BAKITA imshitaki Chenge Kwa Kuharibu Neno "Vijisenti"

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,408
2,000
Kutokana na kisa cha Waziri wa miundo mbinu, Mh. Chenge kufananisha shilingi billioni moja na 'vijisenti', lililotokea hivi sasa ni kuwa; inawawia vigumu sana watu kueleweka kirahisi pale wanapotaka kutumia neno vijisenti kumaanisha 'vijisenti', yaani hela zisizo nyingi, hela haba au pesa zisizokidhi.

Hoja yangu hapa ni kuwa, kwa kuwa aliyesambaratisha neno hili amefanya makusudi na mzigo aliouacha unaleta kero kwa watumiaji wa kiswahili walio wengi, na kwa vile aliye haribu maana ya neno hili ni kiongozi wa juu serikalini; basi, Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) kwa kulinda na kuhakiki matumizi sanifu ya Kiswahili halina budi kumshitaki kiongozi huyu kwa yale aliyosababisha.

Kwa kweli imekuwa kero kwangu na ninaamini kwa wenzangu walio wengi. Je, kweli hamna kipengele ambacho kinamzuia kiongozi kukashfu lugha yetu sanifu kwa kudharirisha maana ya neno linalotumiwa na kukubalika katika jamii?! Naomba mlio wataalam wa lugha msaidie kufafanua hili.

Ahsanteni.

SteveD.
 
Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
250
Kutokana na kisa cha Waziri wa miundo mbinu, Mh. Chenge kufananisha shilingi billioni moja na 'vijesenti', lililotokea hivi sasa ni kuwa; inawawia vigumu sana watu kueleweka kirahisi pale wanapotaka kutumia neno vijisenti kumaanisha 'vijisenti', yaani hela zisizo nyingi, hela haba au pesa zisizokidhi.

Hoja yangu hapa ni kuwa, kwa kuwa aliyesambaratisha neno hili amefanya makusudi na mzigo aliouacha unaleta kero kwa watumiaji wa kiswahili walio wengi, na kwa vile aliye haribu maana ya neno hili ni kiongozi wa juu serikalini; basi, Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) kwa kulinda na kuhakiki matumizi sanifu ya Kiswahili halina budi kumshitaki kiongozi huyu kwa yale aliyosababisha.

Kwa kweli imekuwa kero kwangu na ninaamini kwa wenzangu walio wengi. Je, kweli hamna kipengele ambacho kinamzuia kiongozi kukashfu lugha yetu sanifu kwa kudharirisha maana ya neno linalotumiwa na kukubalika katika jamii?! Naomba mlio wataalam wa lugha msaidie kufafanua hili.

Ahsanteni.

SteveD.

lakini ameomba radhi na kudai kuwa yeye si Mzaramo bali msukuma sasa hata kwa wasukuma neno 'Vijisenti' halipo bali msukuma amezoea wingi 'mahera', Bakita inabidi watupe ufafanunuzi na wanasheria akama anaweza kushtakiwa.
 
Mswahilina

Senior Member
Apr 7, 2008
171
0
lakini ameomba radhi na kudai kuwa yeye si Mzaramo bali msukuma sasa hata kwa wasukuma neno 'Vijisenti' halipo bali msukuma amezoea wingi 'mahera', Bakita inabidi watupe ufafanunuzi na wanasheria akama anaweza kushtakiwa.

Lakini kama unakumbuka, Abdalla Majura mtangazaji wa BBC alimuuliza kuwa "Shilingi bilioni moja sio vijisenti mheshimiwa" yeye akajibu "Inatejemiana na Mtu". Hivyo basi kwake chenge Dola za Kimarekani milioni moja ambazo ni zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni moja ni sawa na mimi ninaposema shilingi 10 (kumi) kuwa ni vijisenti.
 
Phillemon Mikael

JF-Expert Member
Nov 5, 2006
10,178
2,000
kweli mswahilina aby alimuuliza akajibu..."..kila mtu ana kiwango chake..." simply everybody has his or her price tag....inaonekana ili uweze kumhonga chenge ukiwa na bilioni 1 hakuelewi..at least uwe na juu ya hapo..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom