Bakuli la sadaka lililopitishwa Arumeru CCM mmejifunza nini?

EL MAGNIFICAL

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
938
125
wanajamvi ni wazi kwa waliotizama ufunguzi wa kampeni arumeru mjionea wazi jinsi watu walivyohamasishwa na wakahamasika kutoa kitu chochote kama sadaka kuichangia cdm.
Hii inaonesha wazi ni jinsi gani wananchi walivyo na imani na chadema kwani wao ndio wametoa pesa kuimarisha chama, tofauti na ccm ambao wao hutoa pesa ili wachaguliwe.
Je ccm mmepata funzo gani hapa !
Nyie mnatoa pesa kwa wananchi wao wanazipeleka chadema.
Nikiwa bado pale pale Arumeru cdm imejinadi kuwasaidia wananchi ktk kujikwamua kwenye umasikini na ni moja kati ya sera zao ktk mikutano yao nchi nzima.
Kama mmetambua wananchi hao ni masikini je ni fair kuwaomba watoe sadaka japo si lazima !
Na idadi yao kubwa ndio hao waishio chini ya $ 1 !
Nawasilisha.
 
Kutoa ni moyo. Masikini akitoa Tzs. 1 ina dhamani kuliko tajili kutoa Tzs 1m. Nadhani Chadema wanatambua kuwa matumizi yao yanaweza kutoshelezwa na michango midogo kutoka kwa watu wenye mapenzi mema na masikini kuliko CCM kuchukua hela hazina na baada ya muda wanalia serikali haina pesa kumbe wanaziba mapengo ya pesa zilizotumika katika chaguzi (Linganisha kati ya TZS 220m vs TZS 6.2m za kuwapata wagombea)
 
nimeipenda sana hatimaye hata kama wapo watakaoponda ukweli utabaki palepale kuwa sasa vyama makini vinaanza kuonekana. na wanachama wanajua kuwa wanachangia ili lengo linatimie. kumbuka mbunge mmoja wa cdm ni sawa na .......hivyo akiongezeka wa arumeru ni sawa na wakiongezeka 30. hata maneno ya mgombea yanatia moyo kuwa kuna kamanda mwingine anakuja ndani ya kikosi.
 
mkuu ujue siasa ilivyo smtym ni kichefu chefu hayo maneno kwenye mabano akina mwigulu wakiludi kujb ndio utashangaa !
Na ukiwa na roho nyepesi utaishia kusema SIASA NI MCHEZO MCHAFU.
 
nimeipenda sana hatimaye hata kama wapo watakaoponda ukweli utabaki palepale kuwa sasa vyama makini vinaanza kuonekana. na wanachama wanajua kuwa wanachangia ili lengo linatimie. kumbuka mbunge mmoja wa cdm ni sawa na .......hivyo akiongezeka wa arumeru ni sawa na wakiongezeka 30. hata maneno ya mgombea yanatia moyo kuwa kuna kamanda mwingine anakuja ndani ya kikosi.
nimeipenda hii joshua anasema alikuwa mbunge kabla ya saa 6 usiku, siku ya matokeo ya uchaguzi uliopita lakini aliposikia AMEINAMA AMEINUKA hakuwa mbunge tena !
 
Hapo CDM wamejenga OWNERSHIP ya chama kwa wananchi, kwa wao kuchangia fedha ktk kampeni kwahyo wananchi watakuwa wao ndio wamiliki wa kampeni kwa kuwa wao ndio wamefadhili, watalinda kura zao na watamtetea mgombea wao.
Waache watakaoponda waponde tu
 
hivi mkuu ccm nao wakisema wapitishe bakuri inaweza ikashndikana kuchangiwa !
 
Nchi hujengwa na wananchi wenyewe, hii ni sera ya wazi iliyooneshwa na Chadema leo. Na hiyo hufanya kazi tu ikiwa hakuna ufisadi, kuna uaminifu. Wananchi wameonesha imani yao kwa chadema. Hongera Chadema, hongera wameru.
Ccma wabaki na sera zao za kiwiziwizi..... mwisho wao kaburi.
 
Waungwana mimi ni shuhuda wakilichotoke leo ktk ufunguzi wa kampeni za CHADEMA nimeshuhudia kina mama, vijana pamoja na baba zao wakisubiri ufunguzi huo tangu saa nne asubuhi mpaka saa nane mchana waheshimiwa wabunge pamoja na mgombea mwenyewe (Joshua Nassary) walipowasili ktk viwanja vya shule ya msingi Leganga wananchi walianza kushangiliakama ndio kwanza nao wamefika muda huo na walikaa mpaka mwisho wa kampeni hizo na mpaka sasa hivi ni saa 7:40 usiku watu bado wako sambamba na viongozi wa o katika kambi ya CHADEMA iliyoko ktk hoteli ya Rhino hapahapa Usa-River..... Peoplessssss
 
Lengo hasa la bakuli si pesa ni kuwajengea wanachama imani na upendo kwa chama chao wajione kuwa wanashirikishwa, tukio linaonekana kama mzaha lakini ni muhimu sana kwa uhai wa chama. Mwanachana anapotoa hata sh.1 atajiona ameshirikishwa kwa hiyo ana wajibu wa kuhakikisha imetumika vizuri, mfano atahakikisha kura anayoipiga anampa yule anayemwamini kuilinda ile shilingi yake.

Huu si mtindo mpya zamani CCM walikuwa wanachangisha wananchi, kulikuwa na mifuko ya chama mfuko wa tawi,shina nk, nakumbuka hata Nyerere nauli ya kwenda UN kudai uhuru alichangiwa na wananchi. CCM ilikuja kuacha mtindo huu pale chama kilipoingiliwa na wafanyabiashara, kidogo kidogo wakaitwa wafadhiri wa chama mwisho wakakinunua chama kizima, wanachama wakaachwa nje wafanyabiashara wakaingia ndani.
 
kuchangia kampeni ni sawa cdm lakini mbona kuchangia maendeleo kwenu mnaona sy haki? Tunawaangalia kwa macho mawili ninyi ni chama hatari sana.
 
Lengo hasa la bakuli si pesa ni kuwajengea wanachama imani na upendo kwa chama chao wajione kuwa wanashirikishwa, tukio linaonekana kama mzaha lakini ni muhimu sana kwa uhai wa chama. Mwanachana anapotoa hata sh.1 atajiona ameshirikishwa kwa hiyo ana wajibu wa kuhakikisha imetumika vizuri, mfano atahakikisha kura anayoipiga anampa yule anayemwamini kuilinda ile shilingi yake.

Huu si mtindo mpya zamani CCM walikuwa wanachangisha wananchi, kulikuwa na mifuko ya chama mfuko wa tawi,shina nk, nakumbuka hata Nyerere nauli ya kwenda UN kudai uhuru alichangiwa na wananchi. CCM ilikuja kuacha mtindo huu pale chama kilipoingiliwa na wafanyabiashara, kidogo kidogo wakaitwa wafadhiri wa chama mwisho wakakinunua chama kizima, wanachama wakaachwa nje wafanyabiashara wakaingia ndani.

mkuu umeeleza vizuri sana nashukulu kwa darasa huru.
 
Back
Top Bottom