Bakwata Arusha kwa fukuta,walimu wamfungia Mkuu wao Wa shule ofisini

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
572
1,000
Mkuu Wa shule ya sekondari bondeni inayomilikiwa na taasisi ya dini ya Bakwata,jijini Arusha Rahimu Masawe amekiona cha moto Mara baada ya ofisini yake kugeuka lokapu ya kumsurubu baada ya walimu wake kumfungia ndani ya ofisi hiyo kwa zaidi ya SAA sita kama njia moja wapo ya kushinikiza awalipe malimbikizo ya mishahara yao ya miezi mitatu mfulurizo .

Walimu hao zaidi ya 15 walifikia uamuzi huo mapema Leo alhamisi des 7. baada ya kushindwa kuelewana katika kikao cha majadiliano kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu huyo na ndipo walipoamua kumfungia ndani kwa makomeo na makufuri wakitaka pesa zao za mishahara Wa tangu September ,ambapo kwa ujumla wao inafikia sh,milioni 10.

Shule hiyo ya bondeni ni mqli ya Bakwata ila imebinafisishwa kwa mwekezaji Wa kampuni ya Zaim education development ltd ambaye ameitelekeza tangu akabidhiwe September mwaka huu

Pichani walimu wakionekana kando ya mlango Wa ofisi ikiwa imefungwa huku Mkuu Wa shule akiwa ndani

 

Random

JF-Expert Member
Jan 8, 2017
791
1,000
Walimu 15, mishahara ya miezi mitatu, kiasi cha milioni 10, wastani wa tsh 222,222.. hatari
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
41,029
2,000
naona BAKWATA WAMEKUWA WAPIGAJI TU..hawana tofauti nawale matapeli wa Lumumba...yaani yaelekea BAKWATA KUNANUKA HUU NI UZI WAPILI NASOMA KUHUSU HIZI HUJUMA ZAO
 

The Bourne

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
1,077
2,000
Huku dar tunasubiri ofisi aliyotuahidi mkuu wetu wa mkoa,
Namkumbusha tu makonda kwani ahidi ni yenye kuulizwa mbele ya mwenyezi Mungu
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,179
2,000
Sheikh Mkuu Ubwabwa wa Dar amwambie kipenzi chake Bashite aende kuokoa jahazi. Sipati picha ile shule yao ya pale Moshi kwa Sadala iitwayo Kibohae Sec ina hali gani kwasasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom