BAKITA kujaza wajuzi wa Kiswahili SADC

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
BARAZA la Kiswahili Tanzania (BAKITA), limekiri kuwa kuna haja ya kuwa na wanafunzi wengi zaidi wa kusoma masomo ya lugha za kigeni hususani Kireno, Kingereza na Kifaransa ili kuendana na mahitaji ya Jumuiya na Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Bakita imesema ipo tayari kujipanga zaidi ili kuwa na wataalamu wa kutosha katika kukidhi mahitaji ya matumizi ya Lugha ya Kiswahili katika nchi za jumuiya hiyo, baada ya lugha hiyo kuidhinishwa rasmi ndani ya jumuiya hiyo.

Hayo yalibainishwa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Selemani Sewangi (pichani) wakati alipokuwa akizungumza na gazeti la HabariLEO Afrika Mashariki osini kwake mwishoni mwa wiki iliyopita. Sewangi alisema wanapaswa kujipanga vyema ili kuhakikisha kunakuwa na wataalamu wa kutosha katika kukidhi mahitaji yote ya kutumia lugha ya Kiswahili ndani ya jumuiya. Alisema hadi sasa Bakita imeshaandaa Kanzi Data lengo likiwa ni kuendana na mahitaji yaliyopo.

“Tunapozungumzia Kiswahili kuwa fursa ni kwamba nyaraka za SADC zinaweza kusomeka kwa Kiswahili, Kireno, Kiingereza au Kifaransa. Katika muktadha wa aina hii utahitaji huduma ya kutafsiri ili nyaraka hizo zisomeke katika lugha ya Kiswahili,” alisema Sewangi.

Alisema huduma ya kutafsiri nyaraka hizo ni kazi nzito ambayo inahitaji weledi na umakini wa kutosha hivyo kunahitajika wataalamu wazuri wa kuweza kuifanya kazi hiyo bila kupoteza maana iliyokusudiwa. Aidha, Sewangi alisema kutafsiri ni utaalamu ambao anayeifanya kazi hiyo lazima ajue lugha chanzi ambayo inahitaji kutafsiriwa kwa Kiswahili. Mfano Lugha chanzi ambazo zitahitaji wataalamu wa Kiswahili kuzitafsiri kwa Lugha ya Kiswahili ni Kireno, Kifaransa na Kiingereza.

Sewangi alisema wataalamu wa kutafsiri lazima wazijue vyema lugha hizo ili kuifanya kazi ya kutafsiri kuwa bora na iliyokusudiwa. Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma ya Kiswahili (TATAKI) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Aldin Mutembei alisema kuna utaalamu wa kufundisha lugha ya Kiswahili bila kufahamu Lugha nyingine. “Mimi nadhani mchakato huu ufanywe haraka na mamlaka zinazohusika ikiwa ni wizara husika au yeyote anayehusika ndani ya serikali atufungulie mlango, aanze kutudai.

Jamani ee walimu wa Kiswahili leteni wanafunzi au walimu wa Kiswahili aone kwamba hatujawapeleka,” alisisitiza Mutembei akiwa osini kwake. Kwa mujibu wa Bakita, kuna wataalamu wa Kiswahili ambao wameandikishwa wapatao zaidi ya 1,100 lakini kinachowasumbua ni kwa wataalamu hao ikiwa wanafahamu lugha zaidi ya moja ili kuweza kuifanya kazi ya kutafsiri ndani ya SADC. “Ni wataalamu wa Kiswahili wazuri kabisa, lakini je, uwezo wao wa kuweza kukabiliana na haya majukumu mapya ukoje,? Na hilo swali linakwenda moja kwa moja kwenye umilisi (ujuzi) wao wa lugha zingine kama Kireno, Kifaransa na Kiingereza ukoje?” alihoji Sewangi.

Sewangi alisema Tanzania ina wataalamu wengi na wazuri wa Kiswahili, lakini ina wataalamu wachache wanaofahamu lugha mbalimbali za kigeni zinazotumiwa katika jumuiya ya SADC mbali na lugha ya Kingereza. Afrika Kusini ndiyo nchi pekee kutoka SADC ambayo tayari imeshaingiza somo la Kiswahili katika mtaala wake kama ambavyo alibainisha Mkurugenzi huyo wa Tataki. “Afrika Kusini sasa hivi wameomba mtaala kwamba tunaiomba Tanzania ituandikie mtaala ili mtaala huo utumike kufundisha Kiswahili katika shule za Msingi, Sekondari na baadae Vyuo,” Mutembei alibainisha hatua iliyokiwa katika mchakato wa kufundisha Kiswahili nchini Afrika Kusini..
 
Nililisema hili na nikashambuliwa kwa kukosa uzalendo. Nafasi za Afrika ya Kusini tulizikosa kwa sababu ujuzi wa kujua lugha ya kufundishia (medium of instructions) ni wa chini sana!! Mmoja wa wajuzi wa kiswahili kufikia kiwango cha shahada za uzamivu hawezi kuzungumza kiingereza hata kwa makosa (broken English) kwa dakika 5 bila kutokwa na jasho jingi na kuishiwa pumzi. Ndio ataweza kwenda kufundisha Kiswahili Namibia ambako lugha ya kufundishia ni Kiingereza??

Iwe ni lazima sasa anayesoma lugha asome group la lugha. Hii itapanua uwigo wa kupata nafasi za kufundisha katika mataifa mengine. La sivo wajiandae kuwa waalimu wa Kiswahili katika mazingira ya nyumbani.
 
Back
Top Bottom