BAKWATA Ina matatizo ya Uendeshaji. Je, itaziweza Mahakama za Kadhi?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,680
119,316
Wanabodi.

Angalizo: Japo hii ni thread kulihusu Baraza la Waislamu Tanzania, Bakwata, sio thread ya dini, ni thread ya mambo ya utawala yaani pure administration matters kwenye kuzi administer mahakama za Kadhi!.

Leo asubuhi, kupitia Channel Ten Habari, nimemsikia Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Sheikh Alhaj Aboubakary Zubeir, akimshukuru rais John Pombe Magufuli kwa kugharimia matibabu yake, hapo Taasisi ya Moyo ya Dr. Jakaya Kikwete.

Sheikh Mkuu, alizitoa shukrani hizo, alipokuwa akishukuru watu mbalimbali mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini alikolazwa na kutibiwa.

Kwanza hakuna ubaya wowote kwa Rais John Pombe Magufuli na familia yake, kugharimia matibabu ya Mtanzania yoyote muhitaji, au mtu mwingine yoyote, kama Magufuli alivyompatia pesa za matibabu msanii Wastara, wala hakuna ubaya wowote kwa serikali kugharimia matibabu ya Mtanzania yoyote muhitaji, hivyo kwa darja ya wadhifa wake kama Sheikh Mkuu wa Tanzania,
Sheikh Alhaj Aboubakary Zubeir kugharimiwa matibabu na serikali inapaswa iwe ni miongoni mwa haki na ni stahili zake na sio hisani!.

Cheo cha Mufti, kitaifa Kiislamu ni sawa na cheo cha Muhashamu Policarp, Kardinali Pengo, Pengo akilazwa hospitali, na kisha kuomba msaada wa kulipiwa gharama za matibabu na serikali, kitendo hicho kitakuwa ni cha fedheha kwa jamii ya Wakristo Wakatoliki nchini, kwa sababu ni jukumu la Kanisa Katoliki nchini kuwahudumia viongozi wake kwa hali na mali, na sio jukumu la serikali kuwahudumia viongozi wa dini, ila viongozi hao wanao uhalali wa kuhudumiwa na serikali yao, kama Mtanzania mwingine yoyote!.

Kitendo hiki cha Mufti Sheikh Alhaj Aboubakary Zubeir kugharimiwa matibabu na familia ya rais John Pombe Magufuli, kumenifanya niitafakari kidogo BAKWATA katika masuala ya uwezo wa rasilimali za utawala, administration matters. Sheikh Mkuu wa Tanzania, anapaswa kuwa na bima ya afya ya kiwango cha juu, premium class, kiasi akiumwa ghafla akiwa popote alipo, flying doctors wanatua na kumchukua within 3 hours na kumpeleka kwenye hospital ya hadhi ya kimataifa iliyo karibu. Kitendo cha Mufti Sheikh Alhaj Aboubakary Zubeir kugharimiwa matibabu na familia ya rais Magufuli au na serikali, ni dalili kuwa Sheikh Mkuu wa Tanzania hana bima ya afya, hivyo serikali ikabidi iingilie kati kusaidia, kitu ambacho jambo ni jambo la kheri kwa rais Magufuli na familia yake kusaidia au serikali kusaidia, ila hili ni jambo la fedheha kwa Waislamu wa Tanzania.

Kitendo cha taasisi yoyote kutokuwa na fedha za kutosha sio kosa, wala BAKWATA haiwezi kusimangwa kwa ukata au umasikini, lakini kitendo cha kuwa BAKWATA ndio taasisi rasmi ya Waislamu nchini Tanzania, halafu Waislamu ni watu wenye uwezo mkubwa kifedha na kiuchumi, ndio wafanyabiashara wakubwa nchini, haiwezekani taasisi yao ikakumbwa na ukata kiasi cha kutokumuwekea bima ya afya Sheikh Mkuu wa Tanzania.

Nimesema kuna uwezekano BAKWATA ina matatizo ya kiuendeshaji, kwa sababu BAKWATA ninayoifahamu mimi, inazo rasilimali nyingi ambazo zikitumiwa vizuri, zitaweza kuipa BAKWATA uwezo wa kujiendesha na kumuwekea Mufti Bima ya Afya.

Kwa msiofahamu, wapo matajiri kibao wa Kiislamu waliokuwa na mali nyingi, zikiwemo majumba, matajiri hao kwa sababu moja au nyingine, hawakubahatika kupata warithi, hivyo waliacha wosia wa pale watakapo itwa mbele ya haki, mali zote zikabidhiwe kwa BAKWATA ziwe ni mali za Wakfu. Hivyo BAKWATA inamiliki majumba kibao ambayo kama ingekuwa na utawala mzuri, nyumba hizo tena ziko kwenye maeneo very prime, zingekarabatiwa na kutumika kama vitega uchumi vya BAKWATA.

Tena naomba niwape siri, hata vile viyoyozi vilivyofungwa ofisi za Makao Makuu ya Bakwata, ikiwemo ofisi ya Mufti, vimetolewa msaada na taasisi fulani ya Kikiristo!. Cha ajabu, baada ya miaka kadhaa, wawakilishi wa taasisi ile wakaenda kutembelea BAKWATA kuwajulia hali!. Wakashangaa kukuta viyoyozi vyote vimezimwa isipokuwa kiyoyozi kimoja tuu cha ofisi ya Mufti. Wakauliza kama vimeharibika ili wagharimie ukarabati, wakaelezwa viyoyozi vyote ni vizima kabisa, ila haviwashiwi kwa sababu vinakula umeme sana, BAKWATA hawana uwezo wa kugharimia umeme wa LUKU kuviendesha viyoyozi hivyo, hivyo siku zote vinazimwa tuu!. Wakamuomba mfadhili huyo Mkistu, kuifadhili BAKWATA kwa fedha za LUKU kugharimia na umeme wa kuviendesha viyoyozi hivyo!. (Sikufuatilia tena kama hili lilifanyika).

Kama hii ndio hali ya BAKWATA kiuchumi, na mkumbuke BAKWATA wamepewa mamlaka ya kuanzisha mahakama za Kadhi, serikali imekubali itayatambua maamuzi ya mahakama za Kadhi, ila jukumu la uendeshaji wa mahakama hizi, liwe ni jukumu la Waislamu wenyewe na sio jukumu la serikali kuziendesha. Sasa ndugu zangu Waislamu, tujiulize, kama gharama tuu za matibabu ya Mufti ni issue, ilibidi Magufuli atie mkono wake, jee hizi gharama za kuziendesha mahakama za Kadhi, zitawezekana?!.

Namalizia kwa kukumbushia swali la msingi, kuwa hapa ilipo, BAKWATA tayari ina matatizo ya uendeshaji, Jee itaweza kugharimia uendeshaji mahakama za Kadhi?!.

Namtakia Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Alhaj, Aboubakary Zubeir, uponyaji wa haraka aejee kazini kulijenga taifa letu.

Jumapili Njema.

Pasco
Rejea za Mkristo Pasco kutetea Waislamu
Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!. - JamiiForums
 
Mkuu,japo kuna mantiki,lakini kwa mawazo yangu umelenga kumdhalilisha mufti zuberi.
Tofautisha kati ya mufti na kadhi
Kuna kadhi mkuu atakaesimamia hizo mahakama,na kwa maombi ya waislamu,walitaka serikali iendeshe,bakwata inaingiaje hapo..
halafu ulisahau pia baba askofu methodius kilaini,alishapelekwa India kwa hela ya kikwete,unataka tuamini kanisa kubwa kama roma halina fungu la bima kwa kiongozi kama kilaini
 
Hao toka walipouza eneo lile la keko lililotengwa kujengwa msikiti Mkubwa pale mimi nawachukulia kama chombo cha kihuni kwa maslahi yao binafsi kwa mgongo wa dini yetu..chombo kipo kwa ajili ya kuomba na kupata misaada tu na si kuweka mikakati ya kimaendeleo..
 
Mtoa mada usinchekeshe, bakwata ni tawi miongoni mwa matawi ya sisiemu na serikali yake, tena unavyomfananaisha mufti na kadinali ndio unaingia chaka, maana huyo mufti kabla hajachaguliwa kadinali na ccm wanakaa wanampitisha, hivyo kumhudumia na kumgalamia ni jukumu Lao wala hakuna cha ajabu hapo kilichofanyika
 
Pasco Ndugu MTANZANIA kwanza ni kupongeze kuweza kulingamua ufadhili huo !!!!
Hapo umefananisha Ndege wa aina mbili kuwa wote ndege yaani Mwewe (eagle0 na kuku wote ni ndege...!! Toka niifahamu BAKWATA nina amini haijawahi somesha mwananchi njee ya TZ kwa gharama zake !! hiyo toosha kabisa kuProve Umbumbumbu wake !! AIBU TUPU !!
Halafu Unazungumzia BIMA !! ? !! ikiwa fedha za kununua kitu hadi wabembeleze na kuomba obma !!
Mungu anisamehe na ndugu wa isalm wanisamehe!!!
 
mleta uzi kwanza naomba uyajue haya
1.BAKWATA si chombo kinachowawakilisha waislamu wote. nadhani unajua au umesikia harakati nyingi zinafanyika/zimefanyika ili waislamu wa Tanzania wawe na chombo kinachowawakilisha kilichoridhiwa na waislamu wote. usiniulize BAKWATA inamuwakilisha nani kwa sasa mana jibu lake halihitaji PHD kujua
3.Mufti ni wa BAKWATA kama chombo na si wa WAISLAMU WOTE
4.BAKWATA sio inayodai mahakama ya kadhi bali ni WAISLAMU WA TANZANIA
5.kwa kuwa BAKWATA ipo kwa maslahi ya watu "fulani" , hivyo hata uendeshaji wake uko kimkakati huo na usihusishwe na uendeshaji wa mahakama ya kadhi ambayo kimsingi uendeshaji wake hauzingatii BAKWATA bali Qur-an na Sunnah ambavyo havitegemee mikakati na uendeshaji wa watu "fulani"
6.Suala la mufti wa BAKWATA kulipiwa matibabu lipo kimkakati kwa maslahi na kipropaganda ya watu "fulani". Hivyo kuwashukuru "wadau" si geni hilo na lilitegemewa
7.ikiwa unaona waislamu wa Tanzania pamoja na utajiri wao wameshindwa kumhudumia mufti "wao" juwa kua huyo ni mufti wa BAKWATA, ingekuwa ni mufti wao WASINGESHINDWA(ng'ombe haelemewi na nunduye)
8.Mahakama ya kadhi inaweza kuendeshwa BILA uwepo au usimamizi wa BAKWATA ikiwa tu suala hilo litasimamiwa na Waislamu wa Tanzania wenyewe kwa ujumla wao na sheria kuipa meno mahakama hiyo kwa kuitambua uwepo wake na uhuru wake.

Mashaalah majibu mazuri yenye kujitosheleza.

Mleta Mada naamini ukweli ana ujua vizuri, hakuna mtu yoyote anae fuatilia siasa za Tanzania vizuri halafu asijue ukweli kuhusu bakwata.

Bakwata wapo kwaajili ya serekali na kwa maslahi ya serekali wala hawana msaada kwa waislam na kamwe hawa wawakilishi waislam wote wa Tanzania.
 
Sasa kwanino msikivunje,si chenu waislamu! Huwa mpo mbele sana kupinga mambo kinyume na imani yenu! Sasa hili la bakwata kuwa ya kikafiri mbona mpo kimya!
Ni suala la kutumia akili tu. Yuko wapi Sheikh Ponda Issa Ponda? Yuko wapi Almarhum Ustaadh Ilunga Kapungu? Yuko wapi Sheikh Bassalleh? Yuko wapi Ustaadh Prof. Ibrahim Lipumba? Mfumo Kristo umewakandamiza hawa. Wengine wamekufa sio vifo vya ahadi bali Makafiri wamewaua. Wote hawa walikuwa chachu ya kuiondosha Bakwata, lakini Makafiri wamewazidi nguvu. Lakini Inshaaalah Bakwata itarudi kuwa mali ya Waislam. Ni suala la muda tu
 
Makafiri ndio hawa kina Mufti? Maana ndio viongozi wa bakwata.
 
japo si mwislamu naomba nichangie na kama nitawakwaza naomba mnisamehe
Nafikiri tatizo kubwa la bakwata ni usimamizi na uendeshaji wa chombo chao badala ya kusimamia mali zao wamegeuza kama miradi ya watu wachache mfano kama wameweza kuuza mali ya wakfu ambayo kisheria haitakiwi kuuzwa,wameshindwa kuhakikisha shule zao zinafanya vizuri pia bado wana maeneo mengi mazuri ambayo wangeweza kufanya vitega uchumi
 
Waislamu waliowengi hawaiungi mkono BAKWATA sababu licha ya kuwa tawi la CCM imeanzishwa kwa amri ya serikalj ya Nyerere (upo Uzi huu JF)
Pamoja na hayo je ni Mufti ndiye aliyeomba msaada au Magufuli kwa sababu zake ziwazo zozote zile kaamua mwenyewe kulipa
Yawezeka labda kumweka in check or othe political mileage
 
mleta uzi kwanza naomba uyajue haya
1.BAKWATA si chombo kinachowawakilisha waislamu wote. nadhani unajua au umesikia harakati nyingi zinafanyika/zimefanyika ili waislamu wa Tanzania wawe na chombo kinachowawakilisha kilichoridhiwa na waislamu wote. usiniulize BAKWATA inamuwakilisha nani kwa sasa mana jibu lake halihitaji PHD kujua
3.Mufti ni wa BAKWATA kama chombo na si wa WAISLAMU WOTE
4.BAKWATA sio inayodai mahakama ya kadhi bali ni WAISLAMU WA TANZANIA
5.kwa kuwa BAKWATA ipo kwa maslahi ya watu "fulani" , hivyo hata uendeshaji wake uko kimkakati huo na usihusishwe na uendeshaji wa mahakama ya kadhi ambayo kimsingi uendeshaji wake hauzingatii BAKWATA bali Qur-an na Sunnah ambavyo havitegemee mikakati na uendeshaji wa watu "fulani"
6.Suala la mufti wa BAKWATA kulipiwa matibabu lipo kimkakati kwa maslahi na kipropaganda ya watu "fulani". Hivyo kuwashukuru "wadau" si geni hilo na lilitegemewa
7.ikiwa unaona waislamu wa Tanzania pamoja na utajiri wao wameshindwa kumhudumia mufti "wao" juwa kua huyo ni mufti wa BAKWATA, ingekuwa ni mufti wao WASINGESHINDWA(ng'ombe haelemewi na nunduye)
8.Mahakama ya kadhi inaweza kuendeshwa BILA uwepo au usimamizi wa BAKWATA ikiwa tu suala hilo litasimamiwa na Waislamu wa Tanzania wenyewe kwa ujumla wao na sheria kuipa meno mahakama hiyo kwa kuitambua uwepo wake na uhuru wake.

Kula "like" nyingi mkuu
 
Sasa kwanino msikivunje,si chenu waislamu! Huwa mpo mbele sana kupinga mambo kinyume na imani yenu! Sasa hili la bakwata kuwa ya kikafiri mbona mpo kimya!
Nani yupo kimya? unless si mfuatiliaji wa mambo....
unauliza kwa nini tusikivunje, hivi umesahau aliekiunda ni nani? kasome historia ya kuundwa kwake utajua kuwa kwa nini kukivunja ni kigumu.... umewahi kuisikia EAST AFRICAN MUSLIM WALFARE SOCIETY ? Katafute nani aliivunja? na alipoivunja aliunda nini?.....jifunze kufatilia majambo.
 
Tena kuivunja hiyo bakwata ya sasa ni sawa na kuivunja ccm
 
Back
Top Bottom