BAJETI: Yaliyojiri, Uwasilishaji wa mapendekezo kuhusu makadirio ya mapato na matumizi 2017/18

Nililetewa Tax demand notice ya kulipia road licence kwa magari niliyouza kama scrapper/spea miaka sita iliyopita (millioni tatu nililipa) kwakuwa nilikuwa a nahitaji Tax clearance certificate sikuwa na ujanja zaidi ya kulipwa japo nililalamika humu Jf pia niliandika barua TRA kulalamika haikusaidia.

Budget iliyosomwa jana.road licence imefutwa kwa enfluence ya wabunge/wafanyabiashara ambao ni victim (wahanga)kwenye hili.imepelekwa mpaka kwenje majenereta/mashine za kusaga/mitambo italipa kodi hii ya matumizi ya barabara baada ya kuongezwa kwenye mafuta.

Naomba serikali sikivu kwa wahanga wenye vielelezo waliolipishwa hii regressive Tax watu rejeshee hela zetu kwakuwa wenzetu.wamesamehewa.
karibuni

Ndiyo taabu ya Waswahili umeshapewa lifti halafu bado tena unataka upige na honi.
 
Sio regressive tax, unailipa kadri unavyotumia gari lako, is it more of progressive tax
 
Mbona kinyume chake ni kupunguza kodi. Hali ya kiuchumi ya mtu mmoja mmoja si nzuri, mahitaji muhimu bei juu, uamuzi wa kawaida ya mtu ni kupunguza matumizi kwenye mahitaji yasiyo muhimu kama pombe.

Duh! Wewe jamaa ni profesa.

Mtu binafsi hapangiwi matumizi wala vipaumbele katika mahitaji yake kwa kupandisha kodi.
Kupandisha kodi ni kuongeza mapato ya serikali. Hakuna kitu zaidi ya hapo.
 
Duh! Wewe jamaa ni profesa.

Mtu binafsi hapangiwi matumizi wala vipaumbele katika mahitaji yake kwa kupandisha kodi.
Kupandisha kodi ni kuongeza mapato ya serikali. Hakuna kitu zaidi ya hapo.

Ni mtu ambaye hajui matumizi mazuri ya fedha atafikiri kama ulivyoandika. Ni kama mtu anayenunua gari ya bei mbaya na huku kapanga chumba kimoja. Huyo ndiye wewe ambaye unasema Mtu binafsi hapangiwi matumizi wala vipaumbele katika mahitaji yake kwa kupandisha kodi

Lakini kwa mtu makini, atakuwa ametambua kuwa utawala wa Rais Magufuli si wa matanuzi. Sera ya Bajeti ya Serikali yake kwa mwaka 2017/18, haikutoa mwanya wa kupata pesa kwa njia isiyo halali wala nafasi ya kuitumia kwa maisha ya kutanua km vileo na safari zisizo na tija (ukizingatia bei ya mafuta kuongezeka badala ya 'road licence'). Lakini ukitaka kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji au viwanda, kodi zimepunguzwa au kuondolewa kabisa.

Fursa za kazi kwa uzalishaji ziko wazi kabisa katika hiyo bajeti. Huitaji kwenda shule kugundua hilo. Lakini kwa kuwa tumezoea vya kunyonga, vya kuchinja tutavikimbia na kuanza lawama, shutuma, na kebehi zikisindikizwa ni kila aina ya maneno na lugha ya matusi.
 
Umesema vyema sana. Mi nimefurahia sana bajeti hii kama kungekuwa na ruhusa wangepiga wimbo wa simba wa yuda anaunguluma bungeni ili wabunge wacheze na kumpongeza Raisi wetu. Kwa kweli miaka kumi ikiisha tubadilishe sheria Raisi awe anachukuwa miaka 20. Yaani term ya kwanza 10 na term ya pili 10. Tukiona mambo yanaenda vizuri tunaweza badilisha tena yaani awamu ya kwanza miaka 20 na awamu ya pili 20. Haya mambo ya democracy eti miaka 5, hayana maana ni mbinu za wazungu kutupotezea watu wazuri wenye uwezo wa kuiongoza nchi
 
Wanaolalamika humu asilimia kubwa ni ""wapigaji" waliobanwa mbavu.

Nasikia kuweka heshima bar kumekwisha, siku hizi heshima inawekwa nyumbani.

Kwa hilo la nyumbani, tunashukuru ndoa zinazidi kuimarika. Baba anapata muda wa kukagua daftari za watoto tena amekuwa mwalimu wa tution watoto hawachezi mbali.
 
Ni mtu ambaye hajui matumizi mazuri ya fedha atafikiri kama ulivyoandika. Ni kama mtu anayenunua gari ya bei mbaya na huku kapanga chumba kimoja. Huyo ndiye wewe ambaye unasema Mtu binafsi hapangiwi matumizi wala vipaumbele katika mahitaji yake kwa kupandisha kodi

Lakini kwa mtu makini, atakuwa ametambua kuwa utawala wa Rais Magufuli si wa matanuzi. Sera ya Bajeti ya Serikali yake kwa mwaka 2017/18, haikutoa mwanya wa kupata pesa kwa njia isiyo halali wala nafasi ya kuitumia kwa maisha ya kutanua km vileo na safari zisizo na tija (ukizingatia bei ya mafuta kuongezeka badala ya 'road licence'). Lakini ukitaka kuwekeza kwenye kilimo, ufugaji au viwanda, kodi zimepunguzwa au kuondolewa kabisa.

Fursa za kazi kwa uzalishaji ziko wazi kabisa katika hiyo bajeti. Huitaji kwenda shule kugundua hilo. Lakini kwa kuwa tumezoea vya kunyonga, vya kuchinja tutavikimbia na kuanza lawama, shutuma, na kebehi zikisindikizwa ni kila aina ya maneno na lugha ya matusi.

Kuongeza kodi ni kuongeza mapato ya serikali.
Jifunze definition ya kodi.
 
Kuongeza kodi ni kuongeza mapato ya serikali.
Jifunze definition ya kodi.

Pole kwa kung'ang'ania tafsiri yako ya kodi kukidhi mtazamo wako wa kutaka kupinga bajeti.

Ni wewe, na watu wenye mawazo yako, ambao bajeti ya mwaka jana mmeipiga vijembe kwamba imekuwa na kodi zisizochochea ukuaji wa uchumi km utalii na 'transit goods' bandarini.

Kweli nyie watu mna matatizo ya ufahamu, duh! AIBU KWA FIKRA MGANDO HIZO
 
boss ile ni kwa magari ya zamani kama langu nilio lipark bovu lina lo daiwa miaka mitatu asa leo nimelitengeneza ile silipi tena, na kwa wale magari mapya alio nunua leo ana lipia mara moja baada ya hapo alipi tena ila watakukamata kwenye mafuta baba :D so piga hesabu kama ulikua una lipa 250,000 kwa mwaka jua kwenye kila wese litre mule wana kukata kodi yao ya roadlincese naisi kitu kama hicho
Ok asante nimefurahi ni afazali nilipe kidogo kidogo kwenye Mafuta kuliko kulipa nyingi kwa mkupuo
 
Pole kwa kung'ang'ania tafsiri yako ya kodi kukidhi mtazamo wako wa kutaka kupinga bajeti.

Ni wewe, na watu wenye mawazo yako, ambao bajeti ya mwaka jana mmeipiga vijembe kwamba imekuwa na kodi zisizochochea ukuaji wa uchumi km utalii na 'transit goods' bandarini.

Kweli nyie watu mna matatizo ya ufahamu, duh! AIBU KWA FIKRA MGANDO HIZO

Kuongeza kodi ya vilevi ni kutaka hela kutoka kwa walevi. Heshima kwa walevi. Acha dharau kijana.
 
Hawa wabunge sio wawakilishi wa wananchi kabisa, wameshangilia kufutwa kodi ya road license kwakua wamejiangalia wao tu na kusahau maumivu ya wananchi wao......wananchi wa kawaida wanafaidikaje na kufutwa kwa kodi hii ya magari. tutarajie maumivu makali zaidi ya haya tuliyonayo
 
Nakumbuka bajeti ya kwanza ya awamu ya 5 ilpokuwa inasomwa , ama tuseme hata yale maandalizi yake tu huku mitaani ( Tandika Mwembeyanga ) na Temeke yote ilikuwa ni shamrashamra zilizojaa bashasha kutoka kwa wananchi

Mamia kwa makumi ya wananchi yalijazana kwenye kila Tv iliyo mbele yao , Bar zilifurika wafuatiliaji waliojaa matumaini , zipo taarifa kwamba mmiliki wa Kings Palace ya keko yeye aliamua kuweka kiingilio ili kupunguza umati kwenye Bar yake .

Mshangao ni kwenye bajeti ya mwaka huu ! Hakuna hata anayetaka kuifuatilia .

Nini kimetokea ?
Punde utaambiwa umetumwa na mafisadi au Chadema. Kwani wewe hujaona wameondoa road licence na kuiweka kwenye mafuta? Ama kweli mwenye macho haambiwi tazama.
 
Sawa wapinzani wanapiga kila kitu.

Swali:

Umejiuliza ni lipi wapinzani waliwahi kulipinga na mwisho wa siku wakaumbuka?

Labda niulize,kati ya mambo 10 waliopinga wapinzani,ni mangapi yameenda vizuri kinyume na hoja zao?

Hivi hata hii Bajeti inayoishia June 30 mwaka huu ambayo tuliipinga, imefanikiwa kwa kiasi gani?

Akili ujazo wa kijiko cha chai ni hatari sana.
 
Tumejipanga watanzania kwenda tunakoenda? hivi kwanza tunajua tunakoenda? Safari yetu inaelekea wapi kwanza maana mapichapicha tu.

Mipango huku, Vitendo kule, Nini?

Lazima Watanzania tupimwe akili,
Huwezi kuweka Simu Chaji wakati simu haina Betri,
Au huwezi kuchaji Simu isiyokuwa bna Betri

Kwanza tunatakiwa tujue tunataka kwenda wapi, kisha tukakate tiketi ya huko, lakini hii ya kila siku ooooo tuko safarini, tukiulizwa tunaenda wapi tuataja popote tu haitufikishi tuendako.

Madini ni mali ya yani?
Je mikataba inamwelekeza cha kufanya kabla ya kusafirisha? hili nina mashaka nalo kwasababu kama Mchanga tu ni mali ya mwekezaji madini yatakuwaje na mipaka?

Watanzania tuamke jamani hii Nchi inatia aibu sana
Vijana uoga wetu ndio umasikini wetu.
 
Kuongeza kodi ya vilevi ni kutaka hela kutoka kwa walevi. Heshima kwa walevi. Acha dharau kijana.

Wewe ndo unawaza hivyo. Mimi ni babu. "Old is Gold" wasema wenzetu na sisi twasema "Kuishi kwingi kuona mengi". Katika maisha yangu nimejifunza kwamba moja ya umaskini wetu ni kuendekeza maisha ya kutanua, ulevi ukiwa ni mojawapo. Kwa kuwa tu maskini, tunaamini (saikolojia inatutuma) kwamba pombe hupunguza au usahaulisha matatizo. Isije kuwa wewe ni mmoja wao kwa kuwa unatetea kodi katika vileo ipunguzwe! Pole sana The Invincible.
 
Kiukweli mapato ya Seriakali ya awamu ya tano yanategemea kodi kutoka kwa wananchi, na anayedhani magufuli anaweza kupunguza au kuondoa kodi ya kitu chochote kirahisi, basi akapimwe akili. Kinachofanyika wamefunga mlango Wa mbele ila wameenda kutokea mlango Wa nyuma.

Poor Tanzania!!!!!
 
mbona swali jepesi kabisa mkuu.
1. mlimpinga vikali EL na hata mkashinikiza ajiuzuru wadhifa wake kama PM na ikawa hivyo, lakini mliumbuka pale mlipompa ridhaa ya kupeperusha bendera yenu!
2. mlipinga vikali safari nyingi za nje kwa viongozi, mmeumbuka pale mnapokuwa wa kwanza kuhoji mbona mkuu hasafiri?
3. kwa kutumia akili ya kawaida tu unatakiwa kufahamu kwamba, mwanasheria wenu amejiumbua mwenyewe kwa kuipinga ripoti ya prof. Mruma, kwa sababu alinukuliwa na mitandao ya kijamii akisema `pongezi kwa kazi nzuri iliyofanywa na tume' au `mpunga 'ulikuwa bado haujaingia? Sasa mleta uzi sina hakika kwamba hivi vitu huvijui.
 
Sawa wapinzani wanapiga kila kitu.

Swali:

Umejiuliza ni lipi wapinzani waliwahi kulipinga na mwisho wa siku wakaumbuka?

Labda niulize,kati ya mambo 10 waliopinga wapinzani,ni mangapi yameenda vizuri kinyume na hoja zao?

Hivi hata hii Bajeti inayoishia June 30 mwaka huu ambayo tuliipinga, imefanikiwa kwa kiasi gani?

Akili ujazo wa kijiko cha chai ni hatari sana.
`Bora mtu mwenye akili ujazo wa kijiko cha chai lakini anazitumia vizuri kuliko yule mwenye akili nyingi kama mchanga wa pwani asiye weza kuzitumia'-nygax
 
Back
Top Bottom