Bakheresa, Mengi - mnatoa millions kwenye tv, wafanyakazi hoi, mnatufundisha nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bakheresa, Mengi - mnatoa millions kwenye tv, wafanyakazi hoi, mnatufundisha nini?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Pdidy, Aug 26, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,128
  Likes Received: 5,569
  Trophy Points: 280
  Ndugu watanzania,nahisi ni wakati wa kuambiana ukweli hasa pale kwenye mwinuko kabla ya kushuka mlima...nafurahi sana kuona wah wafanyabiashara zao Bw Bakheresa na bw MENGI..kwa kutoa mamiliion mia5 kwenye masaccos...na alot of money kwa waliofunga kama futari...ila bado najiuliza mbona pamoja na pesa zote hizo wafanyakazi wenu wanaendelea kuteseka jamani....ni MAJUZI TU WAFANYAKAZI WA BAKHERESA WAMEGOMA KUFANYA KAZI...BAKHERESA NI STAREHE GANI MNAPATA KWA KUWAPA WATU MKATABA WA MIEZI MIWILI MIWILI NA FAMILIA ZAO HUKU UKIMWAGA MAMILLION KWENYE TV..KWA WAGONJWA NA WNEGINE...HAMJUI BARAKA ZINAANZIA NYUMBANI KWENU....ACHENI KUKIMBILIA KUTOA MISAADA KWA WA NJE HUKU WAFANYAKAZI WENU WAKITUOMBA NAULI ZA KUJA HUKO MAOFISINI MWENU....HYO MNAYOFANYA SI THAWABU KABISA...NA WALA MSITARAJIE KUPATA THAWABU MAANA KWA NYUMA WAPAO WANANUNGUNIKA ....JARIBUNI KUWAJALI WAFANYAKAZI WENU....MUNGU HAPENDI....MH MENGI ITV ...NA MAAKAMPUNI YAKO WATU WENGI WANALALAMIKA MISHAHARA MIBOVU ...MAISHA MAGUMU YYYYYYYYYYYY???????????
  BIBLIA INASEMA BARAKA HUANZIA NYUMBANI....
  NYIE MNATUFUNDISHA NINI????
   
 2. kabila01

  kabila01 JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2009
  Joined: Apr 21, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  tena jana Kampuni ya TBL imetoa milion 200 kudhamini mashindano ya miss Tanzania. wakati wangeweza kuwasaidia kuwalipia Ada wanafunzi wa sekondari zaidi ya 100 kwa mwaka na wangekua wameleta maendeleo makubwa sana kwa taifa. Hapa tunajifunza kua hii misaada wanayotoa inarudi kwao kwa kiwango kikubwa. in any business there is a winner and a looser. so hii misaada yao kwao ndo wanaowin na kwetu sisi ndio tunao loose ndo maana unaona wafanyakazi wao wana hali ngumu
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  something is better than nothing,ndio principle ya hawa jamaa.Walipe wastani wafanyakazi wako pata faida kubwa kwa ajili ya kusaidia wengine kama afanyavyo mengi.Tusimlaumu mengi wakati wote tunataka kugawana keki ya taifa sawa lakini haiwezekani.Mkuu huko vijijini hawalipwi kama wanavyolipwa hao wa ipp au bakhressa.Waacheni kwani japo wanafunaisha wengine nasi tunaona..........
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  Sep 3, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  mwazo ya kikoloni, mawazo ya kupenda kupewa na kusaidiwa saidiwa, waachani kina Mengi , Bahresa na TBL , watumie watakavyo pesa zao.
   
 5. K

  Kaingilila Member

  #5
  Sep 3, 2009
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mara nyingine wadau mtoe mifano ya ukweli na uwazi , hivi walimu wanaosaidiwa kuchangiwa kwenye vikundi saccoss kule vijijini ambao wengi wao wanapata mshaharara chini ya 150,000 unaweza kufananisha na mishahara ya pale IPP ?au ni watanzania wangapi wanaotafuta hizo kazi kwa bharesa na hawazipati na wanaishia kula lakaa moja kwa siku na kule vijijini kuna watu wako hatarini kufa na njaa
  ? je hawa hawaitaji msaada
   
 6. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Sasa mnadhani wanatakiwa wasaidie wakina nani? maana ukisema uangalie watu wakusaidiwa bongo ni kibao, wapo watoto yatima ,vijana wa mitaani ,wasiojiweza wasiojua hata kesho watakula nini etc. Mi binafsi naona hicho wanachofanya ni kizuri coz kwa tabia tulionayo watanzania wengi ya kusubiri kupewa na kutojishughulisha hata kama hao wenye uwezo wangekuwa wangapi bado tu hali itakuwa palepale. Jiulize wakiwasaidia hao wafanyakazi wao na hao wengine je????
   
 7. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Unaweza kua upo kwenye PR wewe. Hatulaumu watu kutumia pesa zao,bali michango wanayoitoa iwe na maana kwa jamii. It doesn't make sense kudeal na mamiss wakati mfanyakazi wako wa kima cha chini hana hata msosi. Shule za jirani watoto hawaendi madarasani kwa kukosa karo. Is that responsible citizenship? CSR lazima ilenge jamii,sio celebrities kila kukicha miss kinondoni,miss ilala,miss ubungo,miss temeke,miss chuo kikuu,miss chekechea etc.
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Sep 4, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  ambacho hujui ni ile kanuni ya quid pro co "something for something" awe Mengi, SSB, aBROMOVICH, DFID.....AU YOYOTE akupapo msaaada tegemea anataka kitu toka kwako.......TBL anadhamini warembo ukiwa ni mkakati wa kujitangaza kimataifa, Voda anadhamini soka kwa malengo hayohayo.........Usimpangie Mengi na SAB PAKUTUMIA PESA ZAO....usipende vya bure....kazi ya serikali ilioko madarakani ni kufinance shughuli zote za kijamii kuanzia Hospitali, Elimu , barabara...
  JIFUNZE UELIMIKE
   
 9. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #9
  Sep 5, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kuzamini ma miss sio CSR ile ni marketing ya kawaida
  CSR na kudhamini ni vitu viwili tofauti, get your facts right before you start talking
   
 10. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Duuuh!!
   
 11. M

  Msindima JF-Expert Member

  #11
  Sep 5, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Hivi hapa mada ni mishahara ya wafanyakazi kucheleweshwa au kutoa michango mbalimbali katika jamii,kudhamini mashindano? nielewesheni tafadhali.
   
 12. M

  Matumaini Member

  #12
  Sep 5, 2009
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Nguvumali umepanga vizuri kazi ya serikali hi kufinance shughuli zote za kijamii kuanzia Hospitali,Elimu n.k. Hili la juzi la serikali kuchangia miss tanzania mamilioni ya pesa kupitia TANAPA unalizungumziaje? Kisingizio ni kupromoti utalii kupitia mamiss. Jiulize kipaumbele ni mamiss au barabara na hospitali? Hao watalii wanakuja kuona jinsi barabara zetu zilivyo mbaya na hospitali zilivyokosa madawa? Kimsingi hii misaada/udhamini kuna wanaofaidika ndio maana wanakosa mantiki kwenye vipaumbele vyao. Nina uhakika walipa kodi tungeambiwa tuchague pesa yetu iende wapi basi wengi wangesema kwenye hospitali na elimu na sio kwenye mamiss. Sina tatizo na makampuni kwa sababu yalianzishwa kwa lengo la biashara (kutengeneza faida) na sio charities lakini kwa hili la serikali...haipo kwa ajili ya biashara!! (au manufaa ya wachache)
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Unajua Mitanzania inapenda sana sifa na kujionyesha inaona ikisadia watoto karo kwenye media haitatokea ndo maana yanafadhiri vichupi ili wapaishwe kweli bongo za mitanzania bado sana ndivyo ilivyo.
   
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Sep 5, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Matumaini wajibu mkubwa wa TANAPA Kupromote utalii, sasa bado naamini mamiss wanavuta watu wengi wakimataifa kwa hiyo kama wakati wamaonyesho hayo watakua wanadisplay mbuga zetu,na maeneo yetu ya utalii ,itatusaidia.
  hoja ya wajibu waserikali kufinance hivyo vitu vya msingi ni moja ya sababu ya serikali yETU kuwepo madarakani kama wakishindwa kuleta huduma za afya elimu,mabarabara...hakika wanapoteza uhalali wakukaa madarakani...na sikina Mengi,SAB KUTOA UFADHILI
   
Loading...