Bajeti ya Serikali ya Zanzibar kusomwa leo

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Bajeti ya Serikali ya Zanzibar kusomwa leo Na Salma Said, Zanzibar

BAJETI ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya mwaka wa fedha wa 2008/09 itasoma leo jioni kwenye Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha na Uchumi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini.


Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee alisema maandalizi yote yamekamilika na kikao hicho kitaanza asubuhi kwa maswali na majibu na jioni Bajeti ya Serikali itasomwa na waziri anayehusika.


Akitoa muhtasari wa bajeti hiyo, Waziri Makame alisema kasi ya ukuaji wa uchumi imekuwa na kufikia 6.8 kutoka asilimia 6.5 katika kipindi cha mwaka jana.


Mwelekeo wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2008/09 umepewa jina la Bajeti ya Maendeleo kutokana na sehemu kubwa ya bajeti hiyo ikiielekezwa kwenye shughuli za maendeleo kuliko matumizi ya kawaida ambapo asilimia 28.7 imeelekezwa kwenye matumizi ya kawaida.


Alisema kasi ya ukuaji wa uchumi wa pato la taifa inatarajiwa kuongezeka kutoka ukuaji wa wa asilimia 6.5 mwaka 2007 hadi asilimia 6.8 mwaka 2008 huku serikali ikihitaji kutekeleza kwa ukamilifu Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini.


Waziri huyo amesema serikali itaendelea kutoa msisitizo kwenye maendeleo ya kilimo na miundombinu kama sekta saidizi.


Dk Mwinyihaji alisema hali ya matatizo yanayoendelea duniani matarajio ya awali yalionesha kuwa uchumi wa Zanzibar kwa mwaka wa fedha 2008/09 utaendelea kuimarika licha ya athari za umeme zuilizojitokeza kwa mwezi mzima sasa.


Alisema kwa mwaka wa fedha 2008/09, serikali inakusudia kutekeleza programu 20 zikiwemo programu mpya tano na miradi ya maendeleo 64, kati yake imo miradi mipya 13.


Alisema malengo ya mpango wa bajeti ya mwaka 2008/09 serikali imelenga kukusanya mapato ya ndani yenye jumla ya Sh134.550 billioni sawa na asilimia 21.4 ya pato la taifa kati ya mapato hayo Sh 124.709 billioni yanayokana na mapato ya kodi na Sh 9.841 billioni yanayokana na mapato yasiokuwa ya kodi.


Dk. Mwinyihaji alisema serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha inategemea kupokea misaada na mikopo kutoka nje yenye thamani ya Sh 205.16 billioni inayojumuisha Sh 23.407 billioni ambazo ni mgao wa asilimia 4.5 ya misaada ya kibajeti (GBS) kupitia serikali ya muungano.


Kati ya fedha hizo zimo pia Sh.8 billioni kutoka Mpango wa Misahama ya Madeni (MDRI).


Serikali alisema pia itaendelea kukopa kwa nia ya kuziba pengo la bajeti kutoka fedha za ndani kwa kupitia mfumo wa Hati Fungate za Serikali ambapo mikopo hiyo imepangwa kupunguzwa mwaka hadi mwaka kwa lengo la kuepukana na athari za kiuchumi ambapo jumla ya Sh 2.0 billioni zitapatikana kupitia kiazio hicho.


Mapato ya viazio vyote hivyo Dk Mwinyihaji amesema yanajumuisha uwezo wa serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2008-09 huku jumla ya mapato yote ni Sh 341.709 billioni.


Waziri huyo alisema serikali ilikadiria kukusanya jumla ya Sh 114.5 billioni mapato ya ndani ikiwa ni asilimia 37.7 zaidi ya makadirio ya mwaka 2006/07 ya Sh 83.1 billioni kiwango hicho cha makadirio ya mapato ya ndani ni sawa na asilimia 17.2 ya pato la taifa kwa mwaka 2007.


Alisema utekelezaji halisi hadi mwezi Machi 2008 ulifikia asilimia 73.6 ya lengo la mwaka sawa na Sh. 84.3 billioni na matarajio ya makusanyo hadi mwisho wa Juni 2008 ni kufikia Sh111.4 billioni sawa na asilimia 97.3 ya lengo kwa mwaka.


Misaada na mikopo kutoka nje hadi mwezi Machi 2008 serikali ilipata Sh 49.1 billioni sawa na asilimia 41.2 ya makadirio ya Sh 119.1 billioni huku upande wa misaada ya kibajeti (GBS) serikali ilipokea Sh 26.1 sawa na asilimia 96.5 katika jumla ya Sh 27.1 billioni zilizopangwa kutolewa mwaka mzima.


Kwa mwaka wa fedha wa 2008/09 matumizi ya kazi za kawaida itakuwa Sh149.4 billioni sawa na asuilimia 43.7 ya matumizi yote huku matumizi ya kazi za maendeleo jumla ya Sh 192.2 billioni sawa na asilimia 56.3 ya matumizi yote yaliopangwa.


Kati ya fedha hizo, Sh 18.5 billioni ni mchango wa serikali na Sh 173.7 billioni zitatokana kwa wahisani wa maendeleo.

http://mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=6243
 
Wabunge ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Wakakilishi sijui sasa hivi wanatakiwa wawe Dodoma au Zanzibar.

Tofauti na Tanzania Bara, majimbo ya Uchaguzi ya Zanzibar yana wawakilishi wawili: Mbunge wa Jamhuri na Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Wakiwa Zanzibar, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanaamua yanayowahusu, ya Zanzibar; Wakiwa Bungeni wanaamua yanayowahusu ya Jamhuri, na yasiyowahusu ya Tanzania Bara (kumbuka BUnge la Jamhuri linapitisha Sheria za aina mbili, za kote kote na za Bara tu).

Very interesting model, to say the least!
 
Na Ali Suleiman, Zanzibar

BAJETI ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) itasomwa leo jioni huku ikionesha kuwapo kiwango cha ukuaji wa uchumi na kuimarika kwa sekta ya utalii na uwekezaji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Uchumi, Dkt. Mwinyihaji Makame, anatarajiwa kuwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2008/9 hapo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi.

Maandalizi ya kikao hicho yamekamilika na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka kambi ya CCM kwa muda wa siku moja walikuwa wamejichimbia Kiwengwa.

Wajumbe hao walikuwa wakipigwa msasa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais Amani Abeid Karume, akiwataka kuelekeza juhudi na nguvu zao katika majimbo ya uchaguzi kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Rais Karume alisema mwakilishi bora ni anayeshughulikia matatizo ya wananchi katika jimbo alimochaguliwa na ambaye pia yuko mstari wa mbele kusaidia maendeleo katika jimbo lingine bila ya kujali itikadi za kisiasa.

Taarifa za Ofisi ya Rais, Fedha na Uchumi ilisema uchumi umekua kwa asilimia 6.8 na kusema tatizo la kukosekana kwa nishati ya umeme kwa mwezi mmoja sasa, halijaathiri mwelekeo wa uchumi.


Baadhi ya mambo ambayo yanatajwa kuchangia ukuaji wa uchumi ni uwekezaji kwa asilimia 37.5 kutoka sh. bilioni 101.3 mwaka juzi hadi sh. bilioni 139.3 mwaka jana.

Pia kuimarika kwa sekta ya utalii na uwekezaji vimechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji uchumi ambapo jumla ya watalii 137,111 waliingia nchini mwaka juzi na kiwango kuongezeka hadi 143,265 mwaka jana sawa na ongezeko la asilimia 4.5. (Majira)

Nje ya bajet kumradhi: Raisi bora ni yule anaepeleka huduma (uteuzi) kulingana na kura alizopata kwenye constituency or kisiwa, ila mwakilishi bora ni yule anaeshughulikia matatizo kwake yeye na jimboni kwa mwenzake bila kujali tofauti za kiitikadi.
Dk mbona unasahau so sooon...
 
Back
Top Bottom