Bajeti ya Marekani ni dolla trillion 4 - hivi Magufuli huwa anawaza nini anaposema Tanzania yaweza kuwa donor country wakati wa Urais wake?

Tang Zhou

JF-Expert Member
Mar 14, 2018
1,208
2,587
Nilikuwa najiuliza zile nchi zinazoitwa donor countries na kiongozi wetu uchumi wake unafananaje - ndipo nikaamua ku-google Federal Budget ya dona kantre ambaye sote tunamjua - Marekani..

And man ohh man - hawa jamaa are filthy rich - if at all rich is the right word to describe them...federal bajeti yao kwa mwaka ni USD 4 trillion....

Sasa ndo nikajiuliza....Rais wetu huwa anawaza nini anaposema nchi hii yaweza kuingia kwenye Club ya dona kantrez kama Marekani katika miaka 10 ya Urais wake??? Au pale anapojitutumua kuwatunishia misuli? Kwa tukorosho hizi kweli?

NA tusisahau Korosho tayari zinatudodea pamoja na kupeleka Jeshi😅😅

Screenshot_2018-12-12-22-57-33-1.png
 
Ukoo wa ufipa mnatafuta kila namna ya kumponda na kumkosoa Rais wetu ilimradi tu mridhishe akili zenu,

sidhani kama kuna hotuba yoyote magufuli alijilinganisha na Marekani kiuchumi, ila nyie mnalazimisha ili mkonge nyoyo.zenu, tushawazoea hamna jema nyie wanaserengeti.
 
Nilikuwa najiuliza zile nchi zinazoitwa dona kantrez na kiongozi wetu uchumi wake unafananaje - ndipo nikaamua ku-google Federal Budget ya dona kantre ambaye sote tunamjua - Marekani..

And man ohh man - hawa jamaa are filthy rich - if at all rich is the right word to describe them...federal bajeti yao kwa mwaka ni USD 4 trillion....

Sasa ndo nikajiuliza....Rais wetu huwa anawaza nini anaposema nchi hii yaweza kuingia kwenye Club ya dona kantrez kama Marekani katika miaka 10 ya Urais wake??? Au pale anapojitutumua kuwatunishia misuli? Kwa tukorosho hizi kweli?

NA tusisahau Korosho tayari zinatudodea pamoja na kupeleka Jeshi😅😅

View attachment 966320
Na wewe unawaza nini?
 
Siku moja nimemsikia Trump akitoa speech kwenye mkutano wa UN anasema Marekani inaanza kutenga bajeti ya almost $700B kwenye jeshi pekee, wakati sisi bajeti nzima haifiki hata $20B!! Mbaya zaidi, utekelezaji wake sidhani kama huwa unafikia at least 70%!!!

Nilitafakari nikajiaminisha kwamba hata Yesu achelewe kwa muda mrefu namna gani, akirudi atakuta hatuna hata ile dalili ya kuifikia Marekani ilipo leo. Never!!! Hasa kwa namna tunavyoenda sasa tukiwa kwenye right traki! Labda siku tukijaribu kuhamia kwenye left traki tunaweza kupiga hatua kidogo, sijui lakini!

Kwa hesabu ya haraka in kwamba, bajeti ya mwaka mmoja ya jeshi tu Marekani inatosheleza bajeti nzima ya bongo kwa miaka 40+...

Bongo bahati mbaya sanaa!!!

Bongo nyosso sanaaa!!!

Usiku mwema!!!
 
Nilikuwa najiuliza zile nchi zinazoitwa dona kantrez na kiongozi wetu uchumi wake unafananaje - ndipo nikaamua ku-google Federal Budget ya dona kantre ambaye sote tunamjua - Marekani..

And man ohh man - hawa jamaa are filthy rich - if at all rich is the right word to describe them...federal bajeti yao kwa mwaka ni USD 4 trillion....

Sasa ndo nikajiuliza....Rais wetu huwa anawaza nini anaposema nchi hii yaweza kuingia kwenye Club ya dona kantrez kama Marekani katika miaka 10 ya Urais wake??? Au pale anapojitutumua kuwatunishia misuli? Kwa tukorosho hizi kweli?

NA tusisahau Korosho tayari zinatudodea pamoja na kupeleka Jeshi😅😅

View attachment 966320
asante kijana wa ufipa kwa kupata cha kuonekana na wewe unafanya kazi
 
Nilikuwa najiuliza zile nchi zinazoitwa dona kantrez na kiongozi wetu uchumi wake unafananaje - ndipo nikaamua ku-google Federal Budget ya dona kantre ambaye sote tunamjua - Marekani..

And man ohh man - hawa jamaa are filthy rich - if at all rich is the right word to describe them...federal bajeti yao kwa mwaka ni USD 4 trillion....

Sasa ndo nikajiuliza....Rais wetu huwa anawaza nini anaposema nchi hii yaweza kuingia kwenye Club ya dona kantrez kama Marekani katika miaka 10 ya Urais wake??? Au pale anapojitutumua kuwatunishia misuli? Kwa tukorosho hizi kweli?

NA tusisahau Korosho tayari zinatudodea pamoja na kupeleka Jeshi😅😅

View attachment 966320
uingereza pia ni Donor pia China Norway Sweden nazo vipi bajeti zao ni $Trillion 4?

Kuna Vitu vingine Simple tu kudadavua! kwani Marekani alifikia vipi hiyo hatua? Tanzania tuna karibu kitu na ao madonor ndiyo wamekuja kukomba huku mara nyingi wakaenda kujiendeleza wao! Sasa kwanini tukiweza kusimamia rasimali zetu vizuri na zikanufaisha nchi yetu vya kutosha why tusiwakopeshe wengine? India mwaka huu katoa Zaidi ya billion 5 kwa Tanzania kwenye miradi ya maji amewezaje?
 
Ni fikra za kijinga kabisa kufikiria kuwa eti mali asilia ndiyo zinaweza pekee kuwafanya muwe matajiri.

Utajiri mkubwa ni kichwani wala siyo kwenye mikia ya fisi na pundamilia.

Utalii wenyewe tunaojivunia unatuingizia $1.9 billion. Afrika Kusini wasio na Serengeti wanaingiza $5 billion kwenye utalii. Egypt wasio na Mikumi wanaingiza $7 billion. Mji, siyo nchi, mji wa Paris usio na Ngorongoro unaingiza zaidi ya $80 billion kwa mwaka. Hapo ndipo inapoonesha kuwa vivutio asilia bila kuwekeza akili, havina maana katika mapato. Kila kitu ni kichwani

Hakuna uwezekano wowote wa kuzifikia mapato nchi kama Norway, kama tutaendelea na ujinga kuwa ukiwa tu na mbuga za wanyama, au dhahabu au Tanzanite, basi weqe ni tajiri. Utajiri wa leo upo kwenye kichwa.
 
Hoja yako nzuri. Ila nadhani kuna vitu vya kuzingatia kwenye ishu ya bajeti hapo na ukubwa wa nchi unazojaribu kuzilinganisha..

Bajeti ya Marekani ni kubwa kweli kweli.. Ni $4.407 trillion kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018.. Lakini bajeti hiyo inaenda kuhudumia watu zaidi ya milioni 325.7..

Isitoshe ukubwa wa USA haulingani na ukubwa wa TZ.. US wana Kilometa za Mraba 9.834 million km² wakati Tanzania hata milioni moja tu hazijafika.. Nadhani tupo kwenye 945,087 km²..

Kuna factors nyingi sana zinazoonesha ni kwa kiasi gani US hatuwezi kufanana nao kwa vingi hivi ila ishu ya bajeti sidhani kama ni big deal kwa sababu ni kulinganisha mbingu na ardhi..

Naamini Tanzania itakuja kuwa donor country kwenye mambo mengi zaidi ukiondoa kwa sasa ambapo inategemewa kwenye ishu ndogo ndogo.. Huko mbeleni tutakuja kuwa donor country kwa kutoa pesa taslimu NA materials ili kusaidia nchi tunazozimudu kuzisaidia.. Inawezekana kabisa.

Tumshukuru Mungu tumepata kiongozi mwenye mawazo makubwa.. Let's think Big altogether.. Inawezekana mazee..
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom