Kachanchabuseta
JF-Expert Member
- Mar 8, 2010
- 7,269
- 675
HISTORIA ya dunia hii imesheheni ushahidi wa kutosha kabisa kutuonyesha kwamba mambo makubwa makubwa ya kutisha chni ya jua yameanza kama masihara na katika vitu vidogo vidogo tu ambavyo watu wangeweza kudhani kwamba havina maana wala msingi wowote.
Ndiyo maana watu makini na viongozi mahiri duniani kote hawapuuzi mambo yanayodhaniwa na wengi kuwa ni madogo au ni ya kupuuzwa, hii ni kwa sababu mambo madogo yasipoangaliwa kwa makini yanaweza kutumiwa na watu wachache yakakuzwa na hata kuwa balaa kwa taifa na jamii husika.
Ninazungumzia kile kilichotokea kwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Mama Fatma Kimario na wafuasi wanaodhaniwa kuwa ni wa CHADEMA. Wakati hakuna mtu mwenye akili zake timamu, ikiwemo safu hii, anaweza kuunga mkono vurugu za aina yeyote ile au matumizi ya aina yoyote ile ya nguvu katika kutatua tatizo, wako watu wanaonyesha kila dalili za kulishadidia suala hili kwa maslahi ya kisiasa.
Na kwa muktadha huo, safu hii inajikita katika kujadili masuala mawili yatokanayo na sakata hilo, kwanza ni taarifa ya BAKWATA na BASUTA kutaka CHADEMA iombe radhi Waislamu kwa kuwa wamemdhalilisha mama huyo kwa kumvua hijabu (au mtandio aliokuwa amejitanda kichwani kama maadili ya Kiislamu yanavyowataka wanawake wa Kiislamu wawe).
Kama ambavyo mchangiaji mmoja katika mtandao wa Jamii Forum alivyochangia kuwa Ndugu zangu Waislamu kwa hili mnapotoka sana. Padri aliyebaka hawezi kusubiriwa avue kanzu yake ndio akamatwe, vazi ni nini kwani? Vazi si alama ya imani ya Uisilamu bali ni utambulisho ambao hata shetani anaweza kujigubika humu. Uisilamu ni upendo, ni moyo wa kujali haki na kuzingatia uadilifu tunapopewa majukumu ya kusimamia haki vitu ambavyo DC yule kwa siku ile alivikosa. Chonde sana viongozi wa BAKWATA na BASUTA tuepuka kuingia kwenye siasa kwa kuwagawa Watanzania kwa kutumia imani zetu hata pale ambapo hakuna uhusiano
Ninaamini Clouds FM wanalijua hili, lakini katika moja ya vipindi vyao, mtangazaji wao( Epharim Kibonde) akizunguza kuhusu sakata hili la Mkuu wa Wilaya wa Igunga, amenishtua na kwa hakika nimeogopa. Mtangazaji huyo katika moja ya vipindi anapolivisha suala hili sura ya kidini kwa kiwango kile, huku akijua kuwa wasikilizaji wake wana viwango tofauti sana vya uelewa sijui alikuwa anadhamiria kuiambia nini jamii.
Mtangazji huyu amekwenda mbali (mbali sana) kupandikiza hisia za udini wa hali ya juu kwenye suala hili, anapozungumzia habari za kwamba eti Waislamu nao wakifikia hatua ya kuwavua watawa Wakatoliki vilemba vyao kama alivyofanywa mkuu wa wilaya, kwa hakika hii ni hatari sana kwa umoja na mshikamano wa taifa hili.
Maadili ya taaluma hii yanatutaka tusema ukweli tu na ukweli mtupu kwa manufaa ya ustawi na mshikamano wa jamii tuliyomo.
Tukifika mahali tukaanza kuwianisha hisia zetu au ushabiki wetu katika mambo tete na nyeti kama imani za dini tunakuwa hatuitendei haki nchi yetu wala sisi wenyewe.
Kwa sababu, hebu tufikiri pamoja kwa sauti, hivi katika hili Ukatoliki au watawa Wakatoliki wamehusika vipi, Je, mtangazaji huyu anaweza kusema kwa uhakika aliyosema anawasemea Waislamu, amefanya utafiti kiasi gani au akajiridhisha kwa kiwango gani suala hili linahusu Ukristo na Uislamu?
Hapana, tusilifikishe taifa hili mahali ambapo halitakuwa tena taifa moja tunalojivunia sasa kwa ajili tu ya kuwanufaisha watu wachache au kwa maslahi ya nani sijui. Hatimaye Tanzania kwa Watazania ni juu ya kila kitu, utaifa wetu unakuja kwanza na mengine yatakuja baadae, tutumie nafasi zetu na mamlaka tuliyo nayo katika jamii kuhakikisha tunahamasisha umoja zaidi kuliko kupandikiza mbegu za kutugawa, tunaweza kudhani ni mbegu ndogo sana, lakini madhara yake ni makubwa kuliko tunvyoweza kufikiri.
Wapo miongoni mwetu, wanachukulia kitu wanachosikia redioni, runigani, au kwenye gazeti kama ni ukweli halisi wa kila jambo, kwa hiyo hata kama tunafanya masihara tusifanye masihara ya hatari namna hiyo, historia ya taifa hili isije ikatuandika kwenye kitabu cheusi.
Mungu ibariki Tanzania
Sosi: Tanzania Daima