BAKWATA ifuate mfano wa KKKT

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,495
51,089
Kanisa la Kilutheri la Kiinjili Tanzania limetoa muongozo kwa viongozi wake wa dini waache kujihusisha na siasa.

Jambo hili ni jema haswa ukizingatia kuwa Kanisa hilo lina waumini ambao wana mrengo wa vyama tofauti vya siasa kwa hiyo siyo busara kwa viongozi wa kiroho wa kanisa hilo wakijihusisha kuwa na upendeleo maalum wa kisiasa kwa vyama fulani.

Kwa bahati mbaya, BAKWATA ya Waislamu inatia aibu. Yenyewe imejinasibisha na watawala na kwa kila ajuaye kusoma matendo, basi hatoacha kung'amua wazi kuwa BAKWATA inatumika na watawala kisiasa na viongozi wake wanatumika kisiasa kwa ajili ya manufaa ya chama tawala CCM.

Tumeona kongamano la dini eti la kupongeza utendaji wa serikali ya awamu ya tano lililoratibiwa na sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam (BAKWATA), Ni dhahiri kongamano hilo ni kampeni ya wazi ya kisiasa ya kumpigia chapuo mgombea wa CCM kupitia mgongo wa dini. Hili ni jambo lisilokubalika hata kidogo!

Nawashauri BAKWATA, kama wanataka kuheshimika mbele ya jamii na umma wa Waislamu kiujumla basi wafanye mambo kwa maslahi ya Waislamu kuliko watawala.

Kwa mfano leo hii viongozi wa dini ya waislamu wako jela takriban miaka sita na ushehe, lakini BAKWATA wapo utadhani hilo haliwahusu. Sijawahi kumsikia Sheikh Mkuu au huyo Alhadi mpenda kukaa karibu na watawala hasemi chochote. Sijawahi kusikia wakiitisha dua kuwaombea afya viongozi hao au hata kuongea na waislamu wenzao juu ya hali na mustakbali wa Waislamu wenzao walioko jela na kesi yao kupigwa danadana kila kukicha.

Swali la msingi la kujiuliza, hao BAKWATA wanapojifanya kujali maslahi ya nchi kwa kutaka upendo baina ya wananchi wao wenyewe wameounyesha vipi huo upendo kwa waumini wenzao wanaosota jela huko miaka na miaka huko bila kuhukumiwa na mahakama nchini?

Kama BAKWATA imeshindwa ku-play role kunusuru Waislamu wenzao huko jela, watajifanya vipi kuwa wao ni chombo cha maslahi kwa nchi nzima?

Nawashauri BAKWATA badala ya huu ushirika na watawala unaowatia upofu kusimama kwa ajili ya masilahi ya waislamu basi waachane na kupenda ulua au kujikurubishakurubisha kwa watawala badala yake wakemee maovu, wasimamie haki, na wawaeleze watawala kuwa jambo kadha wa kadha siyo sawa!

BAKWATA isiwe nyapara wa kuwatuliza Waislamu wanapokuwa na madai yao ya msingi juu ya serikali, au isitumike kama tambala la serikali kujisafisha pindi inapokosea waislamu au hata umma.

Kwa mfano, majuzi hapa Sheikh Ponda alizungumza juu ya teuzi nchini zilizokaa kidini, kwamba katika awamu hik ya utawala, teuzi nyingi zimelalia upande mmoja lakini BAKWATA haikemei suala hili. Sasa katika hali kama hii BAKWATA haitopata heshima stahili kutoka kwa umma wa Waislamu nchini.
 
Bakwata ilianzishwa na mwl Nyerere kwa kushirikiana na Paulo Bomani

1660090_FB_IMG_1514731600839.jpg
 
Gwajima na Kakobe na shehe katimba 2015 mlipokuwa nao chadema bega kwa bega walikuja kuwadhibiti?

Mumekosa support ya viongozi wa dini sahabu hamna political strategy
[/QU
hao ni mateka wenu wapo ccm kimwili kwa vitisho, mmoja baada ya kuunga juhudi amekuwa mtanzania na pasipoti yake mkarudishia,mwingine anaogopa UNO part two hivo ni lzm waunge juhudi kwa lazima.Pili yale makanissa yenye usajili wa pencil kwa hofu ya msajili kupewa maaizo ya kuyafuta ni lazima yawe mateka wa ccm ili yaendelee kusanya sadaka
 
Uzuri ni kwamba tunaungwa mkono na Waumini wao
Mliongea nao lini tarehe ngapi na wapi hao waumini wao? Minute ziko was za kikao na za majina ya waliohudhuria hicho kikao Cha kuwaunga mkono? Mwenyekiti wa kikao alikuwa Nani na katibu alikuwa Nani?
 
Gwajima na Kakobe na shehe katimba 2015 mlipokuwa nao chadema bega kwa bega walikuja kuwadhibiti?

Mumekosa support ya viongozi wa dini sahabu hamna political strategy
Hatuhitaji support ya 'viongozi' wa dini tu bali tunahitaji support ya Watanzania wote.
 
Mliongea nao lini tarehe ngapi na wapi hao waumini wao? Minute ziko was za kikao na za majina ya waliohudhuria hicho kikao Cha kuwaunga mkono? Mwenyekiti wa kikao alikuwa Nani na katibu alikuwa Nani?
Dada mkubwa tayari umeshapanic. Maswali yako ni ya kitoto sana.
 
Back
Top Bottom