Bajeti ya serikali 2012/13-mbovu haina mwelekeo na ni sawa na bajeti ya city council !! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya serikali 2012/13-mbovu haina mwelekeo na ni sawa na bajeti ya city council !!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Macos, Jun 16, 2012.

 1. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  bajeti yetu imesomwa...napenda kuuliza ni vipi bajeti hii itasaidia kuondoa umaskini ? Vipi itaongeza ajira? Vipi itapunguza vifo vitokanavyo na maradhi kwa masikini wasio kuwa na uwezo wa kujilipia matibabu? Vipi serikali inapanga kupunguza vifo vya wazazi na watoto ? Vipi inapanga kupunguza ama kuzuia maambukizi mapya ya h.i.v ,...

  Kwa ufupi bajeti ya mara hii ukichambua inaonesha kama mwandishi alikua ana harkaa tu ya kuandika andika mambo ambayo haya jafanyiwa utafiti ama wasomi wetu wamechoka . Na nimesikia wachambuzi wengi lakini nao pia wame shindwa kuona mapungufu makubwa yaliopo
  yafuatayo ni mapungufu na ambayo inafanya nbajeti hii kuwa mbovu kuliko zote duniani!!


  1. kilimo...bajeti haijazungumza kabisa mikakati ya kuendeleza kilimo, japo bado tunaamini kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wetu...waziri ameshindwa ama hakutaja kilimo kama ni priority..kuna matatizo ya chakula, kuna matatizo ya wakulima wa korosho , mahindi na mpunga(mchele) ameshindwa kueleza kilimo kinachangia kiasi gani katika bajeti ya taifa ama inachangia kiasi gani katika gdp ya taifa !!
  2. hakuna mipango yoyoyte mfano ya umwagiliaji maji mashamba, ama kuanzisha kilimo cha umwagiliaji , jinsi ya kutafuta masoko ya mazao ya kilimo
  3. waziri ameshindwa kueleza akiba ya chakula iliyopo na mikakati ya kuongeza akiba zaidi ili kupunguza bei ya chakula ..hakuna mipango yoyote iliyoitajwa kuhusu ruzuku ya mbolea ama matrekta.kwa ufupi waziri hakutaja chochote katika bajeti yake kuhusiana na kilimo...neno kilimo halikuwemo ndani bajeti hii isipokuwa kwenye msamaha kwa wazalishaji wa zabibu kwa ajili ya mvinyo!! Hiii ni ya mwaka kwa taifa linalojidai kilimo mwanzo lakini bajeti yake imesahau kuweka mikakati ya kuendeleza kilimo
  4. elimu..education...hakuna taifa litaloendelea kiuchumi bila ya kuweka mkakati madhubuti kuhusu kuendeleza elimu...waziri tulitegemea atasema mfano serikali itatoa ruzuku ya vitabu na madaftari bure kwa deprived community ama watoto wa masikini wasio jiweza,mipango ya kujenga nyumba zaid za walimu, mipango ya kuangalia maslahi zaidi ya walimu, mipango ya kuondoa tatizo la manamano ya wanafunzi wanao andamana kufatilia mikopo ya elimu..tulitarajia waziri atatenga bajeti ya kuwa na japi library katika shule za secondary ,kuzidisha uchapaji wa vitabu nk,...jee imetenga kiasi gani kuwapeleka watanzania njee kusomea fani muhimu za kukuza uchumi? Au ndio nafasi hizi mpaka tupate msaada tu? Ni wakati kwa serikali kuwa na mipango ya kupata wataalam walo bobea...na isongejee scholarship za bure.
  5. china walipo jua wanahitaji wasomi wali peleka watoto wao marekani kwa wingi kusomea fani mbali mbali..leo usione vya elea vimeundwa....bila ya elimu taifa huwa la wajinga
  6. kwa ajabu kabisa waziri ameshindwa kutaja elimu kama ni muhimu na kipaumbele katika bajeti yake ya ajabu...kwa ufupi neno elimu limetajwa mara mbili tu katika bajeti hii na halihusiani na sera ya elimu
  7. madini..na gas...waziri wetu ameogopa ana ameshidwa kabisa kutaja pato litokanalo na uchimbaji wa madini...waziri hakutaja mfano uchimbaji wa dhahabu na tanzanite una changia kiasi gani katika pato la taifa ama gnp.
  8. waziri ameshindwa kueleza makampuni hayo ya madini yatachangaia kiasi gani katika bajeti ya tanzania, wakati gold inapanda bei kila siku makampuni hayo yanashindwa kuwekea kodi itokanayo na faida wana yopata.
  9. serikali ingeweza kuongeza corporate tax kwa makampuni haya ya madini mpaka 35%
  10. windfall tax ingetozwa kwa makampuni haya ...na 10% ingesaidia kuondoa malalamiko kwamba sekta hii haisadii chochote kwa taifa.
  11. waziri ameshindwa kutaja kiasi ambacho kitachangiwa katika bajeti kutoka kwenye madini badala yake ..anataja sigara, bia , soda ,,,hii inashangaza sana
  12. waziri pia ameshindwa kutaja kampuni ya pan african inayo chimba gas songo songo itachangia kiasi gani katika bajeti ya taifa..hii kampuni inafanya faida kubwa sana kutokana na gas yetu
  13. waziri haku eleza taifa litapata kodi kiasi gani kutikna na watafutaji wapya wa gas , madini na mafuta, kume kuwapo na ugawaji mkubwa wa vitalu vya mafuta na gas,...na waziri ana shindwa kueleza hawa wata changia kiasi gani katika bajeti ijayo
  14. kuna wageni hawa wanao pewa vitalu vya madini na mafuta ..kuna mtindo wa kuuza hisa zao mara wanapo gundua upatikanaji wa mafuta ama gas...haya mauzo hufanyika nje na kwa mabilion ya dollari...bila ya tanzania kupata chochote .,..tungetarajia serikali ikaanzisha tax regime ya 25% kwa mauzo yoyote yatokanayo na vitalu hivi
  15. pia serikali inashindwa kuweka utaratibu wa ku-tax uuzaji wa shares kwa makampuni ya ndani kwa ma share wa nje...mfano ilipo uzwa celtell..na sasa royal palm kwa serena
  16. kwa ufupi waziri ameshindwa kufanya haya amabyo yangesaidia sana pato la taifa na ingesaidia kupunguza payee hadi tshs 500,000 badala ya kumkata kodi mlala hoi anepata mshahara wa 170,000...
  17. waziri hakugusia chochote kuhusu madini gas na oil exploration
  18. waziri hakugusia kabisa kuhusu afya ya watanzania na serikali imepanga kutumia kiasi gani kupuza maradhi na vifo kutokana na ukosefu wa huduma bora za afya
  19. maji nayo haya kutajwa....
  20. ama mambo mengine mengi mfano kubadili sheria za soko la hisa, ukweli utabaki kwamba soko hili letu ni kama halipo..jee mikakati gani serikali inayo kulifanya likue na lisaidie ukuaji uchumi? Mfano sheria zake za kwa makampuni kuweza ku ji list? Jee hazi hitaji kubadishwa? Jee hakuna uwezekano wa sheria kuruhusu kamapuni ndogo ( sme) kuweza kuwa listed?
  21. yapo mengi niliyo yaona katika bajeti hii ila ukweli sioni ni kwa vipi bajeti hii ina msaidia mlalahoi....labda kama yupo anaweza kunielimasha zaidi
  umaskini hawezi kuondoka kama taifa halina wasomi wajuzi wa mambo walo bonea, taifa lenye watu wenye afya nzuri,watu waenye matumaini na waso kata tamaa ya maisha...
  Ubovu wa bajet ni mkubwa ila sasa naachia hapo kwa wengine kuchangia..ama kukusoa
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Next time tutakuchaguwa wewe uwe waziri wa fedha. Gombea Ubunge.
   
 3. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Naye huyu alimkosoa Mkulo ndo akapewa wizara, Tanzania nchi ya ajabu vyeo ni kwa kuogopa kupingwa????!!!!
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Naona huna la kusema, nawewe mkosoe basi halafu uwe waziri wa fedha.
   
 5. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #5
  Jun 17, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Suluhisho sio kugombea ubunge...wabunge wapo wa kutosha ila tatizo lao wote wanajishughilisha zaidi na 'ufisadi wa vijisenti' kama yule kauza kiwanja, yule kala pesa za halmashauri, yule tenda ya chai kampa dadake, nk nk.

  ufisadi mkubwa upo kwenye sekta ya madini na gas..na mafuta inakuja pia...huku taifa halipati kitu hawa watu wana chukua profit yote , hawalipi corporate tax inayo endana na faida halisi wana yopata, tanzanite ime tajirisha haya makampuni,
  kama mauzo yao haya ya dhahabu yangedhibitiwa basi yagesaidia kuifanya fedha yetu iwe imara..leo bajeti ina tajwa bila ya kueleza sekta hii ita cha ngia kiasi gani haya ni maajabu na wabunge wetu sio leo wala jana wote wana ogopa kuweka msimamo ulo wazi..mpaka lini rasi lima li hizi zitaendelea kutajirisha nchi za wengine badala sisi?

  Dhabu inauzwa nje...akiba inakuwa ya wanaonunua, na fedha yote ya mauzo inabaki huko huko nje..jamani kama hatuna akili ?
   
 6. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #6
  Jun 17, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  wenzetu Botswana wanafaidika kwa nini? jee na wao wana waachia makampuni wasilipe kodi kwa kila kitu wana choagiza kama sisi? hapa tanzania hawalipi kodi ya machine zao, mitambo yao, mafuta yao ya kuendesha magari yao na mitambo...
  lakini pia wana chukua profit yao yote wana tupa loyalty ya 4%
  • botswana loyalty ni 4% mpaka 10% kwa dhahabu
  • tax on profit ni 25% na inaweza kupanda mpaka 50%
  • serikali inakuwa na interest katika kila mgodi..wa 15%
  • madini yana changia 32.4 ya GDP na 50% ya income tax...Jee sisi tumerogwa ?
   
 7. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #7
  Jun 17, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Unajua kwa mujibu wa World bank ...corporate tax kwa migodi ya dhahabu inatakiwa isiwe chini ya 50% ya proft? kwa nini sie tunakuwa magoi goi..jee maslahi binafsi ?
   
 8. Macos

  Macos JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2012
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 1,831
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  waziri na soma bajet bila ya kuwa fahamisha watanzania mwenendo mzima wa uchumi wa tanzania...ukoje unaelekea waapi...bajeti haiweki wazi deni la taifa .
  bajeti ina shindwa kuonesha akiba yetu ya fedha za kigeni ni ngapi..jee ina tosheleza imports za miezi mingapi
  bajeti haisemi vipi hali yetu ya cha kula ...
   
 9. mzamifu

  mzamifu JF-Expert Member

  #9
  Jun 17, 2012
  Joined: Mar 10, 2010
  Messages: 3,496
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Hawa viranja wanajua tunakotaka kwenda lakini hawajui hasa ni njia ipi itatufikisha huko. Nyuki na Dondola wote hutafuta asali: nyuki anaenda kwenye maua lakini dondola anatoboa mbao. hivi ndivyo dunia ilivyogawanyika.
   
 10. B

  Bob G JF Bronze Member

  #10
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Lini ccm wakawa na bajeti ya kuondoa umaskini? waondoe umaskini watatawala tena! nani atakubali kuhongwa Ubwabwa na Tshirt atoe kura Umaskini wetu ndo mtaji wa ccm kuendelea kutawala, kama hutaki umaskini Tanzania Hamia M4C tusaidiane kuwaondoa hawa maharamia na mafisadi ccm
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hiyo bajeti ya wanachuo ndo huwa hivo,,,maana anasubir boom,na serikal nayo inafanya hivo maana inasubir boom la(wanaowaita wahisan)
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wabunge wengi hawajui kabisa mipango ya fedha na uchumi, hususan hii mikubwa ya nchi nzima, hivyohivyo ni kwa wana siasa wengi. Hivi mtu kama Slaa, ndio kachambuwa nini hiyo bajeti? ana cv ipi inayomfanya awe na kauli juu ya bajeti ya nchi?

  Mtu ambae naweza kuukubali uchambuzi wake wa bajeti bila kusita kwa wanasiasa wetu, wa kwanza kabisa ni Lipumba, wengine huwa wanangoja magwiji wa "economics" watoe maoni wao warukie hoja. Tazama bunge utanielewa. Tazama na uchambuzi wa hoja utanielewa, mtu kama Slaa, au Mbowe ambao hata basic accounting hawaijui unafikiri wana ubavu wa kuchambuwa bajeti?
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  maneno ya hekima haya
   
 14. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #14
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwa suala la kuichambua bajeti naowaamin ni Dr Semboja na Lipumba,,,,,,
   
 15. M

  Makupa JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa bajeti iliyowasilisha kwenye bunge letu , imethibitika ya kwamba vyanzo vikuu vya mapato kwa serikali vitaendelea kuwa ni vinywaji na sigara
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Toa pumba hizi.
   
 17. lidoda

  lidoda JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 631
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 80
  Sasa hao wanywaji aw bia na wavuta diagram wakiokoka si uchumi wetu uta kolapsi????!!!! Vingineyo serikali ya CCM iwapigie magoti wachungaji wasiwaokoe wananchi
   
 18. King2

  King2 JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Walevi na waharibu Mapafu.
   
 19. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  ipo siku vyanzo vya mapao vitakua pipi na JOJO..hii nchi kazi sana
   
 20. M

  Makupa JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nina wasiwasi wako na kisomo chako, inakuaje mtu mzima unapinga ukweli shame on you
   
Loading...