Bakuli la sadaka lililopitishwa Arumeru CCM mmejifunza nini?

hivi mkuu ccm nao wakisema wapitishe bakuri inaweza ikashndikana kuchangiwa !
EM, si kwamba CCm hawawezi lakini hili ni jambo la imani zaidi, watu uliowazoesha kuwasomba kwa roli na kuwapa elfu tano tano..haiingii akilini ukianza kuwaomba tena hela uliyowapa. Au kesho yake wakuone unanunua kadi zao, watafikiri inawezekana hela waliyotoa jana ndiyo inayotumika kununua kadi. CCM wanaweza lakini itakuwa ngumu sana kama nilivyosema hili ni jambo lakuaminiana.

Halafu vile vile inategemea na mtu anayekuomba, leo Bharesa akikuomba shilingi elfu utaona kama anakusanifu, wananchi wanajua CCM ina kila kitu si wanaona wanavyotumia mamilioni kwenye chaguzi zao, inakuwa ngumu sana kujifanya hawana pesa na kuanza kukusanya kutoka kwa wanachama.
 
Lengo la cdm ni kuweza kupata hela chafu ziweze kupita hapo huku wakijadia ni michango

Kama kawaida tatizo siyo pesa tatizo ni MATUMIZI..

Asilimia 90% itaenda kwenye kundi lile la KUPATA (mnawafahamu wanatoka wapi)

Sioni tofauti ya chadema na makanisa ya manabii yanayochupukia kama uyoga mjini..

anyway wajing ndio waliowao...
 
chama maskini unazani kitafanyaje? Na mim katu siwezi kuunga mkono chama maskini
Wewe unataka chama tajiri hujiulizi huo utajiri umetoka wapi au unamilikiwa na nani matokeo yake ni kutumikishwa kuwabeba watu fulani fulani kwa kuahidiwa kofia na tsheti.
 
Lengo la cdm ni kuweza kupata hela chafu ziweze kupita hapo huku wakijadia ni michango

Kama kawaida tatizo siyo pesa tatizo ni MATUMIZI..

Asilimia 90% itaenda kwenye kundi lile la KUPATA (mnawafahamu wanatoka wapi)

Sioni tofauti ya chadema na makanisa ya manabii yanayochupukia kama uyoga mjini..

anyway wajing ndio waliowao...


acha kuwa na imani za ajabu hivyo au ulitaka wakupe wewe uzikusanye hizo pesa. Ndiyo maana mabadiliko tz yanakuwa magumu.
 
Lengo la cdm ni kuweza kupata hela chafu ziweze kupita hapo huku wakijadia ni michango

Kama kawaida tatizo siyo pesa tatizo ni MATUMIZI..

Asilimia 90% itaenda kwenye kundi lile la KUPATA (mnawafahamu wanatoka wapi)

Sioni tofauti ya chadema na makanisa ya manabii yanayochupukia kama uyoga mjini..

anyway wajing ndio waliowao...
Huo ni mtazamo wako kila mtu na perception yake.
 
Nilipita pale mida ya mchana Tengeru, vijana walikuwa na shamra shamra sana: nimeingia hata A town utafikiri kuna uchaguzi mkoa wote..Big up CDM. Ngoja tuone na Magamba watatokaje!
 
Huo ni mtazamo wako kila mtu na perception yake.

Kwa mara ya kwanza unajibu kwa upole..aisee umekua hongera..

Kweli huo ni mtazamo wangu..mkiweza kutumia vema (ambayo ni very remote hilo kutokea)

Mnaweza kudhibiti pesa kutoka kwa wauza unga na uchafu mwingine? just curious
 
hakika hii ni picha nzuri kwa jamii.tunaomba waweke namba wazi za kuchangia.nasi tuchangie.
 
hivi mkuu ccm nao wakisema wapitishe bakuri inaweza ikashndikana kuchangiwa !

CCM watapokea toka kwa mafisadi wenzao, tunajua jinsi wafanya biashara wasio waaminifu wanavyojikomba kwa CCM ili iwalinde kwenye biashara zao, tunajua CCM wanavyojaziwa mafuta bure full tank kwenye kampeni lkn sio kwa kuipenda CCM bali kujikomba ili walindwe na waendelee kuinyonya Tz.
 
Waungwana mimi ni shuhuda wakilichotoke leo ktk ufunguzi wa kampeni za CHADEMA nimeshuhudia kina mama, vijana pamoja na baba zao wakisubiri ufunguzi huo tangu saa nne asubuhi mpaka saa nane mchana waheshimiwa wabunge pamoja na mgombea mwenyewe (Joshua Nassary) walipowasili ktk viwanja vya shule ya msingi Leganga wananchi walianza kushangiliakama ndio kwanza nao wamefika muda huo na walikaa mpaka mwisho wa kampeni hizo na mpaka sasa hivi ni saa 7:40 usiku watu bado wako sambamba na viongozi wa o katika kambi ya CHADEMA iliyoko ktk hoteli ya Rhino hapahapa Usa-River..... Peoplessssss



Nimetoka Rhino sasa hivi
 
Hapo CDM wamejenga OWNERSHIP ya chama kwa wananchi, kwa wao kuchangia fedha ktk kampeni kwahyo wananchi watakuwa wao ndio wamiliki wa kampeni kwa kuwa wao ndio wamefadhili, watalinda kura zao na watamtetea mgombea wao.
Waache watakaoponda waponde tu

Wakuu jambo moja lililowazi ni kwamba ccm inauza nchi kwa kupitia mwamvuli wa ubinafisishaji. Pesa wanazozipata wanatumia kuhonga, kununua shaahada za kura, pamoja na kufanyia mambo mengine ya anasa. Kwa upande wa pili wa shilingi CDM wanaikomboa nchi kwa kutumia nguvu ya umma kwa hali na mali. Hata vitabu vya dini vinasema kuwa hakuna mwanajeshi anaeenda viitani kwa gharama zake mwenyewe. Hata makamanda wa CDM ni lazima wapelekwe katika vita hivi vya ukombozi kwa gharama za wenye nchi. Hata Mungu mwenye ndiye mmiliki wa vitu vyote lakini bado anawataka watu wake wamtolee sadaka kila mtu kwa kadiri ya kufanikiwa kwake. Kama huamini hili soma 1Wakoritho 16:1-2. Nawasilisha!
 
ni kweli mkuu.mimi niko manyoni lakini nimechangia.NO. ya mpesa ni
0757-755333
imesajiliwa as CHADEMA ARUSHA.


Namba nyingine ya
Mpesa ni 0763744334
Tigopesa 0655783333 or
Airtel Money 0684425222؛
Verifiy kabla ya kutuma. Namba hizi ni kwa mujibu wa Mh. Mbowe leo hapa Leganga
 
Hii inaonesha kuwa wananchi wa Arumeru wanaimani nzuri na chama kikuu cha upinzani,wito wangu kwa Wameru chagueni CDM
 
kuchangia kampeni ni sawa cdm lakini mbona kuchangia maendeleo kwenu mnaona sy haki? Tunawaangalia kwa macho mawili ninyi ni chama hatari sana.
Unawahukumu mapema mno! Je umewapa nafasi ya kuuendesha uchumi wa nchi ili watoe mchango wao kikamilifu? walioushikilia usukani hivi sasa ndiyo wanatakiwa kuchangia maendeleo sawasawa, sasa wenyewe wakisafiri wanabeba $4000.00 mfukoni huo ndiyo mchango wao? Au wanalala hoteli za laki nne kwa usiku mmoja?
 
Back
Top Bottom