Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,241
Kutokana na kisa cha Waziri wa miundo mbinu, Mh. Chenge kufananisha shilingi billioni moja na 'vijisenti', lililotokea hivi sasa ni kuwa; inawawia vigumu sana watu kueleweka kirahisi pale wanapotaka kutumia neno vijisenti kumaanisha 'vijisenti', yaani hela zisizo nyingi, hela haba au pesa zisizokidhi.
Hoja yangu hapa ni kuwa, kwa kuwa aliyesambaratisha neno hili amefanya makusudi na mzigo aliouacha unaleta kero kwa watumiaji wa kiswahili walio wengi, na kwa vile aliye haribu maana ya neno hili ni kiongozi wa juu serikalini; basi, Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) kwa kulinda na kuhakiki matumizi sanifu ya Kiswahili halina budi kumshitaki kiongozi huyu kwa yale aliyosababisha.
Kwa kweli imekuwa kero kwangu na ninaamini kwa wenzangu walio wengi. Je, kweli hamna kipengele ambacho kinamzuia kiongozi kukashfu lugha yetu sanifu kwa kudharirisha maana ya neno linalotumiwa na kukubalika katika jamii?! Naomba mlio wataalam wa lugha msaidie kufafanua hili.
Ahsanteni.
SteveD.