Bajeti ya Tanzania inawaua wananchi wake kweupe......viroba vimeshika hatamu.

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Kulingana na serikali ya Tanzania kusoma bajeti ambayo kwa kiasi kikubwa inategemea pombe,,yaaani ulabu wakakti maisha ya Wtanzania yakizidi kuwa magumu, wananchi wa tanzania sehemu nyingi waesema wao wanaacha kunywa bia na wanahamia kwenye viroba ambavyo bei yake ni nafuu lakini vinalewesha haraka. Viroba hivi ni vile vyenye muundo wa kikonyagikonyagi.........na vingine ni vya bandia ambapo wajanja wanajaza gongo........nakuwauzia wananchi. Viroba hivi vina madhara mengi kwa afya. Hili ndo litakuwa kimbilio la Mtanzania anyetumia pombe lakini ambaye hana fedha ya kumudu pombe isiyo na madhara mwilini. Kwa nini wale Barick wasibanwe badala la kuacha mashimo tu kwa Watanzania?

images


Hiki ni moja ya tegemeo
la pato la taifa

Pamoja na hayo............kwa walioko maeneo ya mipakani pombe zinatarajiwa kunywewa kwa wingi ambazo ni aina ya viroba zimeshapigwa marufuku nchini zinamotengenezwa lakini kwa tanzania bado vina soko mfano angalia hapa chini

[h=1]Uganda: Poisonous Alcoholic Brands Banned, Leaving 30 Dead[/h]
alcohol_sachets_eeNlQ_16419_470x352.jpg


The banned illegal liquors as Empire Waragi, African Gin, Princes Vodka, Planet Vodka and Rwenzori Gin. Another brand, 3R Zed, is also being investigated.
Dr. Joseph Senzoga, the disease surveillance response coordinator observed that, “They may have taken drinks containing methyl alcohol, a deadly poison,” he says. Methyl alcohol is a poisonous chemical found in paint remover.
Before death, the individual develops the following symptoms: loss of vision, headache, vomiting, diarrhoea, drowsiness, body weakness and coma. (Source : Uganda: Poisonous Alcoholic Brands Banned, Leaving 30 Dead)

Ushahidi mwingine huu (Standard Digital : Killer Ugandan drink popular among Kenyans despite ban)

Report za vifo kutokana na matumizi ya viroba kwa wingi yameripotiwa mara nyingi katika nchi za wenzetu ambao walishajichokea zamani. Sasa ni zamu ya Tanzania. Bia zitapanda na mzuka wote utamalizwa na viroba hata vile vinavyoweza kutuua. Na kwa sasa fanyeni kufuatilia kwenye baa nyingi mtakuta Kitu konyagi kwa sasa inafunika. Kule Kagera vipo viroba ambavyo ni marufuku kunywewa
na wananchi lakini ndivyo vinaongoza kwa kunywewa. Vinaitwa Empire, vingine Vodka, Vingine Lord, ni vikali ajabu. Kiroba kikubwa kweli lakini kinauzwa jero tu. Ukinywa viwili unaweza ukapotea njia usiende kwako.Watanzania tusubirie mengi.

 
Yaani mtaona wenyewe hali isivyo shwari. watu maofisini Hangover hazitoki kuanzia asubuhi mpaka saa12 jioni....ukifuatilia walikunywa viroba au pombe kali sana ambayo inauzwa bei rahisi
 
Bia!, hata iuzwe elfu kumi. Mimi nitakunywa tu. Bora watoto walale na njaa lakini mimi na kinywaji damdam.
 
T Muganyizi, kwani Kanyimbi sio mtanzania wa kawaida?! Wakawaida tukoje?

Jina jenyewe unaliona hilo? "KANYIMBI"..............MTANZANIA wakawaida anakosa fedha ya kula alafu yeye anasema hata bia iwe elfu kumi laima anywe...ujue pombe kwake ni burudani wakati mwingine anakunywa ili pakuche haraka
 
TBL inaongoza kwa kulipa kodi!jee watanzania wangefuata maamrisho ya dini kutokunywa pombe,ina maana govt ingefilisika
 
Wenye vihela hela kidogo kama sisi Tutapiga 'visichana'. Heri kupiga kasichana kamoja ukapata stim za Ndovu 7.. Saving inakuwa kubwa zaidi.. i.e 3000 vs 12600. wow
 
Mimi hata soda nitakuwa sinywi, naanza kutafuta matunda asilia niwe nakula badala ya viburudisho kama hivyo!
 
Wenye vihela hela kidogo kama sisi Tutapiga 'visichana'. Heri kupiga kasichana kamoja ukapata stim za Ndovu 7.. Saving inakuwa kubwa zaidi.. i.e 3000 vs 12600. wow

Unatisha kwa kubajeti.........bora ukalisaidie bunge na mzimu wa bajeti
 
Mimi hata soda nitakuwa sinywi, naanza kutafuta matunda asilia niwe nakula badala ya viburudisho kama hivyo!
Kwa kuwa matunda nayo bei yake haishikiki kwa watu wa kawaida, ni kunywa maji tu inatosha.
 
ulichokisema ni kweli viroba ndio vipo kwenye to ten kwa sasa na huku kaskazini kuna pombe inaitwa banana wine na kimorali vijana wanakunywa sana akiwa na 1100 anapata banana 2 na kiroba cha jogoo wao wanasema kala ndizi kuku vijijini siku hizi ikifika saa nne kama kaburi halijachimbwa huwezi pata kijana mwenye nguvu kwa ajili ya ulevi
 
kuna jamaa yangu zamu yake ya kucheza pool table ikifika lazma atupie kiroba. et ndo inamsaidia kulenga. hafu hachanganyagi ata na xoda. kavkav tu.
 
Back
Top Bottom