Bajeti ya Wizara ya Maji yaelekea kukwama Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya Wizara ya Maji yaelekea kukwama Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bitabo, Jul 9, 2012.

 1. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Wakuu tokea asubuhi leo nimefatilia kwa ukaribu mjadala wa Wizara ya Maji huko Bungeni na nadiriki kusema uwezekano wa Bajeti hii kukwama ni mkubwa.
  Wabunge wengi waliochangia hasa wa CCM (ambao wanatakiwa kuiunga mkono hata kama ni mbovu) leo wamshikilia shilingi yao.

  Mpaka Lusinde ameikataa
  Kessy wa Namanyere anasema wabunge amabo hawana maji kwao then wanaunga mkono hoja ni wanafiki na amewashauri wananchi wawafukuze majimboni. kamshauri na Naisbu spika asiunge mkono maana Kongwa hakuna maji.

  Anasema Sinza mnapaita kwa wajanja ila maji ni shida sijui wanaoga mto msimbazi? halaf mnakaa kuomba miongozo na taarifa hapa bungeni. Amemshauri Raisi aifute wizara ya maji maana haina tija kwa taifa. Anasema zamani ilikuwa wizara ya maji, nishati na madini (wizara moja) ila maji yalikuwa yanapatikana ila sasa iko separate na ndio imekuwa shida zaidi.

  Shabiby wa Gairo anasema wabunge wengi walijua Prof. maghembe asingerudi kwenye uwaziri baada ya yale mabadiliko ya Baraza. Anasema hata vitabu vya bajeti vilivyowasilishwa vina uongo mwingi.

  Wabunge wanashauri waziri apigwe viboko ili maji yapatikane.

  Haya ni maoni ya wabunge wa CCM.

  Wapinzani ndo usiseme

  My take: Kesho Act. PM Sitta anaweza kuja na kauli ya kuinusuru wizara hii
   
 2. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,054
  Likes Received: 1,440
  Trophy Points: 280
  Hii yote ni GERESHA! Wabunge wa CCM wataishia kuiunga mkono. Hawatathubutu kukubali "Kuiabisha" CCM. Kama kweli Wataikataa, basi ntatembea kwa miguu kuuzunguka Mlima Meru, kwa njia ya Kikatiti, Sanya JUU, Olkokola, Arusha Mjini hadi Kikatiti!
   
 3. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  wabunge wa ccm ni wazugaji siku zote wakishaitwa na kuambiwa bunge likivunjwa mkirudi kwenye uchaguzi hapa hakuna mwenye uhakika wa kurudi bungeni watabadilika fasta
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hawa wabunge walikuwa wapi wakati John Mnyika anasema 'tumefika kwa sababu ya uzembe wa bunge na upuuzi wa CCM? Walikuwa wapi?

  Bunge limepitisha mpango wa maendeleo wa miaka 5, na hii ni bajeti ya pili tangu mpango huo upitishwe na bunge. Kwa miaka yote miwili serikali imekuwa inaandaa bajeti kinyume na mpango ulivyo. Badala ya kutenga 35% ya bajeti kwa miradi ya maendeleo wao wamekuwa wanaweka 30%. Kama haitoshi vile, hata pale wabunge - hasa wa upinzani walipojaribu kuliongolea hili, wabunge wa CCM wakiongozwa na mchumi wao wa daraja la kwanza - Mwigulu wakaanza kejeli. Mwigulu aliwaambia hao wabunge kuwa serikali imetenga zaidi ya 35% kwa sababu kuna mambo ya elimu etc. Huu ulikuwa ni usanii na wabunge wa ccm waliingia chaka.

  Sasa less than month, tena kwenye kikao kile kile cha bunge, wanaanza kuhoji bajeti ya maji? Huku si kusimamisha basi kwa nyuma? Porojo za Mwigulu na kibendera chake shingoni sasa kitawanyonga wabunge wa CCM. Na hii ni wizara ya maji, bado wizara ya ardhi.

  CCM wana wabunge wengi wa kuteuliwa, wabune hawa hawana wapiga kura wa kuwahukumu, na ndio maana wamekuwa vinara wa kuzomea bila ya kuangalia hoja zinazowekwa mezani. Kitendo cha wabunge wa kuchagulia kwa upande wa CCM kuingia kichwa kichwa kwenye zomea zomea ya wabunge wa kuteuliwa kitawagharimu sana. Walitakiwa wajue direct link kati ya mpango wa maendeleo wa miaka 5 na key areas kama maji. Haiwezekani serikali imiliki magari ya Tsh 5 trillion lakini watu hawana maji, na huku bunge likiunga mkono hoja mwaka hadi mwaka! Kama wabunge na hasa wa CCM wangeamua serikali ipige mnada mashangingi yote mwezi huu na kununua bajaj hilo lingetokea. Bunge lina nguvu sana kama litafanya kazi yake sawasawa. Lakini kwa mtindo wa zomea zomea watajikuta miaka 5 imepita na ndipo lawama zitakapoanza.

  Na huu ni mwanzo, bajeti ya mwaka kesho itakuwa ngumu sana kwa sababu watajikuta matatizo mengi majimboni mwao bado hayajatatuliwa na muda wa uchaguzi unakaribia. Sitashangaa kusikia watu wananza kulaani wengine kama ilivyokuwa bunge la 9.

  NB: Huyo mbunge wa CCM naona ameamka usingizini, Sinza iko chini ya Mnyika, na amejitahidi sana kufuatilia tatizo la maji.
   
Loading...