Bakhresa tujengee relii kutoka Kariakoo mpaka Mbande

Android 00

JF-Expert Member
May 23, 2013
774
221
Sisi wananchi wa Mbagala,Mbande tunaenda kumwambia Bakhresa atuletee usafiri wa uhakika mbadala wa treni za umeme.
 
badilisha title kwanza,,awajengee tren au reli?
akijenga reli,umeme wenyewe uko wapiwa uhakika?kuna tren za diessel za kasi pia
sio lazima za kutumia ule umeme wa tanesco .
Huyu bwana ana hela kuijenga ni kazi rahisi kwake
atapewa support na waarabu na wahindi wenzake
 
kumbe bakhresa ndio anaokusanya kodi sasa hivi.
kodi akusanye mwingine. reli ajenge mwingine mbona majanga
 
Akuwekee picha ya wapi? Mbagala, mbande au ya Bakhresa

Hilo suala la kudai picha limekuwa kama fasheni hapa jf. Mtu akiwa hana cha kuchangia basi atadai awekewe picha hata kama uzi wenyewe hauendani na picha. Hii ndiyo JF bana!
 
Bahresa ni mfanyabiashara na reli kama hii hata yeye anaweza akajenga na kutoa huduma sio bure na serikali ikaendelea kukusanya kodi zake kama kawaida, Kama ataweza kujenga hii reli italeta mabadiliko makubwa kwa wawekezaji wote wa pande hizi. nilichokiona huku kwetu mbagala kuna ongezeko kubwa sana la watu kuliko sehemu nyingine yoyote hapa dar. na kutokana na barabara zetu kuwa finyu hata kama idadi ya magari ya daladala yataongezeka yatazidisha foleni na badala yake muda wetu utazidi kuishia barabarani.
 
badilisha title kwanza,,awajengee tren au reli?
akijenga reli,umeme wenyewe uko wapiwa uhakika?kuna tren za diessel za kasi pia
sio lazima za kutumia ule umeme wa tanesco .
Huyu bwana ana hela kuijenga ni kazi rahisi kwake
atapewa support na waarabu na wahindi wenzake

Ahsante..
 
Sisi wananchi wa mbagala,mbande tunaemda kumwambia baharesa atuletee usafiri wa uhakika mbadala wa treni za umeme.

Hakuna mfanyabiashara aweza gharimia mabilioni kujenga reli kupeleka mbagala au mbande ambako wateja wengi wako asubuhi na jioni tu.Mabasi ya mbagala na mbande mchana utakuta madereva wamelala kwenye mabasi kwa kukosa abiria.Tena wengi wa kipato cha chini ambao ukiongeza nauli tu mia moja wanaweza kukupiga nondo na kukuloga .Nauli za treni za umeme hawawezi kulipa! Halafu huko mbagala kunaongoza kwa kung`oa mifuniko ya mashimo ya barabarani na kuiuza kama chuma chakavu.Reli itasalimika kweli? Mbagala kuna vibaka hadi wa kuiba ndala za mia tano zilizochakaa ukiweka nje ya mlango.
 
Hilo suala la kudai picha limekuwa kama fasheni hapa jf. Mtu akiwa hana cha kuchangia basi atadai awekewe picha hata kama uzi wenyewe hauendani na picha. Hii ndiyo JF bana!

usisahau na "source plz". teh teh teh.
 
Hahahaha, Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!...hivi umesema unakaa wapi vile?
 
kumbe bakhresa ndio anaokusanya kodi sasa hivi.
kodi akusanye mwingine. reli ajenge mwingine mbona majanga

Mkuu kuna watu wengine kutokana na uelewa wao wanajua bakhresa ndo kila kitu, hawajua kua suala la kuboresha miundombinu ni la serikali.
 
Hilo suala la kudai picha limekuwa kama fasheni hapa jf. Mtu akiwa hana cha kuchangia basi atadai awekewe picha hata kama uzi wenyewe hauendani na picha. Hii ndiyo JF bana!

Kuna mtu aliuliza hivi kwanini watu wa siku hizi hawasomi thread kabla ya kujibu! Kuna jamaa kaja anasema PICHA TAFWAZALI. Sasa sijui mtu kama huyu anadai picha ya nini.
 
uwanja wa chamazi hamuingii kumsupport na bado mnataka awasaidie majukumu yasiyo yake
 
Tena msiende kumuomba bali mwambieni ajenge na mmpe deadline kabisa....yani mimi nilifikiri keshawajengea siku nyingi kumbe alikuwa bado...!
 
Back
Top Bottom