Bakora Sita Kwa Mrembo Mlevi wa Malaysia Zipo Pale Pale | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bakora Sita Kwa Mrembo Mlevi wa Malaysia Zipo Pale Pale

Discussion in 'International Forum' started by Mbonea, Sep 29, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Kartika Sari Dewi Shukarno Tuesday, September 29, 2009 5:09 AM
  Mrembo wa vivazi wa Malaysia ambaye alikamatwa akinywa pombe hadharani atachapwa bakora sita kama kawaida pamoja na shinikizo la mataifa ya magharibi kupinga adhabu hiyo. Mahakama ya kidini ya Malaysia imeamuru mrembo wa vivazi wa Malaysia aliyekamatwa akinywa pombe hadharani, achapwe bakora sita kama adhabu yake ilivyotolewa pamoja na kwamba kesi hiyo iliamsha mgogoro mkubwa wa kimataifa.

  Kartika Sari Dewi Shukarno, 32, alihukumiwa na mahakama ya kidini miezi sita iliyopita kuchapwa bakora sita baada ya kukamatwa akinywa pombe hadharani kwenye klabu ya starehe.

  Kartika atakuwa mwanamke wa kwanza nchini Malaysia kukumbana na adhabu ya kuchapwa bakora. Wanaume wengi washachapwa bakora nchini humo kwa kuvunja sheria mbali mbali za kiislamu.

  Awali Kartika alinusurika adhabu hiyo baada ya serikali kuingilia kati na kudai adhabu hiyo ni kali sana na itaharibu sifa ya Malaysia kimataifa.

  Lakini baada ya mahakama ya sheria za kiislamu katika mji wa Kuantan ambao Kartika alikamatwa akinywa pombe, kukata rufaa kupinga Kartika kuachiwa huru, kesi hiyo ilipitiwa tena na mahakama iliamuru Kartika achapwe bakora sita kama sheria zinavyosema.

  Tarehe ya Kartika kuchapwa bakora hizo bado haijapangwa.

  Malaysia ina mifumo miwili ya sheria. Mfumo mmoja ni wa kawaida na mfumo mwingine unafuata sheria za kiislamu kwaajili ya waislamu wanaokiuka misingi ya kiislamu.

  Raia wa Malaysia wenye asili ya China na India ambao wengi wao si waislamu wao wako huru kunywa pombe muda wowote bila kubughudhiwa.

  Hali ni tofauti kwa raia wa Malaysia ambao ni waislamu kwani matendo yao yoyote yanayokiuka misingi ya kiislamu huamriwa na mahakama za sharia za kiislamu.

  Source: AFP
   
 2. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hawa nao........ Mambo ya mahakama ya kadhi.
   
 3. J

  JackieJoki Member

  #3
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 24, 2009
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Safi sanaaaaaa!!!!!!
  Hapa kwetu je????
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 280
  Duuuuuuuuu hii kali kwa wenzetu pombe inanywewa chumbani??
   
 6. K

  Koba JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo bongo ndio wanataka kuleta hii mahakama ya kadhi kwa waislam?najua jinsi walivyo extremist watatulazimisha na sisi tusio amini utumbo wao...mahakama ya kadhi kaeni nao huko huko au hamieni kwa hao washenzi wanaoishi karne ya pili bado!
   
 7. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  bakora kwenda mbele wakiruhusu iwepo
   
Loading...