Fahamu kuhusu bakteria wa H.Pylori; Athari na tiba yake

everlenk

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
11,627
15,017
1593920132773.png

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU BAKTERIA HUYU
Habari wanajamvi!!!

Naomba kujua tiba ya Helicobacter pylori( H-pylori) ni ipi? Na je huu ugonjwa unatibika ? Je wapo watu walioumwa wakapona?

Nina ndugu yangu yapata sasa miezi 6 anateseka na huu ugonjwa, anatapika sana sana mpaka tumpeleke hospital akipata nafuu akitoka tu hospital ile hali inarudi tena, sasa maisha yetu yamekuwa ni wiki 2 hospital wiki nyumbani.

Kwasasa matibabu anayapata hospitali ya Muhimbili,mara ya kwanza alipima kipimo cha OGD ikaonekana ana michubuko kwenye utumbo na kwamba hiyo ndo inasababisha maumivu makali ya tumbo maana huwa pia anapata hayo maumivu,hali ilivyozidi kuwa mbaya doctors wakasuggest apime H-pylori ambapo ikaonekana ni positive.

Kuanzia wakati huo ameendelea kupata matibabu hapo lakini bila mafanikio yoyote, dawa ambazo alishatumia ni Nexium ,Pantocid, H-pylori kit,fluconazole, Metro,na hizo za kuzuia kutapika lakini hali ndo hivyo wiki moja nyumbani wiki mbili hospital.

Naombeni ushauri juu ya hili nini kifanyike? Asanteni.
---
Wakuu habari za wakati,

Naomba kuuliza, hivi inawezekana mtu akapona hili tatizo la hpylori au anatuliza tu kwa muda, halafu linajirudia tena

Msaada wenu kwa wataalam, ambao wameshaumwa na wazoefu

Asanteni
---

Nina Hp roll positive tangu hii homa imenipata kichwani naona kama kuna fangasi yaani kichwa kama kinachemka kama kinawasha yani hata sikielewi ivi hamna machine ya kuangalia matatizo ya kichwa.

أعراض_جرثومة_المعدة_والقولون.jpg

UFAFANUZI WA JUMLA KUHUSU BAKTERIA WA H PYROL
H. pylori ni kifupi na Helicobacter pylori ni aina ya bacteria ambayo huingia kwenye mwili na kujificha ndani ya mfumo wa chakula. Nikisema mfumo wa chakula hapa ieleweke kwamba ni kuanzia mdomoni unapobugia chakula chako mpaka kwenye puru ambapo unatoa kinyesi baada ya umeng’enyaji kufanyika, hivo kumbe bacteria hwa wanapatikana hata mdomoni na wanaweza kuambukizwa kwa mdomo pia. Sasa kutokana na bacteria hawa kuwa na uwezo wa kujishikiza kwenye kuta za tumbo bila kuathiriwa na tindikali inayomwagwa tumboni basi huweza kusababisha vidonda vya tumbo na saratani pia. Nafahamu kuwa uliwahi kuambiwa kwamba vidonda vya tumbo huletekezwa na tabia ya kutokula kwa wakati ama kukaa na njaa kwa mda mrefu ni kweli ila endelea kusoma makala hiiutajifunza ni kwann H.pylori.

Ukirudi mwanzo nmesema bacteria hawa hupatikana kwenye mfumo wa chakula, kaunzia mdomoni hadi kwenye puru, sasa nini kinapelekea mpaka hawa bacteria kumuingia mtu.Chanzo cha kupata bacteria hwa ni kupitia mdomo. Bacteria hawa hupatikana kwa kiasi kikubwa kwenye maji, hivo kama maji unayokunywa hayajatibiwa ama kuchemshwa basi hatari ya kupata bacteria hawa ni kubwa zaidi, chakula pia unachokula kama kimepata maambukizi ya hawa bacteria basi ukila unameza na hawa bacteria, chanzo kingine ni kupitia ngono, najua kuna kundi kubwa la watu wanaopata maambukizi ya bacteria kupitia kufanya mapenzi kwa kunakohusisha midomo ikiwemo kunyonyana ndimi . Hivo hakikisha mpenzi wako yuko salama kabla hujamuamini manake utajiepusha si tu na H.Pylori bali pia na ugonjwa wa homa ya ini- Hepatatis B.

Vipimo vya namna ya kugundua H.Pylori
Kwa bahati nzuri hospitali zetu nyingi zinatoa huduma ya vipimo kwa gharama nafuu sana hivo kama unapata dalili ambazo nitazielezea hapo chini hakikisha unaenda hospitali kupata vipimo ili uwahi tiba mapema. Dalili hizi ni kama kujiskia tumbo limejaa mda wote hata kama umekula kidogo tu, kutapika na kupata kichefuchefu mara kwa mara, kushuka kwa uzito kwa kasi bila sababu ya msingi, mwili kuwa mzembe na kuchoka sana na maumivu makali ya tumbo, kiungulia, na kupoteza hamu ya chakula, kama tayari uliwahi kuugua vidonda vya tumbo hapo nyuma basi dactari ataangalia rekodi yako ya nyuma na kupendekeza matibabu yanayokufaa.

  • Kwenye tiba ya kisasa (conventional medicine) hatua ya kwanza Dactari wakoatakupatia dawa ya kwanza ni kwa ajili ya kuua hawa bacteria wa H.Pylori . hatua ya pili ni kutumia dawa kwa ajili ya kupunguza tindikali inayomwagwa kwenye kuta za tumbo, bada ya hapo itahitajika kufanya ufatiliaji juu ya mwenendo wa tatizo lako ili kuhakikisha kuwa linaisha kabisa.
  • Tiba asili ya H.Pylori (functional medicine); bacteria hawa wanapotibiwa mara kwa mara kupitia tiba ya kisasa zinazotolewa hospitali hufkia kipindi wanakuwa sugu yaani hawasikii dawa, nmekuwa nikipata kesi kama hizi wagonjwa wengi wanasumbuliwa na vidonda vya tumbo sugu ambavyo haviponi, vimechukua miaka mpaka mitano, mpaka wengine hupoteza tumaini. Basi unaweza kujaribu njia zingine za asili ambazo huweza kuua bacteria hawa.Njia za asili hulenga katika kuua bacteria wabaya tu na kaacha bacteria wazuri, kumbuka miili yetu imeumbwa na bacteria wazuri na wanahitajika ili kuweka msawazo.Kumbuka ni muhimu kufika hospitali kupata vipimo na ufatiliaji wa dactari juu ya tatizo lako. Tumia tiba asili kwa uangalifu na kwa kufata ushauri wa mtaalamu wa tiba asili, usinunue kila dawa mtaani zinaweza kuongeza tatizo badala ya kutibu.
UFAFANUZI NA MICHANGO KUTOKA KWA WADAU
Ugunduzi wa bacteria Helicobacter pylori na namna vinayosababisha vidonda vya tumbo peptic ulcer disease (PUD). Kwa sasa maambukizi ya bacteria Helicobacter pylori yanahusishwa moja kwa moja kama chanzo au kichocheo cha magonjwa yafuatayo:-

MAGONJWA YA MFUMO WA CHAKULA
Ugonjwa wa Uvimbe Kwenye Mfumo wa Chakula (Inflammatory Bowel Disease-IBD),
uvimbe kwenye koromeo la chakula-Esophagitis, uvimbe kwenye mfuko wa chakula anteral gastritis copus gastritis,atrophic gastritis na pangastritis, uvimbe kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo -duodernitis, uvimbe kwenye utumbo mdogo -enteritis, uvimbe kwenye utumbo mpana -crown’s disease, au hemorrhoid- bawasili.

Ugonjwa wa vidonda kwenye mfumo wa chakula (Bowel Ulcer Disease) Vidonda kwenye koromeo la chakula Esophageal ulcers, vidonda kwenye mfuko wa chakula -Gastric ulcers, vidonda kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo -Duodernal ulcers, vidonda kwenye utumbo mdogo- Illem ulcers, vidonda kwenye utumbo mpana Ulcerative colitis.

Saratani za mfumo wa chakula kama vile saratani za mfuko wa chakula gastric cancer ,MALT lymphoma, saratani ya utumbo mpana colorectal cancer (CRC).

Ugonjwa wa vimeng’enyo vya chakula kushindwa kumengenya chakula vizuri (dyspepsia) kutokana na tindikali kuzalishwa nyingi na kali sana hyperchlorhydria au inapozalishwa kidogo sana na isyokuwa kali au kutozalishwa kabisa hypochlorhydria.

MAGONJWA NJE YA MFUMO WA CHAKULA
Ugonjwa wa upungufu wa damu Idiopathic iron deficiency anaemia IDA na Idiopathic thrombocytopenic purpura ITP.

Upungufu wa vitamin B12 deficiency

Magonjwa ya Inni (hepatic Biliary Cirrhosis, hepatic Biliary sclerosis), ugonjwa wa mawe kwenye kifuko cha nyongo (Gall Stone Disease).

Magonjwa ya moyo (Cardiovascular Diseases) kama vile Ischaemic heart disease(IHD) na Ischaemic stroke

magonjwa ya mishipa ya damu (Artherosclerosis) ambayo ni ndiyo chanzo cha mtu kuugua Shinikizo la juu la damu (Hypertension) au Shinikizo la damu kwa wajawazito (Pre- Eclampsia).

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus II)

Magonjwa ya maumivu na kuvimba viungio joints kama vile:- Gout,rheumatoid Arthritis na Osteoarthritis.

Magonjwa ya ngozi, idiopathic chronic urticaria na acne rosacea na matatizo ya mzio Allergies,

Magonjwa ya maumivu na uvimbe kwenye viungo vinavyopatikana sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni Pelvic Congestion Syndrome (PCS) au Pelvic Inflammatory Disease (PID) ambapo imegundulika kuwa yanatokana na maambukizi makubwa ya bacteria Helicobacter Pylori ndani ya utumbo mpana:-

Uvimbe na vidonda kwenye figo- Chronic Kidney Injury (CKD)

Ugonjwa wa mawe kwenye figo -(kidney stone disease),

Ugonjwa wa mawe kwenye kibofu cha mkojo -urine blader stone disease,
Uvimbe,vidonda na kusinyaa kwa njia ya mkojo Urethritis au UTI sugu, na kuvimba tezi dume kwa wanaume-Prostatitis.

Uvimbe au kuziba njia ya mayai kwa wanawake- Salpingitis –uvimbe ndani ya mfuko wa uzazi- Endometriosis dalili zake ni mchango au maumivu ya tumbo la hedhi , kuharibika kwa mimba changa Spontaneous Abortion au kushindwa kushika mimba.

Utasa kwa wanaume na kukosa au kupungua nguvu za kiume-Erectile Dysfunction.

MAAMBUKIZI YA BACTERIA HELICOBACTER PYLORI AFRICA
Tafiti mbalimbali zimethibitisha kuwa vimelea hivi Helicobacter Pylori vinaambukiza kati ya mtu na mtu kupitia mate (Saliva) na pia uchafuzi wa kinyesi cha binadamu kwenye maji na chakula.

Kwenye nchi masikini ukosefu wa maji salama, uchafuzi wa mazingira, na makazi duni yenye msongamano wa watu wengi, unachangia watu wengi sana kupata maambukizo ya vimelea hivi, (Peterson et al., 2000; Aguemon et al., 2005)

Takwimu za shirika la afya duniani (WHO) zinzonyesha kuwa, nchi za Africa, kusini mwa jangwa la sahara, asilimia 80% ya wakazi wake wanaishi na vimelea vya Helicobacter Pylori na asilimia 20 % waugua vidonda vya tumbo, asilimia 60% aidha hawana dalili yeyote au wanaugua magonjwa ambayo hayana dalili zozote, (Mbulaiteye et al., 2006).

nchini Tanzania asilimia 76% ya watoto wenye umri kati 0 hadi miaka 4 walikutwa na maambukizi ya vimelea Helicobacter Pylori na maambukizi yaliongezeka hadi asilimia 99% kwa watu wazima (Mbulaiteye et al., 2006).

Maambuzi ya bacteria Helicobacter pylori huchukua muda mrefu sana kufikia hatua za ugonjwa tafiti zinakadiria wastani wa miaka kumi na tano kwa hiyo watu wengi wanaougua ni wale waliopata maabukizi makubwa wakiwa watoto chini ya miaka kumi na tano (15).

Kuna aina sita 6 za bacteria Helicobacter pylori aina na ukubwa wa dalili za ugonjwa au magonjwa yanategemea mambo makuu matatu, jambo la kwanza ni aina ya bacteria Helicobacter pylori phenotype vilivyo mpata mgonjwa,pili uwingi au kiwango cha maambukizi bacterial load, tatu ni vinasabana na Lewis factor vya mgonjwa husika.

HELICOBACTER PYLORI ANAVYOSABABISHA MARADHI
(PATHOGENESIS IN HELICOBACTER PYLORI INFECTION)

Baada ya mtu kumeza vimelea hivi kupitia mate ya mgonjwa, maji yasiyo salama, chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo salama na mikono michafu,

Vimelea hivi huweka masikani kwa kujichimbia ndani ya uteute unaofunika ngozi laini ya ndani ya mfuko wa chakula na utumbo mpana na kuzaliana na kuwa vingi , vimelea hivi huishi kwenye mfuko wa chakula na kwenye utumbo mpana kama minyoo noninvasive.

Madhara ya maambukizi yanatokana na taka taka ambazo ni sumu kwenye chembe chembe hai na viungo vya binadamu zinazozalishwa na vimelea hivi.

Vimelea hivi huzalisha aina nne za kemikali ambazo ni sumu kwa mwilini mwa binadamu cytotoxin associated gene A (cagA), vacuolating cytotoxin (VacA), lipopolysaccharide (LPS) na ammonia (NH) (T Shimoyama, J E Crabtree Gut et al., 1998;43 (suppl 1):S2–S5).

Kemikali sumu hii cytotoxin associated gene A (cagA) inahusishwa na uharibifu kwenye mfumo wa uzalishaji wa tindikali kwenye mfumo wa chakula na kusababisha tindikali izalishwe aidha kali sana na nyingi kupita kiasi hyperchlorhydria au izalishwe kidogo sana na isyokuwa kali au kutozalishwa kabisa hypochlorhydria, na pia ni kisababishi cha uvimbe na saratani ndani na nje ya mfumo wa chakula.

kemikali sumu vacuolating cytotoxin (VacA) husababisha kutokea kwa vidonda kwenye mfumo wa chakula (Bowel Ulcer Disease).

Kemikali sumu lipopolysaccharide (LPS) inahusika na kusaidia vimelea Helicobacter Pylori visishambuliwe na kinga ya mwili kwa kuipumbaza.

Kemikali sumu ammonia (NH) ni kisababishi cha uvimbe ndani na nje ya mfumo wa chakula na pia huchochea kasi ya kufa kwa chembechembe hai za mwili (apoptosis) na hivyo kudhoofisha utendaji kazi wa viungo muhimu mwilini kama vile kinga ya mwili, figo, moyo, inni, nk.

DALILI ZA MAAMBUKIZI YA HELICOBACTER PYLORI

Ingawa watu wengi wenye maambukizi ya bacteria Helicobacter Pylori hawana dalili zozote asilimia kati ya 20% na 30% wana moja au zaidi ya dalili zifutazo:-

Mgonjwa hujisikia kama anaungua kwa ndani na maumivu makali ya tumbo, tumbo kujaa gesi na kuunguluma (bloating), na Maumivu makali sehemu ya juu ya tumbo, chini ya kifua, (chembe ya moyo)

mgonjwa huupata kiungulia-heartburn hasa baada ya kula chakula chenye asili ya tindikali kama vile viazi, maharage nk.
Kufunga choo au kupata choo kigumu wakati mwingine kinakuwa kama cha mbuzi na chenye uteute mwingi (constipation).

Mgonjwa mwenye maambukizi makubwa ya vimelea hivi, hali huwa mbaya zaidi, kwani kemikali sumu hizi huzalishwa kwa wingi sana, uharibifu unakuwa mkubwa zaidi, kemikali sumu hizi na tindikali hufyonzwa na kusambaa mwili mzima, kupitia mishipa ya damu hivyo kufanya uharibifu kwenye kila kiungo muhimu cha mwili.

Mgonjwa hujisikia mchovu, mapigo ya moyo kuwa ya juu na ya kasi, homa za mara kwa mara, kuumwa kichwa na kipanda uso (migrane headache).

Maumivu ya viungo na misuli ya miguu, mikono, mgongo, mabega ,shingo n.k
Hisia za baridi, joto au ganzi kwenye nyayo za miguu, vidole vya mikono na miguu.
Kichefuchefu, kizunguzungu na kukosa hamu ya chakula.
kupungukiwa damu mara kwa mara, kwa sababu vidonda vinavujisha damu kwa ndani, kinyesi cha magonjwa hubadilika rangi na kuwa cha kahawia, damu nyingi ikivujia mgonjwa hutapika na kuharisha damu mbichi au iliyoganda, hivyo kupelekea mgonjwa kuishiwa damu anemia.

HELICOBACTER PYLORI NA MATIBABU
Matibabu yanayotolewa dhidi ya maambukizi ya bacteria Helicobacter Pylori ni mchanganyko wa dawa tatu za antibiotic au antibiotic mbili na metronidazole na pamoja na dawa za kupunguza tindikali proton pump inhibitor (PPI) HELICO KIT ambazo ni kati ya zifuatazo:-
Levofloxacin, rifabutin, tetracycline, amoxicillin, clarithromycin, metronidazole pamoja na dawa za kupunguza tindikali Omeplazole au pantocid.

Changamoto imejitokeza miaka ya zaidi ya kumi iliyopita kuwa bacteria Helicobacter Pylori amejenga usugu na dawa zote zinazotumika hivyo kushindwa kwa aina hii ya matibabu Duniani kote, na hivyo kuibua haja ya kuwa na dawa mbadala kwa matatizo na magonjwa yanayosababishwa na bacteria Helicobacter Pylori.
(J Gastrointestin Liver Dis.December 2010 Vol.19 No 4, 409-414 Dr Vincenzo De Francesco.Gastroenterologia ed Endoscopia Digestiva, Ospedali Riuniti di FoggiaFoggia, Italy vdefrancesco@ospedaliriunitifoggia.it)

HERBOWORX CLINIC ni taasisi binafsi iliyosajiliwa na msajili wa makapuni BRELA na kusajiliwa na Wizara ya Afya maendeleo jamii kupitia Baraza la tiba asili na tiba mbadala mwaka 2011 kwa lengo kuu moja kutumia sayansi ya tiba kutafiti na kuboresha dawa ya asili inayotokana na mimea ili itumike kutibu na kuzuia magonjwa yanayotakana na vimelea helicobacter pylori.

Netragen Dawa ya tiba asili inayotokana na mimea Natural Herbal therapy ina viambata asili phytochemical :-
(Carissone, carindone, carinol, odoroside H, digitoxigenin, glucose and D- digitalose myrcene, limonene, camphene, canene, dipentene, farnesol, nerolidol, dihydrojasmone, α-terpeneol, citronellal, β-ionone, nerylacetate, linalool and geranyl acetate.) ambavyo kwa kufanya kazi kwa pamoja vimeonyesha uwezo mkubwa kabisa kuua na kuangamiza vimelea helicobacter pylori

Kwa zaidi ya miaka minane(miaka 8) HERBOWORX CLINIC imehudumia zaidi ya wagonjwa 826,000 nchini Tanzania.

Netragen imeonyesha uwezo wa zaidi ya asilimia 80% ya kuweza kua na kuondoa maambukizi ya vimelea helicobacter pylori hivyo kuweza kuponya, kupunguza makali au kumkinga mtu dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na vimelea Helicobacter Pylori.
---
Pole sana ndugu,

Inawezekana kabisa kuwa na h pylori bila kuwa na vidonda vya tumbo. Hawa ni bacteria walio common sana kwenye mazingira yetu. Inakadiriwa asilimia 60 ya watu wana hawa bacteria kwenye matumbo yao, lakini si lazima upate vidonda unapokuwa nao japo ni moja ya factor muhimu zinazopelekea vidonda vya tumbo (ulcers).

Kupata kiungulia maana yake unatengeneza acid nyingi tumboni ambayo inarudi nyumba (reflux) na kuunguza sehemu ya juu ya njia ya chakula yaani umio (oesophagus) na kukusababishia maumivu unayoyasikia (heartburn). Uzalishwaji wa acid nyingi waweza kusababishwa na vyakula vyenye viungo vingi (spicy foods), citric, mkazo (stress), kuvuta sigara, baadhi ya dawa - hasa zilizo katika kundi la NSAIDs kama aspirin na ibuprofen - nk.

Kupunguza au kuepuka vitu hivi itakukinga na kiungulia lakini pia kuna dawa (antiaacids) ambazo zinaweza kupunguza utengenezaji wa acid uliopitiliza na hivyo kukuponya na kiungulia.

Acid kuweza hurudi nyuma kama una tatizo linaitwa hiatal hernia, ambayo husababisha tumbo kupanda juu na kupelekea acid kuingia katika umio (oesophagus) na kusababisha maumivu. Au ile sphincter inayotenganisha tumbo na umio ikiwa imelegea, acid yaweza ingia pia kwenye umio.

Unaweza kuwa na inflammation (kama mikwaruzo fulani) na sio vidonda (ulcers) na ukapata maumivu ya chembe ya moyo pia.

Si vibaya pia ukatibu hao H pylori kwani kwa hali yako wanaweza kukuletea vidonda baadae.

  • Thanks
Reactions: PNC
Ugunduzi wa bacteria Helicobacter pylori na namna vinayosababisha vidonda vya tumbo peptic ulcer disease (PUD). Kwa sasa maambukizi ya bacteria Helicobacter pylori yanahusishwa moja kwa moja kama chanzo au kichocheo cha magonjwa yafuatayo:-

MAGONJWA YA MFUMO WA CHAKULA
Ugonjwa wa Uvimbe Kwenye Mfumo wa Chakula (Inflammatory Bowel Disease-IBD),
uvimbe kwenye koromeo la chakula-Esophagitis, uvimbe kwenye mfuko wa chakula anteral gastritis copus gastritis,atrophic gastritis na pangastritis, uvimbe kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo -duodernitis, uvimbe kwenye utumbo mdogo -enteritis, uvimbe kwenye utumbo mpana -crown’s disease, au hemorrhoid- bawasili.

Ugonjwa wa vidonda kwenye mfumo wa chakula (Bowel Ulcer Disease) Vidonda kwenye koromeo la chakula Esophageal ulcers, vidonda kwenye mfuko wa chakula -Gastric ulcers, vidonda kwenye sehemu ya juu ya utumbo mdogo -Duodernal ulcers, vidonda kwenye utumbo mdogo- Illem ulcers, vidonda kwenye utumbo mpana Ulcerative colitis.

Saratani za mfumo wa chakula kama vile saratani za mfuko wa chakula gastric cancer ,MALT lymphoma, saratani ya utumbo mpana colorectal cancer (CRC).

Ugonjwa wa vimeng’enyo vya chakula kushindwa kumengenya chakula vizuri (dyspepsia) kutokana na tindikali kuzalishwa nyingi na kali sana hyperchlorhydria au inapozalishwa kidogo sana na isyokuwa kali au kutozalishwa kabisa hypochlorhydria.

MAGONJWA NJE YA MFUMO WA CHAKULA
Ugonjwa wa upungufu wa damu Idiopathic iron deficiency anaemia IDA na Idiopathic thrombocytopenic purpura ITP.

Upungufu wa vitamin B12 deficiency

Magonjwa ya Inni (hepatic Biliary Cirrhosis, hepatic Biliary sclerosis), ugonjwa wa mawe kwenye kifuko cha nyongo (Gall Stone Disease).

Magonjwa ya moyo (Cardiovascular Diseases) kama vile Ischaemic heart disease(IHD) na Ischaemic stroke

magonjwa ya mishipa ya damu (Artherosclerosis) ambayo ni ndiyo chanzo cha mtu kuugua Shinikizo la juu la damu (Hypertension) au Shinikizo la damu kwa wajawazito (Pre- Eclampsia).

Ugonjwa wa kisukari (Diabetes Mellitus II)

Magonjwa ya maumivu na kuvimba viungio joints kama vile:- Gout,rheumatoid Arthritis na Osteoarthritis.

Magonjwa ya ngozi, idiopathic chronic urticaria na acne rosacea na matatizo ya mzio Allergies,

Magonjwa ya maumivu na uvimbe kwenye viungo vinavyopatikana sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni Pelvic Congestion Syndrome (PCS) au Pelvic Inflammatory Disease (PID) ambapo imegundulika kuwa yanatokana na maambukizi makubwa ya bacteria Helicobacter Pylori ndani ya utumbo mpana:-

Uvimbe na vidonda kwenye figo- Chronic Kidney Injury (CKD)

Ugonjwa wa mawe kwenye figo -(kidney stone disease),

Ugonjwa wa mawe kwenye kibofu cha mkojo -urine blader stone disease,
Uvimbe,vidonda na kusinyaa kwa njia ya mkojo Urethritis au UTI sugu, na kuvimba tezi dume kwa wanaume-Prostatitis.

Uvimbe au kuziba njia ya mayai kwa wanawake- Salpingitis –uvimbe ndani ya mfuko wa uzazi- Endometriosis dalili zake ni mchango au maumivu ya tumbo la hedhi , kuharibika kwa mimba changa Spontaneous Abortion au kushindwa kushika mimba.

Utasa kwa wanaume na kukosa au kupungua nguvu za kiume-Erectile Dysfunction.

MAAMBUKIZI YA BACTERIA HELICOBACTER PYLORI AFRICA
Tafiti mbalimbali zimethibitisha kuwa vimelea hivi Helicobacter Pylori vinaambukiza kati ya mtu na mtu kupitia mate (Saliva) na pia uchafuzi wa kinyesi cha binadamu kwenye maji na chakula.

Kwenye nchi masikini ukosefu wa maji salama, uchafuzi wa mazingira, na makazi duni yenye msongamano wa watu wengi, unachangia watu wengi sana kupata maambukizo ya vimelea hivi, (Peterson et al., 2000; Aguemon et al., 2005)

Takwimu za shirika la afya duniani (WHO) zinzonyesha kuwa, nchi za Africa, kusini mwa jangwa la sahara, asilimia 80% ya wakazi wake wanaishi na vimelea vya Helicobacter Pylori na asilimia 20 % waugua vidonda vya tumbo, asilimia 60% aidha hawana dalili yeyote au wanaugua magonjwa ambayo hayana dalili zozote, (Mbulaiteye et al., 2006).

nchini Tanzania asilimia 76% ya watoto wenye umri kati 0 hadi miaka 4 walikutwa na maambukizi ya vimelea Helicobacter Pylori na maambukizi yaliongezeka hadi asilimia 99% kwa watu wazima (Mbulaiteye et al., 2006).

Maambuzi ya bacteria Helicobacter pylori huchukua muda mrefu sana kufikia hatua za ugonjwa tafiti zinakadiria wastani wa miaka kumi na tano kwa hiyo watu wengi wanaougua ni wale waliopata maabukizi makubwa wakiwa watoto chini ya miaka kumi na tano (15).

Kuna aina sita 6 za bacteria Helicobacter pylori aina na ukubwa wa dalili za ugonjwa au magonjwa yanategemea mambo makuu matatu, jambo la kwanza ni aina ya bacteria Helicobacter pylori phenotype vilivyo mpata mgonjwa,pili uwingi au kiwango cha maambukizi bacterial load, tatu ni vinasabana na Lewis factor vya mgonjwa husika.

HELICOBACTER PYLORI ANAVYOSABABISHA MARADHI
(PATHOGENESIS IN HELICOBACTER PYLORI INFECTION)

Baada ya mtu kumeza vimelea hivi kupitia mate ya mgonjwa, maji yasiyo salama, chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo salama na mikono michafu,

Vimelea hivi huweka masikani kwa kujichimbia ndani ya uteute unaofunika ngozi laini ya ndani ya mfuko wa chakula na utumbo mpana na kuzaliana na kuwa vingi , vimelea hivi huishi kwenye mfuko wa chakula na kwenye utumbo mpana kama minyoo noninvasive.

Madhara ya maambukizi yanatokana na taka taka ambazo ni sumu kwenye chembe chembe hai na viungo vya binadamu zinazozalishwa na vimelea hivi.

Vimelea hivi huzalisha aina nne za kemikali ambazo ni sumu kwa mwilini mwa binadamu cytotoxin associated gene A (cagA), vacuolating cytotoxin (VacA), lipopolysaccharide (LPS) na ammonia (NH) (T Shimoyama, J E Crabtree Gut et al., 1998;43 (suppl 1):S2–S5).

Kemikali sumu hii cytotoxin associated gene A (cagA) inahusishwa na uharibifu kwenye mfumo wa uzalishaji wa tindikali kwenye mfumo wa chakula na kusababisha tindikali izalishwe aidha kali sana na nyingi kupita kiasi hyperchlorhydria au izalishwe kidogo sana na isyokuwa kali au kutozalishwa kabisa hypochlorhydria, na pia ni kisababishi cha uvimbe na saratani ndani na nje ya mfumo wa chakula.

kemikali sumu vacuolating cytotoxin (VacA) husababisha kutokea kwa vidonda kwenye mfumo wa chakula (Bowel Ulcer Disease).

Kemikali sumu lipopolysaccharide (LPS) inahusika na kusaidia vimelea Helicobacter Pylori visishambuliwe na kinga ya mwili kwa kuipumbaza.

Kemikali sumu ammonia (NH) ni kisababishi cha uvimbe ndani na nje ya mfumo wa chakula na pia huchochea kasi ya kufa kwa chembechembe hai za mwili (apoptosis) na hivyo kudhoofisha utendaji kazi wa viungo muhimu mwilini kama vile kinga ya mwili, figo, moyo, inni, nk.

DALILI ZA MAAMBUKIZI YA HELICOBACTER PYLORI

Ingawa watu wengi wenye maambukizi ya bacteria Helicobacter Pylori hawana dalili zozote asilimia kati ya 20% na 30% wana moja au zaidi ya dalili zifutazo:-

Mgonjwa hujisikia kama anaungua kwa ndani na maumivu makali ya tumbo, tumbo kujaa gesi na kuunguluma (bloating), na Maumivu makali sehemu ya juu ya tumbo, chini ya kifua, (chembe ya moyo)

mgonjwa huupata kiungulia-heartburn hasa baada ya kula chakula chenye asili ya tindikali kama vile viazi, maharage nk.
Kufunga choo au kupata choo kigumu wakati mwingine kinakuwa kama cha mbuzi na chenye uteute mwingi (constipation).

Mgonjwa mwenye maambukizi makubwa ya vimelea hivi, hali huwa mbaya zaidi, kwani kemikali sumu hizi huzalishwa kwa wingi sana, uharibifu unakuwa mkubwa zaidi, kemikali sumu hizi na tindikali hufyonzwa na kusambaa mwili mzima, kupitia mishipa ya damu hivyo kufanya uharibifu kwenye kila kiungo muhimu cha mwili.

Mgonjwa hujisikia mchovu, mapigo ya moyo kuwa ya juu na ya kasi, homa za mara kwa mara, kuumwa kichwa na kipanda uso (migrane headache).

Maumivu ya viungo na misuli ya miguu, mikono, mgongo, mabega ,shingo n.k
Hisia za baridi, joto au ganzi kwenye nyayo za miguu, vidole vya mikono na miguu.
Kichefuchefu, kizunguzungu na kukosa hamu ya chakula.
kupungukiwa damu mara kwa mara, kwa sababu vidonda vinavujisha damu kwa ndani, kinyesi cha magonjwa hubadilika rangi na kuwa cha kahawia, damu nyingi ikivujia mgonjwa hutapika na kuharisha damu mbichi au iliyoganda, hivyo kupelekea mgonjwa kuishiwa damu anemia.

HELICOBACTER PYLORI NA MATIBABU
Matibabu yanayotolewa dhidi ya maambukizi ya bacteria Helicobacter Pylori ni mchanganyko wa dawa tatu za antibiotic au antibiotic mbili na metronidazole na pamoja na dawa za kupunguza tindikali proton pump inhibitor (PPI) HELICO KIT ambazo ni kati ya zifuatazo:-
Levofloxacin, rifabutin, tetracycline, amoxicillin, clarithromycin, metronidazole pamoja na dawa za kupunguza tindikali Omeplazole au pantocid.

Changamoto imejitokeza miaka ya zaidi ya kumi iliyopita kuwa bacteria Helicobacter Pylori amejenga usugu na dawa zote zinazotumika hivyo kushindwa kwa aina hii ya matibabu Duniani kote, na hivyo kuibua haja ya kuwa na dawa mbadala kwa matatizo na magonjwa yanayosababishwa na bacteria Helicobacter Pylori.
(J Gastrointestin Liver Dis.December 2010 Vol.19 No 4, 409-414 Dr Vincenzo De Francesco.Gastroenterologia ed Endoscopia Digestiva, Ospedali Riuniti di FoggiaFoggia, Italy vdefrancesco@ospedaliriunitifoggia.it)

HERBOWORX CLINIC ni taasisi binafsi iliyosajiliwa na msajili wa makapuni BRELA na kusajiliwa na Wizara ya Afya maendeleo jamii kupitia Baraza la tiba asili na tiba mbadala mwaka 2011 kwa lengo kuu moja kutumia sayansi ya tiba kutafiti na kuboresha dawa ya asili inayotokana na mimea ili itumike kutibu na kuzuia magonjwa yanayotakana na vimelea helicobacter pylori.

Netragen Dawa ya tiba asili inayotokana na mimea Natural Herbal therapy ina viambata asili phytochemical :-
(Carissone, carindone, carinol, odoroside H, digitoxigenin, glucose and D- digitalose myrcene, limonene, camphene, canene, dipentene, farnesol, nerolidol, dihydrojasmone, α-terpeneol, citronellal, β-ionone, nerylacetate, linalool and geranyl acetate.) ambavyo kwa kufanya kazi kwa pamoja vimeonyesha uwezo mkubwa kabisa kuua na kuangamiza vimelea helicobacter pylori

Kwa zaidi ya miaka minane(miaka 8) HERBOWORX CLINIC imehudumia zaidi ya wagonjwa 826,000 nchini Tanzania.

Netragen imeonyesha uwezo wa zaidi ya asilimia 80% ya kuweza kua na kuondoa maambukizi ya vimelea helicobacter pylori hivyo kuweza kuponya, kupunguza makali au kumkinga mtu dhidi ya magonjwa yanayosababishwa na vimelea Helicobacter Pylori.
 
Inawezekana likawa tatizo lengine, cha muhimu ni kufanya Vipimo zaidi ili kujua nini kinamsumbua
 
Ndio Mkuu, Ni "Triple Therapy".

Asante sana Mkuu, duh!! Lugha hizi za kitabibu M mweee ... leo naona wamemwandikia arudie tena kipimo cha OGD na kipimo kingine kinaitwa sijui Hgibv sijui nimepatia? Ngoja kesho nitakiandika vizuri nitakupa mrejesho.
 
Wakuu Nje ya Mada na jafari mwijae mgonjwa wangu ana case nyingine pia ambayo ni Sukari ya kupanda na HIV+ je kuna mahusiano yoyote katika huo ugonjwa wa H-pylori na haya Magonjwa? Na nini cha ziada kifanyike?
 
Last edited by a moderator:

Pole Mkuu, Tatizo kubwa hapo Ni HIV+ na ndio lililopelekea manifestation H Pylori infection, kwani kinga imeanza kushuka na kufanya mwili ushindwe kupigana na H Pylori.

Suala la Sukari ya Kupanda Sijajua Limemuanza lini (Japo Ni la kawaida kwa HIV - na +)

Kama ungependa iwe kutunza siri ya huyo mgonjwa njoo PM nijue vitu vichache pia, lakini kama Ni "kawaida" tunaweza endelea hapa hapa. Karibu
 
Last edited by a moderator:
Kwa faida ya wengi hakuna shida tuendeleee hapa hapa mkuu

Itafaa Zaidi, je ni HIV + kwa kipindi cha muda gani, na ameanza kutumia ARVs?

Tatizo la Sukari pia lina muda gani na anapewa tiba za kumsaidia!?

Tatizo la H Pylori tunaweza kuliondoa, ila ningeshauri majibu ya vipimo atakavyofanyiwa kesho hiyo uje navyo hapa (kama majibu yatapatikana haraka) ili tuamue kitu sahihi zaidi.
 
HIV ni 10+ years, Kisukari 8+ yrs. Anatumia ARV ,na Sukari pia anatumia dawa....Kwa kesho nahisi kimoja kitapatikana ila cha OGD mpka jumatatu.
 
Back
Top Bottom