Bajeti yetu ya maadhimisho ya uhuru wa tanganyika hii hapa...ni kilio

kama ungesikiliza bbc swahili leo ndio ungeelewa tz did nothing kwa maadhimisho haya. Kama tumetumia 24b kufanya nothing kuadhimisha, jee tungeadhimisha inavyopasa, tungetumia ngapi?!.

Wana jf wenzangu, tusikalie kulalamika tuu na kulaumu kila wakati!. Sometimes tuwe positive kwenye baadhi ya issues sio kila kitu negative!.

Tumethubutu, tumeweza na tunazidi kusonga mbele!.

laana iko mlangoni mwako...aisee 24b ni kidogo...bila shaka ww sio mtanzania..unafurahia kabisa serekali imetumia fedha kidogo
 
Kwa siku za karibuni nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu kupitia kwa jamaa zangu pale hazina kujua gharama tulizoingia kwa kuandaa haya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika..

Kwa haraka haraka bajeti nzima ya maadhimisho haya ni bilioni 24 na kinara wa matumizi ni hazina wenyewe ambao wametumia karibu bilioni 4.Gharama hizi zinahusisha posho za wafanyakazi wa wizara mbalimbali waliohusika kwenye maonyesho ya miaka 50 ya uhuru na hasa kwa kamati ya maandalizi iliyokuwa chini ya mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda....

Gharama hizi zingeweza kulipa kiasi kidogo cha madeni ya walimu ambacho kinafikia karibu bilioni 64..Je,hii imekaaje watanganyika?

Nawasilisha!!
kwa hiyo sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuni wetu imegarimu pesa yote hiyo???wana JF na jamii yote kwa ujumla serikali yetu sio sikivu, ina dharau, na imejaa wafujaji, hata kama tukiimba hapa kila siku maovu yote yanayofanywa na serikali hawasikilizi la mwadhini wala mchungaji, wamedharau hata bunge letu,maazimio 23 ya kamati ya bunge iliyochunguza kashfa ya richmond hayakutekelezwa, juzi maazimio ya kamati ya bunge iliyochunguza kashfa ya jairo, luhanjo na ngeleja hayajatekelezwa na hayatatekelezwa, hiyo ni mifano michache kuonyesha dharau na kiburi cha watawala wetu sasa cha maana hapa tuanzishe mjadala namna ya kuwalazimisha wafuate na kutekeleza matakwa ya watanzania sio nmatakwa ya matumbo yao...
 
hicho kiasi mbona tumezuruliwa kipo chenyewe ambacho mtajaji kuona aibu atataja kwa dola...ngoja nakileta muda si muda
 
Kadilio la chini kabsaaaaaaaaaaa itakuwa 50billion ukianzia ngazi ya mkoa
Ela Tunazo tatizo vipaumbele
 
Kwa siku za karibuni nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu kupitia kwa jamaa zangu pale hazina kujua gharama tulizoingia kwa kuandaa haya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika..

Kwa haraka haraka bajeti nzima ya maadhimisho haya ni bilioni 24 na kinara wa matumizi ni hazina wenyewe ambao wametumia karibu bilioni 4.Gharama hizi zinahusisha posho za wafanyakazi wa wizara mbalimbali waliohusika kwenye maonyesho ya miaka 50 ya uhuru na hasa kwa kamati ya maandalizi iliyokuwa chini ya mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda....

Gharama hizi zingeweza kulipa kiasi kidogo cha madeni ya walimu ambacho kinafikia karibu bilioni 64..Je,hii imekaaje watanganyika?

Nawasilisha!!

Ndio maana viongozi wa baadhi ya nchi,walikataa kuja waliona ni upuuzi tu huwezi kuspend hela nyingi kwa mambo yasio na faida,hii nchi ni the comedy watazamaji wanatucheka sana.
 
Kama ungesikiliza BBC Swahili leo ndio ungeelewa TZ did nothing kwa maadhimisho haya. Kama tumetumia 24b kufanya nothing kuadhimisha, jee tungeadhimisha inavyopasa, tungetumia ngapi?!.

Wana jf wenzangu, tusikalie kulalamika tuu na kulaumu kila wakati!. Sometimes tuwe positive kwenye baadhi ya issues sio kila kitu negative!.

Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi kusonga mbele!.
I have never doubted ukanjanja, ubinafsi na unafiki wako pamoja na njaa kali ulinayo...hizi ndio sifa kuu za watu ambao wanasuport mambo kama haya ktk nchi hii.
 
Mie bnafsi sina tatzo na kiasi cha pesa ila nalia kuona pesa hii ambayo wemgine wamethubutu kutuambia ni takribani bilioni 50 inatumika huku kukiwa na matatzo lukuki ambayo yalitakiwa yafanyiwe kazi na ndo tungejipongeza

Nchi kama Kenya mfano wakitumia pesa hii kufanya hayo ntawapongeza sana kwani hata kuweza kuunda katiba mpya ya wakenya wote ni jambo kubwa sana,hapa kwetu njia za mawasiliano mbovu,viwanda vimekufa,hatuna huduma za afya za ndani zaidi ya kupeleka watu nje,wanasomeshwa wasiotaka kusoma na wananyimwa nafasi wanaotaka kusoma i.e wanavyuo na mikopo,katiba tumetungiwa sheria ya kukomoana,n.k

Ningeona furaha na nisingehoji thamani ya pesa hyo kama hayo juu walau yangekuwa yapo na yamefanyiwa kazi lakini kwa hali hii haya maadhimisho yamekuwa kazi bure na pesa yetu imeliwa tena
 
Kumbe ndo maana mishahara ya mwezi uliopita ilichelewa kutoka kwa baadhi ya taasisi.Wizi mtupu
 
Yawezekana kuwa kweli mkuu lakini ebu tuvute subira kidogo figa ya ukweli itaibuka na serikali itakubali japo itaaibika sana,hapa sisi ni waisraeli walioko misri tunamsubiri Mussa atuvushe kwenye bahari ya shamu.miili yetu imetiwa ganzi,macho yetu yanaona lakini hayawezi maana mwili umelogwa hauwezi kuact macho yanabaki kutoa machozi.Kibaya zaidi ya vyote ni kulogwa ufahamu,hivi hii si laana kweli???kwa kiongozi mwenye busara asingeingia harama hizi za bure kwanza kwa lipi???Tutayasikia hapa jinsi wajanja,wale werevu walivyotumia sherehe hii kujinufaisha kwa mabilion.la kuvunda halina ubani.
 
Billion 24 nahisi ni ambazo zinajulikana , zisizo julikana ni kama mara 10 zaidi maana kuna halmashauri zinadaiwa kutokana na hizo gharama za uhuru wa nchi isiyo julikana
 
inaweza ikawa kweli mana maonyesho ya pale dar ni zaid ya siku 9 na wizara zote zipo pale na wamefanya makubwa mana mi nitaanzisha library ya vitabu hapa kwa jins nilivyopata vitabu na majarida ya kila namna kuhusu serikali na sekta zake, pili maandalizi ya uwanja wa uhuru na wagen walikwa idadi ilikuwa kubwa so i thnk its okey hayo mabilion japo huku wilayan hawajafaidika kwa lolote zaid ya kuona kwa tv
 
Kama ungesikiliza BBC Swahili leo ndio ungeelewa TZ did nothing kwa maadhimisho haya. Kama tumetumia 24b kufanya nothing kuadhimisha, jee tungeadhimisha inavyopasa, tungetumia ngapi?!.

Wana jf wenzangu, tusikalie kulalamika tuu na kulaumu kila wakati!. Sometimes tuwe positive kwenye baadhi ya issues sio kila kitu negative!.

Tumethubutu, Tumeweza na Tunazidi kusonga mbele!.

kaka unaniboa sana.Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa.Una roho mbaya sana infact huna utu.
 
Matatizo yetu mara nyingi yanaanzia tangu kwenye familia zetu na ndiyo tunapanda hadi tunafika kwa viongozi wa nchi. Ni mara ngapi tunachangiana mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kuendeshea/kugharamia harusi tukijua kwamba na sisi tutakula na kunywa lakini ni wazito/wagumu kuchangia elimu kwa wasio na uwezo au hata wagongwa wanaohitaji misaada? Au kuchangia madawati ya shule?. Na ndiyo sisi hao hao baadaye tunakabidhiwa kuongoza nchi jiulize vipaumbele vyetu vitakuwa kwenye nini kama si sherehe na starehe maana ndiyo msingi tulioanza nao tangu chini.
 
hv mtu mzima upo chokest mbaya hata pesa ya mafuta ya taa kuwashia kandili huna una umuhimu wa kufanya birthday party kweli hadi kualika majirani na huku unadaiwa hadi kodi ya nyumba?
 
Kwa siku za karibuni nimekuwa nikifatilia kwa ukaribu kupitia kwa jamaa zangu pale hazina kujua gharama tulizoingia kwa kuandaa haya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika..

Kwa haraka haraka bajeti nzima ya maadhimisho haya ni bilioni 24 na kinara wa matumizi ni hazina wenyewe ambao wametumia karibu bilioni 4.Gharama hizi zinahusisha posho za wafanyakazi wa wizara mbalimbali waliohusika kwenye maonyesho ya miaka 50 ya uhuru na hasa kwa kamati ya maandalizi iliyokuwa chini ya mtoto wa mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda....

Gharama hizi zingeweza kulipa kiasi kidogo cha madeni ya walimu ambacho kinafikia karibu bilioni 64..Je,hii imekaaje watanganyika?

Nawasilisha!!

Sherehe zilizofanywa sidhani kama zilihitaji fungu kubwa la pesa kiasi hicho. Wajanja wachache watakuwa wamekupua na kujinufaisha kupitia mgongo wa sherehe za uhuru wa Tanganyika.
 
Maskini kuna mamia ya walimu wetu wamepandishwa madaraja tangu mwaka jana lakini hadi leo hawajarekebishiwa mishahara yao.Fedha zipo zinatumika kupigia matarumbeta ya uhuru!Dr Slaa ninakuona hapa.Hebu changia kidogo kuhusu hil!

Naunga mkono hoja. Dr. Uko wapi siku hizi? Njoo hapa jamvini japo kwa siku moja ukae nasi
 
Back
Top Bottom