Bakwata na siasa za uswisi

Netanyahu

Senior Member
Oct 2, 2008
147
22
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka Waislamu nchini na wapenda amani kususia bidhaa na huduma zote kutoka Uswisi.

Tamko hilo limetokana na hatua iliyochukuliwa mwaka jana na Serikali ya Uswisi kupiga marufuku ujenzi wa minara ya misikiti nchini humo na kwa mujibu wa kura ya maoni iliyopigwa, zaidi ya asilimia 50 ya wananchi waliunga mkono, huku 42 wakipinga.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mufti wa Tanzania, Issa bin Shaaban Simba, aliwataka Waislamu pia kutopanda ndege za Uswisi hadi marufuku hiyo itakapokuwa imeondoshwa.

“Ninatoa mwito kwa Waislamu wote duniani kuisusia Uswisi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kibiashara na masuala yote ya kijamii, kama yupo mwenye fedha katika benki ya Uswisi au biashara, basi aziondoshe mara moja,” alisema Mufti.

Mufti Simba alisema anasikitishwa na jinsi Uswisi ilivyoingilia uhuru wa kuabudu, kwa kupinga ujenzi wa minara kwani hata kesho wanaweza kupinga adhana, jambo linaloweza kuleta uchokozi na kufarakanisha watuBARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limewataka Waislamu nchini na wapenda amani kususia bidhaa na huduma zote kutoka Uswisi.

Tamko hilo limetokana na hatua iliyochukuliwa mwaka jana na Serikali ya Uswisi kupiga marufuku ujenzi wa minara ya misikiti nchini humo na kwa mujibu wa kura ya maoni iliyopigwa, zaidi ya asilimia 50 ya wananchi waliunga mkono, huku 42 wakipinga.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mufti wa Tanzania, Issa bin Shaaban Simba, aliwataka Waislamu pia kutopanda ndege za Uswisi hadi marufuku hiyo itakapokuwa imeondoshwa.

“Ninatoa mwito kwa Waislamu wote duniani kuisusia Uswisi katika nyanja za kisiasa, kiuchumi, kibiashara na masuala yote ya kijamii, kama yupo mwenye fedha katika benki ya Uswisi au biashara, basi aziondoshe mara moja,” alisema Mufti.

Mufti Simba alisema anasikitishwa na jinsi Uswisi ilivyoingilia uhuru wa kuabudu, kwa kupinga ujenzi wa minara kwani hata kesho wanaweza kupinga adhana, jambo linaloweza kuleta uchokozi na kufarakanisha watu.

Alisema hatua hiyo ni ubaguzi, chuki na uchokozi dhidi ya dini ya Kiislamu kwa kuwa marufuku hiyo hailengi kukataza ujenzi wa minara ya makanisa ila ya misikiti.

Alisema kitendo hicho cha Serikali ya Uswisi kueneza propaganda chafu dhidi ya Uislamu si cha kiungwana, wakati kwa muda mrefu imekuwa ikifahamika kwa utamaduni wake wa kuvumiliana na kuheshimiana baina ya dini tofauti.

“Kitu hicho kinaliondolea heshima Taifa hilo na kibaya zaidi kwenda kinyume na tamko la Dunia kupitia Umoja wa Mataifa la haki za binadamu linalotaka kila mtu kuwa na haki ya kuabudu,” alisema.

Mufti pia aliwataka Waislamu duniani kote kulinda na kuienzi dini yao na kuhakikisha wanachukua hatua madhubuti kuhakikisha inalindwa.

SOURCE: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=6505&cat=kitaifa


MY COMMENT:


Mufti asilojua ni kuwa huko nchi zinazoitwa za kiislamu makanisa hayaruhusiwi kujenga makanisa na kuweka minara yenye misalaba juu.Kisa wanachosimamia ni kuwa watu wengi ni waislamu na hawataki hilo.Sasa Uswisi wengi wamepiga kura kusema hawataki kama uarabuni na nchi za kiislamu wanavyofanya tatizo liko wapi? Je hizo haki za kibinadamu ni kwa ajili ya waislamu Uswisi na wakristo hawana haki hizo uarabuni na nchi za kiislamu?.Je na nchi zenye wakristo wengi waanze kutangaza kususia kila kitu ikiwemo mafuta toka nchi za kiislamu kwa kuwakatalia kuweka misalaba kwenye minara ya majengo ya ibada?


Uswisi walichofanya ni kuwaeleza waislamu kuwa democracy is not a one way traffic ukikataza mwenzio asijenge mnara wa msalaba kwenye nchi zako za kiislamu ujiandae na wewe kwenye nchi za wenzio kukataliwa na wewe kujenga wako.Natamani nchi zingine zingeiga mfano wa Uswisi ili kushinikiza nchi za waislamu wabadilike na wawe na utamaduni wa kuvumilia imani za wengine.Sio tu watake kuvumiliwa wao tu.


Hili la kusema waislamu wa Tanzania wasusie bidhaa za Uswisi sidhani kama lina nguvu.Waislamu wengi Tanzania hata saa ya mkononi ya Uswisi hawajui inafananaje kwa kuwa hawana na hawana uwezo wa kununua.KAULI YAKE HAINA ATHARI KWA UCHUMI WA USWISI.
 
That is stupidity of beyond belief.Nafikiri hawa BAKWATA wangempinga Sheikh Yahaya Hussein kuhusu kutabiri kifo kuliko kuingilia mambo ya Uswisi.
Ndio maana watu wengi hapa JF tuna wasiwasi na serikali yetu kuendekeza udini.
To be fair wananchi wengi wa USWISI hawajui kama kuna Tanzania inaexist.They dont care!
Leo kulikuwa na suicide bombing huko PAKISTAn unleashed by fellow Muslims.Nigefurahi BAKWATA wangecondemn huu unyama
 
labda bakwata ingeanza kwa kuorodhesha hizo bidha za uswiss
zinazouzwa tanzania kisha apime kama ususiaji wa hizo bidhaa
utakuwa na "impact" gani. bidhaa za uswiss sio saa na shirika la
ndege tuu, hata madawa ya tiba mengine yanatoka huko
uswiss.
 
Onyesha mfano wewe Kwa kususia misaada,na utueleze sera endelevu, za kUUkomboa UISLAMU..na aibu uiepushie jumuia ya BAKWATA,aibu ya kugombania MBUZI kutoka MECCA,wakati sisi bongo tunao wa kutosha.
PIA Viongozi wa BAKWATA NAWASIHI MWACHE kugombamia MSAADA WA NYAMA YA MBUZI KILA MWAKA.
.KWANI..
MBUZI HAO HUTOLEWA KWA AJILI YA YATIMA BAADA YA SwALA YA HIJA.
PIA MUACHE KUPOKEA MISAADA YA YATIMA WAKATI VITUO VYA KUWALEA HATUNA,
TUMBIE KWA,,..
VIPI TUTAJIKOMBOA, ILI TUWEZE KUACHA KUOMBA MSAADA WA FEDHA SERIKALINI KWA
AJILI YA KUKOMBOLEA HAO MBUZI BANDARINI PINDI wanapoingia KUTOKA MECCA.

KUJINUFAISHA KWA KUTUMIA .NEMBO YA MAYATIMA NI, UNAFIKI NA UZANDIKI MWAPASWA KUADHIBIWA NYIE
MNAITIA DINI AIBU.
 
Back
Top Bottom