Bajeti ya upinzani moto; Barabara, reli, umeme, madini, kuikomboa nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya upinzani moto; Barabara, reli, umeme, madini, kuikomboa nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  • Barabara, reli, umeme, madini, kuikomboa nchi

  na Asha Bani

  KAMBI ya Upinzani Bungeni imetoa vipaumbele sita vya mchanganuo wa bajeti mbadala watakayoiwasilisha katika Bunge la Bajeti litakaloanza Juni 7, mwaka huu.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge, Naibu Katibu Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Christina Lissu Mughwai, alisema kipaumbele cha kwanza katika bajeti hiyo kitaelekezwa kwenye miundombinu.
  Alisema kipengele cha pili katika hotuba ya bajeti hiyo itakayotolewa na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa kambi hiyo ni umeme.

  Alisema katika miundombinu wataweka msisitizo kwenye barabara zote muhimu ambazo hazijaanza ili zinze kuanzia mwaka huu wa fedha pamoja na upanuzi wa Bandari ya Mtwara.

  Alisema wataboresha Reli ya Kati ili iweze kufanya kazi ya kusafirisha mizigo na abiria kwa kiwango cha kuridhisha mpaka hapo fedha za kujenga reli mpya itakapopatika pamoja na Shirika la Ndege la Taifa liweze kuongezewa mtaji wa kulifufua hatimaye lijiendeshe kibiashara na kwa ufanisi zaidi.

  Kuhusu kipaumbele cha umeme alisema wataangalia umeme wa makaa ya mawe 1500MW (Souther power complex) migodi ya Mchuchuma, Ngaka na Kiwira, umeme wa gesi (Mtwara gas pipeline) 300 MW kutoka Mtwara, Dar es Salaam hadi Mwanza kwa kutumia PPP kati ya wawekezaji binafsi na NSFF.

  "Pia kutakuwa na mradi kabambe wa kusafirisha na kusambaza umeme mijini na vijijini chini ya TANESCO na REA (Rural Energy Agency)," alisema Christina.

  Alisema kipaumbele cha tatu ni kuwezesha ukuaji wa sekta za uzalishaji na hasa ukuaji wa uchumi wa vijijini kwa kuboresha miundombinu, upatikanaji wa maji safi na salama sambamba na kuongeza ubora wa bidhaa za kilimo na kupeleka umeme vijijini.
  Kipaumbele cha nne ni kusimamia maendeleo ya rasilimali watu, kuwekeza kwenye ubora wa elimu, huku akieleza watahakikisha watoto wanaomaliza kidato cha nne wanapata mafunzo ya ufundi ili waweze kujiajiri wanaporudi vijijini.

  Alieleza bodi ya mikopo ya elimu ya juu inapata fedha za kutosha kutoka kodi ya uendelezaji ujuzi na kwamba 2/3 ya kodi hiyo ambayo inakwenda Hazina ibaki kwenye bodi ili kukidhi mahitaji ya mikopo.

  "Kimsingi lengo la bajeti yetu katika elimu ni kupata elimu bora na si wingi wa majengo ya shule ama wanafunzi wanaomaliza shule na kuanzisha pensheni kwa wazee wote wenye umri zaidi ya miaka 60," alisema Christina.

  Alisema wataanzisha pia bima ya afya kwa wananchi wote itakayokuwa ya lazima kwa watu wote, wafanyakazi na wasio wafanyakazi na ichangiwe na wananchi wenyewe pamoja na serikali. Alisema kipaumbele cha tano ni kuimarisha utawala bora na katika hilo wanapendekeza kuwepo na fedha za kuwezesha mchakato wa kuandika katiba mpya ili Watanzania wote waweze kushiriki mchakato wa katiba mpya.

  Wataimarisha pia TAKUKURU kwa kuanzisha kitengo maalumu kwa ufisadi mkubwa sambamba na mfumo mpya wa kudhibiti mgongano wa maslahi, wafanyabiashara wanaruhusiwa kisheria kuwa wanasiasa ili mradi kusiwe na mgongano wa kimasilahi, kuwe na uwazi wa kutangaza mali za kiongozi.

  Pia kuanzisha ofisi ya bajeti ya Bunge ili kuweka uwazi zaidi kwenye bajeti ya serikali ambapo kwa sasa wabunge hawahusishwi katika kupanga bajeti ya serikali, tunapendekeza itungwe sheria ya bajeti itakayowezesha kuanzishwa kwa ofisi ya bajeti, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri ya watu kufanya biashara na kupunguza urasimu katika ngazi mbalimbali," alisema Christina.

  Katika kipaumbele cha sita ni kuimarisha usimamizi wa mashirika ya umma kwa kuanzisha Office of Public Enterprises, CHC kusimamia hisa za mashirika yote ya umma yaliyobinafsishwa kama kampuni mama.

  Katika kuzingatia hilo kambi hiyo pia itaanzisha ‘National Investiment Fund' kwa ajili ya kutoa mitaji kwa mashirika ya umma na mapato yake kutokana na asilimia ya faida za mashirika inayokwenda kwenye bajeti.

  Pia kusimamia matumizi ya fedha za royalty (mrabaha) kutoka kwenye madini na mafuta na kuanzisha mamlaka ya mafuta na kuibadili TPDC kuwa shirika la kibiashara na mafuta (Petrotan) na Shirika la Gesi (TanGas).

  Katika hotuba yake Zitto ataainisha vyanzo vipya vya mapato na kuboresha vilivyopo katika mchanganuo wa kupunguza bei ya mafuta kwa asilimia 40.

  Alisema vyanzo vingine vya mapato vitakuwa katika kusimamia kupanua wigo wa kodi kwa kuweka lengo la kukusanya mapato ya ndani sawa na 20% ya pato la taifa na kuongeza wigo wa walipa kodi.

  Katika vyanzo hivyo vya mapato pia vitaangalia mfumo mpya wa utawala wa kodi, mfano makampuni yanayofanya kazi hapa nchini lakini yamesajiliwa nje na hivyo wanalipa kodi huko walikosajiliwa.

  Kufuta kodi ya presumptive ambayo inasababisha makampuni madogo (SME) yasijisajili kwani hiyo inasababisha ukwepaji kodi katika sekta isiyo rasmi.

  Atapunguza pia exemptions (misamaha ya kodi) mpaka asilimia 1% ya pato la taifa kutoka 4.5 ya sasa, sambamba na kufuta sitting allowance na kupunguza matumizi yasiyo na maana kwenye maofisi. Alieleza kuwa kodi ya mapato kwa makampuni yote yatakayojisajili katika soko la mitaji kuwa ni 20% na 25% ya PAYE zibaki kwenye halmashauri husika badala ya kupeleka zote TRA. Mashirika ambayo serikali ina hisa yajisajili katika Soko la Mitaji (DSE) ili hisa za serikali ziweze kuuzwa na kuweka sheria kali za kuzuia ukwepaji kodi kwa mashirika makubwa ya nje na hasa kampuni za madini na mafuta.
   
 2. k

  kiloni JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hata ikikatakaliwa na magamba tutaiweka kama kumbukumbu ya kuyashitaki majambazi ya magamba kwa waajiri wao!
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sio swala la kukataliwa ama kukubaliwa isipokuwa binafsi naona ni upumbavu mkubwa sana kuzungumzia vitu hali mkijua kwamba HAVIWEZEKANI chini ya utawala huu. Ni upotezaji muda na fedha za wananchi kwa sababu hivi vitu vyote vilihitajika na vitaendelea kuhitajika toka tupate Uhuru na ndivyo vinavyoongoza maendeleo ya nchi yeyote...

  Sasa chini ya Ufisadi uliopo kuweka mikakati ya ujenzi wa Taifa hali hakuna kiongozi hata mmoja mwenye uzalendo ni hadithi za abunuasi kudanganyana wakati viongozi hawa wanakula mishahara na posho kwa kila kauli zao bungeni..

  Kwanza wekeni sheria mpya ya Uzalendo - Patroit Act provisions ambayo kazi yake kubwa ni kupiga vita Ufisadi kwa nguvu zote..Safisheni kwanza wizara, idara, taasisi, Halamashauri na mashirika ya Umma kuondoa viongozi wote wanaojihusisha na rushwa kwa sababu wanafahamika, kisha ndipo mnaweza kutengeneza budget yenye matumaini ktk ujenzi wa vitu hivi. Kifo cha ATC, TRA, Kiwira na vyanzo vingine vyote za miundombinu haikuwa bahati mbaya kwani budget zilizotangulia zililenga kuimarisha vitu hivyo, lakini kutokana na Ufisadi vilisifadiuwa zaidi TRA ikauzwa kwa wahindi, ATC na South Afrika yote haya yalitokana na mawazo mazuri tu ktk budget yetu isipokuwa utekelezaji wake ndio kazi mpya..

  Nitarudia kusema kwamba huwezi kufikiria kupanda mbegu za mazao shambani kabla hujafikiria usafi wa shamba lenyewe kwa sababu haiwezekani kupanda mbegu bora ktk shamba lenye magugu na Upalilizi wake usiwe kipaumbele... Na bila kuchoka nitasema tena na tena kwamba huwezi kuijaza ndoo maji ikiwa ndoo hiyo imetoboka! Zibeni tobo kwanza kabla ya kufikiria kujaza maji mnapoteza sauti nguvu na muda wa wananchi!

  Hamuwezi kaeni pembeni wenye nia ya kuleta Uzalendo kwanza wachukue nafasi ya kutuwakilisha!
   
 4. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Hii siyo bajeti,ni overview ambayo iko too general for a great thinker to discuss,lets wait till we see the "real" budget ya opposition.
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Sioni jipya wala la maana .
   
 6. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Uwe muwazi kwamba hujui kupambanua, unakariri kama madrasa!
   
 7. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 655
  Trophy Points: 280
  Nonyeshe sehemu ambayo bajeti hii itatoa elimu bure mpaka kidato cha sita.
   
 8. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mengi yanasemwa kila mwaka, lakini wanaotakiwa kufanikisha tusonge mbele wanayafumbia macho huku wakiendelea kusubiri misaada. Tatizo hapa ni maamuzi kuwa magumu na ugumu wakuyatekeleza. That's crazy you know.
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nimeipenda sana signature yako yaani imetoa majibu mazuri sana kwa wanasiasa wa Kitanzania - An empty stomach is a bad political adviser, by Einstein;
   
 10. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kwa akili yako huwezi kuona lolote hapa, naona umeingia choo cha kike.
   
 11. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mkandara, hii ndo sumu kubwa kwa bara letu la Africa, siku tukiacha kutumia hii sumu tutasinga mbele. People become politicians in order to survive against the nature even at the expense of somepeoples lives. We must change they we do things, politics should not be the beggining and the end of our decisions for the country. Natamani sana hao Usalama wa taifa wawe independent siyo kama sasa ambapo kila mtu maarufu ana watu wake ndani ya System.
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Labda ulmaanisha choo cha wanawake, kwani choo cha "kiume" huwa keki?
   
 13. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2011
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,807
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  ???Are you serious!??Kama huoni jipya wala la maana hapo basi nina wasiwasi kuwa uwezo wako ktk uchanganuzi na kufikiria una mapungufu!! i suggest you re read the original post again, this time pay more attention to what is written and take your time!! Usikurupuke!
   
 14. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  saababu hata magamba hawawezi kuwa na jipya sababu ya WIZI!
   
 15. KIMICHIO

  KIMICHIO JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 1,184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  kama wewe usivyo mpya wala wa maana.
   
 16. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #16
  Jun 3, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kobello, Wakishika dola. Si bado mpaka 2015?
   
 17. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kwa uwezo, upeo na ufahamu wako c ajabu kuwa ulivyo
   
Loading...