BAKWATA fungueni akaunti ili waislamu watoe zaka za mali zao

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
2,699
3,088
Umefika wakati sasa kama utawekwa utaratibu mzuri na uwazi waislam wa Tanzania wanaweza wakaanza kutoa zaka za Mali zao wanazomiliki kila mwaka.

Inawezekana kabisa waislam wanatamani sana kutoa zaka za Mali zao kama dini yetu inavyotaka lakini je ! Utaipeleka wapi na itatumika vipi?

Kama utawekwa utaratibu mzuri wa kukusanya hizi pesa zingeweza kusaidia sana kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi miongoni mwa waislam kama vile
  • Huduma za afya
  • Elimu
  • Na hata waislam kuchukua mikopo isiyo na riba

BAKWATA mnatakiwa akili zenu ziwe zinachaji na kuweka ubunifu jinsi ya kuiongoza jamii ya kiislam kisasa bila ya kutoka katika misingi ya dini

Nilisikitika sana kipindi kile mfalume wa morroco anawauliza BAKWATA mnataka nikufanyieni nini mkachagua mjengewe msikiti hivi kweli waislam wa Tanzania tuna shida ya misikiti kwanza uzuri wa msikiti muujenge wenyewe waumini kwa michango yenu mtapata fadhira nyingi kutoka kwa Allah na sio nyinyi mkae tu aje mtu akujengeeni alafu nyinyi kazi yenu kuingia tu kufanya ibada

Mlitakiwa mumwambie mfalume wa Morocco atujengee Hospital au chuo cha ufundi ili watoto wa kiislam wapate ujuzi
 
Umefika wakati sasa kama utawekwa utaratibu mzuri na uwazi waislam wa Tanzania wanaweza wakaanza kutoa zaka za Mali zao wanazomiliki kila mwaka....
wakristo wao zaka nimesikia eti wanawapelekea sijui walawi na wachungaji ziwafae kimaitaji,

Sijajua ukweli upoje,

Na sijajua na kwa upande wa Waislamu zaka Ni kwajili ya kundi gani labda
 
Kuna watu aina 7 ya kupewa zaka...(masikini, wasafiri walioharibikiwa, walio fisabilillah, wanaodaiwa, kuwaachia watumwa huru, fakiri.

Sio suala la undugu wa mtoto wa mjomba wala shangazi

Allah aalam
Wakati wa mtume na maswahaba zakatul limali ilikuwa inakusanywa vipi? Tume elimu kidogo
 
Hiyo itakua ni ajenda ya kuichangia CCM pesa, Kule Zanzibar ilishapitishwa na Baraza la kutunga Sheria, Serekali inataka kukusanya Zaka.
 
wakristo wao zaka nimesikia eti wanawapelekea sijui walawi na wachungaji ziwafae kimaitaji,

Sijajua ukweli upoje,

Na sijajua na kwa upande wa Waislamu zaka Ni kwajili ya kundi gani labda
Uzi wa mdau mzuri ila unauharibu kijinga kabisa.

Wakristo wameingiaje kwenye uzi uhusuo waislam??
 
Mnachekaga na kukebehi sisi wakristo tunapotoa sadaka??!!sasa na nyie mmeona kupewa na waarabu ni sio😂😂 sasa nikuambie tu mmeisha jizoesha hivyo hawatatoa utatoa wewe peke yako watakuambia din sio biashara 🤣🤣🤣 jaribu kuwaambia uone, sisi wakristo raha sana coz tangu watoto tunafundishwa kutoa
 
Mnachekaga na kukebehi sisi wakristo tunapotoa sadaka??!!sasa na nyie mmeona kupewa na waarabu ni sio sasa nikuambie tu mmeisha jizoesha hivyo hawatatoa utatoa wewe peke yako watakuambia din sio biashara jaribu kuwaambia uone, sisi wakristo raha sana coz tangu watoto tunafundishwa kutoa
Zaka tunatoa Mbona Mkuu ila kuna makundi maalum ya kuwapa sio lazima umpe Sheikh au upeleke Msikitini
 
Inawezekana kabisa waislam wanatamani sana kutoa zaka za Mali zao kama dini yetu inavyotaka lakini je ! Utaipeleka wapi na itatumika vipi?
Wewe bwana toa zaka usitoe visingizio, mbona wenzako huwa tunatoa kila mwaka?

Wa kuwapa huwezi kuwakosa hata kidogo, mfano kijijini kwako au ndugu zako ambao hawakutegemei moja kwa moja.

Hata matajiri kama Bakhressa huwa wanatoa zakka lakini hawapendi kujionyesha.
 
Back
Top Bottom