"Baki Na Hamu Zako" Neno lina Ukakasi kusikika Hewani.

Amalinze

JF-Expert Member
May 6, 2012
6,784
5,284
Habari wana Jukwaa,

Kuna wimbo ameutoa mwana FA unaitwa Dume suluari,sitozungumzia kiundani huo wimbo ila kuna mstari mmoja ametamka Vanessa mdee "Baki na Hamu Zako".

Kiukweli hilo neno halifahi kabisa kusikika hewani maana lina maudhui ya matusi,sidhani kama Basata walipitia contents vizuri wa huo wimbo.

Ningependa Radio wajaribu kulifuta hilo neno lisisikike maana linajenga picha mbaya,ukisikiliza nyimbo nyingi za marekani hasa hasa radio edit maneno yenye ukakasi kama hayo wanayafuta wao wenyewe wamiliki wa radio.
 
HIO nyimbo umeiskia lini mkuu Kwa mara ya kwanza

Nimeusikia kama siku ya pili tangu autoe ila nilikuwa sijapata mda wa kuutolea maoni,East Africa Radio huwa wana edit kuondoa maneno yenye ukakasi lakini na wao Leo wameupiga kama ulivyo,kwahiyo Vanessa anakiri kwamba mwanamke ni chombo cha kutolea hamu?
 
Nimeusikia kama siku ya pili tangu autoe ila nilikuwa sijapata mda wa kuutolea maoni,East Africa Radio huwa wana edit kuondoa maneno yenye ukakasi lakini na wao Leo wameupiga kama ulivyo,kwahiyo Vanessa anakili kwamba mwanamke ni chombo cha kutolea hamu?
huo ndiyo ukweli japo unataka kuupindisha kwa vifungu vya gender balance ... ila ukweli utabaki pale pale
 
Ukweli Upi Miss Chaga? Wa Kukaa mbali na yeye kama Dume Suruali au Mwanamke ni chombo cha kutolea Hamu?
 
Nyama ya bata ni tamu nyama ya bata ni tamuuuuuu,,,,,,,,,,,,mwanamke mazingiraaaa,,,,,,,,,,nimesimama kama ngongoti,bingilibingili samasotiiiii........,sindano yako haiumiziiiiiiii,,,,,,,,,Tanesco walijua leo nitauaaaaaa
 
Habari wana Jukwaa,

Kuna wimbo ameutoa mwana FA unaitwa Dume suluari,sitozungumzia kiundani huo wimbo ila kuna mstari mmoja ametamka Vanessa mdee "Baki na Hamu Zako".

Kiukweli hilo neno halifahi kabisa kusikika hewani maana lina maudhui ya matusi,sidhani kama Basata walipitia contents vizuri wa huo wimbo.

Ningependa Radio wajaribu kulifuta hilo neno lisisikike maana linajenga picha mbaya,ukisikiliza nyimbo nyingi za marekani hasa hasa radio edit maneno yenye ukakasi kama hayo wanayafuta wao wenyewe wamiliki wa radio.
Wewe ni mgeni na sanaa?? Naona unatokwa na sumu mwilini kwa kutokuwa na elimu, mbona hapo katumia tafsida au una hila acha kujifanya unajuwa kwingi kumbe mweupe tu
 
Utakuwa na Hamu tu wewe si bure?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom