Bajeti ya Mishahara kupanda kwa zaidi ya asilimia 40! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya Mishahara kupanda kwa zaidi ya asilimia 40!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nnn, Jun 23, 2011.

 1. n

  nnn Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Napenda kufahamu wana jf,kuhusu hawa watumishi wa umma,wamepandishiwa mshahara kwa asilimia ngapi?

  Story toka Raia Mwema:

  Mishahara kupanda kwa zaidi ya asilimia 40!

  WAKATI Bajeti ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ikiwa imepitishwa na Bunge kwa kuacha fumbo la nyongeza ya mishahara kuteguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, taarifa za awali zinabainisha kuwa mishahara inaweza kupanda kwa asilimia zaidi ya 40.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo kutoka katika duru za kiserikali, ongezeko hilo la zaidi ya asilimia 40 linagusa viwango vyote vya mishahara serikalini kuanzia kima cha chini ambacho ni Sh 135,000.

  Hata hivyo Raia Mwema halijaweza kuthitisha rasmi asilimia halisi ya ongezeko kutoka Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kuzingatia ukweli kuwa jukumu hilo linapaswa kutamkwa kwanza na Waziri husika, kwa mujibu wa sheria namba 16 ya mwaka 2003.

  "Mshahara utapanda sana na ni zaidi ya asilimia 40, mambo yatakuwa mazuri tu kwa watumishi wa umma, lakini Waziri ndiye mwenye jukumu la kutangaza nyongeza hiyo kwa kuzingatia matakwa ya sheria," kilieleza chanzo chetu cha habari serikalini, huku taarifa zaidi zikieleza kuwa mbali na mshahara, marupurupu mengine yanaweza kuongeza zaidi kipato cha mfanyakazi wa kima cha chini hadi kufikia takriban sh 300,000.

  Mgogoro wa nyongeza ya mishahara umedumu kwa muda mrefu, huku Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) chini ya Kaimu Katibu Mkuu wake, Nicholaus Mgaya wakiongoza shinikizo dhidi ya Serikali.

  Katika kushinikiza huko, mwaka jana TUCTA walihamasisha mgomo wa wafanyakazi wa umma nchi nzima hatua iliyomsukuma Rais Jakaya Kikwete kutoa maelezo maalumu mbele ya wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam akionya kuwa wanaotaka kugoma watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

  Baada ya mvutano huo, Serikali iliendelea na mazungumzo ili kufikia muafaka kuhusu kiwango kipya cha mshahara na hadi katika maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi, mwaka huu, zilizofanyika mkoani Morogoro, uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa bado hapakuwa na makubaliano rasmi kati ya Serikali na TUCTA kwa niaba ya wafanyakazi.

  Hata hivyo, katika maadhimisho hayo ambayo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi, katika hotuba yake alieleza kuwa Serikali imesikia kilio cha wafanyakazi lakini akibaki kimya katika kutamka namna kilio hicho kilivyotatuliwa.

  Kutokana na Rais Kikwete kukwepa kutamka suala hilo kwenye maadhimisho ya Mei Mosi, huku minong'ono ikisambaa kuwa kima cha mshahara kuongezeka, wengi walitaraji kuwa ingetamkwa katika Bajeti ya Serikali iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Jumatano, wiki mbili zilizopita.

  Katika hotuba yake hiyo, Mkulo alidokeza tu kwamba mishahara hiyo itapanda lakini hakueleza ni kwa kiwango gani na akasema kuwa hilo ni jukumu la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa umma, ambaye anatarajiwa kufanya hivyo wakati atakaposoma Bajeti yake, wiki kadhaa zijazo.

  Gazeti hili liliwasiliana na Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA, Mgaya ambaye alisema si jukumu lake kutaja nyongeza ya mishahara kwa kuwa hilo ni jukumu la Waziri wa Utumishi kisheria.
   
 2. FiQ

  FiQ JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu hata mm naisubiri, Mkulo alisema tuwait hotuba ya Hawa Ghasia, bt kwa magamba wetu hawa dah usikute wameamua kuongeza buku tano tano tu mana wanasema bajeti yao ni nzuri so bidhaa zitashuka bei eti
   
 3. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  watapandisha posho tu mshahara bado.
   
 4. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  asilimia 40 soma raia mwema la jana
   
 5. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  Nasema, usiwaamini wanamagamba, hawawezi kutoa kauli ya ukweli.
   
 6. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  asilimia 40 hzo pesa labda wachume kwenye mti kama majani
   
 7. logbes

  logbes Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAKATI Bajeti ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ikiwa imepitishwa na Bunge kwa kuacha fumbo la nyongeza ya mishahara kuteguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, taarifa za awali zinabainisha kuwa mishahara inaweza kupanda kwa asilimia zaidi ya 40.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo kutoka katika duru za kiserikali, ongezeko hilo la zaidi ya asilimia 40 linagusa viwango vyote vya mishahara serikalini kuanzia kima cha chini ambacho ni Sh 135,000.

  Hata hivyo Raia Mwema halijaweza kuthitisha rasmi asilimia halisi ya ongezeko kutoka Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kuzingatia ukweli kuwa jukumu hilo linapaswa kutamkwa kwanza na Waziri husika, kwa mujibu wa sheria namba 16 ya mwaka 2003.

  "Mshahara utapanda sana na ni zaidi ya asilimia 40, mambo yatakuwa mazuri tu kwa watumishi wa umma, lakini Waziri ndiye mwenye jukumu la kutangaza nyongeza hiyo kwa kuzingatia matakwa ya sheria," kilieleza chanzo chetu cha habari serikalini, huku taarifa zaidi zikieleza kuwa mbali na mshahara, marupurupu mengine yanaweza kuongeza zaidi kipato cha mfanyakazi wa kima cha chini hadi kufikia takriban sh 300,000.

  Mgogoro wa nyongeza ya mishahara umedumu kwa muda mrefu, huku Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) chini ya Kaimu Katibu Mkuu wake, Nicholaus Mgaya wakiongoza shinikizo dhidi ya Serikali.

  Katika kushinikiza huko, mwaka jana TUCTA walihamasisha mgomo wa wafanyakazi wa umma nchi nzima hatua iliyomsukuma Rais Jakaya Kikwete kutoa maelezo maalumu mbele ya wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam akionya kuwa wanaotaka kugoma watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

  Baada ya mvutano huo, Serikali iliendelea na mazungumzo ili kufikia muafaka kuhusu kiwango kipya cha mshahara na hadi katika maadhimisho ya sherehe za Mei Mosi, mwaka huu, zilizofanyika mkoani Morogoro, uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa bado hapakuwa na makubaliano rasmi kati ya Serikali na TUCTA kwa niaba ya wafanyakazi.

  Hata hivyo, katika maadhimisho hayo ambayo Rais Kikwete alikuwa mgeni rasmi, katika hotuba yake alieleza kuwa Serikali imesikia kilio cha wafanyakazi lakini akibaki kimya katika kutamka namna kilio hicho kilivyotatuliwa.

  Kutokana na Rais Kikwete kukwepa kutamka suala hilo kwenye maadhimisho ya Mei Mosi, huku minong'ono ikisambaa kuwa kima cha mshahara kuongezeka, wengi walitaraji kuwa ingetamkwa katika Bajeti ya Serikali iliyosomwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, Jumatano, wiki mbili zilizopita.

  Katika hotuba yake hiyo, Mkulo alidokeza tu kwamba mishahara hiyo itapanda lakini hakueleza ni kwa kiwango gani na akasema kuwa hilo ni jukumu la Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa umma, ambaye anatarajiwa kufanya hivyo wakati atakaposoma Bajeti yake, wiki kadhaa zijazo.

  Gazeti hili liliwasiliana na Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA, Mgaya ambaye alisema si jukumu lake kutaja nyongeza ya mishahara kwa kuwa hilo ni jukumu la Waziri wa Utumishi kisheria.
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  kupandisha mishahara wakati huna mikakati ya makusudi ya kubana matumizi ya serikali kaka hiyo ni ndoto ya mchana. utaniambia.
   
 9. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ingekuwa ni posho na mishahara ya wabunge na wanasiasa wangepandisha kiasi hicho, kwa watumishi wa umma bado ni ndoto,tusubiri muda utazungumza
   
 10. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Thumbs up! I welcome the news.
   
 11. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Pipe Dream
   
 12. J

  Jobo JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huu ni uongo mtupu! Asilimia 40 labda mshahara wa Wabunge!
   
 13. s

  shukia Member

  #13
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mishahara kupanda pasipo jitihada za makusudi za kudhibiti mfuko wa bei ktk bidhaa za msingi ni "
  changa la macho"
   
 14. T

  The Priest JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  kwanini wanaogopa kutaja,eti atatamka waziri husika,changa la macho,wangekuwa wamepandisha lazima mkulo angesema tu...wait and see
   
 15. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hiyo ni ndoto tena ya mchana. wataongeza sh. 26,000 elfu tu!
   
 16. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ndoto za Abunuwasi! Labda wapunguze matumizi makubwa ya Serikali! Kitu ambacho hawawezi!
   
 17. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,085
  Trophy Points: 280
  Haiwezi kuwa kweli ...ni sawa na mbingu ilivyo mbali na ardhi
   
 18. womanizer

  womanizer Senior Member

  #18
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vitoto vya UDOM vitanikoma
   
 19. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo umenena mkuu!
   
 20. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Na wewe ni Great Thinker? Labda Great Sinker.
   
Loading...