Wo shi niubi
JF-Expert Member
- Aug 14, 2015
- 1,266
- 1,649
Hapana budget kwanza inategemea mapato unayokusanya, huwezi ukakusanya bill800 kwa mwezi ukategemea budget ya trillion 30 kwa mwaka, hakuna mfadhili popote duniani anaweza kukupatia ongezeko la budget yako trillion 10 hayupo, ni ukweli usio pingika kuwa awamu ya Magufuli ukusanyi wa mapato uliongezeka kupita awamu zote za nyuma hivyo budget kuongezeka pamoja na kuwa utegemezi ulikuwepo.Ndugu hicho siyo kigezo cha kiuchumi kuongezeka tarakimu ni uwezo na nchi kujiendesha yenyewe kwenye bajeti yake sisi bajeti yetu ni tegemezi
Tuna zunguka sana , kenya kwa mwezi ina kusanya zaidi ya trillion 4 za kitanzania, maana yake uwekezaji kenya ni mkubwa kuliko tz , wingi wa viwanda, wanauza bidhaa nyingi nje ya nchi kushinda tz, mazingira mazuri ya ufanyaji biashara , serikali inakusanya Kodi ipasavyo.
Hivi kweli Tanzania ukusanyi wa Kodi trillion 1.5 kwa mwezi ni Kodi kubwa hii? Tanzania sio nchi ya kukusanya kodi kidogo kiasi hiki huku tukilalamika eti wafanya biashara wanaonewa, kama tunataka kuendelea na kushindana na mataifa mengine lazima tubadili mtazamo na fikra , bado tuna fikra na uelewa mdogo kuhusu dunia inavyokwenda.