya Cuf watafuata ushauri upi? Muda utaongea.
Source Azam Tv
inamaana bakwata wamewapuuza cuf kiasi cha kuwatoa ubinaadamu wao na kuwaona kama watu wasiokuwa na dhamani
hata kama cuf wangekuwa na makosa bakwata wangewashauri cuf na ccm wakae watafute maridhiano kwanza kbla ya uchaguzi
watu wa ulaya wana akili sana ndio maana hawaendi makanisani kwa kuwa wamegundua makanisani kuna sanaa nyingi sana
 
Hili tamko linahitaji ufafanuzi kwa kuwa zanzibar haendeshwi na bakwata na serikali haina dini bakwata imeingiaje humu, na kwa kufanya hivyoo walivyofanya wanajenga umoja wa kitaifa au wanabomoa .
 
Kwa nini wasishauri mazungumzo au haki itenfeke mshindi apewe chake au hivi ndo Dino yao inavyotaka
 
Tamko la bakwata latakiwa kutolewa rasmi na mufti mkuu. Na bakwata ni ya bara kule visiwani wana chombo chao. Sitegemei hilo litakuwa kauli rasmi ya bakwata kwani zanzibar haiwahusu kwa lolote hao bakwata. Pengine hayo yalikuwa maoni yake binafsi shekhe wa mkoa
 
inamaana bakwata wamewapuuza cuf kiasi cha kuwatoa ubinaadamu wao na kuwaona kama watu wasiokuwa na dhamani
hata kama cuf wangekuwa na makosa bakwata wangewashauri cuf na ccm wakae watafute maridhiano kwanza kbla ya uchaguzi
watu wa ulaya wana akili sana ndio maana hawaendi makanisani kwa kuwa wamegundua makanisani kuna sanaa nyingi sana
Mkuu rejea andiko lako maana kinachojadiliwa hapa ni uchaguzi Zanzibar na Bakwata sasa makanisa yanaingiaje hapo?
 
Bakwata acheni hiyo...huyo sheikh wa Dar elimu yake iko vipi.kasoma shule za bweni au day..???Kwa nini anataka kuleta sintofahamu.Kanisa likisema uchaguzi usirudiwe itakuwa vipi...???Sheikh Zuberi tukuombe umpe huyu sheikh wa mkoa job description..hakika anaudhalilisha uislam....Ukimya pia unapeleka ujumbe.Huyo sheikh anaweza ongea na viongozi wa kanisa kuhusu uchaguzi wa znz..????Nina mashaka makubwa.
 
Hili tamko linahitaji ufafanuzi kwa kuwa zanzibar haendeshwi na bakwata na serikali haina dini bakwata imeingiaje humu, na kwa kufanya hivyoo walivyofanya wanajenga umoja wa kitaifa au wanabomoa .
Mkono wa so called Al Hajj Abdullaah Bulembo upo hapo
 
Back
Top Bottom