Bajeti ya Serikali ikishasomwa inaweza kubadilishwa?

Nadhani (Nahisi Wajuvi mtanirekebisha kama nimekosea) hiyo ni ' Proposed Budget ' ambayo imekuwa ' tabled ' na Waziri ili sasa Wabunge waijadili na hata Wadau (Mimi na Wewe) tutoe Mawazo yetu kisha yawasilishwe.

Yapo ambayo yatabadilika na ambayo hayatabadilika vile vile kulingana na ' Presha ' ya ' Kimapokeo ' yake tangia ilivyowasilishwa. Hata hivyo kwa Bunge la sasa usitegemee makubwa kwani ni Bunge la ' Kidhaifu ' sana.
 
Write your reply...ndio ishapita hiyo
Haitakiwi iwe hivyo kama bunge linafanya kazi kwa ufanisi

Vitu vinatakiwa vijadiliwe kwa point ili kama kuna item haina maslahi kwa taifa, iondolewe.

Ndio maana halisi ya upinzani bungeni ili kusudi vitu vijadiliwe kwa maslahi ya Taifa.
 
Hv bajeti aliyosoma Mheshimiwa Mwigulu nchemba ni final au ipo subject to changes kulingana na bunge litakavoijadili na je kuna chance kuwa inaweza kubadilishwa?
Hayo ni mapendekezo tu- itakapojadiliwa na bunge zima kisha na kamati ya bunge zima na kutungiwa sheria ya fedha ndipo tutakapokuwa na bajeti kamili inayotekelezeka kisheria.
 
Hv bajeti aliyosoma Mheshimiwa Mwigulu nchemba ni final au ipo subject to changes kulingana na bunge litakavoijadili na je kuna chance kuwa inaweza kubadilishwa?
Wabunge wanaweza kutoipitisha na kumwambia arudi ajipange upya aje na bajeti nyingine japokua sijawai ona hapa kwetu labda hii itakuwa ya kwanza
 
Hivi bajeti aliyosoma Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ni final au ipo subject to changes kulingana na Bunge litakavoijadili na Je kuna chance kuwa inaweza kubadilishwa?
Yes inaweza kubadilishwa kwa aina tatu.
1. Maoni ya wabunge walio wengi, wakati wa kuchangia, wakipendekeza mabadiliko, waziri anaweza kufanya marekebisho wakati wa majumuisho.

2. Mbunge anaweza kuzuia shilingi kwenye mshahara wa waziri, na kushinikiza harudishi mpaka kifungu fulani kibadilishwe.

3. Bunge linapokaa kama kamati ya Bunge zima kupitisha bajeti, kule kinatajwa kifungu kwa kifungu na kuulizwa kama kinaafikiwa, kisipo afikiwa na walio wengi, waziri analazimishwa kubadili.
P
 
Kwa Tanzania bajeti ikishasomwa huwa haibadilishwi. Kunakuwaga na marekebisho madogomadogo sana yanayotokana na michango ya hoja za wabunge.
 
waziri anaweza kufanya marekebisho wakati wa majumuisho.
Hicho ndicho hufanyika. Mabadiliko huwa ni jambo kubwa, ambalo hubadili sura na dira ya bajeti kabisa.

Bajeti inasomwa, inakataliwa na bunge inarudishwa kwenda kubadilisha halafu inaletwa tena. Haijawahi kutokea nchi hii. Japo kinadharia inaaminika inaweza kufanyika (I stand to be corrected)
 
Yes inaweza kubadilishwa kwa aina tatu.
1. Maoni ya wabunge walio wengi, wakati wa kuchangia, wakipendekeza mabadiliko, waziri anaweza kufanya marekebisho wakati wa majumuisho.

2. Mbunge anaweza kuzuia shilingi kwenye mshahara wa waziri, na kushinikiza harudishi mpaka kifungu fulani kibadilishwe.

3. Bunge linapokaa kama kamati ya Bunge zima kupitisha bajeti, kule kinatajwa kifungu kwa kifungu na kuulizwa kama kinaafikiwa, kisipo afikiwa na walio wengi, waziri analazimishwa kubadili.
P

On a serious note , mbunge gani anaweza kuzuia shilingi kwa bunge la sasa?
 
Hicho ndicho hufanyika. Mabadiliko huwa ni jambo kubwa, ambalo hubadili sura na dira ya bajeti kabisa.

Bajeti inasomwa, inakataliwa na bunge inarudishwa kwenda kubadilisha halafu inaletwa tena. Haijawahi kutokea nchi hii. Japo kinadharia inaaminika inaweza kufanyika (I stand to be corrected)
Kwasabu bunge la chama kimoja cha mapinduzi wanakua wengi sana na hapo ndio chimbuko la unyonge
 
Hivi bajeti aliyosoma Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ni final au ipo subject to changes kulingana na Bunge litakavoijadili na Je kuna chance kuwa inaweza kubadilishwa?
Hahahaha kwa Wabunge wale? Watasapoti upupu wote pale kisha wakitoka hapo wanawalaumu Chadema!
Pale hakuna Mbunge anayejitambua hata mmoja.

Narudia kwamba pale kuna genge la CCM ambalo lipo kwa maslahi binafsi, rejea yule Mbunge Mwanamke wa CCM aliyesema kuwa Ubunge ni Mtamu kiasi kwamba yuko tayari kuua ili asikose ubunge
 
Yes inaweza kubadilishwa kwa aina tatu.
1. Maoni ya wabunge walio wengi, wakati wa kuchangia, wakipendekeza mabadiliko, waziri anaweza kufanya marekebisho wakati wa majumuisho.

2. Mbunge anaweza kuzuia shilingi kwenye mshahara wa waziri, na kushinikiza harudishi mpaka kifungu fulani kibadilishwe.

3. Bunge linapokaa kama kamati ya Bunge zima kupitisha bajeti, kule kinatajwa kifungu kwa kifungu na kuulizwa kama kinaafikiwa, kisipo afikiwa na walio wengi, waziri analazimishwa kubadili.
P
Bwana P iyo namba 2. Imekaaaje naomba unifafanulie nieleweee anazuiaje iyo shilingi kwa namna gani?
 
Hahahaha kwa Wabunge wale? Watasapoti upupu wote pale kisha wakitoka hapo wanawalaumu Chadema!
Pale hakuna Mbunge anayejitambua hata mmoja.

Narudia kwamba pale kuna genge la CCM ambalo lipo kwa maslahi binafsi, rejea yule Mbunge Mwanamke wa CCM aliyesema kuwa Ubunge ni Mtamu kiasi kwamba yuko tayari kuua ili asikose ubunge
Kikweli ccm wanajiwakilisha wenyewe sio wawakilishi wa wananchi inabidi kila mtu ajiwakili mwenyewe hawa watu hata aibu hawanaga
 
Kwa wabunge wa sasa, sidhani kuna hata mmoja anaweza kupinga.
Hata kujaribu kunyoosha mkono wa kuikataa linaweza kuwa kosa la jinai, na yawezekana mshahara/ posho ya mwezi huu asilipwe akilalamika watamwambia wewe siuliipinga bajeti sasa unataka hela itoke wapi.
 
Back
Top Bottom