pinno
JF-Expert Member
- Jan 17, 2013
- 1,213
- 1,228
Kuna video nimeiona, nashindwa tu kuiweka hapa,
ila watanisaidia wenye nayo, maana ipo sana tu mtandaoni,
inamuonesha Mzee SSB, akiingia msibani, kwenye msiba wa wafanyakazi watano wa Azam Media, kuelekea kiti kwake, anampita Katibu wa CCM ndugu Polepole, anampita Rc wa Dar es salaam, almaarufu kama mungu wa Dar, DAB, Makonda, anampita waziri mwenye dhaman na michezo habari na burudani, Mhe Mwakyembe, anasogea kwenye kiti chake anakaa, anampa mkono mzee wa pembeni yake ambaye, sura sio ngeni ila sijamtambua vizuri.
Na anaendelea na taratibu nyingine, wakati huo huo, jicho la kamera, linamtazama Mhe Mwakyembe, na Makonda, ni kama vile wanataka kutoa mkono wa pole kwa mzee, wasalimiane nae, ila wanaona tena kama itifaki itakuwa haijakaa sawa, basi wanabaki wasijue la kufanya, na yeye ni kama vile hana taimu nao, au ukute hata hajawajua. (Inawezekana kabisa akawa hawajui)
Mara anakuja Tiddo, ambaye ni mwajiriwa wake, kama Mkurugenzi wa Azam media ,mzee anasimama anamsalimia Tiddo kwa adabu na heshima.
My take :
1. Mzee anathamini Wafanyakazi wake, na kuwashobokea hao, zaidi ya viongozi wa kisiasa, ambao kwa kawaida mabosi wengi mtaani wangefanya kinyume na hapo,
2. Mzaa yupo busy na mambo yake, na hivi Magu anabadilisha badilisha mawazir na wakuu wa mikoa, ukute jamaa hata hajui in person wazir wa michezo ni nani, watu wake wanajua, kampuni zake zinajua, ila yeye in person hana muda wa kufuatilia hayo na hayana umuhimu kwake.
3. Anapenda kuishi kawaida sana