Bajeti ya Upinzani yavuruga Bunge

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
JUMANNE, JUNI 19, 2012 06:32 NA BAKARI KIMWANGA, DODOMA

*Nchemba, Kapteni Komba wavurumisha matusi
*Wabunge wa CCM washangilia hadharani
*Mulugo, Chikawe, Wassira wampa fedha Nchemba
*Zitto aitaka Serikali kuacha kuendelea kukopa nje


BAJETI ya Kambi ya Upinzani Bungeni, iliyowasilishwa bungeni jana na Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha, Zitto Kabwe, imezua balaa. Jana jioni, baadhi ya wabunge wa CCM waliochangia mjadala wa bajeti hiyo, walionyesha kukerwa nayo kwa kile walichodai haitoi picha halisi ya maisha ya Watanzania.

Aliyekuwa wa kwanza kuvurumisha matusi wazi wazi ni Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba (CCM), ambaye alikuwa akitoa maneno yasiyofaa na kushangiliwa na wabunge wa karibu wote wa CCM kwa kupigiwa makofi.

Nchemba, alisema yeye ni mchumi wa daraja la kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kwamba hajawahi kuona bajeti mbovu na chafu kama iliyowasilishwa na Zitto.

Katika kuonyesha jinsi alivyokerwa na bajeti hiyo, Nchemba alitupa kitabu cha bajeti ya wapinzani, alichokuwa amekishika mkononi wakati akichangia.

Pamoja na hayo, alitaka wabunge wawe wanapimwa akili kabla hawajaingia bungeni.

Pamoja na kutoa kauli chafu na kutupa kitabu hicho, Mwenyekiti wa Bunge, Slyvester Mabumba aliyekuwa akiongoza Bunge kwa wakati huo, hakuchukua hatua zozote licha ya wabunge wa upinzani kuomba mwongozo juu ya kauli za mbunge huyo.

Kutokana na matusi hayo, baadhi ya mawaziri wakiwamo Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo, walimpa fedha Nchemba wakionyesha kuridhishwa na lugha chafu alizokuwa akitoa.

Wakati hao wakitoa fedha hizo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira na baadhi ya mawaziri, walionekana wakichukua fedha mifukoni kwa kuzikunja kwenye karatasi na kuwapa wahudumu wa Bunge wampelekee Nchemba.

Baadaye, Nchemba alionekana akihesabu fedha hizo ingawa hazikujulikana idadi yake kamili.

Pamoja na Nchemba, Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, naye hakubaki nyuma kwani alivurumisha matusi, akisema wabunge waache maneno ya kipuuzi.

Alisema kitendo cha wapinzani kuishambulia bajeti ya Serikali na Serikali kwa ujumla wake, ni upuuzi na wendawazimu na kwamba wabunge wanapaswa kupimwa akili kabla hawajaingia bungeni.

“Watu tuwe tunapimwa kabla ya kuingia bungeni, wale wanaotakiwa kwenda Milembe waende, wanaotakiwa kwenda huku waende maana naona kuna watu wana matatizo.

“Huko tunakokwenda ipo siku tutapigana ngumi humu ndani, ni vema kila mtu akaheshimu chama cha mwingine, siku tukipigana humu ndani mtaumia,” alisema Kapteni Komba na kushangiliwa.

Chanzo kikuu cha wabunge wa CCM kuvurumisha matusi, kilikuwa kauli zilizotolewa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA). Wakati akichangia mjadala huo, Lissu alisema bajeti ya Serikali na Serikali kwa ujumla haina nia ya dhati ya kukomboa Watanzania.

Katika mchango wake huo, Lissu alikuwa akitumia maneno mengi ya kiingereza, mengi yakionyesha kutoridhishwa na mwenendo wa Serikali ikiwamo bajeti ya Serikali iliyowasilishwa bungeni wiki iliyopita na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa.


BAJETI YA UPINZANI
Wakati huo huo, Zitto ameitaka Serikali itoe ufafanuzi wa matumizi ya chenji ya rada kabla ya Bunge halijapitisha bajeti.

Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), alisema hatua ya Serikali kuanza kutumia fedha hizo za rada hazikufuata utaratibu.

Zitto aliyasema hayo jana mjini hapa, alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Kambi ya Upinzani Bungeni ya mwaka 2012/13. Alisema kwamba ni lazima Serikali itoe maelezo ya kina kuhusu fedha hizo.

Alisema kwamba, wakati Kamati za Bunge zilipokaa kujadili taarifa ya Serikali kuhusu mfumo wa mapato na matumizi, Waziri wa Fedha, alitoa taarifa kuhusu fedha za rada zilizorejeshwa kutoka Uingereza, ambazo ni Sh bilioni 72.3.

Alisema fedha hizi zilizopokelewa Machi 26, mwaka huu, wabunge walipokea kwa mshtuko taarifa hiyo ya waziri ya kuwa katika mchakato wa kununua vitabu na madawati kwa kutumia fedha hizo.

“Kitendo cha Serikali kutumia fedha hizi kabla ya kupitishwa na Bunge, kitendo hiki ni kuvunja sheria za fedha, uhusiano na masuala ya Bajeti.

“Hata Waziri wa Fedha alipokuwa anawasilisha hotuba ya bajeti ya mwaka huu hakugusia suala la fedha zilizorejeshwa kutokana na ununuzi wa rada.

“Kwa hali hii, Kambi ya Upinzani inataka maelezo ya Serikali kuhusu fedha hizi na utaratibu uliotumika wa kununua vitabu na madawati katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Mwanza,” alisema Zitto.

Waziri huyo Kivuli wa Fedha, alisema ili kupunguza mzigo wa matumizi ya Serikali, ni lazima magari ya Serikali yapigwe mnada kama njia ya kushusha gharama na kuipa nchi uwezo wa kujiendesha kwa ufanisi.

“Kama kweli Serikali inahitaji kuweka mazingira mazuri ya kujiendesha, sasa ni wakati mwafaka wa kupiga mnada mashangingi ya Serikali kama alivyofanya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

“Mbali na hatua hiyo, bado Kambi ya Upinzani inaendelea kusisitiza kufutwa kwa posho za vikao katika mfumo mzima wa malipo na stahili kwa watumishi wa umma.

“Na katika kulinda gesi yetu ambayo hivi sasa inaendelea kugundulika mkoani Mtwara, ni lazima Serikali ianzishe Chuo Kikuu cha Mtwara kitakachokuwa kinatoa mafunzo ya gesi na mafuta,” alisema.

Kambi hiyo ya Upinzani bungeni, imeitaka Serikali kuiondoa bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa wiki iliyopita, ili ikatayarishwe upya kutokana na kukosa vigezo kwa mujibu wa mahitaji ya Watanzania.


Misamaha ya Kodi
Waziri huyo Kivuli wa Fedha, alisema katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2011/12, Serikali iliahidi kupunguza misamaha ya kodi mpaka kufikia asilimia 1 ya pato la taifa, lakini hadi sasa haijaweza kulitekeleza suala hilo.

“Ukwepaji wa kodi, utoroshaji wa mitaji nje na udanganyifu katika biashara ya kimataifa, huliangamiza taifa letu. Fedha hizi ni zaidi ya jumla ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi.

“Mbali na wizara hiyo, pia fedha hizo ni zaidi ya fedha za Wizara ya Uchukuzi na Nishati na Madini, kwani fedha hizo ni zaidi ya mkopo ambao Serikali itautumia kuidhamini TPDC ili kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam,” alisema.

Mishahara kwa Wafanyakazi
Zitto, alisema Kambi ya Upinzani katika bajeti yake mbadala ya mwaka 2011/12, ilipendekeza kuifanyia marekebisho Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004.

“Pamoja na Serikali kuamua kupandisha kiwango cha chini cha kipato ili kutoza kodi ya mapato kutoka Sh 135,000 hadi Sh 170,000, ni vema ikashusha kodi hii.

“Hali hii haimsaidii mwananchi wa kawaida hata kidogo, nasi Kambi ya Upinzani tunapendekeza kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi kipande hadi kufikia Sh 315,000.


Chenge atema cheche
Wakati Zitto akiyasema hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya Bunge, Andrew Chenge, ameitaka Serikali kuacha misamiati ya kupunguza matumizi na kufuta misamaha ya kodi nchini.

Chenge ambaye ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), alisema kitendo cha kila mwaka kuwa na bajeti ambayo inakinzana na hali halisi ya maisha ya Watanzania hakiwezi kukubalika.

Alisema kuwa, taarifa za mapato kwa mwaka ulioishia Juni 30, mwaka 2011, zinaonyesha kiasi cha Sh trilioni 1.016 kimepotea kwa njia ya misamaha ya kodi kwa mashirika ya umma, hasa katika miradi ya wafadhili, taasisi zisizo za kiserikali na za kidini pamoja na kampuni binafsi na kituo cha uwekezaji.

Alisema misamaha hiyo chini ya sheria ya ongezeko la thamani na misamaha ya kodi katika maduka ya wanadiplomasia yasiyotozwa kodi yalisababisha misamaha hiyo kufikia asilimia 18 ya makusanyo yote kwa mwaka husika wa fedha.

Alisema katika bajeti ya mwaka 2012/13, kamati hiyo inapendekeza Serikali kuchukua hatua za dhati kufuta misamaha ifikie asilimia moja ya pato la taifa kama zilivyo nchi nyingine katika ukanda wa Afrika ya Mashariki.


Deni la Taifa
Chenge, alisema kutokana na taarifa iliyowasilishwa mbele ya kamati hiyo na Waziri wa Fedha, deni la taifa hadi kufikia Machi mwaka huu limefikia Sh trilioni 20.2 kutoka Sh trilioni 17.5 Machi 2011.

Alisema deni hilo ni sawa na ongezeko la asilimia 15.4 na kwamba kati ya deni hilo, deni la nje ni Sh trilioni 15.3 na deni la ndani ni Sh trilioni 4.9.

“Kutokana na umuhimu wa kodi kwa taifa letu, kwa muda mrefu kumekuwa na tabia kwa wawekezaji, hasa wa nje kupewa misamaha ya kodi bila sababu za msingi.

“Zao la pamba ni muhimu sana, kwani linatoa ajira kwa wakulima wadogo wapatao 500,000 na kuwezesha maisha ya Watanzania, kwa hiyo ni wakati mwafaka kwa Serikali kutangaza bei ya pamba.

“Kwa hali hii, ninaweka wazi msimamo wangu ni lazima Serikali itambue bila Sh 1,000 ya kununua kilo ya pamba hakuna pamba na hili Serikali ilitambue,” alisema Chenge.

Wakichangia bajeti hiyo baada ya Kamati ya Fedha na Uchumi, Mbunge wa Sumve, Richard Ndasa (CCM), alivirushia kombora vyombo vya usalama kwa kushindwa kufanya kazi inavyopaswa.

Alisema kuwa, kuathirika kwa mapato ya Serikali kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa malipo hewa katika wizara na idara za serikali, hali inayowafanya wananchi kukata tamaa kwa viongozi wao.

Pia alipinga hatua ya Serikali kutaka kupandisha kodi kwa waendesha pikipiki, huku akionya kwamba hali hiyo itawafanya wananchi kuichukia Serikali yao.

“Kila eneo hivi sasa kumekuwa na malalamiko juu ya vitendo vya rushwa na Serikali inajua, tena kwa kuanzia na wizara ambazo ni vinara wa malipo hewa, zikiwamo TAMISEMI, Wizara ya Fedha na Wizara ya Kilimo.

“Pamoja na uwepo wa mambo hayo, Serikali katika bajeti yake haijasema namna ilivyoshughulikia tatizo hili.

“Kwa mfano hii TAKUKURU imelala mithili ya sanamu lililotegwa katika jaruba la mpunga, watu wanaiba lakini wao wamelala, na si hao tu, hata Usalama wa Taifa. Hivyo kutokana na umuhimu wa bajeti hii tunaviomba vyombo hivi vifanye kazi yake kwa mujibu wa sheria,” alisema Ndasa.

Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed (CUF), alisema kitendo cha Serikali kuwakumbatia wawekezaji kinaweza kuhatarisha usalama wa taifa.

“Kuna wawekezaji ambao huwa wanakuja nchini wakiwa na shida huku wakiweka mikono nyuma lakini baada ya kuingia mikataba na Serikali huanza manyanyaso dhidi ya wazawa, hili katu hatuwezi kulivulimia.

“Kwa kupitia bajeti hii na kama tunahitaji kumkomboa mkulima wa pamba, ni wakati mwafaka wa kuwathamini Watanzania kwa kuhakikisha Serikali inaweka mazingira mazuri ya soko.

“Kila kona wananchi wanalia na pamba yao, lakini Serikali haitoi bei dira katika zao hili, sasa kama wanahitaji kuuza kwa Sh 1,000 waruhusiwe na si kuwanyanyasa wakulima,” alisema Hamad Rashid.


 
Wabunge wa Chama Tawala wanatukana; Mawaziri wahusika wa Sheria wanatoa pesa kupongeza hayo Matuzi, Spika anakaa kimya , Wabunge wote wa Chama Tawala wanashangilia.

Sasa Mwengula ni Mwanauchumi na alisema alifanya kazi Benki Kuu hivi alikuwa anatukana huko Benki kuu pia?
Ni kwanini tunawawaweka watu kama hawa serikalini? wanatakiwa waachwe nje..

292252_373888672675121_719148731_n.jpg
 
Inashangaza sana pale hoja nzito za wapinzani zinapo jibiwa kwa kejeli na matusi na wabunge wa ccm.
Ushauri wangu kwa cdm ni kutokata tamaa bali kuendelea kufanya tafiti kisha kuibua hoja nzito bungeni.Wananchi tunawaelewa.
KWELI Itasimama kesho kama leo haitoshi!
 
Hawa watu wa magamba wanaonyesha ni jinsi gani wasivyokuwa na hoja, wao ni matusiiiiiiiiiiiii... tu. Bajeti isiyotekelezeka kila mwaka. Na sasa wanaonyesha ni jinsi gani walivyo na ambavyo hawatakubali kukabidhi inji kwa makamanda.:llama:
 
Inashangaza sana pale hoja nzito za wapinzani zinapo jibiwa kwa kejeli na matusi na wabunge wa ccm.
Ushauri wangu kwa cdm ni kutokata tamaa bali kuendelea kufanya tafiti kisha kuibua hoja nzito bungeni.Wananchi tunawaelewa.
KWELI Itasimama kesho kama leo haitoshi!

Kweli kabisa, Ukiangalia CHADEMA hawatukani hiyo Bajeti ya Serikali wanatafuta upungufu wake na kuutafutia sahihisho ili iwanufaishe watanzania wote na sio kutukana; Sasa kama ni kutukana kweli nani hapo anaathirika? ni Mwananchi

Sasa Mr. Mchemba hataki kusikia Marekebisho sio kuwa CCM ndio yenye Majibu ya Mwisho ya kusaidia wananchi wa Tanzania, ndio Maana kuna Upinzani... Upinzani hauna Matusi Umefuata haki yao na kuweka Marekebisho.
 
Ukiona mtu anatukana jua ameishiwa sera. Ndio siasa zetu za majitaka zilivyo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom