Bakari Kisongo Wa 'Twanga Pepeta' Anaswa Live Katika Tendo La Kulazimisha Mapenzi

Ibrahim300

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
390
68
Stori imetolewa hapa>>>
Bakari Kisongo Wa 'Twanga Pepeta' Anaswa Live Katika Tendo La Kulazimisha Mapenzi - bkuHABARI


Ufuska mtupu! Mnenguaji wa kiume wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Bakari Kisongo ‘Mandela’ ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kunaswa ‘laivu’ akililia penzi kutoka kwa dada aliyetajwa kwa jina moja la Zainab.

Tukio hilo la aina yake lililoshuhudiwa na ‘fotografa’ wetu lilitokea juzi nje ya Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar ambapo Twanga ilikuwa ikivurumisha burudani ya Sikukuu ya Krismasi.
Bakari Kisongo ‘Mandela’ akilazimisha penzi

Mara baada ya bendi hiyo kumaliza kufanya onesho lake majira ya saa 9:30 usiku, mnenguaji huyo alionekana akizama kwenye Baa ya Uhuru Peak inayotazamana na Mango kisha akamwita msichana huyo ili waondoke.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa karibu, kulitokea kama mtafaruku kwani msichana huyo alikataa katakata kuondoka na mnenguaji huyo.

Baada ya kuona hivyo, Mandela alitumia mbinu mbadala (nguvu) ambapo alimvutia mrembo huyo ndani ya Bajaj iliyokuwa imepaki eneo hilo ndipo mtafakuru ukazuka.

Huku na huku, dada huyo alipata upenyo ambapo alichoropoka na kutoka nje ambapo Mandela naye alimrukia na kuanza kumlilia huku akilazimisha mambo ya kikubwa hadharani ikiwepo ‘kudendeka’.

Hata hivyo, Mungu mkubwa kwa sababu mrembo huyo alifanikiwa kumtoka Mandela kisha akadandia Bajaj nyingine na kuondoka kwa kasi huku akimwacha jamaa na mfadhaiko.

Mashuhuda wa tukio hilo walimponda Mandela wakidai kuwa huo ni ufuska kwani kitendo alichotaka kufanya si cha kuigwa katika jamii.

Wanahabari wetu walipomtaiti Mandela kutaka kujua kulikoni kuomba mambo ya kikubwa hadharani hakuwa na la kusema zaidi ya kusikitika kumkosakosa mrembo huyo
 
Kuna mawili....
1.Huyo mandela ni buzi lako...sema kakusaliti ndo umekuja kumuaibisha humu
2.Inawezekana akawa ni shemeji yako so unamlilia wivu dada yako

Chagua moja kati ya hayo hapo juu
 
Back
Top Bottom