Bajeti ya serikali na fedha iliyotengwa kuanzisha JKT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya serikali na fedha iliyotengwa kuanzisha JKT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kupelwa, Jun 15, 2012.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Bajeti ya serilali iliyosomwa jana imetengwa bilioni 7.5 kuanzisha jeshi la kujenga taifa.

  Hakuna mtu anayepinga kuanzishwa kwake, kutokana na misingi na umuhimu wake. Lakini je, fedha hiyo ni toshelezi kwa vijana 5000 kukidhi mahitaji ;hasa tukizingatia si msimu wa kilimo, kuwa vijana watalima na kupata vyakula.

  Pia ikumbukwe kutakuwa na mavazi rasmi, viatu, madawa, usafiri na utawala.

  Ikumbukwe pia miundo mbinu ya makambi mengi ni chakavu yanahitaji marekebisho makubwa hasa mahanga na mabwaro.

  Pia fedha hizi ninavyofahamu, vijana hawa hupewa fedha za kujikimu kama posho;je fedha hizi zilizotegwa si meremeta nyingine huku mpango huu kutekelezwa kiufinyu nakuwa wenye kero!!.

  Kumekuwa na miradi mingi kama MMEM, MES na mingine imeachwa kutekelezwa ipasavyo kwa kushindwa kutengewa fedha ya kutosha hivyo kuwa kero isiyokidhi matakwa.

  Je, kulikuwa na ulazima kuanzishwa iwapo fedha zilikuwa hazitoshi?nakumbuka mwisho wa siku CAG na wabunge baadaye watakapohoji ufinyu wa utekelezwaji wa mpango huo, kutaibuka, majibu ya kwamba; maswala ya kijeshi ni usalama wa nchi hayapashwi kuhojiwa kama ilivyokuwa kwa merelemeta.
   
 2. H

  Hute JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,921
  Trophy Points: 280
  ulitaka nani alalamike, labda nyie mnaojua hayo mambo ya jeshini ndo mlalamike basi...
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu hiyo hela ni fupi sana haitoshi hata miezi minne
   
 4. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Hili suala linaanzishwa kisiasa mno ili kujijengea umarufu kuelekea uchaguzi 2015; ili kujenga hoja ya kujenga uzalendo kama dhana ya kujenga utaifa au ni kama posho kwa wapiganaji kama ilivyokuwa meremeta.

  Lakini bilioni 7.5 ni kiasi kidogo mno kufanya mpango huo uwe wenye tija. Na kama hakukuwa na fedha, haikuwa na sababu kuanizisha kwa sasa bali hizo zingepelekwa kwenye miradi umuhimu mkubwa kama kilimo au mingine.
   
 5. M

  Mokerema JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kupewa!

  Tuliza huo Mpira , tungojee kwanza tuangalie Kama hao Zumbukuku waliopo Bungeni Kama watapitisha huo upuuzi. Nawashauri hizo Biloni 7.5 zipelekwe kule Ocean Road wakanunue vifaa vya kupima saratani inayoua watu Mia moja kwa siku . Nitawashangaa sana Magamba wakiipitisha. Sijasikia wakijadili changed structure ya JKT. Huyo Mgimwa ni another pumba Kama alivyokuwa Zakhia Hamdani Meghji.

  Huwezi weka misamaha ya kodi kwa wamachinga eti hawapati zaidi ya milioni tatu kwa mwaka? CCM use you're
   
 6. J

  John W. Mlacha Verified User

  #6
  Jun 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  mkileta JKT inabidi msahau kura za vijana 2015. JKT ni janga la taifa % 60 wote watakufa kwa ukimwi.
   
 7. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  CCM wanaamini kuwa vina wengi wanaichukia kwasababu ya kukosa uzalendo, na kwa mujibu wa CCM uzalendo ni kukubaliana na kila kitu amabcho kiongozi wa CCM anafanya na kusema.

  Hivyo basi JKT inaanzishwa kama Barin wash kwa vijana, LAKINI nimekaa najiuliza kuwa kuna mtu yeyote aliyefanya feasibility study kwa niaba ya CCM kuoana kama huu mpango wao utazaa Tangible results (kwa Upande wao)?

  Ninaogopa wanaweza wakaja wakajuta maana kuna uwezekano mkubwa mpango huu ukafire back vibaya mno, Imagine vijana hao wakatoka na mbinu za medani za kivita, na baada ya CCM kufanya uchakachuzi wake kwenye sanduku la Kura ikaamua kutumia jeshi kuzima People's Power, na hao vijana waliotoka JKT wakawa upande wa UMMA?

  What next?
   
 8. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  kabla ya kupitisha hiyo bajeti wakubaliane kwanza kuwa ambao hawajapita jkt na wako kwenye ajira ni lazima kuwa na cheti cha jkt. ili nape, rizimoko, mwigulu, lusinde, . . . . . . wakapige kwata kwanza.
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu jogi unaonekana ulipiga kwata! Kambi gani mkuu, coy na operation gani!!!

  Nimekuwa nikisikia kila mwaka zinatengwa hela kuanzisha upya JKT lakini sijaona chochote. Hiyo billion 7 haitoshi hata Kambi moja yenye kombania moja! Hayo ni masikhara. Vijana inabidi wawe wanakula nyama japo hata mara moja kwa wiki, unajua bei ya ng'ombe huko? Wale wali japo hata mara mbili kwa wiki, unawajua wazabuni wewe? Vijana wavae buti na nguo wapate vigodoro (nina hakika yale ya zamani hayapo tena), wapate mestini na kikombe cha uji! kuna kitu hapo?

  Msiogope sioni JKT ikirudi. Hatuwezi kuimudu tena gharama yake ni kubwa mno.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wivu wa kike
   
Loading...