Bajeti yawabana mabishoo, ni wale wanaopenda kusajili namba binafsi za magari na kuweka majina yao

John Cannor

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
1,464
1,824
Diamond Platnumz ni miongoni mwa mastaa ambao wataathirika na bajeti ya 2016/17. Kwani wamiliki wa magari wanaotaka kusajili namba binafsi kama kuweka majina yao, sasa watalipa Sh10 milioni badala Sh5 milioni za awali, kwa kipindi cha miaka mitatu.
xDiamonf-platnumz.jpg.pagespeed.ic.UMX5kjPQWS.jpg

Bajeti ya Serikali iliyotangazwa huenda ikapunguza idadi ya watu wanaopenda kuonekana tofauti, kwenye usajili wa magari kwa kuandika majina yao badala ya namba.

Akitoa mapendekezo ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2016/17 jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango aliomba Bunge liridhie kufanya marekebisho ya Sheria ya Magari (Kodi na uhamisho wa umiliki) ili kupandisha usajili wa namba hizo.

Namba hizo binafsi zilizoanzishwa miaka minne iliyopita, zinaruhusu mtumiaji kuandika jina au neno lolote kwenye gari lake tofauti na namba za kawaida zinazotumika nchini.
 
Mwasisi wa hii kitu alikuwaga waziri mmoja hivi anaitwa mgi sijui nani vile nae ametoweka ila leo ngoma inasonga
 
Hii inaweza ikashusha mapato badala ya kupandisha watu wakizisusia, I hope wamepiga mahesabu.
 
wanaolipia hizo kitu ni watu wenye pesa yao.. 5M na 10M kwao haina tofauti.. hata wangefanya 15M isingewazuia wao kulipia. Level ya maisha waliofikia inaangalia na kujali "status".. hongereni serikali kwa kuliona hilo..
 
Naam ni kukomoana na pia uwezo finyu wa kutoona mbali. Kwa kutoza milioni 10 kwa miaka mitatu wanaweza kupata watu tuseme 5,000 nchi nzima lakini kama wangekuwa wanatoza milioni 2.5 wangeweza kupata wateja laki mbili nchi nzima na hivyo pato kuwa kubwa zaidi.

Kumbe ishu ni kukomoana sio kuongeza wigo wa kodi ?kwani private number tatizo lake ni nini hasa ?? Badala washushe ili watu wengi wazimudu wanaongeza sijui ili iweje
 
10mil ni sawa na inalipika, hapo mwanzo sikuwa naelewa kwamba malipo ni ndani ya miaka tatu, nilidhani ni mwaka mmoja but anyway huwezi kosa wastani wa mil 3 na nusu ndani ya miezi 12 ikiwa wewe ni mfanya biashara wa ukweli!
 
Hilo halina shida, kodi ikiongezeka kwenye vitu luxury 'visivyo na ulazima' ni sahihi kabisa, ni kama inavyoongezwa kwenye bia na sigara, ila wadau wa kweli hata pesa iongezwe vipi bado wataendelea kutumia
 
hivi kuna mwenye njaa mwenye uwezo wa kulipia hata milion 5 ya zamani..

hapo hawamkomoi mtu..

mtu anamiliki lake oil au mo. dewji ashindwe lipia m 10 kweli??
Sasa hao kina Dewji wako wangapi ?? Ikishushwa lisifanywe jambo la anasa huoni kwamba mapato yataongezeka
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naam ni kukomoana na pia uwezo finyu wa kutoona mbali. Kwa kutoza milioni 10 kwa miaka mitatu wanaweza kupata watu tuseme 5,000 nchi nzima lakini kama wangekuwa wanatoza milioni 2.5 wangeweza kupata wateja laki mbili nchi nzima na hivyo pato kuwa kubwa zaidi.
yaani standard ya maisha tuliyonayo sijui ni lini wataona umuhimu wa kupunguza hili gape kubwa kati ya walionayo na wasionayo ,sioni sababu ya kufanya private number jambo la anasa wangeshusha hata anayemiliki bajaji akitaka aweke ,naimani wangepata mapato makubwa tu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Diamond Platnumz ni miongoni mwa mastaa ambao wataathirika na bajeti ya 2016/17. Kwani wamiliki wa magari wanaotaka kusajili namba binafsi kama kuweka majina yao, sasa watalipa Sh10 milioni badala Sh5 milioni za awali, kwa kipindi cha miaka mitatu.
xDiamonf-platnumz.jpg.pagespeed.ic.UMX5kjPQWS.jpg

Bajeti ya Serikali iliyotangazwa huenda ikapunguza idadi ya watu wanaopenda kuonekana tofauti, kwenye usajili wa magari kwa kuandika majina yao badala ya namba.

Akitoa mapendekezo ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2016/17 jana, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango aliomba Bunge liridhie kufanya marekebisho ya Sheria ya Magari (Kodi na uhamisho wa umiliki) ili kupandisha usajili wa namba hizo.

Namba hizo binafsi zilizoanzishwa miaka minne iliyopita, zinaruhusu mtumiaji kuandika jina au neno lolote kwenye gari lake tofauti na namba za kawaida zinazotumika nchini.
Kila mahali napokuta hii habari mbna anahusishwa sana diamond kwa namna moja au nyingne, kwan ni yy pekee ndo alikua ameweka Tanzania nzima? Wapo watu kibao wameweka sasa kwann tumhusishe diamond ktk hili.. Kuja kwenye mada kimsingi ilitakiwa bei ipunguzwe au ibaki pale pale ili kuvutia wengi zaidi na mapato Kuongezeka but labda kuna takwimu wamepiga wakaona bora waongezee kuja kwenye swala la diamond na wafanya biashara wakubwa 10mil kwa 3 years sio kitu.. Show moja ya diamond inalipa miaka mingapi? Ofcoz tunapata reason zaidi ya kutoona wengi wenye custom plate..
 
Akili nyingine bana, we umeandika kitu gani hapa? ndo maana hii post nimeitupia humu cerebrities forum, kumuhusisha DIAMOND na hii bajeti ni kwa sababu yeye ni moja ya macerebrity ambao wanatumia plate namba za kulipia majina yao.
Jiongeze mkuu.
 
Back
Top Bottom