Bajeti ya wizara ya kilimo na ushirika haikupitishwa kihalali

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Kama kawaida yake, leo hii spika Anne Makinda, kwa jazba, alikataa ushauri uliomtaka aamru bunge kurudia upya zoezi la kupitia bajeti ya wizara ya kilimo na ushirika fungu kwa fungu. Mtoa hoja hiyo, alisema zoezi la kupitisha vifungu hivyo siku ya juma mosi iliyopita ni batili kwakuwa wakati zoezi hilo likiendeshwa hapakuwepo idadi inayotakiwa kisheria kufikia uamuzi wa jambo lolote. Spika alitupilia mbali hoja hiyo kwa nadai kwamba kwakuwa kbunge hilo lilisitisha shughuli zake kabla ya kupiga kura ya kupitisha bajeti nzima, hivyo hakuna kilichoharibika. Kwa maoni yangu msimamo huo ni potovu, upitishaji wa bajeti unaanzia katika kupitisha kifungu kimoja kimoja; kwa mantiki hiyo kwakuwa idadi ya wajumbe waliopiga kura kupitisha hivyo vifungu haikutoshereza si sahihi hata kidogo kusema kuwa bajeti hiyo ilipita. Jambo la kujiuliza sasa, ni zipi hadhari zinazotokana na ukiukaji huo wa taratibu za kupitisha bajeti?
 
Yule maza hajielewi tu yupo msukuleni.Kama vile kabandikwa tu kwenye kile kiti!
 
Back
Top Bottom