BAKITA yaandaa wataalamu wafundishe SADC

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
WATAALAMU wa lugha ya Kiswahili zaidi ya 950, wamenolewa na Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita), tayari kwenda kufundisha lugha hiyo nje ya nchi, hususan nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Hivi karibuni katika kikao cha SADC, kilichofanyika nchini na kushirikisha wakuu wa nchi 16, huku Rais John Magufuli akichaguliwa kuwa mwenyekiti wake, kwa pamoja wakuu hao wa nchi waliridhia Kiswahili kuwa lugha ya nne ya kuendeshea mkutano huo kikiungana na lugha nyingine za Kiingereza, Kifaransa na Kireno.

Lakini, kabla hata ya kukubaliwa huko katika ziara yake nchini Namibia na Afrika Kusini mwaka huu, Rais Magufuli alifanikiwa kuzishawishi nchi hizo kufundisha Kiswahili kwenye nchi hizo, huku Afrika Kusini ikiwa tayari imeshaonesha nia ya dhati ya kuanza kufundisha lugha hiyo shuleni. Akizungumza na gazeti jana, Mchunguzi wa Lugha Mwandamizi Idara ya Istilahi na Kamusi wa Bakita, Wema Msigwa alibainisha kuwa baraza hilo linaendelea na jitihada za kuwaandaa wataalamu wa lugha, huku akibainisha kuwa linachukua wahitimu wa Shahada ya Kiswahili na masomo yanaoendana na lugha hiyo.
 
Hao wataalam wanaandaliwa wap huko dar au wapi? maana sidhan kama BAKITA wana kanzi data ya wataalam wa lugha ya kiswahil
kwa nchi nzima.

Hili ndilo litakalotufanya tuwe nyuma kwa Kenya, niwashauri hili baraza wawe na mfumo wa kuwatambua hao wataalam ili iwe rahis kwa wao kuwapata, kama ilivyo kwa associations zingine lasivyo, kwa kinachoongelewa ni kazi bure.
 
Hii itakuwa fursa kwa vijana ikitumiwa vizuri, vinginevyo kenya na kiswahili chao kibovu watapiga bao
 
Back
Top Bottom