Bakhresa na EWURA hii ndio PPP | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bakhresa na EWURA hii ndio PPP

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Semilong, May 7, 2011.

 1. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ilikuwa jumamosi iliyopita asubuhi maeneo ya mbezi beach, nimeamka asubuhi nikaona ni siku muafaka ya kupeleka gari kwa fundi. Nilivyololiwasha gari nikaona taa ya mafuta iko, red si jambo la kushtua sana kwa ajili ni kawaida kuweka mafuta kwa kudunduliza.

  Baada ya muda nikaanza safari ya kwenda kwa fundi na taa ya red ikiwaka, sikufanikiwa kufika mbali na gari likanizimikia nikiwa maeneo ya mbezi. Ikanilazimu nichukue kidumu kwenda kununua mafuta ya petroli ili niweze kuendelea na safari yangu. Petrol station zote za maeneo ya mbezi zilinikatalia kuniuzia mafuta zikiniambia kuwa zimekatazwa na Ewura na sheria imeshapitishwa nikawa sina ujanja.

  Pamoja na kukataliwa kununua mafuta lakini ilikuwa lazima gari liwake maana yake lilikuwa kando kando ya barabara ambako sio safe kwa watumiaji wengine wa barabara na hata kwa gari lenyewe kukwapuliwa vitu. Hii hali ilinifanya mimi nifanye kitu ambacho kimeniuma sana ili niweze kununua mafuta, ili nilazimu niende kituo kimoja (jina kapuni) ambacho mwanzo kilinikatalia nikambembeleza muuzaji aniwekee mafuta yule jamaa akaniambia atanikata 1000 kwenye elfu 10 kwa ajili kuniwekea mafuta kwenye kidumu anahatarisha kazi yake. Nilikuwa sina mahali pengine pa kukimbilia ikanibidi nikubali kwa shingo upande.

  kitendo cha kutoa 1000 ili niweze kupata mafuta kiliniuma sana nikajiuliza je watu wenye generator kama saloon na small business wanafanyaje. Mbona hata nchi za ngambo kama uk vidumu vinaruhusiwa. Je inamaana mtanzania wa leo haruhusiwi kuishiwa mafuta, je mtz wa leo akiishiwa mafuta gari halina tena kazi?

  kuanzia jumatatu ikanibidi nifanye dodosadodosa hapo mitaa ya ewura nikapata taarifa kuwa kampuni ya bakhresa inanunua hizi chupa za plastic empty kwa ajili ya recycling haitaki hizi chupa ziwekewe petroli na pia wana mpango wa kaunza kutengeneza chupa maalum (?) kwa ajili ya kazi hiyo. Nikajiuliza je hii ndio Public Private Partnership ambayo serikali yetu iemekuwa iki advocate?
   
 2. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mkuu tumoa hata metal containers, nenda Mlimani city kaulize itapata. Ila plastic material is harzadois and against public safety
   
 3. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #3
  May 7, 2011
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  PPP my foot! Huu ni UFISADI tu! Hongera kwa kufanya investigative work nzuri. Sasa tuachie sisi tutaenda EWURA na kwingineko. Bonge la stori!
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  ukiona hivyo ujue kuna biashara ya madumu special toka china ya kuwekea mafuta yataanza kuuzwa!deal la mtu hilo
   
Loading...