BAKWATA: Kumekuwepo na ufungaji holela wa Ndoa za Kiislamu zenye vyeti feki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Dodoma limeagiza wale wote wanaofungisha ndoa za kiislamu kuhakikisha wanakuwa na vyeti halisi vya ndoa na leseni maalumu inayotambuliwa na baraza hilo.

Angalizo hilo limetolewa na Katibu wa Bakwata Wilaya ya Dodoma, Ahmed Msuri alipokuwa akizungumza na mashehe, maimamu na walimu wa madrasa kutoka kata za jiji hilo kwenye kikao cha utendaji kilichofanyika kwa ajili ya uchangiaji wa Mfuko Maalumu wa Shehe Mkuu na Mufti wa Tanzania ambao utasaidia makundi maalumu yenye uhitaji.

Katibu huyo alisema hivi sasa kumekuwepo na ufungishaji wa ndoa za Kiislamu holela zisizo halali ambazo hufanyika mitaani huku wakitumia vyeti bandia ambavyo havitambuliwi na baraza hilo.

Alisema hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa migogoro mingi kwenye ndoa isiyokuwa na tija, ambazo zimeshindikana hata kuzitatua kutokana na wengi wao kugundulika kuwa na vyeti feki vya ndoa.

"Lengo la angalizo hili viongozi mliohudhuria kikao hiki mashehe, maimamu na walimu, ni kuwatambua wanaofungisha ndoa hizo kweli wana vibali halali na wapo kisheria na sio vinginevyo, tunahitaji kuheshimu msingi wa dini ya kiislamu tuliyoachiwa na Mtume wetu Muhamad(S.A.W),"alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Wilaya ya Dodoma, Bashiru Husseni amewataka mashehe na maimamu kujenga ofisi zao kwenye kata ili ziweze kutumika kwa kuondoa kasoro zinazojitokeza ikiwemo hao walimu wanaofungisha ndoa kwa kutumia vyeti feki.

Alisema ofisi hizo zikiwepo wale wote watakaohitaji kufunga ndoa zao watakuwa wakiwafuata ili wapatiwe huduma hiyo muhimu ya kufungishwa, pia wataweza kutatua migogoro kwa njia ya ufanisi zaidi.

Alisema moja ya majukumu yao ni kuhakikisha mashehe wote wa kata wanakuwa na ofisi ili kuleta ufanisi wa katika kazi zao ambapo zitawasaidia pia kuondokana na kufanya kazi zao kwa mazoea.

Chanzo: HabariLeo
 
Kwa hiyo zenye vyeti vya BAKWATA hazina mgogoro?
 
Wameona wanapoteza mlo hapo maana kila cheti wanachukua hela
Bei zao hazijulikani
Taasisi hovyo kabisa
Wajipange
 
Bakwata ni taasisi kama taasisi nyengine ... Wasiwatishe waislam ...
 
Hilo ni sahihi wenzetu wakristo wao wanafata sana utaratibu unasubiria Mungu aje akufungishe ndoa na aisha ambaye anachepuka na mzee wa jirani? tufate utaratibu sio kwmba mtu kujua kusoma kiarabu basi ndi uwe na uwezo wa kufungisha ndoa hapana ndoa ziheshimiwe
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Dodoma limeagiza wale wote wanaofungisha ndoa za kiislamu kuhakikisha wanakuwa na vyeti halisi vya ndoa na leseni maalumu inayotambuliwa na baraza hilo.

Angalizo hilo limetolewa na Katibu wa Bakwata Wilaya ya Dodoma, Ahmed Msuri alipokuwa akizungumza na mashehe, maimamu na walimu wa madrasa kutoka kata za jiji hilo kwenye kikao cha utendaji kilichofanyika kwa ajili ya uchangiaji wa Mfuko Maalumu wa Shehe Mkuu na Mufti wa Tanzania ambao utasaidia makundi maalumu yenye uhitaji.

Katibu huyo alisema hivi sasa kumekuwepo na ufungishaji wa ndoa za Kiislamu holela zisizo halali ambazo hufanyika mitaani huku wakitumia vyeti bandia ambavyo havitambuliwi na baraza hilo.

Alisema hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa migogoro mingi kwenye ndoa isiyokuwa na tija, ambazo zimeshindikana hata kuzitatua kutokana na wengi wao kugundulika kuwa na vyeti feki vya ndoa.

"Lengo la angalizo hili viongozi mliohudhuria kikao hiki mashehe, maimamu na walimu, ni kuwatambua wanaofungisha ndoa hizo kweli wana vibali halali na wapo kisheria na sio vinginevyo, tunahitaji kuheshimu msingi wa dini ya kiislamu tuliyoachiwa na Mtume wetu Muhamad(S.A.W),"alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Wilaya ya Dodoma, Bashiru Husseni amewataka mashehe na maimamu kujenga ofisi zao kwenye kata ili ziweze kutumika kwa kuondoa kasoro zinazojitokeza ikiwemo hao walimu wanaofungisha ndoa kwa kutumia vyeti feki.

Alisema ofisi hizo zikiwepo wale wote watakaohitaji kufunga ndoa zao watakuwa wakiwafuata ili wapatiwe huduma hiyo muhimu ya kufungishwa, pia wataweza kutatua migogoro kwa njia ya ufanisi zaidi.

Alisema moja ya majukumu yao ni kuhakikisha mashehe wote wa kata wanakuwa na ofisi ili kuleta ufanisi wa katika kazi zao ambapo zitawasaidia pia kuondokana na kufanya kazi zao kwa mazoea.

Chanzo: HabariLeo
kwa kiimani ndoa inafungwa na kufungishwa na nani..? inamaan huyo sheih ni mjuaji zaidi ya mtume Mohamed aliye ruhusu ndoa zifungishe na hata ndugu wa kiume wa mwanamke aliyebalehee...
 
Kuna sheria za dini na za Jamhuri. Inapohusu ndoa sheria za Jamhuri zina override sheria za dini. Ndiyo sababu dini inasema mke/mme wakifumaniwa wanazini wapigwe mawe hadi kufa. Lakini jamhuri inasema "NO"
 
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Dodoma limeagiza wale wote wanaofungisha ndoa za kiislamu kuhakikisha wanakuwa na vyeti halisi vya ndoa na leseni maalumu inayotambuliwa na baraza hilo.

Angalizo hilo limetolewa na Katibu wa Bakwata Wilaya ya Dodoma, Ahmed Msuri alipokuwa akizungumza na mashehe, maimamu na walimu wa madrasa kutoka kata za jiji hilo kwenye kikao cha utendaji kilichofanyika kwa ajili ya uchangiaji wa Mfuko Maalumu wa Shehe Mkuu na Mufti wa Tanzania ambao utasaidia makundi maalumu yenye uhitaji.

Katibu huyo alisema hivi sasa kumekuwepo na ufungishaji wa ndoa za Kiislamu holela zisizo halali ambazo hufanyika mitaani huku wakitumia vyeti bandia ambavyo havitambuliwi na baraza hilo.

Alisema hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa migogoro mingi kwenye ndoa isiyokuwa na tija, ambazo zimeshindikana hata kuzitatua kutokana na wengi wao kugundulika kuwa na vyeti feki vya ndoa.

"Lengo la angalizo hili viongozi mliohudhuria kikao hiki mashehe, maimamu na walimu, ni kuwatambua wanaofungisha ndoa hizo kweli wana vibali halali na wapo kisheria na sio vinginevyo, tunahitaji kuheshimu msingi wa dini ya kiislamu tuliyoachiwa na Mtume wetu Muhamad(S.A.W),"alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania Wilaya ya Dodoma, Bashiru Husseni amewataka mashehe na maimamu kujenga ofisi zao kwenye kata ili ziweze kutumika kwa kuondoa kasoro zinazojitokeza ikiwemo hao walimu wanaofungisha ndoa kwa kutumia vyeti feki.

Alisema ofisi hizo zikiwepo wale wote watakaohitaji kufunga ndoa zao watakuwa wakiwafuata ili wapatiwe huduma hiyo muhimu ya kufungishwa, pia wataweza kutatua migogoro kwa njia ya ufanisi zaidi.

Alisema moja ya majukumu yao ni kuhakikisha mashehe wote wa kata wanakuwa na ofisi ili kuleta ufanisi wa katika kazi zao ambapo zitawasaidia pia kuondokana na kufanya kazi zao kwa mazoea.

Chanzo: HabariLeo
Hapo sasa
 
Back
Top Bottom