SI KWELI Bakteria walio kwenye maziwa ya Mtindi ni wale wanaopatikana Ukeni

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
1730361633625.jpeg
 
Tunachokijua
Maziwa mtindi ni maziwa yaliyoganda na yenye ladha ya uchachu, yanaweza kutengenezwa kwa njia ya asili au kwa kuongezewa bakteria wazuri. Yogurt ni aina ya maziwa mtindi yaliyochakatwa kwa kuongezewa bakteria wajulikanao kama Lactobacillus bulgaricus na Streptococcus thermophilus baada ya kuchemshwa kisha huachwa kwa muda wa saa kadhaa katika eneo lenye kiwango cha joto kati ya 110-115°F. Bakteria hao wakiwekwa kwenye maziwa hayo huibadili sukari iliyopo kwenye maziwa ijulikanayo kama lactose kwenda kwenye lactic acid ambayo huyafanya maziwa kuwa laini zaidi na kuyapa ladha ya tofauti.

Kumekuwepo na madai kuwa bakteria wanaopatikana kwenye uke ni sawa na bakteria wanaotumika kutengeneza maziwa mtindi (Yogurt).

Ukweli upoje kuhusu madai hayo?

Uke ni sehemu ya mfumo wa uzazi wa mwanamke ambao una bakteria tofauti tofauti, kwa mujibu wa maktaba ya taifa ya dawa ya Marekani NIH wanaeleza kuwa bakteria wengi kwa uke wenye afya ni aina ya Lactobacillus, bakteria hawa husaidia kudumisha pH ya uke, kuzuia ukuaji wa bakteria hatari ambao wanaweza kusababisha maambukizi. Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na tovuti ya microbial cell factories wanaeleza kuwa aina ya bakteria wa Lactobacillus wanaopatikana katika uke wa binadamu mwenye afya unajamuisha Lactobacillus crispatus, Lactobacillus gasseri, Lactobacillus iners, and Lactobacillus jensenii.

Cecilia Westbrook aliyekuwa mwanafunzi wa shahada ya Uzamivu (PhD) mwaka 2015 alifanya utafiti kwa kutumia bakteria wa ukeni kwake kutengeneza maziwa ya mtindi na baada ya usiku mzima akaja kuonja maziwa hayo na kubaini kuwa yamebadilika na kuwa machachu. Westbrook alichukua kijiko cha mbao na kukiweka ukeni mwake kisha akakitoa kijiko hiko na kukiweka kwenye bakuli lililokuwa na maziwa. Mara baada ya Jaribio hilo mwanabayolojia Rosanne Hertzberger alisema kuwa wazo la kufanya jaribio hilo halikuwa zuri kwani uke una bakteria wa aina mbalimbali wazuri na wabaya, ingawa jaribio lilikuwa zuri.

Taasisi ya uhakiki wa taarifa ya Dubawa ilifanya mahojiano na mtaalamu wa afya, Omale Ogbe ambaye alisema kuwa bakteria waliopo kwenye uke sio sawa na wanaotumika kwenye kutengeneza maziwa mtindi (yogurt) kwa kuwa bakteria wamegawanyika kwenye makundi tofauti. Bakteria hao wanaweza kuwa kutokea katika ukoo mmoja ila wakawa katika makundi tofauti, mathalani bakteria wanaopatikana ukeni Lactobacillus kundi la (Lactobacillus crispatus, Lactobacillus iners, Lactobacillus. jensenii, na Lactobacillus gasser) na bakteria wanaotumika kutengeneza maziwa mtindi (yogurt) Lactobacillus kundi (Lactobacillus delbrueckii subsp. bulgaricus).

Dubawa wanaeleza kuwa huenda bakteria hao wana mfanano lakini hawako sawa. Bakteria wa mtindi huchaguliwa kwa uwezo wao wa kuchachusha maziwa na kuunda ladha na umbile mahususi, wakati bakteria wa uke wanatokea kiasili na wana jukumu muhimu katika kudumisha afya ya uzazi.

Premiumtimes
Lactobacilus species.
Hawa kazi yao ni kutengeneza tindikali(acid) ya lactic. Ambayo kazi yake ni kulinda uke.
 
Ni kweli lactobacillus wanapatikana kwenye mtindi, wanapatikana kwenye kiungo cha utamu, nadhani hata kwenye utumbo wa mtu mzima ama utumbo wa mtoto anaetumia maziwa ya formula.
 
Ni wakati sasa kuanza kutumia kipochi manyoya ya pisi yangu ya pale Africana kutengenezea mtindi kwa kugandisha maziwa fresh.

Naamini maziwa yataganda faster maana ile pisi ina mbususu chachu sana
 
Ni wakati sasa kuanza kutumia kipochi manyoya ya pisi yangu ya pale Africana kutengenezea mtindi kwa kugandisha maziwa fresh.

Naamini maziwa yataganda faster maana ile pisi ina mbususu chachu sana
Unalambaga huko mtindi mchachu mkuu Dah
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom